Wapanga kumburuza Babu wa loliondo kortini

Imani yao ndio iliyotakiwa kuwaponya...imani yao ikakataa kuwaponya.

Imani yao ndio inayotakiwa kufikisha kortini..kama kweli wana nia.Wamwache babu wa watu maana yeye hakusema ni daktari wala mtenda miujiza.Kama walichagua kutokumuelewa aliposema imani ya wanywaji ndo itakayowapona ni makosa yao wenyewe!
................... hivi unatakiwa kuwa na Imani juu ya Dawa au juu ya Mungu ? ..................... Babu aliongea na Mungu, sasa amemuuliza kuhusu huu utata ?
 
Hii imenikumbusha alichosema TB Joshua! Kwamba wachungaji wengi (healing ministries) wanawaombea watu, wasipopona wanajitetea kuwa imani yako haba! Imagine mtu aliyeuza shamba akapata nauli kusafiiri kwa shida unamwambia imani yake haba! Kipimo cha imani ni nini? <br />
<br />
Babu was either smart au huyo mungu wake alimpa tricky hiyo, au kulikuwa na brain nyingine behind Babu yeye akatumika tu!
<br />
<br />
Kaunga upo extremly right!! Kisitumike kigezo cha imani kabisa.. Hapo kuna kamchezo kamefanyika and now it is costing alot of people's lives.. Inakuaje hakuna hata shuhuda mmoja aliyepona hilo gonjwa...?!
 
kila aliyekunywa kikombe na hajapona anatakiwa kunipa mimi sh 1000 kuna kitu mungu alisahau kumpa babu amenipa mimi kwa maelezo zaidi nipm
usidharau,nimeoteshwa.
 
mwacheni babu wa watu,kwanza source yenyewe magazeti ya umbea,njooni mnipime mimi nilienda na niko fit,kama huna imani huwezi kupona iwe kwa mama au kakobe imani kwanza,kamshitaki uone jinsi mashahidi tutajitokeza
 
Nasikia babu ni mwenzetu humu janvini- naomba ani-PM ili akishitakiwa nimtetee bure, hii ni kesi ya kujizolea umaarufu.
 
Fact is "mungu" wa babu alikuwa ni wa magumashi, fake!
Afu hapa ndo mahali huyu babu alinikeraga sana.. Eti anaongea na Mungu, khaaa, mungu yupi sasa ambaye ameshindwa kumtibia hata mgonjwa mmoja tu?.. Aende akatubu upesi manake alitumia vibaya jina la mungu...
 
upumbavu mtupu, kwani walimlipa kiasi gani huyo babu? kila mtu akachukue pesa alizomlipa!! unaendesha kesi kwa sababu ya sh 500. Huu ni ujinga na upofu wa kielimu, kiakili na kiroho.i
 
Mimi toka mwanzo sikuamini hii dawa my husband did.kuna watu aliwapeleka mpaka leo sijawaona kupona.wanataka wamshitaki kwani aliwafunga kamba ili waende?wakubali yaishe UKIMWI HAUNA DAWA ILA UNA KINGA.
 
Mbona kuna wagonjwa wengine wengi tu actually nilisoma kwenye gazeti la mwanchi sikumbuki la tarehe gani waliandika kuwa 70% ya wagonjwa waliokunywa kiKombe cha baBu wamepona magonjwa yaliyokuwa yanawasumbua.

Hawa watu ilibidi waelewe tu kuwa " Kwa Imani utaokolewa", wanasema eti kutumia pesa nyingi kutumia dawa ambayo haitibu ni utapeli, mbona watu wanatumia dawa nyingi tu za hospital kwa gharama kubwa na bado hawaponi, kwa nini hawasemi kuwa ni utapeli. Kwa nini basi wasiwashtaki na madaktari ambo huwa wanatibu watu bila kupona.
 
Hivi babu alikuwa anawasajili (kuwaandika majina) au kuwapa vyeti watu aliokuwa anawapa kikombe?
 
Hivi wanaotaka kumshtaki babu wa watu, ni kesi ya aina gani watafungua mahakamani? Watamdai babu arudishe 500 yao? Kuwalazimisha kusafiri umbali kumfuata sumange?
Ni vema wakatambua kwamba dawa ya babu ilikuwa ni suala la hiari ya mgojwa kwenda ama kutokwenda. Hivyo ni vema walioenda na dhamira zao zinawasuta wakafanya jitihada za kupatana na kweli wanayoifahamu wakaisigina kwa makusudi. Wale walioenda na dhamira zao haziwasuti basi waendelee na ibaada kwa Mungu wa kweli huku wakishukuru kwa kila jambo. Kwa habari ya kesi kuna asilimia 99.9 ya babu kushinda kesi, na wao watakachoambulia ni fedheha na kujiharibu kisaikolojia. Safari ya maisha ya mwanadamu haijawahi kuwa tambarare na wala haitakaa iwe hata tutakapovuka ngambo ile ya pili.
.
 
Utamwambiaje Mtu eti hakupona kwa kuwa hakuwa na imani????? Kama alitoka mwenyewe nyumbani kwake akagharamia usafiri, chakula na malazi mpaka akafika kwa 'Babu' na akajipanga foleni siku tatu ndipo akapata kikombe kisha maradhi ndiyo yakaongeza kasi halafu umwambie 'hana imani ndio maana hakupona'. Jamani tuachane na hizo imani mbofu mbofu.
 
Suala la babu halihusiani na imani bali lilikuwa la kisanii toka mwanzo! We kept on insisting this time and time again lakini watu walikuwa vipofu na hawakuwa na masikio!

Kuna tofauti kubwa kati ya kuombewa ili upone na Mtumishi wa Mungu ambako neno la Mungu linasema inahitajika imani ili uweze kupkea huo muujiza na kitendo cha kupewa kikombe bila kuombewa wala nini!

kikubwa kuliko vyote wakati Mtumishi wa mungu note the use of word Mungu & mungu,alipokuwa akitoa kikombe je? Alikuwa akiwahubiria wagonjwa habari njema ili waokoke? Au nia yake ilikuwa tu kuponya miili yao kutoka kwenye magonjwa? je,si vizuri sana kwa Mungu watu kuponywa roho zao na si mwili maana kinachorudi kwa baba ni roho na si mwili.

Mungu anahitaji roho zetu zirudi kwake na si miili yetu! Remember man is a spirit,he has a soul and he lives in the body! Mungu wa Ibrahim,Isaka na Yakobo anataka roho zetu zisipotee.

Asante sana kwa ufafanuzi mzuri. Watu tulisema tokea mwanzo kuwa babu sio mtumishi wa Mungu wala Mungu hajasema naye bali alikuwa anafanya ushirikina tu. Uponyaji wowote wa Mungu lazima uambatane na kuwafanya watu wamgeukia Mungu wao, waachane na dhambi na kuokoka, full stop
 
Back
Top Bottom