'Wapiganaji' walioko CCM wanapigania nini hasa?

Hivi wana sifa zipi?
Je Magufuli yumo?
Je anaufisadi gani hadi atajwe na Dr. Wa Ukweli?
 
wapiganaji?
hili neno lina utata,...
me nahisi wawe na uwezo wa kukunja na kurusha ngumi,...
wawe wameenda jimu kwa sana,...unasemaje?
 
Huu ni ukweli unaoudhi, maswala maslahi ya nchi na watu wake wabunge wanaoonekana kuvipigania ni wa CCM.
Stela Manyanya sikiliza michango yake na anavyongea kwa uwazi na upole. Na kunawakati alimtaja wazi kwa Jina Zitto Kabwe bungeni akimtuhumu kurudisha mguu nyuma kwenye swala la kupigania ukweli.'

Luhaga Mpina. Watu wamemjua kwenye bajeti ila namkumbuka kwa maswala matatu kabla ya bajeti.
Alikwamisha kifungu kilichotoa adhabu ndogo kwenye mabadiliko ya sheria ya manunuzi ya umma kwa majibizano makali na mwanasheria mkuu
Amepigania mishahara na posho kwa wenyeviti wa vitongoji na madiwani.
Amepigania haki za watu wanaokaa karibu na hifadhi kwa muda sasa.
Hamisi Kigwangala ndiye mbuke pekee anayepigania kikamilifu haki za madaktari na ameshatishwa hadi na chama chake.

CHADEMA IPO, chakushangaza hakuna wanochofanya bungeni kuwasaidia walimu na madaktari. Wanaongea tu. Walifanya nini kwenye swala la kambi lasmi ya upinzani? Au ndo chadema kwanza.

Kuna mbunge wa CCM Aliniambia makinda huwa anawasiliana na Mbowe jinsi ya kuongoza bunge na akasema tutegemee maigizo na c utendaji sikuamini ila sasa naanza kurifikiria upya.

Miongozo inakataliwa watu wanakufa na bunge linaendelea na vikao. Kweli CHADEMA wameshikwa masikio hivi.
 
nakubaliana na wewe ingawa umemsahau Deo Filikunjombe

ndani ya CCM kuna watu wanapigania haki za raia ila kila siku najiuliza wanapigania toka kwa nani ?? maana serikali ni ya chama chao kwa nini wawe makundi mawili

samahani naomba kujua Samwel Sitta yuko wapi maana simsikii kabisa
 
Huu ni ukweli unaoudhi, maswala maslahi ya nchi na watu wake wabunge wanaoonekana kuvipigania ni wa CCM.
Stela Manyanya sikiliza michango yake na anavyongea kwa uwazi na upole. Na kunawakati alimtaja wazi kwa Jina Zitto Kabwe bungeni akimtuhumu kurudisha mguu nyuma kwenye swala la kupigania ukweli.'

Luhaga Mpina. Watu wamemjua kwenye bajeti ila namkumbuka kwa maswala matatu kabla ya bajeti.
Alikwamisha kifungu kilichotoa adhabu ndogo kwenye mabadiliko ya sheria ya manunuzi ya umma kwa majibizano makali na mwanasheria mkuu
Amepigania mishahara na posho kwa wenyeviti wa vitongoji na madiwani.
Amepigania haki za watu wanaokaa karibu na hifadhi kwa muda sasa.
Hamisi Kigwangala ndiye mbuke pekee anayepigania kikamilifu haki za madaktari na ameshatishwa hadi na chama chake.

CHADEMA IPO, chakushangaza hakuna wanochofanya bungeni kuwasaidia walimu na madaktari. Wanaongea tu. Walifanya nini kwenye swala la kambi lasmi ya upinzani? Au ndo chadema kwanza.

Kuna mbunge wa CCM Aliniambia makinda huwa anawasiliana na Mbowe jinsi ya kuongoza bunge na akasema tutegemee maigizo na c utendaji sikuamini ila sasa naanza kurifikiria upya.

Miongozo inakataliwa watu wanakufa na bunge linaendelea na vikao. Kweli CHADEMA wameshikwa masikio hivi.
Subiri matusi sasa.
 
Response ya CHADEMA kwenye huu mgogoro wa madaktari na hata walimu ni sawa kabisa. Kumbuka, kama CHADEMA watazidisha kelele sana, swala zima litageuzwa kuwa la kisiasa jambo na ukishafanya hivyo ujue hakuna hatua yoyote itakayopigwa. Hata ilivyo sasa, CCM (i.e Martha Mlata) wanajitahidi sana ili ionekane kuwa CHADEMA na hata nchi za nje wanachochoa hii migomo!

Kuhusu Mpina, huyu Mheshimiwa ameshagundua CCM ni dhaifu. Mtindo wa kuswaga wabunge (CCM) kama ngombe umeshaleta hasara sana si tu kwa chama chao bali kwa taifa. Na Mpina sasa anaona kuna haja kuwa mkweli badala kuishi kwa mtindo wa fitna. Whether atafanikiwa hilo ni jambo jingine lakini binafsi sidhani kama CCM wana mbunge makini kama Mpina. Ana qualities zote za kuwa 'legislature'.

Ukisikiliza wabunge wengi wanaongea vitu vya hapa na pale, mara kisima jimboni, mara madawati, lakini hawaunganishi na sera/mipango. Mpina ndio anaonekana kufanya hivyo na ndio maana naona ni 'legislature' wa kuigwa hapa Tanzania.
 
Mzee Mwanakijiji, hao makamanda dhidi ya ufisadi wamegawanyika makundi mawili, miongoni mwao wamo wanapinga ufisadi kwa sababu wanauchungu wa dhati na umasikini wa Watanzania ambao ufisadi umechangia kuongezeka kwa umasikini na unaendelea kuitafuna nchi na utaendelea kwa miaka kadhaa ijayo.

Kundi la pili ni la wapinga ufisadi wanaopigania nafsi zao, wanahasira kwa sababu nao wanataka share yao kwenye huo mkate na nafasi zikiwakalia vazuri, nao watafisidi vile vile hivyo nawaweka kundi moja na mafisadi tuu.Kwa mtazamo huo kuna makamanda wenye uchungu na makamanda mafisadi.

Swali ni jee ndani ya CCM, wanapigania nini?. Jibu langu la jumla ni kuwa wanapigania nafsi zao just for survival na wakishapata uhakika wa survival baada ya 2010, mtawashuhudia nao wakifisidi ushahidi ni 'time will tell'.

Kitu kibaya zaidi kuhusu baadhi ya hawa makanda ambacho mtakishuhudia ni kwa baadhi yao kuwapigia magoti mafisadi ili kuwanusuru na panga la CCM kupitishwa kugombea 2010 na wakishapitishwa, wataungana na kuwa kitu kimoja kwa ajili ya kuweka mikakati ya 2015.

Baadhi watakao piga magoti ni wale ambao nguvu ya mafisadi kuhakikisha hawateuliwi na CCM kugombea itatumika, na wakisha toswa na CCM, watatamani kukimbilia upinzani sio ili kuendeleza mapambano, bali kujaribu kuokoa mkate wao wa kila siku na nawahakikishieni, kama mafisadi watamwaga fedha kuhakikisha makamanda hawapiti, na wakihamia upinzani, ndio kwanza sasa chama kitamwaga mapesa zaidi kuhakikisha hakishindwi.

Baadhi ya makamanda watapigwa chini na hapo ndipo itakuwa mwisho wa habari yao, kitakachofuatia ni kwenda kuwalamba miguu mafisadi kwa kurejea CCM wakiwa wametahayari kama alivyofanya yule kinara wa kundi la G-55.

Hizi harakati za kujipambanua kwa pamoja na kuzungukiana majimbo ya wapiganaji zamu kwa zamu huku wakitoa michango ya shilingi 500,000 walizopewa na mshitiri, wakisindikizwa na ka 'kipindi maalum' ndani ya taarifa za habari (no 10min news clip) ya kwenye TV ya mshitiri, hizi ni nyimbo tuu za shangwe na mapambio ya kujinusuru na panga la uteuzi wa CCM mwaka 2010, baada ya hapo kutakuwa hawana hili wala lile.

Sibezi juhudi za makamanda, bali mbinu zilizotumika kuwapambanua bungeni tukianzia kwenye ripoti ya Richmond iliyotumika kumchapa bakora EL kwa kumuhukuma bila kupewa fursa ya kusikilizwa, hivyo ukamanda wao unapimwa ni kwa kiasi gani wanaweza kuzungumza kwa jazba na mapokezi makubwa makubwa kuashiria wananchi wanawakubali.

Wapiganaji wa kweli ni wale ambao wako tayari to take risk kwa kusimama mbali na uvundo kuwathibitishia watanzania kuwa huku tuliko chama kimetekwa na mafisadi, hivyo baada tuu ya kuvunjwa Bunge mwakani, wataonyesha waliposimama na wananchi watawachagua kwenye chama chochote watakacho simama nacho na hawa ndio watakuwa wapiganaji wa kweli kweli.

Wale makamanda wanaopigania nafsi zao, mtawatambua kwa kutokubali kurski nafasi zao ndani ya CCM ambako mafisadi wana upper hand. Hawa watasubiri mpaka watakapo temwa na CCM ndipo waje upande wa pili kujaribu kamari ya upinzani, hawa ndio watakao kwenda na maji kwa sababu upinzani Tanzania ni kwenye baadhi tuu ya maeneo, kuna maeneo mengi CCM inachaguliwa sio kwa sababu imekubalika sana, bali kwa sababu ya mazoea tuu na kukosekana kwa elimu ya uraia.

Kuna sehemu hata akisimamishwa mgombea kiazi vipi, atapita tuu.Kwa vile CCM ina wenyewe, na baadhi ya wenyewe hao ndio hao hao mafisadi na wengine wao ndio hao makamanda, hapa ni mwendo wa mwenye kisu kikali ndie anayekula nyama, na ili ukubaliwe kula nyama ni lazima uchague upande, either with us, or against us, maadamu wenye guvu ni mafisadi, mwenye nguvu mpishe, hao makamanda watajikuta kuliko kuriski loosing, wakijua hawawezi kuwashinda, watatumia formular ya 'if you can't beat them, join them' watajiunga nao na wote wakuwa kwenye tenga moja la samaki, na wote watakuwa ndio hao hao.
Kila nipatapo fursa mara moja moja, hupitia threads za zamani kuzifanyia historical reference ya tulikotoka, hapa tulipo, ili ku determine kule tuendako 2015!.

P.
 
Asalaam wana jamvi:
Nimekuwa nikijiuliza maswali kadhaa juu ya mwenendo na harakati za chama cha mapinduzi (ccm) juu ya hali ya kisiasa,kiuchumi na kijamii,maswali yangu yanajikita kwa kundi linalojihita ni watetea haki na kupinga ufisadi na ukandamizaji wa haki za binadamu,samweli sita,mwakyembe,selelii na james lembeli na wafuasi wao ktk ccm je, wako wapi ktk matukio yafuatayo:-
(1).Moja mbinu chafu za kisiasa zinazofanywa na chama cha mapinduzi(ccm),kama propaganda kidini dhidi ya upinzani,kujihusisha na utengenezaji wa vidio feki na matukio mengine ya kinyama dhidi ya upinzani wanasimama upande gani ktk haya mambo?kauli yao ni ipi?
(2).kuporomoka kwa uchumi na kuinuka kwa mfumuko wa bei huku serekali na ccm ikilidhia kupandishwa holela kwa gharama za umeme,maji na usafiri bila kuangalio ongezeko la kipato cha wakulima na wafanyakazi,ipi kauli yao ktk hili?
(3).Ufisadi ulifanywa na chama chao wanachokitumikia ktk swala JITEGEMEE COMPANY na wao wakijipambanunua kama wapinga ufisadi je,wanaridhika na ufisadi huo?upi msimamo wao?
(4).Dhuluma za ardhi zinazofanywa na ccm na serekali huko ngorongoro dhidi ya wamasai huko ngorongoro,je,wapinga ufisadi na unyanyasaji wa raia wakina samweli sita ili wanalisemea vp?
(5)Kuporoka kwa kasi na janga la kufeli watoto wetu je,hili nalo wamelisemea wapi?
Samweli sita amekuwa akijipambanua kuwa yeye ndie mgombea wa urais mwema na mzuri kuliko wote ndani ya ccm mwaka 2015,bila kujitokeza ktk majanga kama haya mazito yanawatesa watanzania,ili linanifanya kupata majibu juu ya ili kundi la kina sita na wafuasi wake kuwa ni wanafiki na wazandiki wakubwa ambao hawastahili kujihita wateta raia huku wakiishi ktk chama fisadi(ccm) na kundi la wala rushwa wachafu wa matendo kama mwigulu nchemba, kama sita ni mstaarabu kwanini hawakemei watu kama wakina nape,wasira na mwigulu juu ya mataendo ya kikatili na machafu dhidi ya upinzani na raia kama kibanda?ccm imeoza hakuna msafi wote wachafu,hakuna mtetezi wa haki za binadamu na haki za raia ndani ya ccm....ccm ni kichafu kimekufa na kimeoza Sitta na kundi lake aache mara moja kujipambanua kuwa yeye ni mwanaharakati na mpinga ufisadi huku wakiuchekea ufisadi unaofanywa na ccm na ufedhuli wa dhidi ya upinzani.....ccm sio chama cha kisiasa tena ni kundi la wezi tu.
 
Mzee 6 katulizwa, hao wengine watasema nini...yeye ndio kichwa cha kundi, kichwa kikikatwa basi mwili hauna kazi. Unafiki ni mbaya sana.
 
na alipotafuna pesa za CDA ni nini sio UFISADI? AU??? All of them are rotten Snakes trying to SHOW UP their NEW SKINS
 
Back
Top Bottom