Mkuu wangu swala la waraka kutolewa na vyombo vya dini ndicho nachopinga mimi..sio somo zito na kubwa kwangu kuelewa na kukubaliana na upande wowote isipokuwa utaratibu unaotaka kutumika ndio napingana nao..mmh! Mkuu Mkandara, ingawa waraka huo haujatoka lakini introduction iliyotolewa na Ponda inatia mashaka makubwa.
Je wewe upo behind this? (soma quated text from Mwananchi news paper)
To me, kanisa Katoliki na viongozi wake siwajui wala sina haja ya kuwajua kwa sababu sikubaliani na mafundisho yake pia imani zetu ni tofauti.
Mkuu wangu, nazungumza kama mtu asokuwa na imani ya dini.. sasa wewe unapoweza kuona baadhi ya maneno yangu kama ni utovu wa heshima kwa kiongozi wako hapo ndipo inapoja imani yako wewe na sio yangu.Hapa nimekuelewa Kiongozi, maana nilikuwa nashindwa kuelewa imekuje umepoteza objectivity hata kwa vitu vilivyo wazi bro, naamini wewe ni mwelewa sana hasa ukiangalia michango yako kwenye mada zingine. Naona unajisahau unakuwa kama mfia uislamu fulani ingawa hutaki weka wazi. Nadhani umeusoma waraka wa kanisa katoliki, hauna mambo ya kiimani zaidi ya kuelimisha jamii bila kuangalia imani, waelewe somo la uraia na kufanya uamuzi sahihi kwenye changuzi zijazo.
Regards
Masa
Mkuu wangu, nazungumza kama mtu asokuwa na imani ya dini.. sasa wewe unapoweza kuona baadhi ya maneno yangu kama ni utovu wa heshima kwa kiongozi wako hapo ndipo inapoja imani yako wewe na sio yangu.
To me Padre ni binadamu ambaye nitamheshimu kama atakuwa ktk kazi yake.. kama vile namheshimu Mwai Kibaki kuwa rais wa Kenya lakini sina mpango naye. Atakapo taka kuingilia mambo yangu nina kila haki ya kusema sikujui! haina maana nawachukuia Wakenya..
Wakati huo huo nitamdharau Sheikh au Mufti ikiwa atajaribu kuingiza Uislaam ktk serikali kwani sii kazi yake, hana ujuzi huo na elimu yake haiwezi kujenga mwongozo wa nchi..Azungumze kama raia wengine huu ndio mfumo wa kiislaam ulonivutia mimi katika dini hiyo..Kama anataka Siasa bora aingine siasa kama alivyofanya Dr. Slaa/Mtikila au Masheikh wengine.. hapo nitamwelewa na mtazamo wangu kwake utabadilika.
Kwa vipi uone kiongozi wa dini hana ujuzi wa elimu ya kuendeleza nchi?
Nilichoandika mimi -Wakati huo huo nitamdharau Sheikh au Mufti ikiwa atajaribu kuingiza Uislaam ktk serikali kwani sii kazi yake, hana ujuzi huo na elimu yake haiwezi kujenga mwongozo wa nchi.Kwa vipi uone kiongozi wa dini hana ujuzi wa elimu ya kuendeleza nchi?
Dini zinapoingia Siasa!
Kuna pahala na wakati dini na siasa zinaenda sambamba. Chukua nchi kama Saudi Arabia na nchi za Gulf ( UAE, QATAR, BAHRAIN, KUWAIT AND OMAN) Ambazo wananchi wake nearly or wote ni dini moja,Kwa vipi uone kiongozi wa dini hana ujuzi wa elimu ya kuendeleza nchi?
Sijajua hasa sababu ya huo waraka...Ummy Muya
KATIBU wa Kamati ya Kutetea Haki za Waislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, amesema waraka maalum utakaowaongoza waumini wa madhehebu hayo katika uchaguzi mkuu wa mwakani, umekamilika.
Sheikh Ponda aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam ambapo alisema waraka huo umesheheni ujumbe mzito kwa ajili ya Waislamu.
Alisema waraka huo uko tayari kuanza kusambazwa kwa Waislamu wote nchini na huku ukitangazwa katika vyombo vya habari .
"Waraka huu utakuwa mzito sana ukilinganishwa na ule ambao tuliutoa mwaka jana,"alisema.
Kwa mujibu wa Sheikh Ponda waraka huo umeandaliwa na shura ya maimamu, inayojishughulisha na masuala ya siasa.
Tayari Kanisa Katoliki nchini, limetoa waraka wake unaowataka wananchi kuchagua viongozi, waadilifu na wacha Mungu katika uchaguzi wa serikali za mitaa na ule wa mwakani.
Hata hivyo, waraka huo umezua malumbano makali kutoka kwa baadhi ya wanasiasa wakidai kuwa, unaweza kusababisha taifa kusarambaratika.
Akizungumzia maandamano, Sheikh Ponda alisema wanasubiri kumalizika kwa kikao cha Bunge, ili kujiridhisha na hatua zilizofikiwa na chombo hicho katika kushughulikia suala la Mahakama ya Kadhi. "Maandamano ambayo tumepanga yana ujumbe hivyo hatuwezi kuyafanya mpaka kikao cha Bunge kiishe na kufahamu suala hili lipo katika hatua gani,"alisema
SOURCE:MWANANCHI.
Ni kweli kabisa. Kwa vyovyote vile ilivyo, kama watu wataamshwa na kujua nini wajibu wao, itasaidia sana kwa siku zijazo. Wakati huu ambao uongo wa waziwazi unafanyiwa mikakati ya kuaminishwa kwa watu ni muhimu dini nazo zikatoa vipaumbele vyao. Nani atamchagua nani itakuwa ni shauri la mpiga kura.Hii ni kali!
Kwa kifupi wananchi wanaonekana kukata tamaa kabisa... leo nimesikia mazungumzo ya watu tena wananchi wa kawaida kabisa wakisema:
" Vyama vya upinzani ni kama deiwaka tu... chama tawala kinapata fungu kubwa na kuwagawia vyama pinzani kiduchu..hivyo hakuna namna wananchi watapata mbadala wa kuwapa nafuu ya maisha"...
Mimi naona ni vema tu kila kikundi katika jamii wakafanya upembuzi wao na kuandika waraka/makabrasha na kuwaelimisha watu wao ..after all Civic education inapaswa kuwa mchakato endelevu na siyo kusubiri tu wakati wa uchaguzi.Badala ya kuwabeza viongozi wa dini na nyaraka zao nadhani ingekuwa vizuri tukawaunga mkono.