Asalaam wana jamvi:
Nimekuwa nikijiuliza maswali kadhaa juu ya mwenendo na harakati za chama cha mapinduzi (ccm) juu ya hali ya kisiasa,kiuchumi na kijamii,maswali yangu yanajikita kwa kundi linalojihita ni watetea haki na kupinga ufisadi na ukandamizaji wa haki za binadamu,samweli sita,mwakyembe,selelii na james lembeli na wafuasi wao ktk ccm je, wako wapi ktk matukio yafuatayo:-
(1).Moja mbinu chafu za kisiasa zinazofanywa na chama cha mapinduzi(ccm),kama propaganda kidini dhidi ya upinzani,kujihusisha na utengenezaji wa vidio feki na matukio mengine ya kinyama dhidi ya upinzani wanasimama upande gani ktk haya mambo?kauli yao ni ipi?
(2).kuporomoka kwa uchumi na kuinuka kwa mfumuko wa bei huku serekali na ccm ikilidhia kupandishwa holela kwa gharama za umeme,maji na usafiri bila kuangalio ongezeko la kipato cha wakulima na wafanyakazi,ipi kauli yao ktk hili?
(3).Ufisadi ulifanywa na chama chao wanachokitumikia ktk swala JITEGEMEE COMPANY na wao wakijipambanunua kama wapinga ufisadi je,wanaridhika na ufisadi huo?upi msimamo wao?
(4).Dhuluma za ardhi zinazofanywa na ccm na serekali huko ngorongoro dhidi ya wamasai huko ngorongoro,je,wapinga ufisadi na unyanyasaji wa raia wakina samweli sita ili wanalisemea vp?
(5)Kuporoka kwa kasi na janga la kufeli watoto wetu je,hili nalo wamelisemea wapi?
Samweli sita amekuwa akijipambanua kuwa yeye ndie mgombea wa urais mwema na mzuri kuliko wote ndani ya ccm mwaka 2015,bila kujitokeza ktk majanga kama haya mazito yanawatesa watanzania,ili linanifanya kupata majibu juu ya ili kundi la kina sita na wafuasi wake kuwa ni wanafiki na wazandiki wakubwa ambao hawastahili kujihita wateta raia huku wakiishi ktk chama fisadi(ccm) na kundi la wala rushwa wachafu wa matendo kama mwigulu nchemba, kama sita ni mstaarabu kwanini hawakemei watu kama wakina nape,wasira na mwigulu juu ya mataendo ya kikatili na machafu dhidi ya upinzani na raia kama kibanda?ccm imeoza hakuna msafi wote wachafu,hakuna mtetezi wa haki za binadamu na haki za raia ndani ya ccm....ccm ni kichafu kimekufa na kimeoza Sitta na kundi lake aache mara moja kujipambanua kuwa yeye ni mwanaharakati na mpinga ufisadi huku wakiuchekea ufisadi unaofanywa na ccm na ufedhuli wa dhidi ya upinzani.....ccm sio chama cha kisiasa tena ni kundi la wezi tu.
wamekaa kimya katika issue zote hizo muhimu wanasubiri uchaguzi ukaribie halafu ndio waamke na kudai walikuwa wanapinga hayo yote uliyoyataja utamsikia hata salim atadai alikuwa anapinga yote haya. kiongozi mzuri utamjua wakati dhuluma inafanyika na sio wakati wa uchaguzi.