Wanyama 130 wakiwemo twiga watoroshwa KIA kwenda Qatar

Hivi wew ni muislamu safi kwel unaweza upotosha umma kwa maslahi yako binafsi embu tuambie hiyo kesi ilitolewa hukumu wapi

Kumbuka: hakuna Muislam safi wala chafu. Muislam ni Muislam.

Naam, hiyo kesi ilishatolewa hukumu. Labda ulikuwa usingizini.
 
NOVEMBA 26, 2010, saa saba usiku, wakati idadi kubwa ya Watanzania wakiwa usingizini, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kulikuwa na pilikapilika kubwa ya kupakia mizigo kwenye ndege ya jeshi la anga la Qatar (Qatar Emir Air Force).

Mizigo iliyokuwa inapakiwa usiku huo mkubwa katika ndege hiyo haikuwa ya kawaida. Wahudumu walikuwa wanapakia wanyamapori hai 130 wa aina 14 tofauti na shehena kubwa ya nyamapori iliyokaushwa, mizigo hiyo yote ni inayotambuliwa kuwa kati ya rasilimali muhimu za Taifa.

Kwa mujibu wa wafanyakazi wa uwanja huo na raia wema kadhaa, wanyama hao hai 130 pamoja na shehena ya nyama zilizokaushwa vilikuwa vinatoroshwa kwenda Doha, Qatar.

Kwa mujibu wa sheria za Tanzania, mizigo hiyo ilikuwa inaondoka nchini kinyume cha sheria kwa kuwa haikuwa na kibali wala nyaraka sahihi za kiserikali na walioshiriki katika kuratibu na hatimaye kusafirisha mizigo hiyo nao walifanya makosa ya kuhujumu Taifa.

Kati ya wanyamapori hai 130 wakiwa wa aina 14 tofauti, walikuwamo twiga wanne. Twiga hutambuliwa kama alama ya Taifa, sheria za Tanzania zinaharamisha mnyama huyo mpole kuuawa au kusafirishwa kibiashara nje ya nchi.

Shehena ya viroba vya nyamapori zilizokaushwa inaelezwa kuwa ni ya wanyama wengi waliouawa “kijangili” na mtandao wa watu wanaoendesha biashara haramu ya nyamapori.

Ndege hiyo ya Jeshi la Qatar iliwasili KIA Novemba 24, mwanzo ikionekana kama ndege iliyokuwa katika safari za kawaida hadi Novemba 26 usiku wafanyakazi uwanjani hapo waliposhuhudia ikipakia mizigo wakiwamo wanyama hai.

soma zaidi hapa.. Ufisadi Maliasili

Unaweza ukalia jamani mnazidi kututia hasira plzzz !!!
 
Dah toka 2010 ndio unatuletea Leo hiyo topic kina tind lissu hawakuisikia nn ,ww uliye leta maada ni mnafikiiii sn unaleta maada mfuuuu .
 
novemba 24 mwaka jana ndege kubwa kijeshi ya qatar inayojulikana kama emir air force ilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa kia majira ya mchana.ndege hiyo ilikaa uwanjani hapo hadi novemba 26 usiku ambapo ilipakia mzigo wanyamapori hao 130 (rasilimali mhumi kwa taifa la tanzania) pamoja na shehena ya nyamapori iliyokaushwa na kuondoka nayo na wanyama hao walichukuliwa bila kibali wala kulipiwa ushuru.

Kinara mkuu wa uporaji huo ni raia wa pakistan anayeishi eneo la baraa mjini arusha akisaidana na mwanamke moja mkenya ambaye anafanya kazi katika kampuni moja ya uwakala wa ndege wakishirikiana na watanzania wengine wanne ambao ni watumishi wa serikali na uwanja wa kia.polisi aliyekuwepo uwanjani hapo pc sixbert namba d 8713 alijaribu kuhoji vibali vya wanyama hao lakini aliambulia matusi kutoka kwa watumishi wa serikali waliokuwa wanasimamia utoroshaji huo.baadaye askari huyo alitoa taarifa kwa bosui wake mkuu wa kituo cha polisi kia anayeitwa salmin na kesho yake upelelezi ulianza kuhusu tukio hilo.

Upelelezi huo ulifanywa na kikosi maalumu cha polisi kutoka makao makuu lakini hadi sasa miezi mitano baadaye hakuna hatua za maana zilizofikiwa na mamlaka zinahusika zimekuwa kimya ingawa polisi walipendekeza watuhimiwa hao wakamatwe na kufikishwa mahakamani.

My take:iliwachukua maharamia hao siku mbili tu kutorosha wanyama 130 lakini polisi wetu wameshindwa kuchukua hatua kwa miezi mitano.wanyamapori ndiyo rasilimali aliyotupatia mwenyezi mungu sisi watanzania na kwa mtindo huu si wataisha?dhahabu,tanzanite,magogo,samaki????????


Usiulize source plz hiyo ni habari ya ukweli
enzi za mwalimu huo uwanja ungefungwa na hao watuhumiwa wote wangefurushwa within twenty four (24) hours. Lakn ufisadi unawakumbatia manyigu hawa
 
Kumbe kinana katibu mkuu wa CCM wa sasa ndiye mhusika wa kutoroshwa wanyama pori? Inasadikika hata pembe za ndovu ni yeye
 
Back
Top Bottom