Elections 2010 Wapiga kura 500 kila kituo. Twala, twaliwa??????

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Tume inasema kuwa kwa utaratibu wa mwaka huu, kila kituo kitakuwa na wapiga kura wasiozidi 500! Ina maana kama kuna mtu anataka kuiba kura katika ngazi ya kituo, ataiba kura 500 tu katika kituo kimoja (kama ataweza kubadilisha zote). Ina maana pia kuwa kama ktu anataka kuchakachua matokeo kwa significant amount, lazima aratibu wizi wa matokeo katika vituo kadhaa. Lakini pia ina maana kuwa kama kunatakiwa kupelekwa karatasi feki kwenye vituo, itabidi kupelekwa kwenye vituo vingi, hali inayozidisha risk ya kugundulika.

Katika hili ndio maana naamini mafisadi wa kura wameshalifaham, na naamini wana mbinu mbadala ambazo zitaiba kura katika ngazi za juu zaidi ya kituo.

Tukijiimarisha katika kulinda kura zetu kuanzia ngazi ya kituo hadi huko juu, hebu tujiulize 'kwa hii breakdown ya vituo hadi kuwa si zaidi ya wapiga kura 500, tumeula au tumeliwa'?
 
Vipo vituo vya kupigia kura vipo 52,000 waliojiandikisha wapo 19,000,000

Kila kituo kitakuwa na wastani wa wapiga kura 365 kama watajitokeza wote, wakiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu.
 
Tume inasema kuwa kwa utaratibu wa mwaka huu, kila kituo kitakuwa na wapiga kura wasiozidi 500! Ina maana kama kuna mtu anataka kuiba kura katika ngazi ya kituo, ataiba kura 500 tu katika kituo kimoja (kama ataweza kubadilisha zote). Ina maana pia kuwa kama ktu anataka kuchakachua matokeo kwa significant amount, lazima aratibu wizi wa matokeo katika vituo kadhaa. Lakini pia ina maana kuwa kama kunatakiwa kupelekwa karatasi feki kwenye vituo, itabidi kupelekwa kwenye vituo vingi, hali inayozidisha risk ya kugundulika.

Katika hili ndio maana naamini mafisadi wa kura wameshalifaham, na naamini wana mbinu mbadala ambazo zitaiba kura katika ngazi za juu zaidi ya kituo.

Tukijiimarisha katika kulinda kura zetu kuanzia ngazi ya kituo hadi huko juu, hebu tujiulize 'kwa hii breakdown ya vituo hadi kuwa si zaidi ya wapiga kura 500, tumeula au tumeliwa'?

Mkuu hili kwa taarifa yako tumeliwa na mbinu halali ya kuiba kura.Ebu fikiria siyo kila kituo kinawapiga kura 500 kama wakiwa pungufu hizo zilizozidi zitaenda wapi?
Tumeliwa vibaya mnoooooo
 
Nafiri kuna haja ya kuwapongeza NEC,kwa maamuzi mazuri waliyoyafanya!
 
Unamuona mwingine huyo?Yapi hayo ya kuwapongeza ikiwa mpaka sasa hakuna orodha iliyokwisha wekwa hadharani ya watu halali watakao pigia kituo husika.

Uzoefu nilionao katika suala hili ni kwamba huwa ikibaki siku kama tano majina yanatolewa kwahiyo kinachofanyika zile nyumba au kaya ambazo zina walakini wakumpigia kura Jk au mgombea wa CCM majina yao japo yanakuwa siyo yote hayaonekani na muda wa kufuatailia unakuwa umeisha hivyo unakata tamaa na hapo huwezi kupiga kura tena lakini ukienda kwenye kata ambayo hukujiandikisha unakuta jina lako lipo huko sasa hapo nani atakefaidika?

Mi nawapenda JF kwa kuwa wawazi mbona hizi mbinu hamzifanyii kazi na tunakuwa tunapotosha ukweli?Let us be serious japo siyo wote waliojiunga JF ni wanamapinduzi wengine nikupoteza muelekeo mada husika.Mi ningewapongeza NEC kama within these two weeks wawekee hiyo orodha ili mtu ajijue mapema.
 
Mkuu hili kwa taarifa yako tumeliwa na mbinu halali ya kuiba kura.Ebu fikiria siyo kila kituo kinawapiga kura 500 kama wakiwa pungufu hizo zilizozidi zitaenda wapi?
Tumeliwa vibaya mnoooooo

HOFU YANGU NI KWAMBA, MAWAZO YENU KILA SIKU NI KWAMBA KURA ZITAIBIWA!!!! SASA YA NINI KUSHIRIKI UCHAGUZI AMBAO MNAFAHAMU KWAMBA KURA ZITAIBIWA?! KWANINI CHADEMA WASISUSIE UCHAGUZI? I am sure 500 ni idadi ya juu kabisa ya wapiga kura wanaotakiwa kila kituo ili kufanya watu wamalize mapema na kurahisisha zoezi la kuhesabu kura lakini bado mnaona hizo nazo ni njama za kuiba kura!! Ama kweli wapwa mnatapatapa!!!
 
Mkuu hili kwa taarifa yako tumeliwa na mbinu halali ya kuiba kura.Ebu fikiria siyo kila kituo kinawapiga kura 500 kama wakiwa pungufu hizo zilizozidi zitaenda wapi?
Tumeliwa vibaya mnoooooo

NEC wamesema 'maximum'/ 'at most'/ 'ceiling' ni watu 500 na sio kila kituo ni lazima wawe 500!
 
Katika hili ndio maana naamini mafisadi wa kura wameshalifaham, na naamini wana mbinu mbadala ambazo zitaiba kura katika ngazi za juu zaidi ya kituo.

Wizi wa kura ni lazima ufanyike kituoni ukishindikana hapo basi huko mbeleni itakuwa ni vigumu mno. Vyama vyote vitakuwa na fomu za matokeo ya kura katika vituo vyote na vitayajumlisha na kujua jumla yake kwa kila jimbo sasa huko mbeleni utayachakachuaje.......Chunga kura kituo chako na hapo fisadi ujanja utakuwa umewishia.kabisa...............
 
Unamuona mwingine huyo?Yapi hayo ya kuwapongeza ikiwa mpaka sasa hakuna orodha iliyokwisha wekwa hadharani ya watu halali watakao pigia kituo husika.

Uzoefu nilionao katika suala hili ni kwamba huwa ikibaki siku kama tano majina yanatolewa kwahiyo kinachofanyika zile nyumba au kaya ambazo zina walakini wakumpigia kura Jk au mgombea wa CCM majina yao japo yanakuwa siyo yote hayaonekani na muda wa kufuatailia unakuwa umeisha hivyo unakata tamaa na hapo huwezi kupiga kura tena lakini ukienda kwenye kata ambayo hukujiandikisha unakuta jina lako lipo huko sasa hapo nani atakefaidika?

Mi nawapenda JF kwa kuwa wawazi mbona hizi mbinu hamzifanyii kazi na tunakuwa tunapotosha ukweli?Let us be serious japo siyo wote waliojiunga JF ni wanamapinduzi wengine nikupoteza muelekeo mada husika.Mi ningewapongeza NEC kama within these two weeks wawekee hiyo orodha ili mtu ajijue mapema.
Majina yatabandikwa Jumamosi hivyo kutakuwa na muda wa siku zaidi ya saba kufatilia jina lako...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom