Apollo
JF-Expert Member
- May 26, 2011
- 4,920
- 3,221

Imani ni kitu cha kusadikika. Ni kitu kinachoelea akilini tu. Na kitu ambacho hakithibitiki kwa kutumia kanuni za kisayansi au njia na michakato mingine ya kutafutia ukweli. Imani haishikiki, haionekani kwa macho, hainusiki kwa pua, na haisikiki na masikio, na wala haisikiki kwa kuigusa.

Sasa yeye aliweka wazi tokea mwanzo kuwa pasipo na imani hata ukitumia dawa yake basi haitakuwa na nguvu ya kufanya kazi. Kwa maneno mengine, dawa yake hiyo ni ya kipoza-uongo (placebo-effect). Placebos hutumika hata kwenye hospitali za kawaida zinazotumia zana na mbinu za kisayansi katika kutibia. Madaktari hufikia uamuzi wa kumpa mtu kipoza-uongo pindi wagunduapo kuwa huyo mgonjwa husika anasumbuliwa na maruweruwe (matizo yaliyo imaginary).

Kila dawa huwa zina masharti yake. Kuna dawa ambazo unatakiwa kuzimeza na chakula na zingine ambazo haijalishi, unaweza kuzimeza na chakula au pasipo na chakula. Na dawa ya babu pia masharti au sharti lake kuu lilikuwa ni imani. Pasipo na imani ni vigumu kwa hiyo dawa yake kufanya kazi. Hili aliliweka wazi kabisa. Serikali nayo ilifanyia uchunguzi hicho "kikombe" chake na kuona hakina madhara yoyote.

Leo hii mnataka Babu aburuzwe mahakamani kwa misingi ipi? Kwa sababu tu kuna watu wenye magonjwa sugu ambao hawakupona baada ya kupata kikombe? Mbona waliambiwa pamoja na kikombe cha babu wasiache kutumia dawa zao. Kuna aliyedhurika baada ya kupata kikombe? Kuna aliyekufa baada ya kupata kikombe? Je, mnaweza kuthibitisha pasipo wingu la shaka kuwa ni kikombe cha babu ndicho kilichopelekea kudhurika au kupoteza maisha kwa mtu au watu kama wapo iliyowatokea hivyo?

Kwa kweli hapo hamna kesi kabisa. Lakini kwa vile wana haki ya kwenda mahakamani, acha tu waende. Kwa yote ninayoyajua kuhusu Babu nakuhakikishia kuwa ataibuka kidedea labda kuwepo na mengine ambayo hayajulikani.

kweli kabisa.. Anaweza akajitetea hawakupona kwa sababu hawakuwa na imani.