Wassira awakana 'watoto wake' waliojiunga na CHADEMA...

Naomba kujuzwa wadau,hivi wale jamaa wa gombe si huwa wanaishi kiukoo kwa makundi makundi,sasa huyu ni wa kichina nini mbona anakana uzao wa ukoo wake?na yule wa marekani mbona hajamsemea?
 
Ubinaadamu kazi nyie! Mtu akiwa CCM kwanza anabadilika anakuwa kama mnyama kwanza: ona hili zee linawakana watoto wake: angeulizwa kama anaweza KUWAJUA muone angesemaje:

Hivi kwa mfano ESTER NA LILIAN wangekuwa wametwaa medali za dhahabu OLYMPIC . Je huyu mzee mbaguzi angeita waandishi kuwakana hadharani na kudai ni kashfa kwake?
 
Sijaona mantic katika hoja yake anamaanisha watoto wake hawana haki ya kuingia chama wanachokitaka? Sijambo la ajabu kuona mtu kaacha dini ya wazazi wake sembuse mtu kuacha chama cha wazazi wake.

Kama watoto wake wanakuwa katika chama fulani kwa kuzuiwa na baba yao basi nadhani hao watoto wanayo haki ya kushitaki kwasababu wamenyimwa haki yao ya kuamua kuwa wanachama wa chama chochote ili mradi hawavunji sheria yoyote ya nchi.
 
Zee la Gombe limefunguka, wale walijitambulisha kuwa ni wa ukoo wa Wassira, hawakusema wao ni watoto wa SI TEVIN WASSIRA. Yeye ndiye anajiona supper sana, kumbe hakuna lolote. Sura yenyewe ile, ndiyo mtu anaweza kung'ang'ania ajitambulishe kwa jina lake?
 
Mkuu ni kweli hujui kwanii amekimbilia kwenye media?
Nitakuelewa ikiwa pia ungehoji kwanini CDM kukimbilia media kupoke wanachama hawa wawili tu tena na vigogo wakati kilasiku watu wanajiunga kimya kimya cdm

Wakati mwingine unaweza kukuza jambo ukidhani unajisafisha. Sasa mjadala utaanza wa familia yake, watoto, mahusiano yake (na tunajuwa alikuwa maarufu sana kwa wale wa mama wa mtaa wa maandazi -msasani). Yeye angeendelea kupiga mzigo, na hata hiyo publicity ya CHADEMA ingefikia tamati. Unakumbuka hatua ya Zuma kuingilia kati ile cartoon ya 'lunch box' yake? Isue ilisambaa kama mvua.

Na Wassira kusema kuwa si watoto wake, kwa mila ya Tanzania let alone za Mara mtoto wa kaka yako ni watoto wako, wanatumia u-bin sawa. ah good luck to him.
 
Kinachoendelea hapa ni michezo ya kisiasa tu....
Jana hapa kila mtu alimtolea maneno ya kashfa Wasira kwakuwa tu watoto wake wamejiunga CDM, media zikapamba na vigogo wakawapokea kwa mbwembwe nia ni kummaliza wasira kisiasa

Lakini leo kajibu si watoto wake wa kuzaa kama inavyoripotiwa na kupambwa tunaanza kumuita mjinga

Tatizo ni CDM wenyewe kuupamba sana ujio wa hao mabinti as if wamemkomoa Wasira na kwakuwa wasira nae kichwa maji katumia njia ile ile kujibu
 
Ebu tusiwe double standard, Dr. Slaa kuna mawili aidha kapotoshwa ama kaamua kupotosha kwa makusudi.Nilichokitambua mimi jana hasa baada ya kupewa kadi kwa mbwembwe ni kuwa Watoto wale ni wa Wasira wa kuzaa.Niliamini hasa baada ya Slaa kumu-attack huyu mzee moja kwa moja na ndicho Watanzania wengi walikitambua jana.

Tuache tabia ya kuelezea matokeo na kusahau chanzo.Hapa chanzo ni Slaa na Wasira ni matokeo tu.Inashangaza Pro CDM kugeuza Wasira kama ajenda.Tuache ushabiki na isiwe ''kajamba kuku pafyumu,bata aaaagh''.Hiki kizazi cha ajabu kabisa.
 
Kwa iyo hata kama ni watoto wa kaka ake hawapaswi kumuita baba????

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
Watu mnakuza mambo yasiyo na tija. Wakiwa watoto wake au wasiwe watoto wake, amewakana au hajawakana, na wamejiunga na cdm, tatizo ninini? Usiku mwema.
 
Amejichanganya mwenyewe yani mara aseme sio wanju mara ni wa ndugu yangu! Naona kakosa hoja kabisa kwani akikubali atakufa?

Naona ccm uongo kwao ni ukweli.
 
Watu mnakuza mambo yasiyo na tija. Wakiwa watoto wake au wasiwe watoto wake, amewakana au hajawakana, na wamejiunga na cdm, tatizo ninini? Usiku mwema.

Tatizo ni wassira kusema kuwa watoto wa kaka yake sio watoto wake.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
What goes around comes around.Hii ndio balaa ya kuhusudisha watoto wa vigogo.Slaa anatakiwa kubadilika sasa na aache umbeya, inanishangaza sana Rais mtarajiwa anashindwa kupata taarifa za uhakika na kuona kama kuna haja ya kuita media ama lah.

Na sisi watoto tuwe na tabia ya kuwataja Wazazi wetu halisi hata kama ni ''wauza kuku'' ama mafundi ''viatu'' hii habari ya kutumia majina,bila kutofautisha ama kufafanua hasa pale inapobidi ni ''kaugonjwa'' kengine hapa Bongo.

CCM wamezoea chokoza na kuzushia watu sasa CDM wameamua kuwa offensive watatembezwa kwa kucha mambo yasiohusu siasa mpaka wakose muda wa kufanya siasa.Mkapa alijuta Arumeru.Wassira ni zamu yake kusema kama ameweza wakana watoto wake (kwa mila za kiafrica) yaani waridhi wa pili kama hakubahatika watoto, ni vipi atawajali watanzania.Ningekuwa mimi ni Slaa kesho tuu ningepand akatk media nim-quote Mkapa Arumeru na wassira kwenye hili..Na ningewaita CCM wote watu wa hovyo na wabauguzi wanadanganya watanzania kuwa wanaweza wajali wananchi.
 
Kinachoendelea hapa ni michezo ya kisiasa tu....
Jana hapa kila mtu alimtolea maneno ya kashfa Wasira kwakuwa tu watoto wake wamejiunga CDM, media zikapamba na vigogo wakawapokea kwa mbwembwe nia ni kummaliza wasira kisiasa

Lakini leo kajibu si watoto wake wa kuzaa kama inavyoripotiwa na kupambwa tunaanza kumuita mjinga

Tatizo ni CDM wenyewe kuupamba sana ujio wa hao mabinti as if wamemkomoa Wasira na kwakuwa wasira nae kichwa maji katumia njia ile ile kujibu

Jana ilisemwa kuwa ni watoto wa wassira wamejiunga cdm wala haikusemwa kuwa ni watoto wa kuwazaa, sasa kama sio big issue uyo wassira angenyamaza leo alivyojitokeza ndo kazidi kusambaza habari hii hata kwa wale ambao walikua hawajaijua.
Mtu mshamba anapojaribu kufanya jambo flani ili aonekane mjanja hujikuta anakosea na kuzidi kuonekana mshamba maradufu.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
naona wengi mnachangia kwa kumnukuu mh wazri lakini hamnukuu maneno haya

"wale ni watoto wa kaka yangu, kwaiyo ni wa ukoo wetu. na kwenye ukoo wetu hatukuwalea watu kwa misingi ya chama wala dini, wale watoto wanahaki ya kujiunga na chama chochote cha siasa"

nampongeza ukoo wa wasira kwa kuwalea watoto wao katika misingi hii. hii itachangia sana kupunguza usultani katika utawala. kama ukoo wa karume, mwinyi, malecela, kikwete, ndesamburo, na ukoo wa Mtei wangekuwa na maadili haya, kusingekuwa na kelele izi za sasa juu ya watawala kurithishana mamlaka hapa nchini
 
Ebu tusiwe double standard, Dr. Slaa kuna mawili aidha kapotoshwa ama kaamua kupotosha kwa makusudi.Nilichokitambua mimi jana hasa baada ya kupewa kadi kwa mbwembwe ni kuwa Watoto wale ni wa Wasira wa kuzaa.Niliamini hasa baada ya Slaa kumu-attack huyu mzee moja kwa moja na ndicho Watanzania wengi walikitambua jana.

Tuache tabia ya kuelezea matokeo na kusahau chanzo.Hapa chanzo ni Slaa na Wasira ni matokeo tu.Inashangaza Pro CDM kugeuza Wasira kama ajenda.Tuache ushabiki na isiwe ''kajamba kuku pafyumu,bata aaaagh''.Hiki kizazi cha ajabu kabisa.

Slaa alisema mabinti hawa ni wa wassira wala hakusema ni watoto wake wa kuwazaa.
Na bado hawa ni watoto wake coz ni watoto wa kaka yake.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Nadhani wassira angetumia akili tuu na kuchukua credit kwa kuwa na familia yenye demokrasia.Na yeye ni muumini mzuri wa demokrasia.Kakamatwa offguards sasa itabidi akawajibu wazee wa kwao,kauli aliyosema hilo tuu linamtosha kumpa taabu kisiasa na kifamilia.
 
Chadema bana!!!? kwa cheap popularity tu hamjambo. Oooh watoto wa wasira wajiung na chadema! Kumbe uongo mtupu!
Mmeshaanza kuwa waongo hivi hamjashika madaraka na hamna kubwa la kuficha, mkipata madaraka itakuwaje!
Hizo ni siasa uchwara.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom