Watanzania kwa kupenda siasa na kuongea maneno mengi vitendo sifuri ndio wenyewe.
Kwanini hawa watu wa dini hawatoi waraka juu ya kilimo bora na namna ya kumsaidia mwumini aweze kujitegemea? Kwanini hawatoi waraka juu ya elimu bora kwa vijana wetu na namna ya kuzisadia shule za vijana wetu ziweze kuwa nzuri?
Wache wote watoe lakini ni kama tunapoteza muda kujadiliana mambo ambayo yanaeleweka na kilichobaki ni sisi kwenye majumba yetu na kwenye jamii yetu kuyatekeleza.
Hivi kuna mtu ambaye hajui madhara ya ufisadi mpaka ahitaji waraka kuyaelewa? Kwanini basi hatufanyi kitu pamoja na kujua ubaya wake?
Mtu mwenye njaa atachukua pesa kutoka kwa fisadi hata akijua kufanya hivyo ni vibaya.
Juhudi ifanyike kuwafanya watu waweze kujitegemea; hilo ndilo muhimu kuliko mengine yote. Kuna mwana JF aliandika hapa kwamba mwenye njaa hawezi kuwa na mawazo huru. Mimi nakubaliana naye.
Tukiondoa umaskini uliokithiri na tukiwasaidia vijana wetu kupata elimu bora, hao mafisadi hawatakuwa na muda mwingi wa kutunyanyasa.