Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
Rev Ushauri mzuri.
Lakini sometimes is easy said than done kama uwanja wa mpira kwenye mashindano ambayo timu uipendayo inacheza na wewe uko bench unavyoweza kukosoa mchezaji wakutegemewa alivyojifunga goli.
Tatizo kubwa linalotusumbua ni life after the action you decide to take. Kwa nchi kama za kwetu unaweza kujikuta wewe kwa mob psychology ukaishia kuwa Bangusilo maana kati ya hao kumi na moja walio ji identify huenda wawili tu ndo wanamaanisha na wengine sitaki na taka. Ukiangalia wewe ndo tegemeo la ukoo mzima na family iliinvest kwa wewe kufika hapo what do you do?
Vita kama hiyo rahisi kwa watu ambao calculated risk is more than 50% sasa who knows may be thats what they are doing sasa si ndiyo na wewe ukawa mpiganaji wa wanyuma (comanding unit) msituni na wao wako front line? Kama hata waliweza kuwa consult at certain point huoni hata hapo wali dare?
Felister,
If they are FEARFUL of life after sction, then they do not deserve an audience!
Mandela was Bangusilo, and so was Mrema, Lumumba, Kenyatta, Njelu Kasaka, Jumbe, Hamad including Kawawa and Nyerere.
Wao wanaogopa Chama na hatua za Chama kuwminya haki yao? Sasa mlalahoi atasemaje?
Kwa wao kuogopa Life After Action, kunatangazia umma wazi kuwa Chama chao na Serikali yao si kwa ajili ya Wananchi, haifuati haki wala kujali utu, haina Demokrasia na ni Chama na Serikali gandamizaji.
Let say walipokutana Butiama, waliwakilisha hoja ya Chama kutoa karipio na adhabu kwa Lowassa, Chenge, Karamagi na msabaha kwa kuliingiza Taifa hasara kutokana na Uzembe na mazingira ya Rushwa? Je waliwasilisha hoja kutaka hawa Wanne wavuliwe Ujumbe wa CC na NEC? Je walishurtisha hawa jamaa Wanne na Rostam waombe radhi kwa makosa waliyofanya?
Kama walifanya hivyo na hawakusikilizwa na kupuuzwa, kwa nini wanaendelea kuinadi CCM na kudai CCM ni chama bora?
Hivyo vita vyao vinapaswa kuwa dhidi ya mfumo mbovu na si kung'ang'ania kutajana majina ya waliohujumu!