Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,320
Tume inasema kuwa kwa utaratibu wa mwaka huu, kila kituo kitakuwa na wapiga kura wasiozidi 500! Ina maana kama kuna mtu anataka kuiba kura katika ngazi ya kituo, ataiba kura 500 tu katika kituo kimoja (kama ataweza kubadilisha zote). Ina maana pia kuwa kama ktu anataka kuchakachua matokeo kwa significant amount, lazima aratibu wizi wa matokeo katika vituo kadhaa. Lakini pia ina maana kuwa kama kunatakiwa kupelekwa karatasi feki kwenye vituo, itabidi kupelekwa kwenye vituo vingi, hali inayozidisha risk ya kugundulika.
Katika hili ndio maana naamini mafisadi wa kura wameshalifaham, na naamini wana mbinu mbadala ambazo zitaiba kura katika ngazi za juu zaidi ya kituo.
Tukijiimarisha katika kulinda kura zetu kuanzia ngazi ya kituo hadi huko juu, hebu tujiulize 'kwa hii breakdown ya vituo hadi kuwa si zaidi ya wapiga kura 500, tumeula au tumeliwa'?