Dawa ya Ukimwi ipo imefichwa stoo

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
949
2,865
Tukiwa katikati ya maambukizi ya ugonjwa wa "red eyes" ambayo inaambukizwa na kirusi nikaukumbuka ugonjwa wa Ukimwi ambao nao inaambukizwa na kirusi.

Kama ilivyo kwa Ukimwi,patient zero aliitoa wapi hii "red eyes" ikiwa red eyes inasababishwa na mvua zinazonyesha na kusababisha unyevunyevu angani,je patient zero wa Ukimwi aliutoa wapi ugonjwa wa Ukimwi!?

Tufikiri kwa pamoja,kirusi cha Ukimwi kina RNA na mwili wa binadamu una RNA na DNA,inakuwaje kirusi cha Ukimwi chenye RNA kijipenyeze kwenye mwili wa binadamu kikajiweke kwenye DNA ya binadamu na kuuteka mfumo mzima wa DNA ya binadamu, kwa kuudanganya mwili wa binadamu kuwa RNA ya kirusi cha Ukimwi ndio DNA ya binadamu!? Je hii si akili ya binadamu kutengeneza kirusi cha RNA ambacho kitakwenda kufanya kazi ya DNA kwenye mwili wa binadamu!?

Utakubaliana nami,siku hizi hakuna vifo vingi vya Ukimwi,kwa nini!? Kwa sababu dawa ya Ukimwi imebadilishwa na dawa ya sasa haina madhara makubwa kwa binadamu,hadi miaka ya 2000 dawa ya Ukimwi ilikuwa TLE,hii E ilikuwa na madhara mengi hasa ya kisaikilojia,mgonjwa wa Ukimwi akinywa akilala anapata "nightmare" anajiona anakufa anaanza kupata tatizo la kisaikolojia na anaacha kunywa dawa na mwisho anakonda na tunamzika akiwa na kilo sita,

Hivi sasa dawa ya Ukimwi ni TLD, wametoa E wameweka D ,hii D haina madhara ya kisaikolojia kama kuota kufa,kwa namna hii wagonjwa wa Ukimwi wameweza kutumia dawa kama inavyotakiwa na wengi wakienda kupima wanakutwa hawana Ukimwi, kwa sababu wanatumia dawa kikamilifu kama inavyotakiwa,

Nimalizie kwa kusema kwamba,aliyetengeneza kirusi cha Ukimwi anayo dawa ya kuponya Ukimwi kaiweka stoo, anasubiri muda wa kuitoa tuombe huyo mtu asife. Hayati Rais Magufuli aliwahi kuwachallenge Wazungu,akihutubia kutoka kijijini kwake Chato,alisema inakuwaje dawa ya Ukimwi inafanyiwa utafiti toka mwaka 1980 halafu dawa ya COVID inafanyiwa utafiti kwa miezi tisa na kuletwa Afrika!? Akili kichwani mwenu waafrika wenzangu.
 
Umechambua kitaalam hasa.

Baadhi ya watu wanasema kuwa ukimwa, zaidi ni ugonjwa kisaikolojia kuliko kuwa ugonjwa wa kukosa kinga. Hiyo nightmare ilikiwa ni ugonjwa mbaya zaidi kuliko kirusi chenyewe.

Na ndiyo maana hata wakati ule wa mwanzo ambapo ukimwi ilikuwa ni wimbo wa kila mahali, watu wenye maambukizi waliokuwa wanaishi nao kwa muda mrefu, walikuwa ni wale wasiojali.

Wale ambao walijali sana na kujawa na hofu wakati wote, wengi wao waliondoka mapema sana tangu walipoambiwa kuwa wamethirika.
 
IMG_0991.jpg

Hizi kitu nazo wanasema zinamchango wake. Ingawa nawasiwasi na madhara yake.
 
Back
Top Bottom