Ndege ya Qatar C17 iliyosafirisha twiga ilipata kibali

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,899
images
images
Ndege kubwa ya jeshi la Qatar ambayo inasemekana kutumika kutorosha wanyamapori 152 wakiwa hai, ilipata vibali vyote vya kutumia anga la Tanzania.

Pia ndege hiyo, aina ya C17 yenye namba za usajili MAA/MAB, iliomba kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa shughuli za kidiplomasia.

Hayo yalielezwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini hapa na shahidi wa 26 upande wa mashtaka, Kanali Nathaniel Paulo Msemwa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kitengo cha Operesheni na Mafunzo.

Miongoni mwa wanyamapori waliobebwa na ndege hiyo ni twiga wanne wenye thamani ya Sh170.5 milioni waliosafirishwa kwenda Arabuni.

Akitoa ushahidi wake kwa kuongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Evetha Mushi, Kanali Msemwa alisema Novemba 11, 2010 alipokea nyaraka tatu zinazohusu vibali vya ndege hiyo kutumia anga la Tanzania.

Moja ya nyaraka hizo ni maombi yaliyopokelewa kwa fax na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kutoka ubalozi wa Qatar uliopo Sanaa, Mashariki ya Kati.

"Hiyo barua iliyokuwa na neno urgent (haraka) ilikuwa inaomba kibali kwa ajili ya ndege hiyo na tayari ilikuwa imeridhiwa na kamishina wa Wizara ya Mambo ya Nje," alisema Kanali Msemwa.

Kibali hicho chenye namba MMJ/2145/0018/Nov10 kilichopokelewa mahakamani kama kielelezo kinaonyesha ndege hiyo ingetua KIA Novemba 24, 2010 na kuondoka kuelekea Qatar Novemba 26, mwaka huo. Kanali Msemwa alisema vibali hivyo vilipelekwa kwao (JWTZ) kwa sababu ya usalama wa nchi na usalama wa ndege yenyewe kwa vile ilikuwa ni ya kijeshi, ingawa ilikuwa katika kazi ya kidiplomasia.

Alieleza kwamba wakati ndege hiyo ikiwa KIA, ilikuwa chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na jeshi liliwajibika tu wakati ndege hiyo ikiwa katika anga la Tanzania.

Shahidi wa 27, Inspekta Filicheshi Mlabule kutoka Idara ya Upelezi ya Polisi, alisema kabla ya upelelezi, mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Paul Sarakikiya alisema upelelezi wa awali ulionyesha kuwa wanyama hao walisafirishwa bila kibali.

Chanzo: Mwananchi
 
Je na kibali cha Mamlaka ya Usafiri wa Anga ambao wanasimamia Usafiri huo kilikuwepo? Tunajua kuwa hakuna ndege iwe ya kiraia, kidiplomasia au kijeshi inayotakiwa katika anga la nchi yoyote bila mamlaka inayohusika na Usafiri wa anga kuwa na taarifa.
 
Taarifa inasema ndege ni ya Qatar, wakati picha inaonesha dege limeandikwa UAE Air Force, kumaanisha kuwa hiyo ni ndege ya United Arab Emirates, mbona sielewi hapa?
 
Hivi U.A.E ndio Qatar? Hebu someni hiyo ndege. Mji mkuu wa Qatar ni Doha UAE Dubai. Mbona mkorogo?

Pili. Nadhani ndege kupewa kibali cha kutua sio tatizo, tatizo ni je walisema wanakuja kuchukua wanyama? Kama waliombea kibali sababu A wa kaja kufanya B mwenye kutoa kibali hana hatia.
 
images
images
Ndege kubwa ya jeshi la Qatar ambayo inasemekana kutumika kutorosha wanyamapori 152 wakiwa hai, ilipata vibali vyote vya kutumia anga la Tanzania.

Pia ndege hiyo, aina ya C17 yenye namba za usajili MAA/MAB, iliomba kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa shughuli za kidiplomasia.

Hayo yalielezwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini hapa na shahidi wa 26 upande wa mashtaka, Kanali Nathaniel Paulo Msemwa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kitengo cha Operesheni na Mafunzo.

Miongoni mwa wanyamapori waliobebwa na ndege hiyo ni twiga wanne wenye thamani ya Sh170.5 milioni waliosafirishwa kwenda Arabuni.

Akitoa ushahidi wake kwa kuongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Evetha Mushi, Kanali Msemwa alisema Novemba 11, 2010 alipokea nyaraka tatu zinazohusu vibali vya ndege hiyo kutumia anga la Tanzania.

Moja ya nyaraka hizo ni maombi yaliyopokelewa kwa fax na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kutoka ubalozi wa Qatar uliopo Sanaa, Mashariki ya Kati.

“Hiyo barua iliyokuwa na neno urgent (haraka) ilikuwa inaomba kibali kwa ajili ya ndege hiyo na tayari ilikuwa imeridhiwa na kamishina wa Wizara ya Mambo ya Nje,” alisema Kanali Msemwa.

Kibali hicho chenye namba MMJ/2145/0018/Nov10 kilichopokelewa mahakamani kama kielelezo kinaonyesha ndege hiyo ingetua KIA Novemba 24, 2010 na kuondoka kuelekea Qatar Novemba 26, mwaka huo. Kanali Msemwa alisema vibali hivyo vilipelekwa kwao (JWTZ) kwa sababu ya usalama wa nchi na usalama wa ndege yenyewe kwa vile ilikuwa ni ya kijeshi, ingawa ilikuwa katika kazi ya kidiplomasia.

Alieleza kwamba wakati ndege hiyo ikiwa KIA, ilikuwa chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na jeshi liliwajibika tu wakati ndege hiyo ikiwa katika anga la Tanzania.

Shahidi wa 27, Inspekta Filicheshi Mlabule kutoka Idara ya Upelezi ya Polisi, alisema kabla ya upelelezi, mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Paul Sarakikiya alisema upelelezi wa awali ulionyesha kuwa wanyama hao walisafirishwa bila kibali.

Chanzo: Mwananchi

Hilo wala si la kushangaa kwa sababu sio rahisi dege kubwa kiasi hicho liingie nchini bila kujulikana habari zake
 
kibali cha kutua tz au kutulia tz kina mahusiano gani na wanyama wetu???,waturudishie wanyama,no diplomac there!!!,wanyama warudi,wahusika waadhibiwe pia..hata kama kuna mkno wa jeshi!!!tumechoka raslimali za nchi kugeuzwa mali ya watu binafsi..INAUMA SANA KUONA WATU WANATUFANYA WATZ WAJINGA..WE ARE NOT STUPID AISEE...
 
Je na kibali cha Mamlaka ya Usafiri wa Anga ambao wanasimamia Usafiri huo kilikuwepo? Tunajua kuwa hakuna ndege iwe ya kiraia, kidiplomasia au kijeshi inayotakiwa katika anga la nchi yoyote bila mamlaka inayohusika na Usafiri wa anga kuwa na taarifa.

Huyo amejibu kwa niaba ya jeshi na si mamlaka ya usafiri wa anga. Rudia kusoma "jeshi liliwajibika tu wakati ndege hiyo ikiwa katika anga la Tanzania.".

Pengine ni ktk process tu ya kujua ukweli lakini kwangu mimi ndege kuwa ktk anga la Tanzania na kupewa vibali kwa shughuli ya kidiplomasia siyo issue kubwa... Tunataka watuambia Categorically hao wanyama waliwindwa lini?kwa vibali vipi? wakahifadhiwa wapi? walisafrishwaje? vibali vyote hivyo viliidhinishwa na nani? Ujangili siku hizi ni Diplomasia? Pale KIA/JRO kuna vyombo vyote vya Usalama; Walichukua hatua gani kuzuia ndege kuondoka? kama walipewa vibali vya kuruhusu hiyo ndege kuchukua mali hai wetu, vibali hivyo vilisainiwa na nani? hao watu wako wapi? pato kutokana na hao wanyama zimeingizwa kwenye mfuko upi serikalini?.... Kama CCM walikuwa wanatafuta fedha za Uchaguzi kama kawaida yao basi si vibaya Watanzania wakajua Ukweli ....
 
Vigogo C.C.M Na Watoto Wao wako SAHIHI mwisho wa siku wanatimulia HUKO.MASIKINI WENZANGU WA KANGA NA KOFIA NDO MAZUZU !
 
Taarifa inasema ndege ni ya Qatar, wakati picha inaonesha dege limeandikwa UAE Air Force, kumaanisha kuwa hiyo ni ndege ya United Arab Emirates, mbona sielewi hapa?

Kamuone daktari wa macho au umejipa upofu wa lumumba
 
Huyo amejibu kwa niaba ya jeshi na si mamlaka ya usafiri wa anga. Rudia kusoma "jeshi liliwajibika tu wakati ndege hiyo ikiwa katika anga la Tanzania.".

Wanyama na jeshi wapi na wapi? Jeshi halona mkono hapo. Wanaohusika wachukuliwe hatua
 
Kwa wataalamu wa mambo ya Usalama....hivi majasusi wetu walishindwa kudetect kitu na kufatilia uhalali wa wanyama hai kusafirishwa tena na ndege ya kijeshi? Hata kama system iliyopo inawabinya kuchukua hatua walishindwa hata kuvujisha kwa public ili kuvuruga Uhaini wa kiwango hiki? Kama hawakuwa na habari basi nchi yetu haipo salama .....just matter of time ku prove hatuko salama .....wanasiasa wanawaza namna watavyobaki madarakani tu......
 
Wanyama na jeshi wapi na wapi? Jeshi halona mkono hapo. Wanaohusika wachukuliwe hatua

Umesoma kuwa huyo ni shahidi kaitwa mahakamani, ili aeleze kwanini ndege ya Kijeshi ya nchi nyingine imeingia na kutuwa Tanzania, jeshi lilikuwa wapi? ndiyo anatoa ushahidi wake.

Hivi hizi shule huwa mnaenda kujifunza ujinga?
 
Huyo amejibu kwa niaba ya jeshi na si mamlaka ya usafiri wa anga. Rudia kusoma "jeshi liliwajibika tu wakati ndege hiyo ikiwa katika anga la Tanzania.".

Ninalijua hilo. Lakini kumbuka pia Mamlaka inawajibika pale ndege hiyo inapokuwa katika anga la nchi husika. Ndiyo maana kibali cha jeshi huwa siyo cha mwisho kuruhusu ndege kuingia katika anga la nchi yoyote bali mamlaka inayohusika na Usafiri wa anaga ndiyo mhusika mkuu. Pale ambapo ndege hizo zinatakiwa kutokuwa too ya kupita katika anga, ndege za jeshi na kidiplomasia zinasameahewa na kwa jinsi hiyo Wizara ya mabo ya nje au/na jeshi utoa taarifa kwa mamlaka hiyo kutoa kibali bila tozo.
 
Sasa wewe unataka mtu wa Jeshi awajibie Mamlaka ya Anga? si ungoje ushahidi wa mtu wa Mamlaka ya anga usikie atasema nini?

Hivi hizi shule huwa mnaenda kujifunza ujinga?
 
Duh!! hii ni advanced poaching, hadi ndege inatumika sasa.... kadoda11 Geza Ulole Bulldog

Wewe nyang'au hebu kwanza katatue matatizo ya poaching ya roho za watu huko Mpokoteni:

[h=1]On the front line of Kenya's war on poaching[/h] [h=2]Dozens of park rangers are killed by poachers each year. One of Kenya's most experienced reveals his battle scars and talks about the increasingly tough task of protecting Africa's wildlife[/h]
kenya-poaching_2999255b.jpg
"John Mutiso has put poachers behind bars, but six months later – due to what he calls 'dodgy dealings' – the same men are back on their conservancy hunting elephants" Photo: GETTY

Source: On the front line of Kenya's war on poaching - Telegraph

Usifikiri hilo ni tatizo la Tanzania tu, hata Kenya kuna matatizo hayo.
 
Back
Top Bottom