Simulizi: Msaliti asakwe

kapingili

Senior Member
Jul 4, 2012
155
192
MSALITI ASAKWE - 1
IMEANDIKWA NA : PATRICK J. MASSAWE
*******
Simulizi : Msaliti Asakwe
Sehemu Ya Kwanza (1)

MAJIRA ya saa nane za mchana, walionekana vijana watatu, wakiwa wamekaa upande wa baa, ndani ya hoteli maarufu ya The Tropic Inn. Ni hoteli iliyojengwa juu ya kilima kidogo, kando ya barabara kuu, iendayo jijini Kigali na kwingineko.
Hali ya hewa ilikuwa ni ya baridi, ilifuatiwa na manyunyu pamoja na ukungu mzito mweupe, uliofunika milima yote iliyozunguka eneo maarufu la Nyakarambi, Mkoa wa Kibungo, ulioko eneo la mpakani, kati ya nchi ya Rwanda na Tanzania .

Muda wote vijana wale walikuwa wamekaa katika meza ya pembeni, wakila na kunywa, na pia kujadiliana mambo muhimu kwa sauti ya chini. Meza iliyokuwa mbele yao ilikuwa imesheheni vinywaji vya kila aina, bia pamoja pombe kali aina ya wiski, ili kuiondoa ile baridi iliyokuwa ikiwaingia barabara maungono mwao ingawa walikuwa wamevalia makoti mazito.

Baridi ilikuwa ni kitu cha kawaida katika maeneo yale yaliyokuwa yamezungukwa na milima nyingi. Ingawa wote walikuwa bado vijana, hawakuwa na haja ya kukaa na wanawake, ambao walikuwa wamejazana ndani ya baa ile wakiwa kama kivutio kikubwa kwa wateja! Ukweli ni kwamba walikuwa wamefika pale kupanga mikakati yao muhimu sana , ambayo hawakutaka mtu yeyote aisikie zaidi ya wao kama walivyo. Na ndiyo maana wakajichimbia kwenye kona ndani ya ukumbi ule wa baa.

Vijana wale walijulikana kwa majina ya Roman, Obale na Laurento, ambao kitaaluma walikuwa ni wanajeshi waliokuwa wamepitia mafunzo maalum ya kijeshi na kufuzu vizuri. Ni mafunzo ambayo yalikuwa yakifanyika katika misitu mikubwa iliofungamana ya Kibungo.

Vijana wote watatu, walikuwa na maumbile makubwa ya kimazoezi, kutokana na ile suluba ya kuishi msituni kwa muda mrefu. Pia, hawakutofautiana sana kiumri, kwani walikuwa na umri kati ya miaka ishirini na mitano, au zaidi kidogo. Hakika walikuwa vijana wabichi bado, ambapo walikuwa wamefika pale Nyakarambi kwa usafiri wa gari aina ya Toyota Land Cruiser, wakitokea katika makazi yao ya siri yaliyoko katika msitu wa Kibungo, palipokuwa na kambi maalum ya kijeshi iliyokuwa inamilikiwa na waasi.

Ni kundi la waasi lililokuwa linaongozwa na Ofisa Mwanajeshi, Kanali Fabio Rushengo, ambaye ni mhusika mkuu na mmoja wa askari waliohusika na mauaji ya kimbari, yaliyotokea nchini Rwanda mnamo mwaka 1994, ambayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya laki nane! Ni mauaji ambayo yaliutikisa ulimwengu mzima kwa jinsi walivyouawa watu wengi kwa mara moja!

Vijana, Roman, Teobale na Laurent walikuwa na sababu maalum iliyowafanya wafike pale Nyakarambi, ambayo ni juu ya kupanga mpango wa kumtoroka kiongozi wao, Kanali Fabio Rushengo, baada ya kuchoshwa na maisha ya kukaa msituni kama nyani, wakiwa na mawazo ya kuipindua serikali halali iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia.
Kwa upande wao waliona ni sawa na ndoto ya mwendawazimu anayeota asichokifahamu! Basi, ndipo walipoamua kukutana katika mji ule mdogo wa Nyakarambi, ulioko umbali wa kilometa 30 kutoka mpakani Rusumo, upande wa pili wa nchi ya Rwanda .

Sehemu ile palikuwa na kituo kikubwa, ambacho hapo awali kilitumika kupokea wakimbizi waliokuwa wanarudi nchini kwao kwa hiari yao mwenyewe, baada ya kuridhishwa na hali ya usalama wa maisha yao . Ni Kituo kilichosimamiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) wakati ule kwa upande wa nchi ya Rwanda .

Vilevile mji ule ulikuwa na starehe za kila aina, hasa ukizingatia palikuwa na mkusanyiko wa watu wengi, wakiwa ni wafanyabiashara na madereva wa magari makubwa yanayosafirisha mizigo kati ya nchi za Tanzania , Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Kongo.

Kijana Roman ndiye aliyekuwa kiongozi, alivuta pumzi ndefu na kuzishusha. Halafu akawaangalia Teobale na Laurent kwa zamu, jinsi walivyokuwa wanakunywa bia aina ya Primus ndani ya bilauri kubwa, ikiwa kama vile alikuwa anawakagua, nao, Teobale na Laurent wakawa wanamwangalia kwa kuashiria kwamba walimsubiri aanze kuzungumzia kilichowafanya wakutane muda ule.

Kiutaratibu wao ni kwamba walikuwa wanamheshimu sana kiasi ambacho walimpendekeza awe kiongozi wao kwa sababu alikuwa ni jasiri asiye na woga!

“Natumaini wote tu wazima…” Roman akawaambia kwa sauti ndogo.
“Sote tu wazima, ndiyo maana tumekutana hapa,” Teobale akasema kwa sauti ndogo.
“Na nyote mnaelewa kilichotuleta hapa Nyakarambi, na kukaa kikao hiki,” Roman akaendelea kusema
“Tunaelewa kilichotuleta,” akaongeza Laurent huku akimwangalia Roman.
“Vizuri kama mmenielewa,” Roman akasema na kuongeza. “Hapa tumekuja kuongelea suala la kiongozi wetu Kanali Fabio Rushengo!”

“Ndiyo. Ni suala hilo lililotuleta hapa!” Teobale alijibu kwa niaba yao wawili na Laurent.
“Basi, inabidi tuachane naye, na kujiondoa katika kundi lake; ambapo ni kama tunapoteza muda kwa kuishi msituni muda wote. Eti ni kuukwepa mkono wa serikali ya Rwanda , ambayo siyo rahisi kuiangusha!” Akaendelea kusema Roman. “Cha muhimu sasa ni kuondoka kabisa hapa nchini Rwanda , na kukimbilia sehemu nyingine na kujisalimisha kwa Maafisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi. Baada ya kujisalimisha kwao, tutawaeleza uovu wote wa Kanali Fabio Rushengo, bila shaka wao watatusaidia na kutupatia ufumbuzi, au wenzangu mnasemaje?”

Baada ya Roman kusema vile, Teobale na Laurent wakaangaliana. Halafu Laurent akavuta pumzi na kusema: “Ni wazo zuri sana Roman. Lakini kwa ninavyofahamu, kwa mtu katili kama Fabio, hawezi kutuacha hai baada ya kugundua kwamba sisi tumemsaliti? Ukizingatia yeye ana medani ya ukamandoo katika masuala ya kivita?”
“Kwani unafikiri anaweza kutufanya nini?” Roman akamuuliza Laurent.

“Ni lazima atusake popote pale tutakapokimbia, na hatimaye kutuangamiza! Fabio ana mtandao mkubwa sana hadi sehemu za mipakani!”

“Kweli, anaweza kufanya hivyo. Lakini kabla hajatumaliza sisi, tutakuwa tumemmaliza yeye!” Roman akasema kwa msisitizo na kujiamini.

“Hebu tupe mipango,” Teobale akasema na kuendelea. “Tummalize kivipi?”
“Kwa njia rahisi sana . Si mnajua kuwa Kanali Fabio alikuwa ni mtu wa kuhifadhi kumbukumbu zake nyingi zinazohusu mipango yake ya maovu?”

“Kweli. Fabio ni mtu makini sana , kwani huwa anahifadhi kumbukumbu zake kwa kuziweka ndani ya Diski ya Kompyuta (Kihifadhia vitu kama vile, Maandishi, picha, sauti nk.) ambayo huichapa mwenyewe kwenye kompyuta, na kuzificha anapojua ndani ya ofisi yake!” Laurent akasema kwa umakini.

“Naam!” Akadakia Roman. “Basi tutaondoka na Diski mbili zenye mpango mzima wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, kuanzia mwanzo mpaka mwisho!”

Wenzake hawakumwelewa kwamba wangeondoka nazo vipi angali Diski zilikuwa zimefichwa sehemu ya siri? Teobale na Laurent wakamwangalia Roman baada ya kusema vile.

“Umesema jambo la maana Roman. Sasa hizo Diski tutaipataje?” Teobale akauliza.
“Hiyo ni kazi rahisi sana . Mimi naifahamu vizuri ofisi ya Fabio, na sehemu anapohifadhi nyaraka zake nyeti. Ni ndani ya droo iliyoko katika kabati maalum la chuma, hivyo kazi hiyo niachieni mimi, kwani nitaichukuwa kirahisi!” Roman akasema akiwapa moyo wenzake.

“Lakini cha muhimu tujue kwamba baada ya kutekeleza mpango huo, tutakimbilia wapi, yaani sehemu ya kwenda kujisalimisha!” Akasema Laurento.

“Kazi rahisi tu…” akadakia Roman. “Tutakimbilia sehemu za Ngara, nchini Tanzania , ambapo kuna Ofisi za Umoja wa Mataifa. Baada ya kufika tutawaeleza yote kwamba tumemtoroka Kanali Fabio, kiongozi msaliti, aliyeko katika msitu wa Kibungo, hivyo sisi tuko tayari kuwa mashahidi dhidi ya maovu yake punde atakapokamatwa. Hilo ni wazo langu jamani, tuchangie!

“Nimekubaliana na huo mpango wako kama ulivyopanga!” Laurent akasema huku akitabasamu.
“Ama kweli hicho ni kichwa!” Teobale naye akasema na kuongeza. “Mia kwa mia nimekubaliana nao kama ulivyopanga. Cha muhimu sasa tupange ni siku gani gani ya kuondoka!”

“ Kama tutafanikiwa, basi hatutakuwa na muda wa kupoteza. Tutaondoka muda wowote kwa kupitia katika barabara yetu ya siri, eneo la Rusumo kwa kutumia usafiri wa pikipiki yetu kubwa, ambayo ina uwezo wa kutubeba wote watatu. Baada ya kufika katika mto Rusumo, tutakuta kuna walinzi wenzetu, ambao huwa wanalinda. Ili wasitushtukie, tutawadanganya kwamba tuko doria katika kuimarisha ulinzi sehemu ile ya Rusumo, mpakani. Bila shaka watakubali na kuturuhusu kuvuka ng’ambo ya pili ya mto…”

“Tutaipakia pikipiki yetu ndani ya boti na kuuvuka mto ule mpaka upande wa pili na kuendelea na safari yetu kuelekea Ngara , Tanzania . Ni matumaini yangu mpaka hapo tumeelewana wapiganaji wenzangu!” Roman akamaliza.
“Hakuna shaka…umeeleweka vizuri,” Teobale akasema huku akiungwa mkono na Laurent.
Ni kwamba waliridhika!

“Ok, kama ni hivyo, ni vyema tumalizie vinywaji vyetu, kasha tuondoke!” Roman akawaambia.
Walipomaliza vinywaji, ilikuwa imetimu saa kumi na mbili za jioni. Wakanyanyuka na kutoka nje ya hoteli ile ya The Tropic Inn, iliyokuwa juu ya kilima kidogo, kilichofanya mandhari ya pale ipendeze hasa ukizingatia ilikuwa imezungukwa na miti mingi, pamoja na miamba michache yam awe iliyokuwa imechongwa kwa ustadi wa hali ya juu.

Wakaliendea lile gari Toyota Land Cruicer walilofika nalo, ambalo lilikuwa katika sehemu ya maegesho. Wakapanda na kuondoka kuelekea katika Kambi yao kwa kuifuata barabara ya vumbi, iliyokuwa inakatiza katika makazi ya watu, na hata, na hata vijijini katikati ya milima mingi. Ni hadi walipofika katika kambi yao na kuonekana kama walikuwa wametoka katika matambezi yao ya kawaida. Kumbe walikuwa na agenda ya siri! Ni usaliti dhidi ya Kiongozi wao Kanali Fabio Rushengo!

Ukweli ni kwamba hawakuwa na njia nyingine zaidi ya hiyo!
*******
Kanali Fabio Rushengo alikuwa ni mwanajeshi aliyefuzu katika medani ya kivita, na aliyepata cheo katika umri mdogo wa ujana tu kutokana na kujituma kwake, pamoja na elimu aliyokuwa nayo. Yeye alikuwa ni mmoja wa wahusika wa machafuko yaliyotokea nchini Rwanda , mwaka 1994.

Baada ya mauaji yale ndipo alipokimbilia eneo la Kibungo, akitokea jijini, Kigali , akiwa na wafuasi kadhaa waliomuunga mkono, ambao walijichimbia ndani ya msitu ule mzito ili wasiweze kukamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya mauaji yale ya Kimbari yaliyoutikisa Ulimwengu!

Hata hivyo, viongozi wengi wa Serikali ya Rwanda hawakujua kwamba Kanali Fabio alikuwa bado mzima, kwani walijua ameshakufa muda mrefu katika machafuko yale, baada ya gari aina ya Jeep, alilokuwepo kulipuliwa na kombora zito la ‘ RPG’ (Rocket Propeller Gun) kule jijini Kigali .

Ni kwamba gari lile kabla halijalipuka, aliwahi kuruka nje na kukimbia katika maficho, ukiwa ni mtego aliokuwa ameutega yeye, ili kuwalaghai watu wasiweze kujua. Na ndiye aliyekuwa akiendesha machafuko yale kwa baadhi ya Wahutu na Watusi wenye msimamo wa wastani ndani ya nchi ya Rwanda .

Ili asiweze kujulikana, baada ya kukimbilia ndani ya msitu wa Kibungo, Kanali Fabio alijibadili sura yake kwa kufanyiwa upasuaji (Plastic Surgery) na mtaalamu aliyemuagiza kutoka nje ya nchi, kwa malipo manono. Hivyo sura yake ikawa ni nyingine tofauti na ile ya mwanzo, na akawa anatembelea sehemu mbalimbali bila kujulikana, kiasi cha kumsaidia kuratibu mipango yake ya nyuma. Na ili wasiweze kujulikana, ndani ya msitu ule wa Kibungo, walianzisha kijiji kidogo, na kushughulika na kilimo ili kuficha maovu yao .

Pia, wasaliti hao, walikuwa wamekimbilia ndani ya msitu huo wakiwa na silaha nyingi za hatari, ambazo walikuwa wamezihifadhi ndani ya handaki chini ya ardhi. Ni handaki lililokuwa limechimbwa kwa ustadi wa hali ya juu, ambapo kwa nje palikuwa na mitambo ya kufua umeme-jua uliosaidia kuzalisha umeme ule katika eneo lile la nyumba za kambi. Umeme ule ulisaidia kuendesha mtambo wa mawasiliano ya siri, ambao ulikuwa siyo rahisi kwa mtu yeyote kugundua zaidi ya wao wenyewe!

Kwa ujumla kundi lile liliweza kuwasiliana na watu wa aina mbalimbali kwa kuendesha vitendo vyao vya kijasusi, kiasi cha kuweza kudumu kwa muda mrefu bila bughudha yoyote tokea mauaji yale ya kimbari yatokee. Wakawa wanapanga mipango ya kuihujumu Serikali wakiongozwa na kanali Fabio, aliyekuwa na nguvu za kutosha, hasa ukizingatia umri wake ulikuwa miaka 47 hivi, akiwa mtu shupavu mwenye mwili uliojengeka kutokana na mazoezi aliyokuwa anafanya kila siku ili kuuweka mwili wake imara!

Kielimu, Kanali Fabio alikuwa ni msomi wa elimu ya kidato cha sita, na pia Chuo Kikuu cha Kigali . Baada ya kuhitimu masomo yake ya Chuo Kikuu, ambapo alisomea Uhandisi wa Mitambo, alijiunga na Jeshi la Rwanda kabla machafuko yale hayajatokea, ikiwa ni kazi aliyoipenda, akiwa na ndoto ya kuja kuwa kiongozi mkubwa siku moja; tena kiongozi wa nchi!

Tuseme alipenda sana madaraka!

Ni hadi yalipotokea mauaji yale ya Kimbari, yaliyosababishwa na machafuko ya kikabila, ambapo Kanali Fabio alichangia kuhamasisha baadhi ya askari wa chini yake, kufanya mauaji yale! Yalikuwa ni mauaji ya Wahutu na Watusi wenye msimamo wa wastani, ambao hawakuwa na hatia yoyote!
Ni hatari!

Baada ya machafuko yale ndipo Kanali Fabio alipoamua kukimbilia ndani ya msitu wa Kibungo akiwa na wafuasi wengi vijana. Pia, walikuwa na silaha nyingi walizoiba katika maghala ya kuhifadhia silaha sehemu mbalimbali, kwani hakukuwa na udhibiti wowote, ni harufu ya damu ilikuwa inanukia kila pembe ya nchi!
Ni kuchinjana tu!

Roman alikuwa kijana mjanja sana , ambaye alijua anachofanya. Baada ta kupanga ule mpango wao wa kumtoroka mkuu wao, Kanali Fabio, kila sekunde, dakika na saa, alikuwa hachezi mbali sana naye, kwani walikuwa na ukaribu, tofauti na wapiganaji wengine. Nia yake ilikuwa ni juu ya kuweza kuzipata zile Diski mbili, zenye siri ya maovu, ambazo Fabio alikuwa amezihifadhi ndani ya ofisi yake iliyojitenga na makazi yao kwa umbali kias

Kwa vile Kanali Fabio alikuwa anamwamini Roman, hakumtilia shaka kabisa. Lile lilikuwa ni kosa kubwa sana alilofanya, kwani siku ya tatu tu, tokea wapange mpango ule wa kumtoroka, Roman alipata mwanya wa kuingia ndani ya ofisi ya Kanali Fabio, baada ya yeye kutoka nje ya kambi ile kwa shughuli zake binafsi. Baada ya kuingia, Roman akaliendea kabati la chuma lililokuwa mle ofisini, akapekuwa ndani yake na kufanikiwa kuzipata Diski mbili walizokuwa wanazihitaji.
Alifanikiwa kuzipata ndani ya droo mojawapo, kati ya droo kama kumi hivi alizokuwa amehifadhi vitu mbalimbali vilivyoweza kuuendesha ule mtandao wao. Ukweli ni kwamba alikuwa amefanya kazi ya ziada sana , baada ya kupekuwa kwa uangalifu sana . Baada ya kufanikiwa, Roman akalifungua lile kabati kama lilivyokuwa mwanzo, kisha akatoka huku akiwa na matumaini. Akaenda kuwasiliana na vijana wenzake, Obale na Laurento, ambapo walipanga mpango wa kutoroka usiku uleule kabla Kanali Fabio hajawashtukia.

Ilipotimu saa mbili za usiku, wote watatu walikuwa wameshajiandaa vya kutosha, wakiwa wameiandaa ile pikipiki kubwa aina ya Kawasaki . Waliijaza mafuta ya kutosha, pamoja na ya akiba yatakayoweza kuwafikisha katika safari yao waliyodhamiria. Giza nene lilikuwa limetanda eneo zima la msitu wa kibungo.

Lakini ni giza ambalo halikuwazuia kutimimiza azma yao ya kutoroka kama walivyopanga. Ili isijulikane kama wameondoka ndani ya kambi ile usiku, wakatoka kimya kimya, huku wakiikokota ile pikipiki bila kuitia moto, hadi walipofilka mbali. Wote watatu wakaipanda na kuifuata barabara ya siri iliyokuwa inakatiza katikati ya msitu uliokuwa na milima na miteremko mikali sana . Roman akiwa mtaalam, ndiye alikuwa anaendesha ile pikipiki kubwa! Wakakata mbuga!

Kwa vile barabara ile ilikuwa mbaya, walitumia saa moja na nusu kufika eneo la Rusumo, ambapo palikuwa na ule mto mkubwa sana . Ni mto Rusumo uliokuwa na upana wa mita 120 hivi, na ili kuuvuka ilibidi kutumia mtumbwi au boti. Vilevile ni mto uliotumika kama mpaka wa nchi za Rwanda na Tanzania , ambapo walitegemea kuwakuta walinzi, vijana wawili ambao pia ni waendesha boti maalum inayotumika kuwavusha watu ng’ambo ya pili ya mto ule. Ni vijana waliojulikana kwa majina ya Ndayize na Wizimana.

Walinzi wale, walikuwa wameshauona mwanga wa pikipiki ile kuanzia mbali, ikiwa inaelekea pale walipokuwa. Hivyo wakaamua kubanisha juu ya kilima kidogo, sehemu iliyokuwa na kibanda chao cha ulinzi, kilichoezekwa kwa nyasi. Wakawa wanaangalia kwa makini watu wale walivyokuwa wanaelekea sehemu ile usiku ule, bila kutoa taarifa yoyote.
Ndayize na Wizimana walikuwa na bunduki zao aina ya Sub-Machine Gun ‘AK 47’ tayari kwa kufyatua risasi kama angetokea adui. Roman na Obale wakafika katika eneo lile na kusimamisha pikipiki. Hata hivyo walikuta pakiwa kimya, bila kuwaona wale walinzi. Wakashuka na kuamua na kuamua kutoa ishara zinazowafanya watambuane katika kundi lao, ambapo Roman alipoanza sauti kali iliyokipasua kile kimya cha usiku ule kwa kusema: “Chuiii!”
“Simbaa!” Wizimana aliitikia ishara ile wakiwa bado wamebanisha juu ya kilima kile.

Halafu walinzi wakashuka kuwafuata baada ya kugundua ni wenzao, ambapo baada ya kuwafikia, waliwakuta ni Romeo, Teobale na Laurent wakiwa wamesimama kando kidogo ya pikipiki yao , na pia wamevalia majaketi mazito ya kukabiliana na baridi.

“Oh, ni nyie?” Ndayize akasema huku akiiweka bunduki yake vizuri.
“Ni sisi watu wa kazi!” Akasema Roman.
“Karibuni jamani…” Ndayize akamwambia.
“Ahsante sana …”

“Vipi jamani, mbona usiku wote huu? Safari ya wapi?” Ndayize akauliza.
“Jamani sisi tuko safarini, kwetu ndiyo kumekucha!” Akasema Roman na kuendelea. “Si mnajua bosi, Fabio ametupangia kazi ya kufuatilia fununu za maadui ng’ambo ya pili ya mto huu. Hivyo sisi ndiyo tunavuka kwenda kufanya upelelezi juu ya fununu hizo!”

“Hakuna tatizo…mnaweza kuendelea na safari, ngoja tuwavushe…” Ndayize akasema huku akiuamini ule uongo!
Wote wakaiendea ile boti kubwa iliyokuwa imeegeshwa kando ya mto Rusumo. Ni boti iliyokuwa na injini ya Yamaha, na kwa kusaidiana, wakaibeba ile pikipiki na kuipandisha juu ya boti, halafu wakaisukuma ndani ya maji, kasha wakapanda.
Nahodha wa boti alikuwa ni kijana Ndayize, ambaye aliitia moto na kuondoka kwa mwendo wa kasi na kuelekea upande wa pili wa mti ule, ambao ni upande wa nchi ya Tanzania. Ni sehemu iliyokuwa na vichaka vilivyofungamana na kulizidisha giza lile la kutisha!

“Oh, tumefika jamani!” Roman akasema baada ya kufika upande wa pili, ambapo hawakuchukuwa muda mrefu.
“Na kweli…” akaongeza Teobale.

Baada ya kufika ukingoni, wote wakashuka ndani ya boti, kisha wakasaidiana kuitoa ile pikipiki, ambayo baadaye, vijana Roman, Teobale na Laurent waliipakia na kuwaaga, Ndayize na Wizimana. Hata hivyo walinzi wale waliendelea kuwaangalia nusu wakiwaamini nap engine kutowaamini! Lakini hawakuwa na la kufanya. Pikipiki ile ikaondolewa kwa mwendo wa kasi kulitoka eneo lile la Rusumo!

“Turudi zetu…” Wizimana akamwambia Ndayize huku akiirukia boti yao .
“Hakuna shida,” Ndayize akasema halafu akaendelea. “Hivi ni kweli unawaamini hawa jamaa, kwamba wametumwa kazi na bosi usiku huu?”

“Hata mimi sijui. Lakini si ndiyo walivyosema wao?”
“Tumefanya kosa sana kuwaamini.”
“Sasa ulitakaje?”

“Tungemuuliza kwanza bosi…”
“Basi, hakuna jinsi…twende zetu…”
Hatimaye, Ndayize na Wizimana wakarudi ng’ambo ya pili ya mto, upande wa Rwanda , kuendelea na kazi yao ya ulinzi. Lakini ukweli unabakia kwamba, vijana wale walikuwa wamewatoka kiaina! Walikuwa wanakwenda kumchoma kiongozi wao, Kanali Fabio.

Ama kweli ulikuwa ni ujasiri wa hali ya juu!
********
Safari iliendelea usiku ule, huku pikipiki ikichanja mbuga. Roman alikuwa akiiendesha huku akiifuata njia ya mkato isiyo rasmi, hadi walipofika katika barabara kuu ya lami inayotoka nchini Rwanda , kuelekea Tanzania , kupitia kituo cha ukaguzi, Uhamiaji na Ushuru wa Forodha mpakani Rusumo. Sehemu yote ilikuwa kimya kabisa, kukizungukwa na pori tu. Hakukuwa na dalili za kuishi kwa binadamu katika eneo lile zaidi ya wanyama wadogo wadogo tu.

Baada ya kuiacha barabara ile, wakaifuata hadi walipofika katika kitongoji cha Benaco, eneo la Ngara. Wakaiacha barabara ya lami na kuifuata ya vumbi hadi walipotokeza eneo la Kumunazi. Roman akiwa ni mwenyeji, aliiendesha ile pikipiki kuelekea katika makambi ya Wakimbizi ya Lukole, wakati ule yalikuwa yakihifadhi wakimbizi kutoka nchi za Burundi na Rwanda , ambao wengi wao walizikimbia nchi zao kutikana na machafuko na mapigano ya kikabila, kati ya Wahutu na Watutsi.

Hatimaye wakafika kwenye kizuizi cha upekuzi wa kuingia ndani ya makambi, ambapo palikuwa na walinzi maalum. Ni walinzi waliowekwa na Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, ambao huteuliwa kutoka katika makundi ya wakimbizi, hasa wale wanaojua lugha ya kiswahili kwa ufasaha. Katika kizuizi kile, palikuwa na kibanda kilichokuwa kando ya barabara upande wa kushoto. Mlinzi mmoja akatoa amri huku akimulika tochi.
“Simamaa!”
“Sawa!” Roman akasema na kusimamisha pikipiki.
“Zima taa na ujitambulishe!” Amri ikaendelea kutolewa.
Roman akazima taa.
“Jitambulisheni!” Wakaambiwa!
“Sisi ni Wakimbizi!” Roman akasema.
“Wakimbizi?” Mlinzi yule akauliza kana kwamba alikuwa hajamwelewa.
“Ndiyo…wakimbizi!” Akasistiza Roman.
“Wakimbizi kutoka wapi?”
“Tunatoka nchini Rwanda !”

“Mh, makubwa!” Mlinzi yule akasema, kisha akaenda kuwasiliana na mkuu wao.
Hatua iliyofuata ilikuwa ni kuwapeleka Roman, Laurent na Teobale katika Kituo cha Polisi kilichokuwa ndani ya kambi ya wakimbizi ya Lukole, Ngara. Ni kituo kilichokuwa umbali wa kilometa mbili hivi kutoka pale kwenye kizuizi. Nia yao ilikuwa ni kwenda kupata ufumbuzi, ukizingatia wale walikuwa ni wakimbizi kweli, waliokuwa na sababu za msingi, ingawa wakimbizi wa Kinyarwanda walikuwa wamesharudi nchini Rwanda muda mrefu, baada ya nchi yao kuwa katika hali ya usalama.

Mpaka muda ule vijana, Roman, Teobale na Laurent wanafikishwa kwenye Kituo cha Polisi, palikuwa pameshapambazuka. Askari waliokuwa pale walifanya mahojiano nao, na baada ya kuridhika nao, wakawakabidhi kwa Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani, ambapo ilikuwa mlemle kambini.

Maofisa wale wakawachukuwa na kuwasafirisha hadi mjini Ngara, katika Ofisi za Umoja wa Mataifa. Nao wakafanya mahojiano nao na kuona walikuwa wanafaa kuwa mashahidi muhimu dhidi ya Kanali Fabio, msaliti wa Ser
Siku ileile jioni yake, vijana wale walitafutiwa makazi ya muda mjini Ngara, ili ufanyike utaratibu mwingine wa kuweza kuwasafirisha sehemu yoyote itakapopangwa. Hakika walijiona kuwa wamejikomboa kutoka mikonono mwa Kanali Fabio Rushengo. Wakataka kuyaanza maisha mapya kama wao, bila kutegemea kuishi msituni wakipokea amri ya mtu mmoja!
********

Asubuhi siku ya pili kulipambazuka vizuri. Kanali Fabio aliamka na kuendelea na utaratibu wake wa kila siku wa kujua mwenendo mzima wa shughuli za ulinzi wa kambi ile yao . Hata hivyo Fabio alishtuka baada ya kutowaona vijana wake watatu, Roman, Obale na Laurento, kwani ilikuwa ni lazima wapige ripoti kila asubuhi. Na hata baada ya muda aligundua kwamba walikuwa wamemkimbia, kwani waliondoka na vitu vyao muhimu, pamoja na ile pikipiki yao kubwa aina ya Kawasaki , ambayo haikuwepo katika gereji ya kuhifadhia vyombo vya moto.

Kanali Fabio akiwa amechanganyikiwa, akaingia ndani ya ofisi yake na kufanya upekuzi wa kina baada ya kuingiwa na wasiwasi, na ndipo alipogundua kuwa vijana wale walikuwa wameondoka na zile Diski mbili zilizokuwa na ule mpango mzima wa mauaji ya Rwanda ! Ukweli ni kwamba hakuwaelewa walikuwa na maana gani kumtoroka, tena wakiwa na ile siri kubwa ya mauaji aliyokuwa ameificha muda mrefu sana .

Basi hakutaka kupoteza muda, Fabio akaamua kumwita msaidizi wake wa karibu, aliyejulikana kwa jina la, Emmanuel Miburo, au kifupi Emma. Halafu akamwambia wakutane kwenye chumba cha mikutano, ambacho huwa wanafanyia mikutano mara kwa mara. Chumba kilikuwa kimejengwa kwa matofali ya kuchoma na kuezekwa juu kwa nyasi, ndani yake pakiwa na viti vilivyotengenezwa kwa miti iliyochimbiwa chini, na juu yake kuezekwa mabanzi.

Emma aliusikiliza ule wito wa mkuu wake, Kanali Fabio na kuingia mle ndani ya chumba na kumsubiri. Fabio akaingia mle ndani, ambapo hakukaa kitini kama kawaida yake, akawa amesimama huku ameshika kiuno chake na kutikisa kichwa!

Alikuwa akisonya ovyo!
“Nashindwa kuelewa!” Kanali Fabio akamwambia Emma.
“Kuelewa nini mkuu?” Emma akauliza huku akimshangaa kwa kumuoana akiwa katika hali kama ile!
“Nimechanganyikiwa!”
“Kwani vipi mkuu...umechanganyikiwa nini?” Emma akamuuliza baada ya kumwona akiwa katika hali kama ile! Ni kweli, amechanganyikiwa!
“Sijui ni kitu gani kinaendelea!”
“Hebu niambie mkuu…kuna nini?”

“Hivi una habari kuwa umetokea usaliti ndani ya kambi yetu?” Kanali Fabio akamwambia.
“Sina habari mkuu!”
“Basi elewa hilo! Hapa kambini usaliti umetokea! Na mpaka hivi sasa ninapoongea na wewe hapa ndani ya chumba hiki, wenzetu, Roman, Teobale na Laurent wametoroka hapa kambini na vitu vyao vyote!”
“Mungu wangu! Wametoroka?”
“Ndiyo!” Fabio akasema na kuendelea. “Na mbaya zaidi wameondoka na Diski zangu mbili, zenye taarifa zangu ya siri nilizohifadhi ndani yake!”

“Mh, makubwa! Mkuu unasema kwamba walitoroka jana usiku?”
“Ndiyo, lakini taarifa za kutoroka kwao nimezipata leo asubuhi, kutoka kwa walinzi waliokuwa zamu katika mto Rusumo. Ni Ndayize na Wizimaana, ambao waliwaona wakiwa na ile pikipiki kubwa ya hapa Kambini.”
“Sasa sijui watakuwa wameelekea wapi?” Emma akaendelea kuuliza.
“Ukweli ni kwamba sielewi…lakini nasikia walipovuka mto Rusumo, walielekea upande wa Tanzania , kwenye makambi ya wakimbizi yaliyoko Ngara!”

“Hata mimi nahisi watakuwa wamekimbilia huko. Lakini cha kujiuliza ni kwa nini wamechukuwa zile Diski?”
“ Hilo ndiyo la kujiuliza!” Fabio akasema na kuendelea. “Naona kwamba wana sababu zao, hasa ukizingatia kwamba hawakuacha ujumbe wowote!”
“Mh, hii kali!” Emma akasema huku ameinamisha kichwa chake chini!
“Sasa sijui tufanyeje Emma? Hebu naomba ushauri!”
“Ushauri wangu ni kuwafuatilia kama watakuwa wamekimbilia Ngara , Tanzania , ambapo sisi ni wenyeji!”
“Kwa hivyo unanishauri nitume mtu?”
“Ndiyo mkuu!”

“Itabidi nikutume wewe!”i
“Usitie shaka mkuu! Nitakwenda mimi mwenyewe!”
“ Safi sana Emma…” Kanali Fabio akasema na kuendelea. “Ndiyo maana nakuamini!”
“Ni hivyo mkuu, kwa vile mimi ni mzoefu ndani ya makambi yale. Nitakwenda kupeleleza, kama itakuwa wamefika kule, tutajua la kufanya, ikiwa yote ni kusubiri maelekezo!”

“Basi, tutafanya hivyo…itabidi uwafuatilie huko, ambapo ukiwapata itakupasa uwalipue baada ya kuhakikisha umezipata zile Diski zangu. Mimi nakufahamu sana Emma, hakuna muda wa kupoteza…tupange safari!”
“Ndiyo mkuu… mimi ni mtu wa kazi. Napendelea nisafiri kesho, siku ya leo itakuwa ni kwa ajili ya maandalizi!”
“Hakuna tatizo…kajiandae!”

Kanali Fabio na Emma Miburo wakamaliza kupanga mikakati yao ya kuwasaka wale wenzao waliowasaliti na kuikimbia kambi ile. Baada ya kumaliza kila mmoja akaendelea na shughuli zake, ambapo Emma alikwenda kujiandaa kwa ajili ya safari ile ya mtafutano, ambapo hakujua kama angefanikisha kuwapata.

Ukweli ni kwamba alijua kuwa vijana wale, walikuwa ni watu wenye medani za kivita, hivyo siyo rahisi watoroke, halafu waje kupatikana tena! Walijua walichokuwa wanafanya!Emma Miburo alikuwa ni mmoja wa wale watu makatili sana .
Hapo mwanzoni alikuwa askari katika Jeshi la Rwanda , ambapo alijiunga pindi alipomaliza elimu ya Sekondari, kidato cha nne, ikiwa ni kazi aliyoipenda tokea mwanzoni akiwa mdogo, hasa ukizingatia baba yake alikuwa Mwanajeshi. Ndiyo kusema alikuwa ametokea katika familia ya kijeshi na kuishi katika Kambi za Kijeshi!

Baada ya machafuko yale yaliyotokea nchini Rwanda , ndipo Emma alipojiunga na kundi la Kanali Fabio, baada ya kuhamasishwa kwamba angefaidika. Na kweli, akapewa cheo cha msaidizi wake.

Akiwa na umri wa miaka 35 tu, Emma alikuwa jasusi wa hali ya juu, na mjuzi wa kutumia silaha za aina mbalimbali, ambazo alijifunza kutokana na kuipenda kazi ile ya jeshi. Hakika alikamilika kila idara!

Vilevile Emma hakuwa mgeni nchini Tanzania , kwani alikuwa ameshatembelea sehemu mbalimbali, kama mkoa wa Kagera, hasa katika makambi ya wakimbizi ya Benaco, Wilayani Ngara. Pia, aliwahi kutembelea mikoa ya Mwanza, Kigoma na Arusha katika mizunguko yake. Ndani ya jiji la Arusha, Emma aliwahi kukaa akiwa ni mwenyeji wa mfanyabiashara mmoja maarufu, aliyeitwa, Paul Rugoye, aliyekuwa anamiliki kampuni ya kuhudumia watalii, na nyinginezo.

Emma aliweza kuishi vizuri bila kubughudhiwa na mtu yeyote, kwani hakuna aliyejua kwamba alikuwa raia wa nchi jirani ya Rwanda .
Basi, huyo ndiye mtu hatari na jasusi, Emmanuel Miburo!

********
Mjini Ngara, nchini Tanzania , Maafisa wa Umoja wa Mataifa, walikuwa wameshaomba kibali kwa Wizara ya Mambo ya Ndani, kwa ajili ya kuwasafirisha vijana, Roman, Teobale na Laurent, mpaka mkoani Arusha, ilipo Mahakama ya Watuhumiwa wa Mauaji ya Rwanda yaliyotokea Mwaka 1994. Na ile ilikuwa ni baada ya taratibu zote kukamilika siku ile ya pili yake tu tokea watoroke nchini Rwanda . Ili waweze kuwahishwa Arusha, na pia kuepuka mtego wa kuwadhuru,walikodiwa ndege ndogo, ambayo ingewafikisha mapema.

Majira ya saa moja za asubuhi, wote watatu walichukuliwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser hadi katika uwanja mdogo wa ndege, ulioko katika vilima vya Ngara, nje kidogo ya mji, sehemu yenye miteremko mikali. Ingawa uwanja ule ulikuwa umejengwa mlimani, lakini sehemu yenyewe ilikuwa tambarare, hasa ukizingatia maeneo yote yalikuwa na milima na mabonde mengi. Baada ya kufika pale uwanjani, wakaikuta ndege ndogo aina ya Cessna Caravan ya kampuni ya kukodi.

Wote wakapanda wakiongozwa na Maafisa wawili wa Umoja wa Mataifa, waliokuwa wasindikizaji. Na dakika mbili baadaye rubani akaiwasha ndege na kuiondoa kuelekea katika njia yake ya kurukia, hatimaye akaitoa kwa mwendo wa kasi na kuirusha kuelekea upande wa Mashariki. Ilikuwa ni safari ndefu, lakini baadaye ndege ile ilifika Arusha na kutua kwenye uwanja wa ndege ulioko Kisongo, jijini Arusha.

Wote wakashuka na kupokewa tena na Maafisa wa Umoja wa Mataifa, waliofika na magari yao . Roman, Teobale, na Laurent wakapanda ndani ya gari mojawapo na kuondoka pale uwanjani, kuelekea sehemu waliyotafutiwa makazi ya muda. Walikuwa wametafutiwa nyumba nzuri ya kuishi iliyojengwa kwa ajili ya mashahidi muhimu wa kesi za watuhumiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda.aa

Makazi yao yalikuwa eneo la Njiro, lililoko nje kidogo ya jiji la Arusha, ikiwa ni sehemu iliyotulia, zilipojengwa nyumba nyingi zinazomilikiwa na wafanyakazi wa mahakama ile, wengi wao wakiwa raia wa nje ya Tanzania . Ni nyumba iliyokuwa inalindwa kwa muda wa saa 24 na walinzi maalum, ili wasiweze kudhurika na watu waovu, wengi wao wakiwa ni wale waliohusika kwa njia moja ama nyingine katika kufanikisha mauaji yale, walioukwepa mkono wa sheria.

Baada ya kuhakikisha usalama wao, vijana, Roman, Teobale na Laurent, walijichimbia ndani ya nyumba ile huku wakipanga mikakati yao juu ya kutoa ushahidi ule wa Diski, na jinsi ya kuweza kuwasiliana na Maafisa wa Umoja wa Mataifa. Hata hivyo wakaona kuwa ni busara wangezitoa punde zitakapohitajika. Wakazichimbia sehemu za siri huku wakimwazia kiongozi wao, Kanali Fabio atakavyochanganyikiwa!
********

Nchini Rwanda , ndani ya msitu wa Kibungo, katika kambi ya waasi, Emmanuel Miburo, msaidizi wa Kanali Fabio alikuwa ameshajiandaa vya kutosha, punde tu alipopanga safari ile ya kuwafuatilia vijana, Roman, Teobale na Laurent, Ngara, nchini Tanzania , ambapo alihisi kuwa wamekimbilia huko. Hakika alikuwa ameandaa baadhi ya zana zake za kazi kama, bastola, visu maalum, na dawa za aina mbalimbali zikiwa ni pamoja na za sumu pamoja na za usingizi, ambazo zingemsaidia sana katika kazi ile ya kijasusi!

Alipomaliza, Emmanuel akaondoka kwa kupitia njia ya halali, kwani alikuwa na Hati ya kusafiria iliyomtambulisha kama ni mfanyabiashara anayesafiri nchi mbalimbali za ukanda wa Maziwa Makuu, kama vile, Burundi , Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo , Uganda na Tanzania . Hivyo alipitia ‘Boda’ ya Rusumo na kuvuka mpaka upande wa Tanzania , halafu akachukuwa usafiri wa gari dogo hadi katika kitongoji kidogo cha Benaco.

Pale akashuka na kufanya utaratibu wa kutafuta chumba cha kupanga katka nyumba ya kulala wageni, na kwa sababu alikuwa amezoeleka na watu wengi, hakuwa na wasiwasi wa kufichuka kwa mpango wake mwovu wa kufanya upelelezi!
Emmanuel alipanga nyumba ya wageni ya Kivulini Gesti, iliyokuwa maarufu sana katika kitongoji kile, ikiwa inatumiwa na watu wengi, hasa madereva wa magari makubwa ya mizigo yanayolala pale usiku wakati wakiwa safarini kuelekea nchini Rwanda na kwingineko.

Ilipotimu saa sita za mchana, Emmanuel aliamua kuelekea katika makambi ya wakimbizi ya Lukole, yaliyokuwa umbali wa kilometa kumi na tano kutoka katika kitongoji kile cha Benaco. Akachukuwa usafiri wa teksi, ambayo ilimfikisha ndani ya kambi na kumshushia eneo la Sokoni, palipokuwa na pilikapilika nyingi za watu.

Akiwa ni mtu mzoefu ndani ya kambi ile, Emmanuel alizunguka kutwa nzima na kujichanganya na wakimbizi wengine. Akawa anapeleleza kwa kila anayefahamiana naye, ambapo alifanikiwa kupata taarifa zile kuhusu vijana, Roman, Teobale na Laurent. Akaambiwa kuwa ni kweli walifika kujisalimisha kwa polisi wanaolinda usalama, na kisha kupelekwa kwa Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Ndani, pamoja na wale wa Umoja wa Mataifa na kufanya mahojiano nao!
Ni hatari!

Pia, Emmanuel aliambiwa kwamba vijana wale walikuwa wameondoka kwa ndege asubuhi ile, kuelekea Arusha, tayari kuwa Mashahidi Muhimu, baada ya kuwa na ile siri nzito. Baada ya kuzipata habari zile, Emmanuel akaondoka ndani ya kambi ile ya wakimbizi, na kurudi Benaco alikopanga chumba. hakika alirudi akiwa amechanganyikiwa sana , kwani hakutegemea kabisa kama vijana wale walikuwa wameamua kufanya vile.

Akakodi teksi iliyomfikisha na haraka akaingia chumbani na kumharibarisha Kanali Fabio Rushengo, kwa kutumia simu ya mkononi, ambayo mtandao wake ulitumika katika nchi mbalimbali duniani.
“Emma Miburo hapa mkuu!” Emma alijitambulisha baada
ya kumpata kwenye laini.
“Ndiyo Emma…habari za huko…”
“Habari za huku siyo nzuri mkuu!”
“Una maana gani?”
“Nimefanikiwa kufika hadi ndani ya kambi ya wakimbizi ya Lukole, Ngara. Nimefanya upelelezi wangu na kugundua kuwa vijana wale ni kweli walikuwa wamefika kujisalimisha kwa Maafisa wa Umoja wa Mataifa!”
“Mh!” Fabio akaguna. “Baada ya kujisalimisha?”
“Wakawaelewa shida yao iliyowapeleka nchini Tanzania , ambayo siyo nyingine zaidi ya kukukimbia wewe!”
“Kunikimbia mimi?”
“Ndiyo mkuu!” Emma akasema na kuendelea. “Tena mbaya zaidi, wamesema kwamba wana siri nzito dhidi yako ambayo hata mimi sijaijua!”
“Mungu wangu! Ni zile Diski zangu tu, zenye mambo yangu ya siri!” Kanali Fabio akadakia.
“Na kingine zaidi ya hapo mkuu, ni kwamba wameshasafirishwa kwenda Arusha, katika Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya Mauaji ya Rwanda !”
“Oh, basi Emma!”
“Basi nini bosi?”
“Basi…basi…rudi haraka tupange mipango mingine kabla mambo hayajaharibika!” Kanali Fabio akamwambia.
“Sawa Mkuu…nitafanya hivyo!”
Baada ya Emmanuel kupewa maagizo yale, akaamua kuwa ni lazima afunge safari ya kurudi Kibungo, nchini Rwanda punde patakapopambazuka tu. Na kweli palipokucha Emma aliondoka kwa njia ile aliyokuja nayo hadi nchini Rwanda katika kambi ya waasi!
Kazi ilikuwa bado!
********

Paul Rugoye alikuwa ni mfanyabiashara maarufu jijini Arusha , Tanzania , ambaye alikuwa anamiliki kampuni ya kuhudumia watalii, iliyojulikana kwa jina la Rugo safaris, ambayo makao yake yalikuwa Arusha. Ni kampuni iliyokuwa na wateja wengi sana kutokana na zile huduma nzuri walizotoa.

Basi, Paul Rugoye ndiye aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu, akifuatiwa na wasaidizi wake, kama vile, Meneja, Mhasibu na wengineo, ambao walikamilisha safu ya uongozi wa kampuni ya Rugo Safaris.

Ingawa Paul Rugoye alikuwa mfanyabiashara, pia alikuwa ni jasusi hatari sana . Alikuwa kishirikiana na Kanali Fabio Rushengo kwa njia moja ama nyingine. Akiwa na umri wa miaka ipatayo hamsini hivi, Paul alikuwa ni mzaliwa wa Mkoa wa kibungo, nchini Rwanda .

Lakini kwa kipindi chote alijifanya ni mzaliwa wa Wilaya ya Ngara, Mkoani Kagera, na kabila lake ni Mhangaza, ingawa ni kweli kwamba alizaliwa upande wa Tanzania . Ndiyo tuseme kuwa ndugu zake wengi walikuwa nchini Rwanda , ambao idadi kubwa wakiwa wahanga wa mauaji ya kimbari.

Akiwa jijini Arusha, Paul Rugoye alikuwa akifanya upelelezi, chini ya kivuli cha kumiliki ile kampuni ya kuhudumia watalii, akimsaidia Kanali Fabio. Nia yake ilikuwa ni kuweza kugundua watu waliotegemea kutoa ushahidi katika Mahakama ile ya mauaji ya Rwanda , inayoendeshwa na Umoja wa Mataifa. Halafu kinachofuata ni wao kumaliza kwa njia za kijasusi wanazozijua wenyewe. Hakika walikuwa ni watu hatari sana !

Ndipo Kanali Fabio akiwa nchini Rwanda , alipoamua kumpigia simu Paul Rugoye, na kumweleza lile tatizo la kusalitiwa na wale vijana watatu, Roman, Teobale na Laurent, ambao walikuwa wameshawasili jijini Arusha. Baada ya kumaliza kumweleza yote, akamalizia kwa kusema:

“Sasa naomba ushauri wako…”
“Aisee…kuna kazi…lakini, sisi tukiwa watu wa kazi, hatushindwi kitu!” Kanali Fabio akamwambia kwa sauti ya kujiamini na kusisitiza!

“Unayosema ni kweli…” Paul alisema na kuendelea.
“Sasa usihofu. Mimi nitapanga mipango kambambe. Tuma vijana wako wa kazi, kama watatu hivi, waje hapa jijini Arusha, ambao tutafanya nao kazi na kuwasambaratisha wasaliti hao kabla hawajaleta madhara yoyote kwa upande wetu!”

“Kuhusu vijana wa kazi, hakuna tatizo, nitawachagua leo hii hii. Lakini tatizo jingine ni namna ya kuwasafirisha kutoka hapa nchini Rwanda hadi huko Arusha.”
“ Hilo lisikutie hofu. Mipango yote nitaipanga mimi, na jinsi ya kuwachukuwa vijana hao kutoka huko mpaka Arusha.”
“Sawa Paul…nakutegemea wewe!”
“Usihofu…tutawasiliana zaidi.”
Kanali Fabio na Paul wakakubaliana katika mpango ule, ambapo alikubaliana katika mpango ule, ambapo alikubali kuratibu mpango mzima wa safari ile ile, kuanzia Rusumo, Ngara, hadi jijini Mwanza , Tanzania .
Fabio akapanga kuwachagua vijana wake shupavu, aliokuwa anawaamini sana , ambao ni Jean Rutaga, France Bizimana na Pierre Bisamo.
Ni vijana waliokuwa na taaluma ya kijasusi wa hali ya juu!
********

MAJIRA ya saa tatu za usiku, Kanali Fabio alikuwa amekaa ndani ya chumba cha mikutano. Alikuwa anawasubiri vijana wake, Jean , France na Pierre, ambao alikuwa ameshawaeleza juu ya kukutana kwao kwa ajili ya kazi ile ya kukata na shoka. Ingawa yeye alitakiwa awe mtu wa mwisho kufika, lakini alijikuta ametangulia kwa ajili ya wasiwasi uliokuwa unamtawala. Muda wote aliokuwa amekaa pale, Fabio alikuwa akiangalia saa yake na kuendelea kuwaza juu ya zile Diski mbili, na mpango mzima wa mauaji ya Rwanda aliyokuwa ameyapanga.

Kama Diski zile zikiwafikia wahusika, basi angehusishwa na mauaji yale, kitu ambacho hakupendelea. Tuseme vijana wake waliomtoroka, wangekuwa mashahidi muhimu, ambao wangewezesha kukamatwa kwake, ingawa alikuwa amesahaulika muda mrefu sana , na pia alishabadilisha sura yake kwa kuwekewa ya bandia!

Sasa iweje wamharibie mipango yake?
Haiwezekani!
Ni lazima wafuatwe kule walipo!
Wafutwe katika dunia
Wakati Kanali Fabio akiwa katika lindi la mawazo, vijana maalum, Jean, Pierre na France wakaingia ndani ya chumba kile cha mikutano walichoahidiana kukutana usiku ule.
“Mkuu tumefika!” Pierre akasema kwa niaba ya wenzake, wakiwa bado wamesimama.
“Oh, karibuni na mkae…” Fabio akasema huku akivuta pumzi ndefu.
“Ahsante mkuu!” Wote wakasema na kukaa vitini.
“Vizuri sana !” Kanali Fabio akasema huku akiwaangalia vijana wake, na kukubali kweli walikuwa ni watu wa kazi!
Baada ya kukaa, wakaendelea kumwangalia Kanali Fabio aweze kuwapa majukumu aliyokuwa amewaitia usiku ule. Ukweli ni kwamba walijua kuwa kulikuwa na kazi muhimu, hasa ukizingatia haikuwa kawaida ya kiongozi wao kutangulia katika chumba cha mikutano kabla yao , kama alivyofanya siku ile. Kwa vyovyote kuna jambo kubwa lilikuwa limemkwaza!

Kimaumbile, kijana wa kwanza, Jean alikuwa mrefu, mwenye umbile la miraba minne liliojengeka vyema. Alikuwa na umri wa miaka 30 hivi, akiwa Jasusi tegemeo kwa Kanali Fabio. Kijana wa pili, France , naye alikuwa amefuzu kama Jean, na tatu ni Pierre, ambaye naye alikuwa na taaluma kama wenzake wawili.

Wote walijazia miili mithili yua wabeba vyuma! Hakupoteza muda, Kanali Fabio akawaeleza madhumuni mazima ya ile safari yao ya kuwafuatilia wenzao waliowasaliti, Roman, Teobale na Laurent, waliokimbilia jijini Arusha, nchini Tanzania . Halafu akamalizia kwa kusema: “Ni matumaini yangu kuwa nyote mko tayari kwa kazi!”

“Ndiyo, sisi tuko tayari kwa kazi!”
“Tuko timamu mkuu!” Pierre akasema.
“Tuko tayari mkuu!” Akaongeza France .
“Vizuri sana kama mko tayari,” Kanali Fabio akawaambia na kuendelea. “Nimeshafanya mawasiliano yote na Paul Rugoye, aliyeko Arusha , Tanzania , ambaye ataratibu safari yenu nzima. Mtatoka hapa kambini kwa usafiri wa gari mpaka Rusumo kwa kutumia barabara yetu ya siri inayokatiza msituni, hadi kwenye mto Rusumo. Baada ya kufika pale mtoni, mtavushwa na boti mpaka ng’ambo ya pili, upande wa Tanzania . Mkishavushwa tu, mtatembea kwa miguu umbali wa kilometa tatu hivi, mpaka mtakapofika katika barabara kuu iendayo Benaco kutoka Rusumo.

“Pale mtakuta gari moja aina ya Mitsubishi Fuso, la mizigo, likiwa limeegeshwa kwa kuwasaidia nyie. Dereva wake ameshapewa maelekezo yote kuwa awachukuwe hadi Mwanza, na baada ya kufika jijini Mwanza, mtakuta usafiri mwingine uliotayarishwa na Paul Rugoye, wa kuwafikisha Arusha…sijui mmemnielewa?” akamaliza Fabio.
“Tumekuelewa mkuu…” wakasema kwa pamoja.

“Ok, kama mmenielewa, nifuateni…” Kanali Fabio akawaambia.
“Sawa mkuu…” vijana wale wakasema huku wakinyanyuka na kumfuata nyuma.
Walielekea na kuingia ndani ya handaki maalum, ambamo ndani yake kulikuwa na silaha za kila aina. Baada ya kuingia ndipo alipowapangia majukumu mengine, pamoja na kuwapatia zana za kazi, na mavazi yaliyoweza kuficha silaha za hatari, zikiwemo bunduki fupi fupi aina ya ‘Uzi,’ bastola za kijeshi, na mabomu ya kutupa kwa mkono. Pia, akawapa dawa maalum za vidonge, ambazo zilikuwa sumu kali iliyoweza kuua mara moja, ambavyo hutumiwa na majasusi wanapokuwa wamezidiwa ili wasiweze kutoa siri kwa jinsi walivyokula kiapo!

Mbali ya silaha hizo, pia walikabidhiwa vifaa vya mawasiliano, ambavyo vingewasaidia kuwasiliana watakapokuwa Arusha. Baada ya kuchukuwa vifaa vyao vyote, wakatoka ndani ya lile handaki hadi nje, ambapo walikuta gari aina ya Toyota Land Cruiser likiwasubiri tayari kwa safari ile kuelekea Rusumo mpakani!
“Jamani, usafiri ndiyo huu hapa!” Kanali Fabio akawaambia.

“Ni sawa mkuu!” Wote wakasema na kujiandaa kuingia ndani ya gari.
“Haya, nawatakia safari njema. Lakini kumbukeni kuwa mawasiliano ni muhimu sana !”
“Tutafanya hivyo mkuu!”
Wakamalizana.

Hatimaye wote wakapanda ndani ya lile gari, ambapo dereva alikuwa ndani yake akiwasubiri. Akalitia moto na kuliondoa eneo lile la kambi. Ulikuwa ni usiku wa saa tano, na sehemu yote ilikuwa giza tupu. Hata hivyo baada ya saa moja na nusu wakawa wamefika Rusumo, mbali kidogo na ule mto. Dereva akalisimamisha gari kando ya msitu mzito, na vijana, Jean, Pierre na France wakashuka wakiwa na ile mizigo yao midogo, kisha wakamruhusu aondoke kurudi Kambini.

Baada ya dereva kuondoka, vijana wale wakabaki wakijadiliana jambo fulani harakaharaka, halafu wakapanda ile boti iliyowavusha hadi nga,ambo ya pili ya mto na kushuka. Boti ikarudi ilipotokea ikiendeshwa na walinzi. Vijana wale wakaanza kutembea kwa mwendo wa kasi kuelekea sehemu waliyoelekezwa, huku wakishindana na lile giza la usiku. Baada ya kutembea umbali wa kilometa tatu wakaifikia barabara kuu ya lami iliyopita katikati ya mabonde na milima, ambapo waliahidiwa kulikuta lile gari likiwasubiri wao.
Kazi nzito!

*******
Katikati ya kiza kizito, gari moja, lori, aina ya Mitsubishi Fuso, lilikuwa limesimamishwa kando ya barabara, kama vile lilikuwa limeharibika. Kwa muda ule lilikuwa limefunikwa turubai nyuma, wakati dereva na utingo wake wakiwa wamejifungia ndani sehemu ya mbele. Hakika sehemu ile ilitisha sana hasa ukizingatia usalama wake ulikuwa mdogo, kutokana na majambazi waliokuwa wakiteka magari yaliyokuwa yanasafiri katika barabara ile, na kupora chochote walichoona kinawafaa. Wengi wa majambazi yale, ni wakimbizi waliowahi kuwa wanajeshi nchini mwao.

Hata hivyo dereva wa gari lile aliyeitwa Antoni Mjivumi, hakuwa na wasiwasi wowote baada ya kuhakikishiwa usalama wake na Paul Rugoye, aliyemkodi kwa gharama kubwa sana . Na ni kwa ajili ya kuwabeba vijana wale, Jean , France na Pierre, kwa siri kuwasafirisha hadi jijini Mwanza, kukwepa wasiweze kushtukiwa katika mipango yao waliyopanga.

Wakiwa ndani ya gari, dereva Antoni Mjivumi, na utingo wake, Cosmas Kishoka, waliweza kusikia vishindo vya miguu ya watu waliokuwa wanatembea kama wanalijongelea gari lao. Kwa vile sehemu yote ilikuwa kimya kabisa, sauti iliweza kusikia, hata ya wadudu wadogo waliokuwa wakilia kule porini. Utingo Cosmas akanyanyua kichwa chake na kuangalia kule nje kulipokuwa na kiza kizito, halafu akamwambia dereva:

“Haloo, Mjivumi eee!”
“Eee…unasemaje Cosmas?”
“Nasikia mchakacho huko nje, kama vile watu wanatembea…”
“Labda ni wale watu tulioambiwa kuwa tuwasubiri!” Dereva akasema huku naye akinyanyua kichwa chake.
“Naona kuna watu watatu…” Cosmas akasema baada ya kuwaona wale watu watatu, Jean , France na Pierre.

“Basi ndiyo wenyewe…”
Baada ya sekunde kadhaa watu wale wakalifikia gari na kusimama. Dereva akaufungua mlango na kuwaangalia watu wale waliokuwa wamevalia makoti makubwa yaliyofanya watishe katika kiza kile!
“Usalama uko?” Dereva akauliza.
“Hakuna shaka, usalama upo!” Jean akasema huku akiwasha tochi yake kubwa.
“Karibuni jamani…”
“Ahsante sana …hamjambo?”
“Sisi hatujambo.”
“Tumeelekezwa kuwa tutaukuta usafiri wa gari hapa.”
“Hamkukosea…ndiyo hapa…” Anton Mjivumi akasema na kuendelea. “Na ndiyo tunawasubiri, hivyo pandeni garini!”

Utingo Cosmas akawafungulia mlango wa upande wake, nao wakaingia ndani ya gari lile, sehemu ya nyuma ambapo palikuwa na uwazi mkubwa wa kuweza kukaa watu wale. Kwa kawaida magari mengi ya safari huwa yana sehemu ya ziada, ambayo huwa na kitanda cha kupumzikia, au hata kulala. Basi sehemu hiyo ndiyo waliyotumia vijana wale hatari kujichimbia kwa ustadi mkubwa pamoja na mizigo yao . Pia, walikuwa wamefunikwa na pazia zito, kiasi kwamba siyo rahisi kwa mtu kugundua palikuwa na watu waliojificha zaidi ya utingo na dereva.

Kusema kweli dereva yule, Anton Mjivumi, hakujua lolote kuhusu watu wale’ kama walikuwa hatari. Baada ya kupanda garini, akalitia moto na kuliondoa kwa mwendo wa kawaida na wote wakiwa kimya kabisa, hakuna aliyezungumza na mwenzake. Lakini kwa upande wa utingo Cosmas hakuwa na amani na watu wale waliojificha baada ya kupanda ndani ya gari lile? Hata hivyo hakusema kitu hadi walipofika katika kitongoji cha Benaco, penye njia panda ya kwenda Karagwe na Mtukula. Wakati huo ilikuwa imeshatimu saa 12 za alfajiri, kukiwa kumeshapambazuka.

Dereva akalipaki gari wakajipatia kifungua kinywa na walipomaliza wakaendelea na safari yao kuifuata barabara inayoelekea maeneo ya Nyakaura, Runzewe, Biharamulo na Kahama. Kwa bahati nzuri hawakukutana na kizuizi chochote hadi walipofika Biharamulo, ambapo kwa muda wote Cosmas alikuwa na wasiwasi na watu wale waliokuwa wanaongea lugha ya Kinyarwanda na kifaransa! Na mara nyingi wakiliongelea jiji la Arusha, na pia kuwa na kipeperushi kilichokuwa na ramani ya jiji hilo .

Baada ya kutoka Biharamulo, wakaendelea na safari kuelekea Mwanza. Vijana, Jean, Pierre na France wakawa wanawasiliana kwa simu zao za mkononi na Bw. Paul Rugoye, aliyekuwa jijini Mwanza, kuwapokea. Hakika yote yalizidi kumchanganya utingo Cosmas! Akayaweka rohoni! Lakini akipanga kuwa ni lazima aje kuyalipua baadaye itakapobidi.

Dereva akaendelea kuendesha gari huku akipangua gea moja baada ya nyingine. Hakuwa na mawazo mengine zaidi ya kuwazia safari yake afike salama akiwa na wale watu alioambiwa awachukue, na mara nyingine alikuwa akivuta sigara na kupulizia moshi nje ya dirisha.
ITAENDELEA

TODAYS
 
Simulizi : Msaliti Asakwe
Sehemu Ya Pili (2)

BAADA ya kutoka Biharamulo, wakaendelea na safari kuelekea Mwanza. Vijana, Jean, Pierre na France wakawa wanawasiliana kwa simu zao za mkononi na Bw. Paul Rugoye, aliyekuwa jijini Mwanza, kuwapokea. Hakika yote yalizidi kumchanganya utingo Cosmas! Akayaweka rohoni! Lakini akipanga kuwa ni lazima aje kuyalipua baadaye itakapobidi.
Dereva akaendelea kuendesha gari huku akipangua gea moja baada ya nyingine. Hakuwa na mawazo mengine zaidi ya kuwazia safari yake afike salama akiwa na wale watu alioambiwa awachukuwe, na mara nyingine alikuwa akivuta sigara na kupulizia moshi nje ya dirisha.
*******
Usafiri wa kwenda jijini Arusha ulikuwa umeshaandaliwa na Paul Rugoye, ambaye aliamua kuwafuata yeye mwenyewe. Kwa kutumia gari lake jipya kabisa aina ya Ranger Rover Vogue Sports, ambalo alikuwa amelinunua hivi karibuni kwa kiasi kikubwa cha fedha. Akiwa ni dereva mzuri wa gari, aliondoka Arusha na kusafiri kuelekea Mwanza, ambapo alitumia saa chache tu kufika kwa vile hakuwa na sababu zozote za kumfanya awe anasimama njiani. Alikuwa amejikamilisha kwa kila kitu.
Hivyo baada ya Paul Rugoye kufika jijini Mwanza, alipanga kwenye hoteli nadhifu ya Rizano, iliyoko katika Barabara ya Nyerere, ambayo ni sehemu waliyokubaliana kukutana, ambapo pia mmiliki wa hoteli hiyo walikuwa wanafahamiana wakiwa wote ni wafanyabiashara wakubwa. Yeye Paul alikuwa amefika pale siku mbili zilizopita huku akifanya mawasiliano na watu wake, wakiwa katika safari nzima ya kutokea nchini Rwanda hadi Mwanza.
Gari lile Mitsubishi Fuso lilifika jijini Mwanza salama. Baada ya kufika, vijana, wakashuka na kuagana na dereva, Anton Mjivumi, pamoja na utingo wake, Cosmas, kwa kuwafikisha salama.
Walimkuta Paul Rugoye akiwasubiri kwa gari lake, sehemu ile ya Nyamagana walipofika na kulipaki lile lori. Bila kupotez\a muda, wote wakaingia kwenye gari la Paul wakiwa na mizigo yao yote iliyokuwa na vitu hatari. Safari ikaanza palepale, dereva akiwa ni Paul, kwani hakupenda kumpa kazi ile mtu yeyote, kwa kuhofia kushtukiwa. Hakuna jasusi anayemwamini mtu kirahisi! Ndivyo alivyokuwa yeye!
“Habari za safari jamani…” Paul Rugoye akawaambia punde tu baada ya kupanda ndani ya gari.
“Safari siyo mbaya sana mkuu!” Jean akasema.
“Lakini tushukuru Mungu ametufikisha salama bila matatizo...” akadakia Pierre .
“Kwa nini unasema hivyo?’ Paul akauliza huku akimwangalia Jean.
“Ilikuwa ngumu na yenye mashaka!”
“Mashaka kama yapi?”
“Juu ya wale watu waliotufikisha hapa!”
“Una maana dereva na utingo wake?”
“Ndiyo.”
“Wamefanya nini?”
“Mimi binafsi, nina wasiwasi na yule utingo wa lile gari tulilokuwa timepanda. Kwa sababu muda wote alikuwa anatuangalia sana , kana kwamba anatuchunguza!”
“Hata mimi nilikuwa na wasiwasi naye sana …” akaongeza Pierre .
“Anaweza kutuchoma yule. Na kwa mbinu zangu za kijasusi simwamini!” France naye akadakia kwa msisitizo!
“Aisee…basi ingebidi auawe!” Paul akasema na kuendelea.
“Mbona hamkusema mapema mpaka tumeondoka?”
“Lakini tumechelewa!” Akasema Jean.

“Tuendelee na safari…” France akadakia.
Safari ikaendelea…
Ilikuwa ni safari ndefu, huku wakiipita mikoa ya Shinyanga, Tabora, Singida na hatimaye walipofika jijini Arusha kunako majira ya saa saba za usiku. Hawakupenda kulala njiani kwa kuhofia usalama wa watu wale, ukizingatia walikuwa watu wa hatari waliokuwa na silaha. Baada ya kufika,wakafikia kwenye nyumba ya Paul Rugoye iliyoko eneo la Kijenge.
Ni nyumba iliyotumika kuhifadhi magari yake, na pia kama gereji, ambapo haikuwa rahisi kwa mtu yeyote kugundua kama kulikuwa na watu waliofikia pale, kwa sababu ilikuwa imezungukwa na uzio madhubuti wa michongoma.
Kwa kuficha uovu wake, mbali na nyumba iliyokuwa Kijenge, Paul alikuwa anamiliki nyumba nyingine ya kifahari iliyo eneo la Sakina, sehemu alipokuwa anaishi na familia yake. Hivyo basi, vijana, Pierre , Jean na France wakafikia ndani ya nyumba ile na kukabidhiwa vyumba maalum vya kupumzika ili kuondoa uchovu wa safari ile ndefu.
Lakini kabla ya kupumzika, wakiwa ni watu wa kazi, wakaanza kuzichambua silaha zao na kuzifanyia usafi!
Ama kweli vijana wale walikuwa wamejindaa vya kutosha, kiasi cha kuweza kupambana na vyombo vya dola. Walipomaliza kuweka kila kitu sawa, wakalala kuutafuta usingizi ili kesho yake waanze kazi rasmi!
********
Ndani ya jiji la Mwanza hali ilikuwa tofauti kidogo, kwani utingo wa gari aina ya Mitsubishi Fuso, Cosmas Kishoka, lililiowasafirisha vijana, Jean, Pierre na France, kutoka Rusumo mpaka jijini Mwanza, hakuwa na imani zaidi ya kuwa na wasiwasi nao. Hata baada ya kushuka na kupanda gari jingine aina ya Ranger Rover, na kupotea machoni mwao, roho yake ilikuwa bado ikimuhimiza kufanya jambo. Ni kujua watu wale walikuwa na agenda gani ya siri!
Akiwa na dereva wake, Anton Mjivumi, walikwenda kulipaki gari lao eneo la Nyamagana, jirani na Uwanja wa Mpira wa Miguu wa Nyamagana, halafu wakaagana kila mmoja akaelekea nyumbani kwake kupumzika. Ni baada ya kutoka safari ile ya mashaka, ambayo kila mmoja hakujua ina siri gani ndani yake kutokana na kulipwa fedha nyingi.
Basi jioni yake ilimkuta utingo Cosmas akiwa ndani ya baa ya Florida Inn, iliyoko mtaa wa Kaluta, alipokwenda kujiburudisha kwa kujipatia bia moja mbili tatu, ikiwa ni baa aliyoizoea sana , pamoja na kukutana na marafiki.
Cosmas aliendelea kunywa taratibu na jamaa zake huku wakiongea maongezi ya kimaisha kwa ujumla,au hata masuala mengine ya ujana kwa kiasi fulani. Hata hivyo Cosmas akajikuta akielezea juu ya ile safari yao ya kutoka Rusumo, Ngara, hadi pale jijini Mwanza, wakiwa na wale watu watatu, ambapo yeye aliwaita wa ajabu ajabu. Alieleza kirefu huku wenzake wakimuuliza maswali kadhaa kutikana na watu hao waliotoka nchini Rwanda kwa njia ya siri!
Mmoja kati ya watu hao, aliokluwa anakunywa nao, ni kijana mtanashati, Frank Mbuga. Huyu hakuna mtu aliyekuwa anajua anafanya kazi gani, zaidi ya kumwona akitanua.
Ni kwamba alikuwa ni Afisa Usalama wa Taifa, ambaye alianza kuzichekecha habari zile na kuziona zilikuwa na umuhimu wa hali ya juu kiusalama juu ya watu wale. Kwa vile walikuwa wanafahamiana, Frank akamwomba Cosmas wakutane faragha, ili wazungumze suala lile. Cosmas hakubisha, wakatoka nje ya baa ile na kusimama sehemu ya kupaki magari, kando ya barabara mtaa wa Kaluta.
“Samahani Cosmas kwa kukutoa huku nje…” Frank akamwambia.
“Ah, usijali sana braza, ni mambo ya kawaida tu,” Cosmas akasema huku akiwa na hamu ya kutaka kujua alichomwitia.
“Unajua wewe na mimi tumefahamiana kwa muda mrefu sasa…”
“Ni kweli kabisa…”
“Na kazi ninayoifanya unaifahamu.”
“Ndiyo…nasikia nasikia ni Afisa Usalama wa Taifa kama sijakosea…”
“Hujakosea!” Mbuga akamwambia na kuendelea. “Ndiyo maana nikakuita hapa nje ili unisaidie jambo moja muhimu sana.”
“Jambo gani hilo ?”
“Ni juu ya ile habari uliyokuwa unasimulia mle ndani kuhusu wale watu watatu mliotoka nao kule Rusumo, Ngara, na kuja nao hapa Mwanza…” akasema Frank Mbuga.
“Oh, kumbe ni jambo hilo …niulize tu.”
“Vizuri sana . Hivi wale watu watatu unaohisi ni Wanyarwanda ni kweli?”
“Ndiyo. Nahisi hivyo kutokana na lugha waliyokuwa wanaongea,
“Cosmas akasema na kuendelea. “Ni kinyarwanda na kifaransa, na hiyo nilijua kwa sababu mimi kikabila ni Muha wa Kigoma. Hivyo lugha waliyoongea inafanana na ya kwetu!”
“Mliwachukuwa sehemu gani?”
“Tuliwachukuwa eneo la mpakani, Rusumo, kama kilometa tatu hivi kutoka mpakani.”
“Ina maana mliwapa lifti?”
“Hatukuwapa lifti, bali dereva wa gari letu ndiye aliyekodiwa na mtu mmoja tajiri, wa Arusha, ili awachukuwe na kuwafikisha hapa Mwanza. Sisi tulikuwa tumetokea nchini Rwanda kupeleka mzigo wa mchele kutoka Kahama, ambazo ndizo shughuli zetu.”
“Unamfahamu huyo mtu aliyemkodi dereva wako?” Frank akaendelea kumuuliza.
“Kwa kweli simfahamu…lakini ni tajiri kutoka jijini Mwanza. Baada ya kufika hapa Mwanza, wakapanda gari jingine aina ya Ranger Rover, ambayo ni ya kampuni ya kuhudumia watalii kwa jinsi nilivyoiona. Walipopanda tu wakaondoka mara moja bila kuongea lolote la ziada…”

“Je, wakati wakiwa ndani ya gari lenu uliwaona wakifanya nini mpaka ukawatilia mashaka?”
“Niliwasikia wakiongea lugha yao , ambayo mimi naifahamu. Na mara nyingine wakisoma ramani ya mji wa Arusha, na pia walikuwa na mizigo, mabegi kila mmoja na la kwake!”
“Makubwa!” Frank akasema. “Mimi nawatilia masghaka watu hao! Ni kwa nini waingie hapa nchini kinyemela bila kufuata utaratibu?”
“Ndiyo maana na mimi nikawa na wasiwasi mkubwa!”
“Basi, nashukuru sana Cosmas, itabidi nizifanyie kazi habari hizi!”
Baada ya kumaliza mazungumzo yao wakarudi ndani ya baa na kuendelea na vinywaji. Frank akawa ameyahifadhi yote kichwani mwake, hakupenda kufanya mzaha. Aliona ni vyema habari zile azifikishe Makao Makuu ya Usalama wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ili waweze kuchukuwa tahadhari na watu wale, ambapo hata yeye hakujua waliingia nchini kwa madhumuni gani! Hivyo Frank hakuendelea kukaa pale Florida Baa, bali aliaga na kuondoka akiwa amepanga ni lazima atoe taarifa usiku uleule bila kuchelewa!
Ndiyo. Aliamua kumpigia simu Mkuu wa Usalama wa Taifa, Brigedia Matias Lubisi, ili awe na taarifa hizo mapema iwezekanavyo ukiwa ndiyo utaratibu wao wa kufikishiana kila taarifa wanazozipata. Baada ya kutoka nje, Frank akaliendea gari lake aina ya Toyota Sprinter, lililokuwa sehemu ya maegesho.
Akapanda na kuondoka katika ofisi zao za Mwanza, ambazo ziko ufukweni mwa Ziwa Victoria , mkabala na Bandari ya Mwanza na siyo mbali sana na Makao Makuu ya Polisi, Mwanza, na Kituo Kikuu cha Polisi. Ni ofisi zilizoko katika jengo la kizamani la ghorofa tatu, lililojengwa kando ya majabali makubwa ya mawe yaliyofanya mandhari ya sehemu ile ivutie na kuonekana kama yalipangwa.
Frank alipofika akalipaki gari lake na kushuka. Halafu akaelekea ndani ya jengo lile na kupandisha ngazi hadi katika ghorofa ya pili ilipo ofisi yake. Alipoufungua mlango tu, akapokewa na ukimya wa pekee kwa usiku ule hadi alipokaa kwenye kiti chake.
Mbele yake palikuwa na simu mbili, moja ya mawasiliano ya ndani tu, na ile nyingine ya kutoka nje. Kwa vile alikuwa ameamua kumtafuta mkuu wake, akachukuwa mkonga wa simu na kumpigia ukizingatia sehemu ile ndiyo aliyoiona bora zaidi.
“Haloo…Matias Lubisi anaongea…” Brigedia Lubisi akaipokea.
“Mkuu…ni mimi Frank Mbuga…naongea kutoka jijini Mwanza.”
“Oh, Mbuga…habari za huko?”
“Habari ni nzuri mkuu...”
“Ndiyo, naona umenipigia simu muda huu, bila shaka kuna chochote!”
“Ndiyo mkuu, nimekupigia simu usiku huu, ili nikujulishe taarifa muhimu ambazo nimezinyaka hapa Mwanza.”
“Ni taarifa gani hizo?”
“Nimekutana na kijana mmoja, ambaye ni utingo wa magari makubwa ya mizigo...” Frank akamwambia yote aliyoelezwa na kijana Cosmas. Halafu akamalizia:
“Hivyo basi, kuna watu watatu wameingia hapa nchini wakitokea nchini Rwanda ambao hawajulikani wamekuja kufanya nini!”
“Nashukuru sana kwa kunipa taarifa hizo, tutazifanyia kuanzia kesho!” Brigedia Matias Lubisi akasema baada ya kumwelewa vizuri Frank Mbuga.
“Haya mkuu…usiku mwema!” Akamaliza Frank.
Hakika roho yake ilisuuzika baada ya kuzifikisha habari zile muhimu!
********
Brigedia Matias Lubisi, Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, alikuwa amekaa zaidi ya nusu saa ndani ya ofisi yake asubuhi ile. Alikuwa akitafakari jambo lile zito ambalo lilitakiwa kufanyiwa ufumbuzi wa kina na kwa haraka ukizingatia alikuwa ni kiungo muhimu katika idara ile. Ni kuhusu ile simu aliyopigiwa usiku wa jana kutoka jijini Mwanza, na Frank Mbuga. Kwa upande wake aliona kuwa taarifa ile siyo ya kupuuza, hivyo akaona ni vyema atayarishe vijana wake wa kazi aliokuwa anawaamini iliwafuatilie kadhia ile jijini Arusha!
Ingawa siku ile ilikuwa ni ya Jumamosi, na ni ya mapumziko, ilimbidi Brigedia Matias Lubisi kwenda ofisini kuweza kupanga mikakati ya kazi ile. Pia, alimtaarifu Katibu Muhtasi wake, Bi. Mary, aweze kufika kazini kutokana na dharura ile. Naye hakupinga akafika ofisini kama kawaida na kusubiri maelekezo. Hakika Bi. Mary alikuwa mwanamke shupavu, aliyekuwa akikutana na misukosuko mingi hasa zinapotokea kazi za dharura kama zile ambapo inabidi awepo kazini. Tuseme alikuwa mtu mzoefu sana ambaye hakuchoka wala kukata tamaa
Brigedia Matias Lubisi alikuwa mtu mchapakazi ambaye hakupenda kupitwa na taarifa zozote anazopata, ambazo zinaweza kuhatarisha Usalama wa Taifa kwa ujumla. Yeye alichaguliwa kujiunga na idara ile baada ya kupitia mafunzo maalum ya kijeshi, na pia kulitumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania .
Ni baada ya utendaji wake mzuri ndipo alipohamishiwa katika idara ile. Ingawa alikuwa na umri wa miaka 53 lakini alionekana bado kijana kutokana na kuutunza mwili wake kwa kufanya mazoezi mara kwa mara. Kitu uzembe kilikuwa mwiko kwake!
Kwa muda wote aliokuwa amekaa pale ofisini, aliamua kumteua kijana James Upele, kuifanya kazi ile ya kufuatilia taarifa zile, akishirikiana na mwanadada, Sajini Sofia Mlanzi. Hao ni wapelelezi mashuhuri aliowaamini! Hivyo hakupoteza muda akabonyeza namba kumpigia Luteni James, ambapo alimpata:
“Mkuu…Luteni James hapa…” upande wa pili ukasema.
“Lubisi hapa…habari za asubuhi.”
“Nzuri mkuu…naomba maelekezo…”
“Maelekezo ni kwamba nakuhitaji ofisini muda huu…na kama una ratiba nyingine kwa sasa uiache kwanza, kwani kuna jambo la dharura limetokea, unanipata?”
“Nimekupata Mkuu na hapa niko timamu!” Luteni James akasema kwa nidhamu ya hali ya kikazi.
“Usikawie tafadhali!” Brigedia Matias Lubisi akasisitiza na kukata simu.
Baada ya kutoa maelekezo yale, Brigedia Matias Lubis akabaki ndani ta ofisi yake akimsubiri James, na pengine akiliwazwa na runinga iliyokuwa kwenye kona, ambayo ilikuwa ikiendelea na matangazo yake.
Ofisi za Idara ya Usalama wa Taifa ziko eneo la Upanga, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es Salaam , ikiwa ni sehemu tulivu sana . Ni ndani ya jumba la ghorofa nne, ambalo kwa mtu wa kawaida asingeweza kujua kama ilikuwa ni ofisi zaidi ya makazi ya mtu. Basi, ofisi ya Brigedia Matiasi Lubisi ilikuwa katika ghorofa ya tatu.
********
Hakuna kitu kilichomchanganya Luteni James kama kile, kwani mipango yake aliyokuwa amepanga kwa siku ile ya Jumamosi ilikuwa imeharibika, baada ya kuitwa na mkuu wake wa kazi. Siku hiyo ya aina yake, James alikuwa na ahadi ya kukutana na mchumba wake, Diana, mwanadada mrembo wa kutamanisha, ambapo walikuwa wamepanga kwenda kustarehe katika ufukwe wa Coco , Oysterbay, baada ya kutengana kwa muda mrefu ukizingatia alikuwa masomoni.
Basi, siku hiyo, kijana huyo mtanashati, Luteni James alikuwa na raha ya pekee, sasa mpango mzima umetibuka. Ni Diana Msofe, msichana mwenye umri wa miaka 26, kwa muda mrefu alikuwa anasoma kwenye Chuo Kikuu cha Sokoine, Morogoro, akisomea Uchumi. Kwa hivyo ulikuwa ni muda muafaka wa kustarehe, kubadilishana mawazo, pia kukumbushana mengi ya zamani, na kupanga mipango ya kufunga ndoa.
Baada ya kupigiwa simu, Luteni James aliingia maliwatoni kuoga, na alipomaliza akarudi chumbani na kuvalia nadhifu. Kisha akatoka nje ya nyumba yake aliyokuwa anaishi eneo la Oysterbay. Akaliendea gari lake aina ya Toyota Civa, lililokuwa ndani ya banda na kuondoka nalo kuelekea ofisini. Haikumchukuwa muda mrefu akafika ofisini na kuliegesha sehemu ya maegesho. Kwa ujumla sehemu yote ilikuwa kimya kabisa, ukizingatia ilikuwa siku ya Jumamosi. Akashuka na kuliendea lile jengo la ofisi na kupandisha ngazi kuelekea katika ghorofa ya tatu.
Luteni James alifika kwenye ofisi ya Katibu Muhtasi, Bi. Mary, ambayo ilikuwa ni ya mwanzo kabla hujafika kwa mkuu wao, Brigedia Matias Lubisi. Ndani ya ofisi ile akamkuta akichapa kazi kwenye kompyuta, na alipoinua kichwa chake akamwona ni James akiingia kwa hatua za taraibu. Akaacha kuchapa na kumwambia: “Karibu James…”
“Ahsante…za saa hizi dada Mary…” James akasema.
“Nzuri kaka James…karibu.”
“Natumaini bosi yupo…”
“Ndiyo, anakusubiri…”
Luteni James akagonga mlango na kuingia ndani ya ofisi ya Brigedia Matias Lubisi. Akamkuta amekaa katika kiti cha mzunguko akimsubiri yeye, na kama kawaida akamsabahi na kukaa kwenye kiti kilichokuwa mbele yake wakawa wanatazamana.
“Karibu James...” Brigedia Matias Lubisi akamwambia huku akimwangalia kupitia chini ya miwani yake aliyovaa.
“Ahsante mkuu...” Luteni James akasema anagali bado amesimama.
“Keti tafadhali...”
Luteni James akavuta kiti na kukaa wakitazamaba sambamba na mkuu wake.
“Usishangae kukuita ghafla ofisini James...”

“Hapana, siwezi kushangaa, hiyo ni moja ya kazi zetu...”
“Vizuri sana , basi, kuna jambo muhimu nataka kukueleza. Ndiyo maana nikakuita Jumamosi hii ya leo.”
“Ndiyo mkuu…nakusikiliza…”
Brigedia Matias Lubisi akamweleza yote Luteni James, juu ya kazi ile ya kufuatilia watu wale, kwa mujibu wa simu aliyokuwa amepiga Frank Mbuga, kutoka jijini Mwanza.
Halafu akamalizia kwa kusema: “…Sasa nakutuma kazi hiyo ya kufuatilia watu hao walioingia hapa nchini kinyume cha utaratibu, ambao wametokea nchini Rwanda , kupitia njia za panya, mpakani Rusumo, Ngara, kuelekea Arusha. Sisi tukiwa ndiyo tunashughulika na Idara ya Usalama wa Taifa, ni budi kulifuatilia jambo hili kwa kina. Inawezekana ikawa ni vinara wa magenge ya uhalifu waliojipenyeza kuja kufanya hujuma kadhaa ndani ya nchi yetu yenye Amani na utulivu!”
Brigedia Matias akameza mate na kuendelea: “Safari ya kwenda Arusha mtaongozana na Sajini Sofia Mlanzi, ambaye naye yuko njiani kuja hapa ofisini. Kwa hivyo unatakiwa ujiandae, na kuhusu masurufu ya safari yanaandaliwa na ofisi ya fedha, na mhasibu nimeshamtaarifu, sijui umenipata?”
“Nakupata mkuu…” Luteni James akasema na kuendelea. “Tena nimefurahi baada ya kunishirikisha na Sajini Sofia . Sofia ni askari mzuri aliyenisaidia katika operesheni nyingi sana . Ukweli ni kwamba nimeridhika!”
“Nashukuru kwa hilo . Basi, usafiri wa ndege utakuwepo, ambao ni wa ndege ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania . Mtakapofika Arusha mtapokewa na Meja Bombe, ambaye atawapa maelekezo yote. Pia, mtakuwa chini yake mtakapokuwa pale Arusha. Hivyo nawatakia safari njema, isipokuwa tuwe tunawasiliana mara kwa mara kwa kila hatua zinavyokwenda. Na hiyo ni kwa ajili ya usalama zaidi!” Akamaliza Brigedia Matias Lubisi.
“Ndiyo mkuu…yote nimeyasikia. Kilichobaki ni utekelezaji tu,” Luteni James akamaliza, kisha akamuaga mkuu wake na kuelekea ofisini kwake.
Baada ya kuingia ofisini na kukaa tu mwanadada, Sajini Sofia Mlanzi akagonga mlango na kuingia. Moja kwa moja akaelekea kwenye kiti kimojawapo na kukaa huku akionyesha sura ya tabasamu kama kawaida yake.
“Ndiyo mkuu…kumekucha…” Sajini Sofia akamwambia.
“Na kweli kweli kumekucha Sofia ….natumaini na wewe umekurupushwa kama mimi.”
“Ni kweli nikumekurupushwa…”
“Basi ndiyo hivyo, si unajua ndiyo tulikuwa tunajiandaa kwa kuianza wikiendi? Tena mbaya zaidi nilikuwa na miadi ya kukutana na mchumba wangu, Diana, tukapunge upepo ufukwe wa Coco , Oysterbay. Si unajua kwamba hatujaonana naye muda mrefu?” Luteni James akamwambia Sajini Sofia.
“Oh, pole sana mkuu…”
“Nimeshapoa…tupange mipango yetu ya safari…” Luteni James akasema huku akimwangalia Sofia kwa makini, akiamini kwamba kweli alikuwa mwanamke wa shoka aliyepangwa naye kazi.
Ni mwanamke mrembo aliyeumbika kike kwa kila kiungo chake. Alichaguliwa kujiunga na Idara ya Usalama wa Taifa baada ya kumaliza mafunzo maalum ya kijeshi. Kielimu alikuwa amehitimu kidato cha sita katika moja ya shule za Sekondari hapa nchini. Yeye hakuwa mwanamke legelege, alikuwa mkali katika mapigano ya aina mbalimbali aliyofundishwa chuoni. Kiumri alikuwa na umri wa miaka 28 hivi, akiwa bado hajaolewa!
Ndiyo. Luteni James aliridhika kuwa naye!
Kwa upande wa Luteni James Upele, alikuwa bado kijana, mwenye umri wa miaka 35 hivi, ambapo alichaguliwa kujiunga na idara ile baada ya kufanya vizuri katika mafunzo ya kijeshi, pia alikuwa na elimu ya kidato cha sita. Mbali ya hayo alikuwa mkali katika sanaa ya mapigano kama , Judo na Kareti, na utumiaji wa silaha za kila aina. Alikamilika katika kila idara kiasi cha kufanya awe bidhaa muhimu sana.
Luteni James na Sajini Sofia wakapanga mipango yao ya safari ya kwenda Arusha hapo kesho yake. Wakaagana na kuahidiana kukutana kesho yake. Hata hivyo, James hakwenda nyumbani kwake kwa ajili ya maandalizi, isipokuwa aliamua kuelekea Kinondoni Mkwajuni, nyumbani kwa mchumba wake, Diana Msofe, kwani walikuwa wameahidiana kukutana jioni ile ya Jumamosi.
Ni Jumamosi ya aina yake!
********
Saa nane za mchana, Luteni James alisimamisha gari nje ya nyumba ndogo iliyokarabatiwa vizuri. Ni moja kati ya nyumba zilizokuwa za Shirika la Nyumba la Taifa zilizouzwa, ambapo ndipo alipokuwa anaishi Diana Msofe. Baada ya kushuka garini akaelekea ndani ya nyumba ile, ambapo mlangoni alikutana na Diana aliyekuwa anakwenda kumpokea.
“Oh, karibu sana James…” Diana akasema huku akimwewesa.
“Ahsante sana Diana…” James akasema huku akitabasamu.

“Nilifikiri hutatokea kwa vile ahadi yetu haikuwa muda huu.”
“Ni kweli Diana…” James akasema huku akiingia pale sebuleni na kukaa katika kochi dogo.
“Kulikoni?” Akauliza Diana.
“Kilichonifanya nichelewe, ni kwamba wakati wanajiandaa kuja huku, nikaitwa na Bosi wangu, mzee Matias Lubisi…”
“Mh, Jumamosi hii?”
“Ndiyo hivyo tena…ni kazi!”
“Aisee…kuna nini tena?” Diana akauliza huku akianza kuwa na wasiwasi.
“Ni mambo ya kikazi tu. Ninasafiri kwenda Arusha kama unavyojua kazi zetu…”
“Ina maana hata miadi yetu ya leo ndiyo basi tena…haitowezekana?”
“Itabidi iwe hivyo mpenzi. Vumilia tu, nitarudi na kukutana tena.”
“Ni sawa…na hiyo ni moja ya shughuli za kikazi,” Diana akasema huku akimkumbatia James.
“Nashukuru umeelewa hilo …” James akamwambia huku akimfuata machozi mchumba wake Diana.
Ingawa Diana hakuifurahia safari ile, James hakujali sana . Ilikuwa ni wajibu wake na nilazima atekeleze. Basi kilichofuata pale, Diana akamtayarishia chakula kizuri ambacho walikula wote kama wapenzi wawili, kisha wakaendelea kunywa vinywaji laini huku wakiongea hili na lile, hadi ilipotimu saa tatu za usiku, ndipo James alipoondoka kwenda kujitayarisha kwa safari ya kwenda Arusha.
Baada ya kufika nyumbani kwake, Oysterbay, James akaanza kupanga nguo zake chache na kuziweka ndani ya begi, na pia akachukuwa vifaa vidogo vya upelelezi, pamoja na bastola yake ambavyo vyote alivihifadhi vizuri. Alipomaliza kupanga kila kitu, James akaingia bafuni na kujimwagia maji ya baridi. Alipomaliza akaingia chumbani kwake kulala, kuutafuta usingizi uliokuwa mbali…
********
Ndani ya jiji la Arusha, kwenye nyumba ya Paul Rugoye, eneo la Kijenge, vijana watatu, Jean, Pierre na France, walikuwa wameamka asubuhi na mapema ikiwa ni siku ya pili yake tokea wafike pale. Baada ya kuamka wakafanya mazoezi ya viungo katika sehemu ya nyuma ya nyumba ile, ambapo ilikuwa siyo rahisi kuonekana, ikiwa ni mahali ambapo walionyeshwa na mwenyeji wao Paul Rugoye, kabla hajaondoka usiku, kuelekea nyumbani kwake, Sakina, na kuahidiana kukutana asubuhi tayari kwa kupanga mikakati ya kazi inayowakabili.
Baada ya kumaliza kufanya mazoezi yao , wakaingia bafuni na kuoga, katika mabafu yaliyokuwa mlemle ndani. Wakati wote huo Paul alikuwa ameshafika kutoka nyumbani kwake, akakuta vijana wake wameshamaliza kuoga, na wanamsubiri yeye ili awape maelekezo zaidi. Vijana wote watatu walikuwa wamekaa katika chumba kimoja kilichokuwa kama ukumbi mdogo na mbele yao pakiwa na runinga kubwa wakiangalia, na pia walikuwa wakifungua kinywa kwa chai nzito na mapochopocho waliyoletewa na Paul asubuhi ile.
Kamwe, Paul hakupenda vijana wale waonekane nje na mtu yeyote zaidi ya mlinzi mmoja wa pale, aliyekuwa ameshapewa karipio kali kwamba asieleze chochote anachokiona ndani ya nyumba ile, zaidi ya kunyamaza. Baada ya kumaliza kufungua kinywa, ndipo Paul na vijana wake wakaamua kukaa kikao ili kupanga cha kufanya, yeye Paul akiwa ndiye kiongozi na mwenyeji wao jijini Arusha.
“Ndiyo ndugu zangu…natumaini mambo shwari sasa…”
“Mambo ni shwari. Tunachosubiri ni kazi tu!” Kijana Pierre akasema.
“Ni kweli, tupe kazi!” Akadakia Jean.
“Tupe kazi!” Akaongeza France .
“Hakika mnanipa moyo kuwa mna hari ya kazi. Sasa tupange cha kufanya. Kazi yenyewe itaanza leo jioni, na mpangilio wake utakuwa kama ifuatavyo. Mimi nitaondoka na wewe Pierre kuelekea eneo la Njiro, ambapo ndipo walipopewa hifadhi watu wetu tunaowatafuta, Roman, Teobale na Laurent. Hivyo basi, nyie France na Jean mtasubiri humu ndani kama watu wa akiba, sisi tutaenda kuifanya kazi hiyo ukizingatia mimi ni mwenyeji na mtu tajiri na ninayejulikana, siyo rahisi kushtukiwa wala kutiliwa mashaka. Sijui mnanipata?”
“Mpango wako ni mzuri kama unavyosema. Na kiusalama siyo vizuri tukaongozana wote,” Kijana Pierre akasema.
“Hakuna tatizo,” Jean naye akasema.
“Ulivyopanga ni sawa mkuu!” Akaongeza France . “Tuko kwa ajili ya kazi!”
“Ni vizuri sana kama mmenielewa,” Paul Rugoye akamaliza kusema.
Halafu wakaendelea kupanga mikakati yao huku wakipitia vielelezo muhimu, na pengine walikuwa wakisafisha silaha zao walizotoka nazo nchini Rwanda , na kuzipangilia katika mpango unaotakiwa. Baada ya kumaliza wakabaki wakiangalia runinga angalau kupoteza muda, ukizingatia walikuwa na muda mrefu sana wa kukaa ndani ya nyumba ile kwa kukwepa kuonekana!
********
Hali ya hewa ilikuwa ni shwari huku kijua cha asubuhi kimechomoza upande wa Mashariki mwa jiji la Dar es Salaam . Kwenye Uwanja wa Ndege wa Jeshi la Anga, Ukonga, ndege ndogo aina ya ‘Twin Otter’, ilikuwa imepaki tayari kwa safari ya kwenda Arusha. Kando yake alionekana Rubani Mkuu akiikagua ndege ile sehemu zote kwa kuizunguka na Msaidizi wake naye alikuwa akimfuatilia kwa makini. Asubuhi hiyo iliwakuta Luteni James na Sajini Sofia wakiwa pale uwanjani tayari kwa safari ya kwenda Arusha katika kazi ile maalum. Baada ya muda wakapanda ndani ya ndege pamoja na abiria wengine na rubani akaiwasha na kuiondoa kwa mwendo wa taratibu kuelekea katika barabara yake ya kurukia, na pia akiwasiliana na waongoza ndege waliokuwa katika chumba cha mawasiliano.
Halafu akaongeza mwendo na kuipeleka kwa kasi na hatimaye kuirusha angani kuelekea Arusha. Wakati wote huo, James na Sofia walikuwa kimya kabisa hadi ndege ile ilipotulia angani. Hata hivyo haikuwa safari ya kuchosha sana hadi walipofika Arusha na kutua salama katika uwanja wa ndege wa Arusha. Pale wakapokewa na Meja Bombe, aliyefika pale kwa gari aina ya Land Rover 110 ya Idara ya Usalama wa Taifa, pamoja na dereva, kijana Peter. Peter akaenda kuwapokea ile mizigo yao baada kushuka ndani ya ndege ile ya jeshi. Wote wane wakapanda ndani ya gari na kuondoka kuelekea katikati ya jiji, walipokuwa wametayarishiwa vyumba vya kulala, na pia kupitia ofisini ili kupanga mikakati ya kazi ile.
Dereva akaliondoa gari na kuelekea moja kwa moja hadi katika ofisi za Idara ya Usalama wa Taifa zilizoko Barabara ya Boma, katikati ya jiji la Arusha. Baada ya kufika, dereva akaliingiza gari kwa kupitia getini kwa kuifuata barabara ndogo ya kokoto iliyozungukwa na miti pande zote kuelekea katika jengo la ofisi ile iliyokuwa umbali wa mita thelethini kutoka getini. Kama yalivyo majengo yaliyojengwa zamani, lilikuwa ni jengo la ghorofa moja lililojificha kwa kuzungukwa na miti ya aina mbalimbali iliyofanya mandhari ya pale ipendeze. Isitoshe palikuwa na waya uliokuwa na seng’enge.
Kwa ujumla eneo lote lilikuwa kimya kabisa, hasa ukizingatia ilikuwa siku ya Jumapili. Baada ya dereva kulipaki gari, wakashuka na kuelekea katika ofisi ya Meja Bombe, iliyokuwa katika sehemu ya chini, tayari kwa kupanga mikakati ya kazi. Wakakaa katika viti vilivyokuwa mbele ya meza ya Bombe na kuanza kumsikiliza.

“Karibuni Arusha…” Meja Bombe akawaambia.
“Ahsante mkuu!” Luteni James akasema.
“Ahsante Mkuu…” naye Sajini Sofia akasema.
“Ni matumaini yangu nyote mnaelewa kilichowaleta hapa Arusha…”
“Ndiyo mkuu, tunaelewa. Ni majukumu ya kazi!” James akasema.
“Basi, ndiyo kama mlivyosikia. Ni kwamba kuna watu wameingia hapa Arusha kinyemela bila kujulikana, hivyo inawabidi kufanya upelelezi wa kina, ukizingatia hatuwafahamu watu hao, na sehemu walipofikia. Cha muhimu ni kuwa makini sana huku mkijua kwamba mnapambana na watu msiowajua. Ili nisiwachoshe mpaka muda wa kupumzika, napenda kukutaarifu James, kuwa umepangiwa kufikia nyumba ya wageni ya Serena Inn …” akanyamaza kidogo huku akiwaangalia.
“Kila kitu kimeshalipiwa. Wewe Sofia utafikia katika hoteli ya Victoria Villa, iliyoko mtaa wa Bondeni, na mtakapotoka hapa, dereva atawapeleka…” Meja Bombe akamaliza kusema.
James na Sofia wakamwelewa. Halafu wakaondoka kuelekea katika hoteli waliyopangiwa ili kupumzika na kujiandaa kwa kazi ile nzito!
********
Jioni ya siku ile, majira ya saa mbili za usiku, Paul na Pierre walikuwa wameshajiandaa vya kutosha, tayari kwa safari ya kwenda eneo la Njiro. Walivalia nadhifu, mavazi maalum, ambayo kwa mtu wa kawaida angeona kama ni suti, kumbe ni nguo zilizokuwwa zimebeba silaha ndani yake, kama bastola zilizosheni risasi, sumu kali, visu maalum vya kijasusi, na hata mikasi ya kukatia waya. Ni vifaa ambavyo hutumiwa mara nyingi na Majasusi!
Hatimaye wakapanda gari dogo aina ya Toyota Corolla, ambalo ni kati ya magari kadhaa aliyokuwa anamiliki Paul. Baada ya kupanda, wakaondoka ndani ya makazi yale, dereva akiwa ni yeye mwenyewe. Ndani ya nyumba waliachwa Jean na France, wakisubiri kuletewa taarifa za upelelezi ule. Kama kawaida eneo lile la Kijenge Maghorofani palikuwa kimya kwa muda ule, hasa ukuizingatia ni sehemu waliyokuwa wanakaa watu wastaarabu, hivyo Paul akaendesha gari kuelekea Njiro, ambapo hapakuwa mbali sana . Ni umbali wa kilometa nne na nusu hivi kutoka Kijenge.
Dakika ishirini baadaye wakafika Njiro, huku giza lilishaingia, hivyo wakalipaki gari lao katika maegesho nje ya baa moja wakionekana kama watu wa kawaida tu waliokwenda kustarehe. Eneo lile la Njiro lilikuwa limejengeka sana , huku sehemu kubwa ikiwa ni ya kibiashara hususan grosari nyingi za kuuza pombe. Basi, ili kuvunga wasijulikane nia yao , walizunguka na kuingia katika baa mojawapo na kunywa bia mbili tatu katika kuvuta muda.
Tena walikaa sehemu iliyokuwa na giza , kuepuka Pierre asitambuliwe, na muda wote waliokaa, walikuwa wakiangalia saa zao, kusubiri muda muafaka ufike hawakupenda kufanya kazi za kubabaisha. Ni hadi ilipotimu saa tatu za usiku, ndipo Paul na Pierre walipotoka ndani ya baa ile, ambapo wateja walikuwa ni wachache. Wakajifanya kama wanaliendea gari lao, halafu wakalipita na kuufuata uchochoro mmoja uliotokeza upande wa pili wa maduka na uzio wa nyumba za Umoja wa Mataifa, sehemu ambayo haikuwa na taa nyingi za ulinzi na kufanya pawe na giza kiasi.
Kwa usiku ule walionekana kama watu waungwana wakitazama zile nyumba zilizokuwa zimezungukwa na uzio imara wenye urefu wa futi saba kwenda juu. Ili wasijulikane nia yao , wakapitiliza hadi mwisho wa nyumba zile. Wakiwa katika mwendo wa kawaida, wakafika katika sehemu iliyokuwa na mti mkubwa wa mwembe uliokuwa umefungamana na kusababisha giza . Paul na Pierre wakasimama pale kwa muda sambamba na mti ule. Wakawa wanachunguza bila kuonekena na mtu yeyote, kwa vile walikuwa wamevalia suti nyeusi zilizofanana na giza . Wakasimama kwa muda, hadi Bw.Paul aliposema kwa sauti ndogo:
“ Pierre …”
“Mkuu!”
“Sasa tupange la kufanya!”
“Ni jambo la maana…”
“Sasa wewe utaingia ndani…”
“Hakuna tatizo…nitaingia ingawa kuna ulinzi mkali!”
“Ni sawa Pierre , jitahidi. Mimi nakusubiri hapa nje, ukichelewa sana nakufuata!”
“Hakuna shaka!” Pierre akasema halafu akapiga hatuia mbili ili ajiandae kuuruka ule uzio. Ni uzio ambao kwa mtu kama yeye haukumpa shida kwani alikuwa mtu wa mazoezi.
Baada ya kuuruka uzio, Pierre akatua ndani bila kutoa kishindo. Sehemu ile aliyotua ilikuwa imezungukwa na miti mingi iliyosababisha vivuli vya giza , ambavyo vilimsaidia sana Pierre aweze kunyata kuelekea katika nyumba zile. Na katikati yake ndipo ilipokuwa ile nyumba maalum, walipowekwa wale vijana, Roman, Teobale na Laurent. Kwa muda wote walikuwa chini ya ulinzi mkali wakilindwa usiku na mchana na walinzi maalum. Ndani ya nyumba ile palikuwa na nafasi ya kutosha iliyowatosheleza, ikiwa na kila kitu muhimu kama vile, simu, runinga na samani zilizohitajika kwa ujumla.
Hatimaye Pierree alifanikiwa kuifikia ile nyumba bila kuonekana na mlinzi yoyote, kwani alikuwa anatumia ujuzi wa hali ya juu. Akaanza kuchunguza ndani ndani, lakini hakuweza kuona chochote au hata mtu; kwani milango ilikuwa imefungwa. Pierre akasimama kwa muda bila kufanya papara, kisha akamwona mlinzi mmoja akizunguka upande wa pili bila kumwona yeye sehemu ile aliyobanisha sambamba na ukuta. Mlinzi yule aliyekuwa na koti jeusi, kofia na buti za kijeshi, akampita tu bila kumwona. Hivyo hakumkawiza, Pierre akakusanya nguvu lililompata sawia mlinzi!
Mlinzi yule akaachia mguno mdogo akaanguka chini na kupoteza fahamu kabisa. Na dakika chache akakata roho. Pierre akaisogeza ile maiti na kuisukumia katika giza lililokuwa katika bustani za maua . Tukio lile lilikuwa limefanyika haraka sana bila mlinzi mwingine kugundua. Lakini wakati Pierre amesimama pale, akijiandaa kusonga mbele, akasikia sauti za nyayo za mlinzi mwingine aliyekuwa akimsogelea. Naye akampita bila kujua kwamba Pierre salikuwa mawindoni. Ile kumpita tu, akamrukia mlinzi yule na kumkaba ipasavyo na pia kuondoka naye ili wakamhoji kule nje ya uzio alikomwacha Paul.
Pierre akaondoka naye huku akiwakwepa walinzi wengine, hadi alipofika kwenye uzio ule wa michongoma. Kwa kutumia nguvu akamrusha mlinzi nje ya uzio, ambako alipokelewa na Paul, ambaye alimlaza chini ya ule mti mkubwa wa mwembe. Pierre naye akauruka uzio na kumwendea mlinzi aliyekuwa na Paul, wakati naye alikuwa amechanganyikiwa bila kujua kilichokuwa kinaendelea; kwani baada ya kuachwa apate kupumua vizuri, aliweza kuwaona watu wawili wamemdhibiti huku wakimwonyesha bastola kumtaka asifanye fujo ya aina yoyote
“Sisi ni watu wa kazi! Tunataka utujibu maswali tutakayokuuliza!” Pierre akamwambia baada ya kumwinamia pale alipolazwa yule mlinzi.
“Nyie watu wa kazi?” Mlinzi yule naye akauliza huku macho yamemtoka pima!
“Mh, mbona siwaelewi?”
“Basi utatuelewa!” Pierre akamwambia. Halafu akamshindilia ngumi ya nguvu iliyompata barabara kwenye taya la upande wa kulia kiasi cha kutoa mlio wa kuvunjika!
“Mh, Ooohps!” Mlinzi yule akaguna baada ya kipigo kile! Ama kweli alikiona kifo kinamnyemelea!
“Wewe ni mlinzi?” Pierre akamuuliza tena!
“Ndiyo…mimi ni mlinzi…”
“Vizuri. Tunajua kwamba kuna vijana watatu waliotokea nchini Rwanda wamefikia hapa, je, ni kweli?”
“Inawewzekana…ni kitu kama hicho.”
“Tuambie wanakaa nyumba gani?”
“Mh,” Mlinzi yule akaguna na kuendelea. “Kwani wanawahusu nini jamani? Sipaswi kuwaambia!”
“Hebu tujibu, na siyo kutuuliza maswali sisi! Nilishakuonya!”
“Sasa nitawajibu nini wakati mimi sikuelewi? Kwani nyie akina nani mnaniuliza tena kibabe?”
“Hupaswi kujua!”
“Basi na mimi sijui!”
“Unaleta jeuri sivyo? Sasa mimi nakuua!” Pierre akamwambia mlinzi yule na kumwekea bastola kichwani mwake kwa kuukandamiza kwa nguvu!
“Mama yangu!” Mlinzi akasema
“Haya, sema!” Pierre akasisitiza!
“Oh, ngoja niseme!”
“Ni kweli kwamba…” mlinzi yule akaanza kusema kwa sauti ndogo. Lakini kabla hajaendelea zaidi, gari moja likatokea na kuelekea katika upande waliokuwa wao huku likimulika taa zenye mwanga mkali. Sehemu ile palikuwa na barabara ndogo iliyokuwa inakatiza kutoka katika nyumba ile, kitu ambacho tokea mwanzo, Paul na Pierre hawakugundua!
“Mh, imekuwaje tena?” Pierre akauliza huku akisitisha zoezi lile huku akimdhibiti yule mlinzi kwa kumvutia nyuma ya mti ule wa mti wa mwembe!
“Ni gari linakuja huku! Ni bora tujifiche nyuma ya huu mti…atatuharibia kazi!”
Lile gari lililokuwa kama linapitiliza, likapunguza mwendo na kuwafuata pale walipokuwa, Paul na Pierre, wakiwa na mlinzi. Wala gari halikupunguza mwanga wa taa zake, kuashiria kuwa dereva yule alikuwa amewaona na kuwashtukia baada ya kumbana mlinzi aliyekuwa amevaa sare za kazi.
“Tumeshtukiwa Pierre!” Paul akamwambia huku amekamata bastola!
“Ni kweli!” Akadakia Pierre!
“Sasa tufanyeje?”
“Tummalize huyu dereva kwani atatuharibia kazi!”
“Na huyu mlinzi je?”
“Mmalize vilevile!”
“Sawa…” Pierre akasema na kuikamata shingo ya mlinzi ambayo ilivunjika!
“Hik!” Mlinzi akaguna na kukata roho!
“Ok, sasa mshughulikieni huyo dereva!”
Pierre akaikamata vyema bastola yake na kuielekeza kwenye lile gari lililokuwa limesimama pale likiwamulika. Akafyetua risasi mbili ambazo zilimpata dereva, ambaye aliguna na kufa palepale huku akiuachia usukukani na kulalia kiti, na damu nyingi kumtoka katika jeraha la risasi zilizompata kichwani!
Baada ya mauaji yale, Paul na Pierre wakaondoka haraka sana kwa kuufuata uchochoro ule waliokuja nao. Wakaliendea gari lao katika sehemu ile walikoliacha, na kuondoka kurudi katika maficho yao Kijenge, wakati huo ikiwa imetimu saa tano za usiku. Hata hivyo Paul na Pierre hawakutegemea kama wangekumbana na kizuizi kile kilichowaharibia kazi yao ya upelelezi dhidi ya wasaliti wao!
********
Alikuwa ni kijana Deo Mshanaki, dereva gari aina ya Toyota Land Cruiser, la Umoja wa Mataifa, aliyeuawa baada ya kuwashtukia Paul Rugoye na Pierre, wakiwa wamebanisha chini ya mti wa mwembe. Hivyo basi, purukushani zile ziliwashtua wakazi wa eneo lile na kuwafanya wakimbilie, na kulikuta tukio lile la mauaji ya dereva na wale walinzi wawili waliokuwa wanalinda katika zile nyumba za Umoja wa Mataifa.
Haraka sana wakapiga simu polisi kujulisha tukio lile la kinyama. Baada ya dakika kumi na tano hivi, askari polisi wakafika pale wakiwa na magari mawili aina ya Toyota Land Cruiser wakiwa wamejizatiti kwa silaha. Pia, walikuwepo askari wengine wa Kikosi cha Mbwa, na wataalam wa picha, milipuko na alama za vidole. Wote wakashuka ndani ya gari na kulizingira eneo lile, ingawa waliotenda kosa lile walikuwa wameshaondoka kitambo!
Katika msafara ule walikuwepo viongozi wa polisi wa ngazi za juu, na pia makachero, ambao walianza kufanya uchunguzi katika maeneo mengi. Wakaokota yale maganda ya risasi mawili, yaliyofyetuliwa na Pierre na kumuua Deo. Wakachukuwa maiti ya mlinzi aliyeuawa kule ndani na kufichwa katika bustani ya maua , halafu wakaiunganisha na ile ya yule mlinzi mwingine aliyeuawa kule nje na kuachwa chini ya mwembe. Basi, maiti zote tatu zikachukuliwa na kupelekwa katika Hospitali ya Mount Meru kuhifadhiwa.
Usiku mzima askari polisi walifanya msako wa nguvu huku wakitumia mbwa wa Polisi, lakini haukusaidia kitu, kwani watuhumiwa wale walitumia usafiri wa gari. Ni hadi palipokucha, ikiwa ni siku ya Jumatatu. Hali ilikuwa ni mbaya katika jiji la Arusha, kiasi cha kuwashtua watu wengi sana . Haikujulikana kama watu wale walikuwa na maana gani, na kwa sababu gani. Mkuu wa Upelelezi akateua makachero kadhaa kufanya upelelezi dhidi ya mauaji yale, ambapo kiini chake kilikuwa hakijajulikana na Jeshi la Polisi. Wakauanza upelelezi wao eneo loa Njiro.
Jiji la Arusha halikukalika! Hali ya hatari ikanukia sehemu zote, hasa katika vitongoji, ambapo ulifanyika msako wa nguvu wa askari wa Jeshi la Polisi. Walioambulia kadhia ile ni walevi ni walevi na wauzaji wa pombe haramu za gongo na bhangi, ambao hawakuhusika na tukio lile kabisa. Wengi walikuwa ni vijana wa kijiweni, waliosombwa kwa wingi na kuzijaza mahabusu za polisi. Lakini si Paul Rugoye na vijana wake, Jean, Pierre na France waliohisiwa kufanya mauaji yale, kwani walikuwa wamejichimbia katika maficho ndani ya nyumba iliyoko Kijenge, wakiendelea kupanga mipango iliyowakabili.
Ilikuwa ni lazima waimalize kwa njia yoyote ile!
Mauaji ya wale walinzi wawili, na dereva, Deo, yalitokea usiku ule, ikiwa wapelelezi wale mahiri wa Idara ya Usalama wa Taifa, Luteni James na Sajini Sofia, wamewasili jijini Arusha. Ukweli ni kwamba yaliwashtua sana kiasi cha kujua ni kazi ya watu wale watatu waliotokea nchini Rwanda , ambao walikuwa wanawafuatilia!
Kazi ilikuwepo!

ITAENDELEA
0.jpeg
 
Simulizi : Msaliti Asakwe
Sehemu Ya Tatu (3)

Meja Bombe alikutana faragha na vijana wake, Luteni James na Sajini Sofia, ofisini kwake, na kuzungumzia suala la mauaji yale yaliyofanyika. Wakiwa wameshajua watu waliotenda unyama ule, Bombe akawahimiza wauanze upelelezi mara moja, huku akiwaambia wawe makini na watu hao hatari ambao walikuwa wanajua wanachokifanya!
Na sehemu waliyofikia haikufahamika!
Ni hatari sana kumsaka adui usiyemjua alikojichimbia!
Anaweza kukuwahi na kukulipua!
Luteni James na Sofia wakagawana kazi na kuanza upelelezi, ambapo James aliamua kuelekea Njiro Hill, katika makazi ya mashahidi muhimu, Roman, Teobale na Laurent. Nia yake ilikuwa ni kwenda kufanya mahojiano nao, ili aweze kupata mwanga na kujua pa kuanzia. Sofia yeye alipanga kuanzia kwa kuzunguka katika mitaa ya Kijenge, ambapo alihisi kuna uwezekano mkubwa ikawa wale watu hatari wamefikia kule, katika maficho ambayo hayajajulikana. Ni giza tupu!
Baada ya kupangiana majukumu, wakaachana kila mmoja akielekea uelekeo wake lakini wakiwasiliana kwa simu kadri kila hatua zinavyokwenda. Kwa kutumia usafiri wa teksi, James alielekea Njiro kama msafiri yeyote wa kawaida hadi katika nyumba za Umoja wa Mataifa. Ili asishtukiwe, akateremka mbali kidogo, na nusu nyingine akatembea kwa miguu hadi alipofika katika geti la kuingilia mle ndani.
Getini palikuwa na walinzi wawili waliokuwa na silaha, hivyo James akajitambulisha na kuruhusiwa kuingia kwenda kuwaona mashahidi wale, akielekezwa na mlinzi mmoja wao na pia Afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa. Wakafika kwenye nyumba moja iliyokuwa katikati ya nyumba nyingine. Wakaingia ndani na kukaa kwenye sofa kubwa, katika ukumbi mdogo, ambapo pale walikuwepo vijana wale, Roman, Teobale na Laurent, wakiwa wamekaa wakiangalia runinga. Ukweli ni kwamba hawakuthubutu kutoka mbali zaidi ya eneo lile, kwani walishapatwa na wasiwasi baada ya mauaji ya walinzi, na yule dereva wa Umoja wa Mataifa.
Afisa yule akamtambulisha Luteni James kwao kabla ya kuanza mahojiano. Nao wakamwelewa na kumpa fursa ya kuwahoji.
“Natumaini hamjambo…” Luteni James akawaambia huku akiwaangalia.
“Sisi hatujambo…” wote wakajibu.
“Vizuri sana , kama mlivyotambulishwa, mimi ni mpelelezi kutoka Idara ya Usalama wa Taifa. Naitwa Luteni James Upele. Ni mwanajeshi niliyefuzu…na kama sikosei na nyie ni wanajeshi!”
“Ni kweli, sisi ni wanajeshi, wapiganaji wa msituni mkuu!” Roman akasema kwa heshima ya kijeshi!
“Nasikia nyie ni wakimbizi kutoka nchini Rwanda …na mmeamua kukimbia ili kuja kujisalimisha katika Mahakama ya Umoja wa Mataifa sivyo?” James akawauliza.
“Ndiyo, tumeamua hivyo! Kumkimbia kiongozi wetu, Kanali Fabio Rushengo, baada ya kuchoshwa na sera zake za vita…” Roman akasema na kueleza mengi kwa kirefu ambapo Luteni James akamwelewa baada ya kuanikiwa uovu wake wote!
“Sasa nyie mnafikiri amefurahi baada ya nyie kumtoroka?”
“Kwa kweli hajafurahi, hasa ukizingatia tuna siri yake yake kubwa, ambayo tunatoka ijulikane wazi!”
“Basi, kuna watu watatu wameingia hapa Arusha, wakitokea nchini Rwanda . Je, inawezekana ni yeye aliyewatuma, hasa ukizingatia haya mauaji yanayotokea?”
“Ina maana Fabio ametuma watu?” Roman akauliza badala ya kujibu.
“Ndiyo. Ni hao walioua wale walinzi pamoja na dereva!”
“Mungu wangu! Atakuwa ametuma watu wake kuja kutumaliza ili tusiweze kutoa siri zake!”
“Je, unaweza kuwatambua?”
“Kwa kweli siwezi kuwatambua, kwa vile kundi letu lina watu wengi!”
“Unafikiri hapa Arusha watakuwa wamefikia wapi, au sehemu gani? Au labda wanafikia wapi, au sehemu gani? Au labda wana mwenyeji yeyote aliyewahifadhi na wao kufanya vitendo hivi bila ya kujulikana?” James akaendelea kuhoji kwa umakini wa hali ya juu baada ya kuona mahojiano yanaendelea vizuri.
“Unajua Kanali Fabio anajuana na watu wengi sana katika mtandao wake. Hivyo siwezi kujua wamefikia sehemu gani!”
“Mh, kuna kazi kubwa!” Luteni James akasema na kuendelea. “Hata hivyo inabidi mjihadhari sana na watu hao. Na sisi tunaendelea na upelelezi ili tuwadhibiti!”
“Sawa mkuu, tunawatakia kazi njema ili muweze kuwakamata!” Akamaliza kusema kijana Roman.
Baada ya kumaliza mahojiano yale, Luteni James akaondoka eneo lile kwa kutembea kwa miguu hadi alipofika katika barabara kuu ya lami inayoelekea katikati ya jiji la Arusha. Akionekana kama mtu wa kawaida tu, James akachukuwa simu yake ya mkononi na kumtafuta mwenzake, Sajini Sofia, ukizingatia walikubaliana kupigiana simu kila muda, kinachoendelea.
“Haloo…mkuu!” Sofia akaipokea. “Mambo vipi?” James akauliza.
“Uko wapi saa hizi?”
“Mimi niko eneo hili la Kijenge.”
“Na mimi niko hapa Njiro. Nimemaliza kuwahoji wale vijana, je, una lolote?”
“Ndiyo mkuu…ninalo!”
“Nimegee…”
“Kuna watu wawili nawatilia mashaka, ambao nawafuatilia…”
“Wanaelekea wapi?”
“Naona wanaelekea katika hoteli ya Mount Kijenge…na mimi nitaingia humo.”
“Ok, wewe ingia ndani na mimi nafuatilia gari ofisini. Nitakuja kulipaki nje ya hoteli hiyo, na wewe unijulishe kinachoendelea…”
“Sawa mkuu…nitafanya hivyo!”
Baada ya mawasiliano wakakata simu.
Luteni James akasimamisha teksi na kumwambia dereva ampeleke katikati ya jiji, ilipo ofisi ya Idara ya Usalama wa Taifa. Kama kawaida ili asijulikane, akashuka mbali kidogo na nusu akatembea kwa miguu na kuingia eneo la ofisi kwa kupitia upande wa nyuma. Na ile ilikuwa ni kwa ajili ya kujihadhari kama kuna mtu yeyote aliyekuwa anamfuatilia, ashindwe kugundua. Baada ya kuingia akachukuwa gari aina ya Nissan Patrol, ambayo ilikuwa na mafuta ya kutosha.
James akapanda gari na kulitia moto. Akaondoka nalo kuelekea eneo la Kijenge hadi alipofika katika hoteli ya Mount Kijenge, ambapo alilipaki sehemu ya nje, ambapo palikuwa na magari mengine ya wateja. Ni hoteli iliyokuwa na hadhi ya kitalii, yenye ghorofa saba, na imezungukwa na mandhari ya kupendeza. Pia, ilikuwa imezungukwa na miti mingi na bustani ya maua . Upande wa kusini palikuwa na bwawa la kuogelea, na baada ya kulipaki hakushuka ndani ya gari, bali alibanisha na kuanza kuwasiliana na Sajini Sofia kwa simu ya mkononi.
“ Sofia …” James akaita kwa sauti ndogo isiyoweza kusikika.
“Sema mkuu!” Sofia akasema.
“Nipe taarifa…”
“Mambo safi …nafuatilia windo langu…sijui wewe uko wapi?”
“Mimi niko nje ya hoteli…nimebanisha ndani ya gari…”
“Poa…nitakujulisha kinachoendelea…”
“Hakuna shaka…”
********
Akiwa katika upelelezi wake, Sajini Sofia aliwatilia mashaka vijana wawili ambao walishuka katika gari moja , ambalo hata hakuweza kulisoma namba zake mara moja. Ni vijana waliokuwa na maumbile ya miraba minne, huku maongezi yao yakionyesha siyo raia wa Tanzania , ingawa walijichanganya tu kwa kujifanya ni wenyeji. Vijana wale wakaingia ndani ya hoteli ya Mount Kijenge, ili kujipatia chakula na vinywaji kidogo katika kusafisha koo, na pia kuangalia mandhari.
Vijana wale walikuwa ni Jean na Pierre, waliokuwa wameshushwa na dereva wa Paul Rugoye, aitwaye Meku, ambaye hakujua kilichokuwa kinaendelea zaidi ya kuondoka zake. Walikuwa wamewaaga wenzao na kuwaahidi kurudi mapema hasa ukizingatia hoteli ile ilikuwa jirani tu na yalipokuwa makazi yao , katika nyumba ya Paul Rugoye eneo la Kijenge Maghorofani.
Baada ya vijana wale kuingia ndani ya hoteli, naye Sofia akaingia na kukaa sehemu ambayo haikuwa mbali na walipokaa Jean na Pierre, ambao walikuwa wameagiza vyakula na vinywaji. Sofia naye akaagiza kinywaji laini aina ya Malta Guinnes, na soda moja aina Pepsi cola. Akaendelea kunywa taratibu na mara nyingine akiangaza macho yake pande zote. Ukweli ni kwamba hakuna mtu yeyote aliyemshtukia kama alikuwa ni mpelelezi aliyekuwa kazini kwa muda ule!
Sajini Sofia alikuwa ni mwanamke mwenye uzuri wa asili, ambaye aliwavutia wanaume wengi sana , hasa wale wenye uchu wa kutaka kila mwanamke aliyekatiza mbele yake. Kila mmoja alipenda wae wake daima, ammliki, astarehe naye, na kumtumia apendavyo kwa kukidhi haja yake kingono kwa muda wowote atakavyo! Huo ndiyo ukweli wenyewe!
Kwa muda wote Sofia alikaa pale akiwaangalia Jean na Pierre waliokuwa wakiongea mazungumzo yaliyokuwa yakimshtua sana . Kwani walikuwa wakiongea kifaransa na Kinyarwanda kidogo, kwa kusisitiza jambo walilokuwa wanaongelea. Hata hivyo akavuta subira mpaka atakapouona mwisho wake. Lakini kadri Sofia alivyoendelea kuwaangalia watu wale, ndivyo wasiwasi ukaongezeka, kwani mbali ya kuongea, pia walikuwa wanawasiliana kwa simu zao mara kwa mara kiasi cha kuwafanya wawe bize!
Ingawa walikuwa majasusi wa hali ya juu, kamwe hakuweza kugundua kama palikuwa na mpelelezi wa Idara ya Usalama Wa Taifa, aliyekuwa jirani yao akiwachunguza. Hata hivyo, Sajini Sofia akiwa mwanamke mpelelezi anayeijua vyema kazi yake, ikambidi atumie ujuzi wake wa upelelezi aliowahi kuutumia mara kwa mara. Sofia alitambua fika kuwa sumu ya mwanaume ni mwanamke, tena mwanamke mzuri kama yeye! Basi, ili kummaliza Jean na Pierre, akapanga kama anakwenda msalani. Akanyanyuka na kuondoka huku akipita katika eneo lile walilokaa, jirani kabisa na meza yao , huku akiutikisa mwili wake teketeke, kiasi kwamba lile gauni alilokuwa amevaa liliweza kuonyesha umbile lake kwa ndani lilivyokuwa!
Ni umbile liliokuwa linavutia, lililoumbika mfano wa namba nane, ambalo wanaume, Jean na Pierre walimwona na kuridhika kweli alikuwa ni mwanamke tishio! Hasa kwa Jean, aliyekuwa amemhusudu kitambo tangia amwone. Akashindwa kuvumilia na kuendelea kumwangalia Sofia alivyokuwa anakwenda msalani akijitupa huku na kule!
Ulikuwa mtego tosha!
********
Jean aliguna na kumwangalia mwanadada Sofia . Halafu akachukuwa glasi yake ya pombe na kupiga mafunda kadhaa huku akitikisa kichwa chake na pia akitabasamu!
“Vipi Jean, mbona unaguna?” Pierre akamuuliza huku akielewa kuwa Jean alikuwa ni mdhaifu kwa wanawake, hasa anapokaa muda mrefu bila kukutana nao!
“Umekiona kile kipande cha mtoto?”
“Nimekiona…si mchezo!”
“Basi si uongo. Kimenivutia na kuamsha ashki zangu zilizokuwa zimelala!”
“Unasema kimekuvutia?”
“Haswaa!”
“Umeshaanza?” Pierre akamuuliza.
“Nimeanza nini?”
“Mambo ya wanawake tuyaache!”
“Tuyaache kivipi?”
“Si unajua kwamba tumekuja hapa kwa kazi maalium, ambayo haipaswi kufuata mengine.”
“Unachosema ni kweli Pierre . Lakini unajua tokea tutoke Kibungo , Rwanda , sijagusa kitu kinachoitwa mwanamke, na huo ni mwiko kwangu!”
“Hivyo unatakaje?”
“Nataka nikate kiu kidogo…mara moja siyuo mbaya sana !”
“Wewe unamwamini yule mwanamke?”
“Kumwamini kivipi?”
“Asiwe shushushu!”
“Hapana…hawezi kuwa shushushu. Hii ni nchi ya Amani ya Tanzania , hakuna mtu wa kuweza kutushtukia!”
“Kwa hivyo tusimtilie shaka!”
“Ni kitu kama hicho!”
“Ok, kwa vile kazi ni lazima na dawa, unaweza kujaribu bahati yako. Vilevile nahisi mwanamke yule ni malaya tu!”
“Na kweli…wala usimtilie wasiwasi, ngoja arudi nijaribu!”
“Poa tu, mimi nitakuwa mlinzi wako.”
“Hakuna shaka.”
Pamoja na kuwa na taaluma ya ujasusi, Jean na Pierre, walifanya kosa sana kumwamini Sajini Sofia. Hawakumtilia shaka kuwa ni mpelelezi, wenyewe wakavuta subira na kumsubiri palepale!
Hakika palikuwa patamu hapo!
********
Sajini Sofia alipoingia msalani akaufunga mlango vizuri kuhakikisha sauti haiwezi kutoka nje. Akachukuwa simu ya mkononi na kumpigia Luteni James aliyekuwa kule nje ya hoteli ile, amekaa ndani ya gari. Baada ya kumpata akamwambia juu ya vijana, Jean na Pierre waliokuwa ndani ya hoteli, na kumwambia akae tayari kwa kazi, kwani alikuwa na mpango wa kuwaingiza mtegoni. James akamwelewa na kumhakikishia kuwa alikuwa imara. Walipomaliza kuwasiliana, Sofia akatoka kule msalani na kurudi katika ile sehemu aliyokuwa amekaa mwanzo.
Kama kawaida, Jean akabaki akimwangalia Sofia alivyokuwa anaingia na kumsindikiza kwa macho hadi alipokaa kitini. Ukweli ni kwamba alionyesha kuwa na matamanio, kiasi kwamba Sofia alipomtupia jicho, alimkonyeza na kuonyesha ishara za kumtaka kimapenzi. Ni kitu ambacho Sofia alikitegemea, hivyo akamlegezea macho Jean bila kulaza damu, akijua alikuwa kazini.
Jean hakuvumilia, akamuaga Pierre na kunyanyuka kuelekea katika meza aliyokuwa amekaa Sofia . Alikuwa anatembea kwa mwendo wa madaha huku akijiamini sana akijua kuwa alikuwa hajashtukiwa kama yeye alikuwa jasusi aliyetumwa kikazi. Baada ya kufika akavuta kiti na kukaa huku akitabasamu, halafu akasema kwa sauti ndogo:
“Natumaini kuwa hujambo mwanamke mzuri…”
“Mi’ sijambo, sijui wewe…” Sofia akamwambia.
“Samahani naona umekaa peke yako. Unaonaje tukijiunga wote?”
“Sawa tu, karibu, hakuna wasiwasi…”
“Lakini unaonaje tukakae pale nilipokuwa mwanzo, ambapo kuna mwenzangu?” Jean akamwambia huku akimwonyesha pale alipokaa Pierre .
“Hakuna wasiwasi…” Sofia akakubali huku naye akiangalia upande ule.
“Vizuri twende,” Jean akasema, halafu akamshika mkono Sofia na kumpeleka katika ile meza yao .
Wakakaa pale na kuendelea na vinywaji. Kwa vile Jean alikuwa na usongo na Sofia, akaamua kumweleza ukweli wake kwamba alikuwa amemhusudu na kumwomba washirikiane kimapenzi kama uwezekano. Akiwa anajua kilichompeleka pale, Sajini Sofia aliamua kumkubalia ombi lake huku akijua kwamba alikuwa anakwenda kumfungia kazi. Baada ya kukubaliwa ombi lake, Jean alifurahi sana , kiasi kwamba hakupoteza muda, akapanga chumba namba 0018 kilichokuwa katika ghorofa ya kwanza, ndani ya hoteli ya Mount Kijenge .
Ni kitu kama bahati kwa upande wa Sofia, kwani Jean aliamua kumtanguliza kwanza ndani ya chumba kile, halafu yeye akabaki akiongea machache na Pierre aliyekuwa hana muda na kitu wanawake, zaidi ya kazi iliyompeleka. Na pale walikuwa wakipeana majukumu kwamba wawe makini sana , hasa kwa Jean ahakikishe anaficha silaha yake, bastola isionekane. Basi, ile ndiyo nafasi ya pekee iliyotosha kwa Sofia kuwasiliana na Luteni James, akimwambia wakutane chumba namba 0018 ili wamdhibiti!
Baada ya maongezi, Jean akapandisha ngazi hadi katika ghorofa ya kwanza, na kukiendea chumba kile alichoingia Sofia . Alipoufungua mlango akamkuta Sofia amekaa kwenye kochi moja wapo mle chumbani. Ni chumba kilichokuwa nadhifu, na pia kimeenea vitu muhimu, kama kitanda kimoja kikubwa, kilichotandikwa vizuri, runinga, friji ndogo, simu na vinginevyo. Basi Jean alipoingia akafikia kukaa katika kochi na kubaki wakiangaliana kwa muda.
“Mambo vipi sasa?” Jean akamuuliza.
“Hakuna wasiwasi,” Sofia akasema huku akibonyeza simu yake kwa siri na kutumia ujumbe Luteni James, aliyekuwa kule nje kwamba mambo yalikuwa mazuri, hivyo ajiandae kupandisha ghorofani ndani ya chumba kile.
“Mimi nakusikiliza wewe…” Jean akamwambia huku akinyanyuka kujiandaa kuvua nguo zake.
Jean akavua huku vifaa vyake vya siri, ikiwemo bastola na kuvihifadhi vizuri ili Sofia asivione! Hata hivyo Sofia alikuwa ameshaziona ukizingatia alikuwa kazini! Akajua kwamba alikuwa uso kwa uso na mtu hatari! Jasusi!
Sajini Sofia naye akazivua nguo zake huku akimsoma Jean, na pia akivuta subira mpaka Luteni James atakapofika pale na kuweza kumdhibiti Jean kama walivyokuwa wamepanga baada ya kuwasiliana kwa simu.
“Mbona una wasiwasi?” Jean akamuuliza Sofia , huku akiwa amebakiwa na bukta baada ya kuzivua nguo zake na kuzitundika ndani ya kabati la nguo. Na humo ndipo alipoiweka ile bastola yake aina ya Magnum maalum ya kijeshi.
“Mi’ sina wasiwasi…” Sofia akasema kwa sauti ndogo. “Basi njoo huku…” Jean akamwambia huku akijisogeza kitandani, na pia akiwa na uchu wa kufanya ngono!
“Usiwe na papara braza!” Sofia akamwambia Jean hukuakiipapasa bastola yake!
Alitegemea Luteni James kuingia mle chumbani muda wowote!
*******
Luteni James aliunyanyua mkono wake wa kushoto na kuiangalia saa yake. Kisha akalitupia macho jengo lile la Hoteli ya Mount Kijenge, lililiokuwa limefichwa na vivuli vya miti iliyolizunguka kwa kiasi fulani, lakini huku sehemu ya juu ikionekana. Ulikuwa na muda muafaka wa kwenda kuwaingilia Jean na Sofia kule katika chumba namba 0018. James akatoka pale harakaharaka na kupandisha ngazi kwa miguu badala ya kutumia lifti, akatokeza kwenye korido ndefu iliyokuwa na milango pande zote mbili, na milango ikiwa na namba.
Ndipo Luteni James alipokiona chumba hicho katika ghorofa hiyo ya kwanza, na bila kupoteza muda, akatoa ufunguo malaya na kuufungua mlango ule na kisha kuusukuma ndani kwa kasi na kuingia mle ndani bastola ikiwa wazi mkononi! Ulikuwa kama mzimu!
Wakati huohuo, Sajini Sofia naye alichomoa bastola yake na kumwelekeza Jean aliyekuwa haamini kilichojiri. “Mungu wangu!” Akajisemea moyoni, huku akijilaumu kwa kufanya uzembe wa kuwekwa chini ya ulinzi! Kisha akaangalia kule kwenye kabati alikoweka nguo zake pamoja na silaha!
Akachanganyikiwa!
“Uko chini ya ulinzi!” Sofia akasema huku amemkazia macho Jean. Ni macho ambayo muda si mrefu yalikuwa yamelegea katika huba! Sasa yalionyesha ushenzi mtupu!
“Huna ujanja, salimu amri!” Luteni James naye akamwambia huku akimsogelea Jean, ambaye alivunga tu, kama mtu aliyesalimu amri. Alikuwa ni mtu asiyependa kushindwa kirahisi, au kukamatwa. Akapanga shambulizi la kushtukiza!
Jean akajizungusha hewani kisarakasi ili kukabiliana na zile bastola mbili zilizokuwa zimemwelekea yeye. Akafanikiwa kuipiga bastola ya Sajini Sofia ambayo iliruka na kutua mbali kidogo!
“Mh, Sofia akatoa mguno kidogo huku akiiangalia bastola yake iliyokuwa ikigaragara pale chini kwa kuzunguka!
“Shenzi sana !” Jean akasema huku akijigeuza kulipeleka pigo jingine kuelekea kwa James! Lakini James akaliona pigo lile na kurudi nyuma, kiasi cha kufanya pigo lile lipitilize…na kwa haraka akarudisha pigo kubwa kwa Jean ambaye alianguka chini!
“Oohps!” Jean akaguna.
“Tafadhali sana usijiguse!” James akaendelea kumwambia!
“Oh! Mbona siwaelewi?” Jean akauliza huku akiyatoa macho yake!
“Hutuelewi sivyo?” Sofia akamwuliza!
“Ndiyo, wewe si tulikubaliana kuja kustarehe? Sasa mambo ya kuwekana chini ya ulinzi yametoka wapi?”
“Hebu tulia!” James akamwambia na kuendelea. “Wewe tunakuhitaji sana .”
“Mnanihitaji kwa nini?”
“Tunataka ujibu maswali yetu tutakayokuuliza.”
“Ah, nyie ni polisi?”
“Kwa vyovyote utakavyotuita, tulia hapo kitini utujibu maswali tutakayokuuliza!” Luteni James akamwambia.
Jean akakaa kwenye kiti huku akiwa amechanganyikiwa! Hakuamini kilichokuwa kinaendelea mle chumbani!
“Hebu tuambie wewe ni nani, jina lako, umetokea wapi, na umekuja kufanya nini hapa Arusha…haya sema!”
“Sidhani kama kuna sababu zozote za kunifahamu!” Jean akasema kwa kuonyesha kiburi cha hali ya juu!
“Una maana hutaki kusema?” James akaendelea kumuuliza huku akiikandamiza bastola juu kifuani mwa Jean.
“Sisemi…kama ni kuniua niue tu!” Jean akasema.
“Kwa hivyom unataka kufa sivyo?”
“Ndiyo, nimes haapa kufa! Sisemi!” Jean akasema huku akipanga cha kufanya! Halafu bila kutegemea, akashusha mkono wake na kuupeleka kwenye bukta yake! Akachomoa kitu kilichokuwa ndani ya mfuko wa bukta, mfano wa pipi. Akakitupia mdomoni, kikiwa ni kitendo cha haraka sana ambacho hata James na Sofia hawakukitegemea!
“Anafanya nini?” Luteni James akauliza huku akijarubu kumzuia!
“Nafikiri anatumia mbinu za kujiua!” Sajini Sofia akasema.
Walikuwa wameshachelewa! Baada ya Jean kukitupia mdomoni tu, akaanza kuuzungusha ulimi wake huku akimumunya na kutafuna kama Bazoka. Kumbe alikuwa anatafuna kidonge cha sumu kali inayoweza kuua haraka, ambayo ni sumu inayotumiwa sana na majasusi kujiua ili wasitoe siri. Na kweli baada ya kukitafuna tu, akaanza kulegea na kuutoa ulimi wake nje!
Akabaki akikoroma!
“Vipi Sofia?” James akamwambia Sofia .
“Mhn!” Sofia akaguna!
“Umeona?”
“Ndiyo mkuu…nimeona. Ameamua kujiua ili asitoe siri!”
“Ni kitu kama hicho!” Luteni James akasema na kuendelea. “Kweli hawa ni watu hatari sana . Iwapo wenyewe hawauthamini uhai wao, watauthamini wa watu wengine?”
“Hawatauthamini kamwe!”
Hatimaye Luteni James na Sajini Sofia, wakaipekuwa ile maiti ya Jean na baadhi ya nguo zake, hasa ile bukta aliyokuwa ameivaa, ambapo walikuta baadhi ya vidonge katika mfuko wa nyuma. Na katika nguo zake wakakuta vifaa maalum vya upelelezi, kama, vinasa sauti, bastola na Pasi ya kusafiria ya bandia, iliyotolewa Kigali , nchini Rwanda . Vyote wakaviweka sehemu moja, na walipomaliza kuipekuwa wakaivisha nguo na kuilaza pale chini ya sakafu kwa kuifunika na shuka waliyoitoa pale kitandani.
Ndipo Luteni James alipoamua kumpigia simu Mkuu wa Upelelezi, Mkoa wa Arusha, kumjulisha juu ya tukio lile. Baada ya kupiga simu, James na Sofia wakatoka ndani ya chumba kile na kuteremka ngazi hadi nje ya hoteli ile lilipokuwa gari, ambalo James alifika nalo kwa siri. Wakafungua milango na kuingia ndani gari hilo aina ya Nissan Patrol, halafu wakatulia ndani kwa muda huku wakiangalia kilichokuwa kinaendelea. Hata hivyo wakiwa bado mle ndani ya gari, James akaamua kumpigia simu Meja Bombe, ili kumweleza tukio la kifo cha Jean, na baada ya kumpata akamweleza yote katika simu ya mkononi. Akamalizia kwa kusema:
“…Kwa hiyo sisi tuna wasiwasi kwamba watu hao ni wale waliotokea nchini Rwanda kwa nia ya kuwadhuru wale mashahidi muhimu waliotoroka kwenye kambi ile ya waasi…”
“Na mashahidi wenyewe si wako katika makazi yao kule Njiro?” Meja Bombe akamuuliza.
“Ndiyo, mashahidi wale wako katika nyumba maalum za Umoja wa Mataifa,” James akasema
“Basi, nendeni mpaka huko, ili mkaangalie usalama kwa ujumla. Inawezekana watu wale wakaenda kuwadhuru kama walivyofanya kwa wale walinzi, pamoja na dereva wa Umoja wa Mataifa…” Meja Bombe akasisitiza!
“Tutafanya hivyo Mkuu…tene tunahisi wao ndiyo waliofanya mauaji ya makusudi!”
“Ndiyo, fanyeni hivyo!”
“Sawa mkuu!”
Baada ya kuwasiliana James akamgeukia Sofia na kumwambia:
“ Sofia bado tuna kazi…”
“Nipe ujumbe!”
“Tunakwenda Njiro kwa mujibu wa Meja Bombe alivyoagiza…”
“Ndiyo kazi tuliyoijia huku, ukizingatia wale ni watu hatari sana . Usiku ewa leo wanaweza kufanya jambo lolote baya dhidi ya wale mashahidi wanaotakiwa kutoa ushahidi wao katika Mahakama ya Umoja wa Mataifa, inayoshughulikia Watuhumiwa wa Mauaji ya Kimbari, yaliyotokea nchini Rwanda !”
“Ndiyo maana napenda kushirikiana na mtu kama wewe, kwani una moyo wa kishujaa!” Luteni James akamwambia Sajini Sofia.
“Hakuna shaka! Wote tuko bega kwa bega!” Sofia akasema.
Safari ya kuelekea Njiro ikaendelea…
*******
Ndani ya ukumbi ule wa vinywaji na chakula, kijana Pierre alikuwa amekaa akimsubiri mwenzake, Jean, aliyekwenda kustarehe na mwanadada mrembo, Sofia . Lakini alikaa kwa muda mrefu bila kumuona mwenzake, Jean akitokea. Na pia alipojaribu kumtafuta kwa kumpigia simu yake ya mkononi, iliita kwa muda bila kupokelewa. Pale ndipo Pierre aliposhtuka na kujua kwamba kuna jambo baya lilikuwa limetokea baada ya kuingia na yule mwanadada ndani ya chumba namba 0018 katika Hoteli ya Mount Kijenge.
Kwa haraka sana Pierre alikatoka nje ya hoteli ile. Halafu akasimama karibu na uzio wa michongoma uliokuwa karibu na sehemu ya maegesho ya magari. Halafu akachukuwa simu yake na kuanza kumpigia Paul Rugoye, na kumjulisha hali halisi ilivyokuwa. Akiwa ni mtu aliyekuwa macho muda wote, hakukawia kufika, ukizingatia sehemu ya maficho yao haikuwa mbali na hoteli ile. Ni umbali wa mita mia tatu hivi, ikiwa imetenganishwa na barabara pamoja na majumba ya maghorofani, eneo la Kijenge.
“ Pierre !” Paul akamwita punde tu alipomfikia pale aliposimama.
“Mkuu...” Pierre akaitikia.
“Kuna nini?”
“Kuna tatizo!”
“Tatizo gani?”
“Jean hajarudi mkuu!”
“Hajarudi...sikuelewi!”
“Hajarudi mkuu...nashindwa kuelewa!”
“Kwani alikwenda wapi?”
“Alipandisha juu ghorofani…katika chumba namba 1008…”
“Kufanya nini mle chumbani?”
“Alikuwa na mwanamke. Alikwenda kupunguza uzito!”
“Mungu wangu…kwa hiyo?”
“Nimejaribu kumwita kwenye simu…lakini haipokelewi!”
“Hali itakuwa mbaya sana kama Jean amekamatwa! Ni kwa nini amejiingiza katika mambo ya wanawake mapema namna hii?”
“Si unajua tena mkuu? Lakini hakuna haja ya kulaumiana…tupange la kufanya!”
“Na kweli tufanye hivyo!” Paul Rugoye akasema huku akimlaani moyoni kwa kujihusisha na mambo ya wanawake! Dainma wanawake ni sumu, na mara nyingi hutumiwa katika masuala ya upelelezi!
Lakini wakati, Paul Rugoye na Pierre, wakiwa bado wamesimama kando ya gari lao, wakayaona magari mawili ya polisi, aina ya Land- Cruiser yakiingia pale hotelini na kupaki sehemu ya maegesho. Ndani yake kulikuwa na askari polisi kadhaa, ambao waliteremka haraka, wengine wakiwa wamebeba machela. Wakaingia ndani ya hoteli ya hoteli ile, ambapo walikaa kwa muda wa nusu saa hivi, na walipotoka, walikuwa wameubeba mwili waJean, aliyekuwa amekufa, ambao waliuingiza ndani ya gari moja wapo. Paul na Pierre walishuhudia kwa macho yao wenyewe kiasi cha kuwafanya wachanganyikiwe!
“Mungu wangu! Ina maana Jean kafa?” Paul Rugoyeakamwambia Pierre.
“Ndiyo hivyo! Naona maiti yake inachukuliwa na polisi…inawezekana alikuwa amepata upinzani mkali na kuamua kujiua kwa kutafuna vidonge vya sumu!”
“Ni kitu kama hicho…amekufa kishujaa!”
“Na kweli, sijui imekuwaje wametugundua mapema namna hii. Twende tukapange mikakati ya kazi!” Paul Rugoye akasisitiza!
Hatimaye Paul na Pierre wakaondoka katika eneo lile la hoteli, kwa kutumia gari alilofika nalo Paul. Wakaelekea yalipo maficho yao , huku wakijua walikuwa wanafuatiliwa nyendo zao, huku wakiwa hawajakamilisha ile kazi waliyotumwa na Kanali Fabio, ya kuwaangamiza vijana wasaliti, Roman, Teobale na Laurent, na kuzipata zile Diski walizoondoka nazo katika ngome yao !
Baada ya kufika tu, wakaamua kukaa kikao mara walipogundua ni kweli mwenzao Jean alikuwa amekufa. Hivyo wote watatu, Paul, Pierre na France wakaingia ndani ya chumba maalum, kilichokuwa mfano wa chumba cha mkutano.
“Nimeonekana sifai!” Paul Rugoye akasema.
Wote wakawa wanamsikiliza kwa makini!
“Nasema hivyo kwa jinsi tulivyojulikana mapema. Na nyote mnaona hali ilivyo, ni kwamba mkono wa dola umeshtuka, na sasa uko mbioni katika upelelezi ili waweze kutukamata. Kwa hivyo basi tufanye juu chini kuimaliza operesheni yetu!”
“Unayosema ni kweli mkuu,” Pierre akasema na kuongeza. “Hali imekuwa mbaya ukizingatia mwenzetu Jean ameshakufa, na maiti yake iko chini ya uchunguzi wa Polisi. Sasa si watagundua kuwa Jean hakuwa M-tanzania, ni lazima tufanye hujuma dhidi ya wale wasaliti wetu!” “Ok, jiandaeni tuondoke muda huu huu tukafanye kazi. Hakuna kusubiri siku!” Paul Rugoye akaambia Pierre na France!
“Hakuna shaka, twendeni!” Pierre akasema.
“Kazi ni moja tu!” France akadakia.
“Lakini…” Paul akasema. “Hata hivyo naona tusiende wote. Ni lazima abakie mmoja, ili tuache nguvu ya akiba nyuma. Hatuwezi kwenda wote na kuteketea!
“Ni sawa, sasa abaki nani?” Pierre akauliza.
“Utabaki wewe Pierre …lakini tutakuwa tunawasiliana mara kwa mara. Na mimi nitaondoka na France, pamoja na dereva wangu, Meku, ambaye hajui chochote kinachoendelea katika mipango yetu!”
Baada ya kuafikiana, Paul Rugoye na France wakatoka ndani ya chumba hadi nje. Wakaliendea gari, Toyota Chaser, lililiokuwa limepaki na dereva wake, Meku, akiwa ndani. Wakapanda na kuondoka kuelekea Njiro, kama alivyoelekezwa na bosi wake wa Kampuni ya Rugo Safaris. Hakujua kilichokuwa kinaendelea, kwani akiwa kama mwajiriwa, ilibidi afuate amri ya bosi wake bila kuhoji!
Paul na France walikuwa wamejiandaa vya kutosha, wakiwa wamejizatiti na silaha za hatari, bunduku fupi aina ya ‘Uzi’ bastola, mabomu ya kutupa kwa mkono.
Walifika eneo la Njiro majira ya saa tatu.
“Simamisha gari hapa,” Paul Rugoye akamwambia dereva Meku.
“Sawa bosi,” Meku akasema huku akipunguza mwendo. Halafu akalipaki kando ya barabara
“Sasa,” Paul Rugoye akasema. “Natumaini ramani ya eneo hili unaifahamu vizuri.”
“Naifahamu vizuri,” France akasema.
“Haya, wewe nenda kafanye uchunguzi kwanza. Mimi nitabaki hapa kama muda wa nusu saa hivi, halafu ndiyo nitakufuata. Si unajua siyo vizuri kuongozana wote?”
“Hakuna wasiwasi, mimi natangulia, na nitakujulisha kwa simu kinachoendelea…” France akasema huku akiufungua mlango.
Halafu France akashuka na kuelekea katika makazi yale ya nyumba za Umoja wa Mataifa, huku akijikinga na vivuli vya miti mingi iliyokuwa katika sehemu ile. Kwa alikuwa amevalia mavazi meusi, ilikuwa siyo rahisi kuonekana katika kiza kile, mpaka alipouruka uzio na kutua ndani. Paul na dereva Meku, walibaki ndani ya gari huku wakimwangalia France alivyokuwa anapotelea gizani. Hata hivyo, Meku, dereva akawa na wasiwasi kidogo na watu wale, kwani hakujua walifika eneo lile la Njiro kwa minajili gani usiku ule! Tena kama walikuwa wanavizia kitu! Hata hivyo hakusema chochote zaidi ya kusubiri!
********
Luteni James na Sajini Sofia walikuwa wameshafika Njiro muda mrefu, kabla hata Paul , France na Meku, dereva, hawajafika. Baada ya kufika katika nyumba za Umoja wa Mataifa. Wakabanisha sehemu nzuri, ambapo waliweza kuwaona walivyofika na gari lao, eneo lile. Wakasubiri waone watakavyofanya baada ya kusimama kwa muda. Pia, waliona walivyokuwa wakipeana majukumu, na mpaka France alivyoondoka na kuwaacha wenzake kuelekea katika nyumba na kuuruka uzio ule kuingia ndani.
Luteni James na Sofia wakaamua kumfuatilia France kwa mwendo wa kinyaninyani, kisha nao kuuruka uzio na kutua ndani. James akazunguka upande wa pili kumzungukukia France , na Sofia naye akamzungukia upande mwingine huku bastola zikiwa mikononi mwao. Kwa vyovyote walijua kwamba France alikuwa anakwenda kufanya madhara kwa wale mashahidi muhimu walipkuwa ndani ya vyumba vyao!
France alipofika kwenye mlango mkubwa wa kuingilia ndani, akajaribu kuufungua kwa kuutikisa mara kadhaa. Wakati huo James alikuwa ameshamfikia karibu, pasipo yeye kujua. Akamrukia kwa kumshtukiza na kumpiga pigo la nguvu lililiomfanya apepesuke, lakini hakuanguka. Akageuka na kukabiliana naye huku akitoa vipigo kadhaa ambavyo vilimpata James na vingine aliviona na kuvikwepa kiufundi!
“Shenzi sana !” Luteni James akasema huku akijiandaa kummaliza!
“Huniwezi!” France akamwambia James, halafu akajizungusha hewani na kutua nyuma ya ukuta uliotenganisha nyumba. Kilikuwa ni kitendo cha haraka sana , ambapo France alijiandaa kutumia bunduki yake aina ya ‘Uzi’ inayotoa risasi mfulilizo ili kummaliza!
Luteni James akayatoa macho yake pima! Ukweli ni kwamba alikosa uamuzi wa haraka wa kufanya. Kumbe upande wa pili, Sofia alikuwa ameshamzungukia France upande wa nyuma; na kumfuata kabla hajaleta madhara kwa James! Kilikuwa kitendo cha haraka!
“Wewe mshenzi!” Sofia akamwambia!
“Vipi tena?” France akajiuliza baada ya kusikia sauti ya mtu nyuma yake!
“Umekwisha!” Sofia akamwambia huku akitoa vipigo kadhaa, ambavyo vilimfanya aidondoshe ile bunduki!
“Huniwezi we mwanamke!” France akamwambia huku akijiweka vizuri kwa mapigano!
Na alishajua kwamba Sofia ndiye aliyemwagiza Jean siku ile ndani ya chumba namba 0018.
“Nitakumaloiza kama mwenzako!”
“Ndiye wewe uliyemwua Jean?”
“Ndiyo mimi! Bado wewe!”
“Jaribu!” France akasema huku akijirusha hewani ili kumrukia Sofia kwa miguu yote miwili! Lakinhi Sofia akamsubiri na kumdaka!
“Lazima nikumalize!” Sofia akamwambia huku akimbamiza kichwa chake ukutani kiasi cha kunfanya aone nyotanyota!
“Oh, aibu…” France akasema huku damu zikimtoka mdomoni.
“Aibu ya nini? Wewe si mwanaume?”
“Oohps!” France akavuta pumzi ndefu, halafu bila kutegemea, akatumia njia ile ile aliyotumia Jean! Akatoa kidonge kimoja cha sumu kali. Akakiweka mdomoni kwa haraka na kukitafuna kisha kukimeza!
“Mungu wangu!” Sofia akasema baada ya kumwona France akitafuna kidonge cha sumu! Muda siyo mrefu akalala chini huku macho yakimtoka, pamoja na ulimi kutoka nje ya mdogo nje yam domo! Alikuwa amekata roho!
Luteni James alikuwa amesimama akiyashuhudia mapigano yale makali dhidi ya Sofia na France, ambapo yeye hakupendelea kuingilia! Alimwamini Sofia kuwa ni mwamke wa shoka!
“Vipi tena, imekuwaje?” James akamuuliza.
“Ndiyo hivyo tena…naye amejiua!” Sofia akasema na kuendelea. “ Ni watu hatari sana !”
“Ni kweli ni watu hatari, twende zetu, huyo mwache hapo hapo!”
“Poa, tuwaandame wale kule nje!” James na Sofia wakamwacha France pale alipoangukia. Wakaondoka na kuuruka uzio, kasha kutokeza nje, sehemu lilipokuwa lile gari, Toyota Chaser walilofika nalo, Paul, Pierre , France na dereva Meku. Baada ya kulifikia gari, wakamkuta Meku anasinzia, lakini Paul hakuwepo! Ukweli ni kwamba alikuwa ameshatoroka baada ya kuyashuhudia yale mapigano makali yaliyomshinda kwenda! Hakupenda kufa akijiona!
ITAENDELEA
0.jpeg
 
Simulizi : Msaliti Asakwe

Sehemu Ya Nne (4)

JAMES na Sofia wakamwacha France pale alipoangukia. Wakaondoka na kuuruka uzio, kasha kutokeza nje, sehemu lilipokuwa lile gari, Toyota Chaser walilofika nalo, Paul, Pierre , France na dereva Meku. Baada ya kulifikia gari, wakamkuta Meku anasinzia, lakini Paul hakuwepo! Ukweli ni kwamba alikuwa ameshatoroka baada ya kuyashuhudia yale mapigano makali yaliyomshinda kwenda! Hakupenda kufa akijiona!
“Haloo, kumekucha!” Luteni James akamwambia Meku aliyekuwa ameegemea kiti.
“Tayari bosi?” Meku akauliza baada ya kushtuka usingizini! Aliodhani ni bosi wake, Paul Rugoye! Kumbe ni adui!
“Hebu toka humo ndani ya gari!” James akamtoa Meku ndani ya gari.
“Imekuwaje tena?” Meku akauliza huku akiona sura nyingine!
“Hebu tueleze, humu ndani ya gari, mlikuwa watu wawili, mwenzako yuko wapi?” James akaendelea kumwuliza huku amemnyooshea bastola! Akachanganyikiwa!
“Alielekea huko mlipotoka nyie!”
“Naomba utueleze ukweli!”
“Jamani mtaniumiza bure!” Akalalamika Meku na kuendelea. “Mimi ni dereva tu, si husiki na jambo lolote!”
“Aliyekuagiza kuja hapa ni nani?”
“Ni bosi wangu, Paul Rugoye…” “Tulikuwa naye ndani ya gari, baada ya ya kuja hapa tukiwa watu watatu. Akaniaga kuwa anamfuata mwenzake aliyeelekea kule, lakini hajarudi yeye wala mwenzake!”
“Huyo Paul ni bosi wako kivipi?”
“Kwani humfahamu?” Meku akauliza na kuendelea. “Ni mtu anayejulikana sana , akiwa mmiliki wa klampuni ya kuhudumia watalii, ya Rugo Safaris…”
“Vizuri sana , basi itabidi tuondoke na wewe. Utatusaidia sana !” Luteni James akamwambia Meku aliyekuwa bado ameshangaa!
“Kwenda wapi?” Meku akauliza!
“Tunajua wenyewe!”
“Oohps!”
Baada ya kuhakikisha maiti ya France imechukuliwa na kwenda kuunganishwa na ya Jean katika Hospitali ya Mount Meru, wakamchukuwa Meku na kuondoka naye. Wakampeleka kwenye ofisi zao maalum zilizoko Barabara ya Boma, kwa mahojiano zaidi, ambayo yangewasaidia kuhitimisha kazi ile iliyokuwa inawakabili!
*******
Pierre aliyekuwa amebaki katika ile nyumba ya mafichoni, Kijenge, alipenda kujua maendeleo ya wenzake, Paul na France, baada ya kwenda kule Njiro. Baada ya kupiga simu ya mkononi, hakuwapata, lakini muda siyo mrefu, Paul Rugoye akatokea huku akiwa ametweta ovyo!
“Vipi mkuu?” Pierre akamuuliza.
“Oh, makubwa!” Paul Rugoye akasema.
“Imekuwaje?”
“Jamaa wametuzidi maarifa!” Paul akaendelea. “Na mpaka muda huu tunapoongea, France keshakufa kwa kutafuna vidonge vya sumu baada ya kuzidiwa!”
“Mh, makubwa!” Pierre akasema.
“Baada ya kuona vile, ikanibidi nikimbie na kumwacha dereva wangu Meku akiwa amelala ndani ya gari. Nikakodi teksi iliyonifikisha hapa muda huu!
“Tumeharibu kila kitu!”
“Tumeharibu kivipi?”
“ Kama umemwacha yule dereva akiwa hai, basi atasema yote baada ya kukamatwa na kuhojiwa na polisi!”
“Sijaharibu kitu!” Paul Rugoye akasema kwa kujiamini na kuendelea. “Hata kama wakimhoji hawaelewi chochote! Isitoshe mimi ni mtu mzito sana hapa Arusha. Ninafahamika kwa wema ninaotenda hasa kusaidia jamii!”
“Kama ni hivyo ni sawa, lakini sikutegemea kama tungepata upinzani mkali namna hii, ukizingatia tumeshawapoteza Jean na France. Tumebaki wawili tu!”
“Usikate tamaa, kazi hii tutaifanya sisi wawili!” Paul Rugoye akasema kwa msisitizo!
Mjadala ukafungwa!
Usiku ule Paul Rugoye na Pierre hawakulala kabisa, na wala Paul hakwenda nyumbani kwake, eneo la Sakina, ilipo familia yake. Kutokana na hali ile iliyojitokeza, walikaa na kupanga jinsi ya kuwapata wapelelezi wawili waliokuwa wanawatibulia mipango yao mingi!
********
Asubuhi iliwakuta Luteni James na Sajini Sofia wakiwa ndani ya mgahawa maarufu wa Baracuda, uliopo katika Barabara ya Makongoro, jijini Arusha. Pale walifika ili kujipatia kifungua kinywa, ambapo waliagiza supu na chapati na kuendelea kula taratibu huku kila mmoja akiwazia ile kazi iliyokuwa inawakabili mbele yao . Ukweli ni kwamba adui yao walikuwa wameshamfahamu!
Ukweli huo waliupata jana yake usiku baada ya kumhoji yule dereva, kijana, Meku, ambaye alisema yote kuhusu bosi wake, Paul Rugoye, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Rugo Safaris. Pia, aliwaeleza jinsi ya kumpata katika ofisi yake iliyoko katika barabara ya Sinoni. Basi ndipo walipopanga mpango kabambe wa kumwingilia katika ofisi yake kwa nia ya kumpeleleza!
Hakika waliamua!
“ Sofia ,” Luteni James akamwita.
“Mkuu James,” akaitikia Sofia .
“ Kama tulivyopanga, inabidi leo niivamie ile ofisi ya Paul Rugoye ili niupate ukweli, na tuweze kufanikiwa kuwatia mbaroni. Mimi nitakwenda pale kama mteja wa kawaida ninayehitaji kukodi gari la shughuli za starehe. Baada ya hapo nitaondoka na kuahidi kurudi baadaye kulichukuwa. Nafikiri kama watakuwa wamenishtukia, wataweka mtego wao wa kuniteka nyara pindi nitakaporudi safari ya pili, ili wanipeleke katika maficho yao , na kunibana wajue mimi ni nani!”
“Safari ya pili nitakaporudi katika ofisi ile,” James akaendelea kusema. “Tutaongozana wote wakati huo ukiwa umebanisha nje, ukiwa ndani ya gari letu bila wao kujua. Basi, watakaponiteka na kuondoka na mimi, wewe utalifuatilia gari lao nyuma bila wao kujua. Ni mpaka katika maficho yao , sijui umenipata?”
“Nimekupata mkuu…Kumbe kichwa chako ni cha mtu wa kazi!” Sofia akamwambia James. “Hakuna kitu kitakachoharibika!” “Ndiyo hivyo nilivyotaka Sofia …”
“Basi, hakuna shaka…”
Wakaendelea kupanga mpango wao huku wakiendelea kula supu. Kwa mtu yeyote aliyewaona pale walipokuwa, kamwe asingewashtukia kama walikuwa wapelelezi, zaidi ya wapenzi wawili, kwa jinsi walivyokuwa wameshabihiana. Baada ya kumaliza, wakaondoka katika mgahawa ule wa Baracuda kurudi katika ofisi za Idara ya Usalama wa Taifa, ambazo hazikuwa mbali na pale. Wakaondoka kila mmoja akifuata uelekeo wake kwa ajili ya usalama zaidi, kama kuna mtu yeyote aliyekuwa anawafuatilia.
Hatimaye wakafika katika ofisi maalum waliyokuwa wametengewa, na kusubiri wakati muafaka.
Majira ya saa tano za mchana, Luteni James akaondoka pale ofisini kwa miguu na kuifuata Barabara ya Boma taratibu. Alikuwa amevalia nadhifu suti ya rangi ya udongo iliyompendeza, na alikuwa katika safari ya kwenda katika ofisi za Rugo Safaris. Alipofika kwenye makutano ya barabara ile ya Boma na Sokoine, eneo la mnara wa saa, akaifuata barabara ya Sinoni kama anaelekea Faya. Hatimaye akafika kwenye ofisi ya Kampuni ya Rugo Safaris, akiwa kama ni mteja wa kawaida, ambapo sehemu ya mapokezi alipokelewa na mwanadada mrembo, aliyekuwa amekaa ndani ya kichumba kidogo kilichokuwa na dirisha la kioo. Kwa kutumia lugha nzuri ya kibiashara alimkaribisha James huku akimwambia:
“Karibu…karibu nikusaidie…”
“Ahsante sana …nisaidie tafadhali…” Luteni James akamwambia mwanadada yule aliyekuwa na umbile la kutamanisha.
“Sijui nikusaidie nini?”
“Ninataka kukodi gari kwa ajili ya shughuli zangu binafsi, maana nimeona hii ni kampuni inayojishughulisha na ukodishaji wa magari kwa wateja wa kawaida, na pia kwa watalii. Hivyo naomba unijulishe utaratibu ninaotakiwa kuufanya.”
“Ni sawa kaka…unajua utaratibu wetu ni kwamba ukitaka kukodi gari, ni lazima umwone Mkurugenzi Mkuu mwenyewe. Yeye atakuambia utaratibu mzima…” akasema mwanadada yule.
“Ni sawa dada, nielekeze tu...” Luteni James akamwambia huku akimkagua vizuri kwa macho yake ya kipelelezi.
“Sawa...” mwanadada yule akasema. Halafu akaunyanyua mkonga wa simu na kupiga ile ya ndani kwa ndani na kuongea.
“Bosi…kuna mgeni hapa…anataka kukodi gari…haya bosi…” James alikuwa bado anamwangalia, ambapo baada ya kumaliza kuongea na bosi wake, akamgeukia na kumwambia kwa sauti nyororo na ya kuvutia:
“Ingia katika ofisi hiyo hapo yenye mlango wa kioo, utamkuta Mkurugenzi.”
“Nashukuru sana ,” Luteni James akasema, halafu akanyanyua hatua kuuendea ule mlango wa kioo uliokuwa na maandishi yaliyosomeka, ‘Mkurugenzi Mkuu.’ Akagonga mara mbili, kisha akausukuma na kuingia ndani.
Baada ya kuingia ndani ya ofis ile, akamkuta Paul Rugoye akiwa amejaa tele katika meza yake, na kabla ya kusalimiana, James na Paul wakatupiana macho ambayo yaligongana na kila mmoja kuonyesha ishara fulani, hasa kwa Paul, aliyekuwa na wasiwasi sana ! Sura yake ilionyesha uchovu wa hali ya juu, ambao haukuwa mwingine zaidi ya ule wa kuhangaika kuwatafuta vijana wale wasaliti, ili wawamalize!
“Karibu…” Paul Rugoye akamkaribisha LueniJames huku akimwangalia kwa makini.
“Ahsante sana …” James akasema huku akikaa kwenye kiti.
“Nimeshakaribia. Mimi naitwa Bw. Joseph Mika…” James akajitambulisha kwa kudanganya jina lake.
“Karibu sana Bw. Mika…”
“Nimekuja hapa kwa ajili ya kukodi gari kwa ajili ya shughuli zangu binafsi.”
“Vizuri… sana . Hapa tunakodisha magari ya kila aina, lakini inategemea unataka gari la aina gani, kwani hapa tuna magari kama Toyota Land Cruiser, Land Rover 110 Defender, Corolla, Noah, na nyinginezo. Ni magari ambayo yako katika hali nzuri kabisa, hayana tatizo!” Paul akamwambia James huku akiendelea kumwangalia kwa jicho la pembeni hasa ukizingatia na yeye alikuwa ni jasusi hatari. Kwa kawaida watu wa aina hiyo wanapokutana huwa wanashtukiana mapema!
“Mimi nahitaji gari aina ya Land Rover 110 Defender, ambayo itasaidia katika shughuli zangu. Pia, naomba unipatie utaratibu…” Luteni James akamwambia Paul Rugoye.
“Hakuna tatizo. Itabidi ujaze fomu na kuambatanisha malipo kama ukipenda kutanguliza. Lakini pia, ukipenda kulipa baada ya kulitumia gari, ni uamuzi wako. Sisi hatuna kipingamizi…” Paul Rugoye akamwambia na kuendelea.
“Sasa sijui utahitaji kwa muda huu?”
“Hapana. Sitalichukuwa muda huu, bali nitaliangalia, halafu nije kulichukuwa baada ya masaa matatu hivi, kwani kuna sehemu nyingine napitia...”
“Hakuna shaka. Twende ukachague…” Paul Rugoye akamwambia James.
Wote wakanyanyuka na kuongoza kuelekea sehemu ya nyuma ya ofisi, ambapo palikuwa na magari kadhaa yamepaki. Baada ya kuyakagua, James akaamua kuchukuwa gari aina ya Land Rover 110, ambalo aliahidi kwenda kulichukuwa baadaye. Paul akamkubalia huku akiwa ameshamshtukia kuwa alikuwa ni mpelelezi aliyekwenda kumpeleleza baada ya kugundua yeye anahusika katika mpango ule wa msako wa vijana mashahidi muhimu!
“Utakuja kulichukuwa saa ngapi?”
“Nitarudi kulichukuwa majira ya saa tisa za alasiri…naomba muniandalie…”
“Ok, utalikuta tu, kwani ofisi inafungwa saa kumi na moja za jioni…”
“Basi nitarudi.”
“Karibu tene…”
Paul na James wakaagana.
Paul akarudi ofisini kwake, na James akapitia pale mapokezi, alipokuwa yule mwanadada mrembo anayehudumia. Akamuaga huku akimuahidi kurudi baadaye kulichukuwa lile gari. Akatoka nje na kutembea kwa mwendo wa haraka nambele akachukuwa teksi iliyompeleka alikopanga chumba, Serena Inn Hotel.
********
Haikumwingilia akilini Paul Rugoye aamini kwamba mgeni yule, Luteni James, alikwenda ofisini kwake kwa ajili ya kukodi gari. Alimshtukia kuiwa ni mpelelezi aliyekwenda pale katika harakati za kumpeleleza, na si vinginevyo. Kwani katika kazi yake ya ujasusi aliyoifanya kwa muda mrefu, alishakuwa mzoefu tosha. Hivyo baada ya kurudi ofisini tu, akapanga mpango wa kumwekea mtego punde atakaporudi kulichukuwa lile gari. Muda ule aliokuwa amepanga.
Alichoamua Paul Rugoye, ni kumteka nyara Luteni James, na kumpeleka kwenye maficho yao kule Kijenge, ambapo angewatumia vijana wale wawili, Toni, ambaye ni mlinzi wake wa karibu, pamoja na Pierre aliyebakia baada ya wenzake kusambaratishwa. Hakupoteza muda, Paul akawapigia simu Pierre na Toni wafike pale ofisini mara moja tayari kupangiana mikakati yao ya kazi.
Baada ya robo saa tu, vijana wale waliiingia pale ofisini na kujikalia kwenye viti vilivyokuwa vimeizunguka meza ya Paul. Walipokaa, ndipo alipowapangia kazi ile, juu ya kumdhibiti Luteni James punde atakaporudi safari ya pili. Basi wakakubaliana kukaa tayari kwa kujificha mle mle ndani ofisini, na atakapotokea ni kumdaka mithili ya Panya anayedakwa na Paka!
Ndiyo, walijiamini!
Toni alikuwa ni kijana mwenye umri wa miaka 30 hivi, akiwa na mwili mkubwa uliojengeka. Huyo aliajiriwa kama mlinzi kwenye kampuni ya Rugo Safaris, na alikuwa amefuzu mafunzo ya aina mbalimbali ikiwemo ya sanaa ya mapigano. Na kwa mbali alikuwa anaujua ule mpango wa bosi wake, Paul Rugoye, kwamba ni mmoja wa majasusi wanaosaidia waasi nchini Rwanda . Hata hivyo hakumfuatilia sana bosi wake kwa vile alikuwa anamlipa mshahara unaokidhi mahitaji.
Pamoja na kupewa maelekezo yale ya kumdhibiti James, wote hawakujua kwamba yeye James alikuwa amejipeleka pale makusudi tu, na wala hakuwa bwege. Alitaka wamteke nyara aweze kuyagundua maficho yao yaliyoko Kijenge, ambayo mpaka muda ule walikuwa hawajui yalipo!
Hakika ulikuwa ni mtafutano!
Wote walikuwa wanawindana!

********

Ndani ya chumba alichokuwa amepanga Luteni James, katika hoteli ya Serena, mkakati wa mwisho ulikuwa unapangwa na wale watu wawili, James na Sofia. Ulikuwa ni mkakati wa kumwingilia Paul Rugoye ofisini kwake, na ile ilikuwa ni baada ya James kumpigia simu Sofia amfuate pale kwa sababu za kiusalama zaidi. Isiwe kuna watu wanaowafuatilia. Ukweli ni kwamba watu wale wenye taaluma ya ujasusi, walikuwa hawaaminiki kabisa.
“ Kama tulivyokuwa tumepanga mwanzo...” Luteni James akasema na kuendelea. “Nimefanikiwa kufika kwenye ofisi ya Rugo Safaris, na kuonana na mtu wetu anayeitwa Paul Rugoye…” James akamweleza yote Sofia na juu ya kukubaliwa kwenda kukodi gari moja, ambalo ameahidi kwenda kulichukuwa baadaye!
“Aisee, wewe jasiri sana !” Sofia akamwambia. “Lakini hawajakushtukia kweli?”
“Inawezekana atakuwa amenishtukia, kitu ambacho mimi nilipenda iwe hivyo. Pia, nategemea kwamba nitakaporudi baadaye, ni lazima waandae mtego wa kuniteka nyara ili kujua mimi ni nani. Sasa kama tulivyoongea tokea mwanzo, tutakuwa wote sambamba katika safari ya kwenda katika ofisi ya Rugo Safaris…unanipata?”
“Nakupata mkuu!” Sofia akasema.
“Mimi nitatangulia…halafu wewe utanifuata nyuma ukiwa na gari letu la idara, ambalo lina vioo vya giza . Gari hilo utalipaki mbali kidogo na ofisi ile, sehemu iliyojificha kando ya jengo hilo . Hapo ndipo utafuatia nyendo zote kwa yote yanayotendeka kwa kutumia vifaa vyetu vya mawasiliano, ambavyo vinanasa kutokea mbali!
“Nimekuelewa mkuu. Nitafanya yote kama ulivyonielekeza, na kazi utaiona!” Sajini Sofia akasema kwa kujiamini!
“Unanipa moyo Sofia , hivyo jiandaeni vilivyo hasa tambua kwamba mimi nitakuwa sina silaha yoyote. Silaha zote utakuwa nazo wewe ndani ya gari…” Luteni James akaendelea kumpa mikakati Sofia , alimwelewa!
Walipomaliza kujiandaa, ilikuwa imetimu saa nane za mchana. Hivyo wakaamua kuondoka, James akitangulia kwa teksi, halafu nyuma akafuatiwa na Sofia aliyekuwa na gari aina ya Nissan Patrol. Baada ya kufika akalipaki katikati ya magari mengine yaliyokuwa kando ya barabara ya Sinoni. Ni sehemu ambayo ilikuwa siyo rahisi kushtukiwa, ambapo pia aliweza kuiona ofisi ile. James alipofika, akashuka kutoka kwenye teksi iliyomfikisha pale. Akaingia ndani ya ofisi ile, ambayo mara ya kwanza alifika na kuahidi kurudi baadaye.
Kumbe huku nyuma, Paul Rugoye alikuwa ameshatayarisha vijana wake maalum, Pierre na Toni, mijitu iliyoshiba katika kuabiliana na Luteni James.
Pia, kwa upande wa Pierre, alikuwa na uchungu wa kuuawa kwa vijana wenzake, France na Jean, aliotoka nao salama nchini Rwanda .
“Ohooo! Umekuja siyo?” Paul Rugoye akamwambia huku akitoa tabasamu la uongo!
“Ndiyo, nimekuja kikamilifu, ni kulichukuwa gari tu kwa ajili ya matumizi niliyokusudia...” Luteni James akamwambia kabla hata hajakaa kitini.
“Haya, unaweza kwenda huko uani ukapatiwe utaratibu wa kulichukuwa!” Paul Rugoye akamwambia bila kumpa nafasi ya kukaa.
“Nashukuru sana ,” Luteni James akasema.
Halafu akatoka ndani ya ofisi ya Paul Rugoye, na kuufuata mlango mmoja ambao utokea sehemu ya uani yalipo magari. Ni mlango uliokuwa umerudishiwa tu, ambapo ilitegemea yeye ndio aufungue na kuweza kutokeza kule uani. Kila alipokuwa akiusogelea ule mlango, mapigo ya moyo wake yakaongezeka kasi yake.
Akahisi hali ya hatari!
Kwa vyovyote James alijua kuwa pale mlangoni alikuwa ametegeshewa mtego ili akamatwe, kitu ambacho pia alikuwa amekitegemea. Baada ya kuufungua mlango ule na kutokeza uani, akashtukia akivamiwa na watu wawili walioshiba!
Ni Toni na Pierre! Kwa vile L:uteni James alikuwa ameshawaona, alikwepa na kuruka mbele kidogo na wenyewe wakajikuta wakigongana wenyewe kwa wenyewe! Wakatoa miguno hafifu ya hasira na maumivu makali! Hata hivyo wakafanikiwa kumdhibiti baada ya kumpa kipigo cha kumlegeza, kilichomfanya adondoke chini.
Pamoja na kudondoka, Luteni James hakupoteza fahamu, bali alivunga tu ili aweze kuwapeleleza vizuri. Basi kilichofuata ni kwa vijana, Toni na Pierre kumbeba James msobemsobe na kumpakia ndani ya gari moja aina ya Land Rover Discover, lililokuwa na vioo vya giza .
Dereva alikuwa ni Toni, wakaondoka pale kuelekea katika maficho yao , eneo la Kijenge, huku wakiwa na furaha ya kumpata James!
Wakati huo, Sajini Sofia aliyekuwa kule nje, ndani ya gari, akaliona gari liliomchukuwa Luteni James likiondoka. Na wakati huo pia, kifaa chake cha mawasiliano kilitoa mlio wa hatari, kuwa bosi wake alikuwa ametekwa akiwa ndani ya gari lile liliopita jirani yake, hivyo naye akaliondoa gari na kuanza kumfuatilia hasa ukizingatia magari yalikuwa ni mengi kwa muda ule barabarani.
Wakiwa katika mwendo wa wastani, wakaifuata barabara ya Kijenge hadi walipofika katika mzunguko wa barabara, mkabala na Hoteli ya Mount Kijenge . Wakauzunguka mzunguko ule na kuifuata barabara inayoelekea Njiro Hill. Kwa mbele kama mita ishirini hivi, gari lile lilionyesha ishara ya taa na kupinda upande wa kushoto kwa kuifuata barabara ndogo ya changarawe, iliyokuwa inapita karibu na nyumba za AICC eneo la Kijenge Maghorofani.
Sajini Sofia aliyekuwa anawafuatilia nyuma, aliamua kupitiliza na barabara ile kama anaelekea Njiro, hadi alipofika katika njia panda inayoelekea viwandani, kando ya mlima Themi. Akalisimamisha gari kando ya barabara, sehemu iliyokuwa na miti mingi ya muarobaini, halafu akashuka huku amechukuwa begi dogo lililokuwa na silaha ndani yake, ambazo ni silaha alizokuwa ameziweka muda mrefu tu, kisha akaufunga mlango wa gari na kuondoka kwa miguu kuufuata uchochoro mmoja ambao ulitokeza katika barabara waliyopitia Toni na Pierre, waliomteka Luteni James. Ni sehemu iliyokuwa kimya hasa ukizingatia walikuwa wanaishi watu walionazo, kwani kila nyumba ilizungukwa na uzio, pamoja na geti madhubuti la chuma.
Huku akijiamini, Sajini Sofia alitembea kwa mwendo wa haraka na kuchepukia uipande wa pili wa nyumba zile, palikuwa na nyumba kubwa iliyokuwa na geti la chuma lililoweza kuonyesha ndani. Kwa haraka Sofia aliyatupa macho yake kule ndani, ambapo aliona kuna gereji iliyokuwa na magari machache yaliyohifadhiwa.
Basi, mle ndani ndipo lilipoingia lile gari aina ya Land Rover Discover lililomchukuwa James. Getini palikuwa na mlinzi mmoja aliyekuwa na bunduki, akiangaza macho yake pande zote. Lakini Sofia hakusimama, bali alipitiliza hadi mwisho wa uzio ule wa michongoma na miti iliyofungana. Mlinzi yule akiwa makini na kazi yake, alimshtukia Sofia na kumfuata kwa mwendo wa haraka!
“Haloo dada…” mlinzi yule akamwita Sajini Sofia.
“Mh!” Sofia akaguna tu, na kutaka kuendelea na safari kwa kujifanya kama vile hakumsikia.
“Samahani dada…nakuomba…”
“Mimi?” Sajini Sofia akamwuliza huku akijisogeza karibu na kichaka kimoja kilichofungamana kando ya uzio wa michongoma.
“Nisubiri hapo!”
“Haya…”
“Hujambo dada?”
“Mi’sijambo…sijui wewe…”
“Mimi mzima…” mlinzi yule akasema na kuongeza. “Sijui unaelekea wapi?”
“Mbona unaniuliza hivyo?” “Nauliza kwa sababu ni kazi yangu! Isitoshe barabara hii haitokezi upande wa pili…kumezibwa! Upo?”
“Aisee?” Sofia akasema baada ya kuona kuwa hakuwa na ujanja tena!
“Kwani ulikuwa unakwenda wapi, pengine ninaweza kukusaidia…” Mlinzi yule akamwambia Sofia . Hata hivyo akili ya haraka ikamjia Sofia kichwani mwake na kuamua jambo la kufamnya papo kwa hapo!
“Nakwenda huku…” akamwambia.
“Huku wapi?” Akauliza mlinzi yule huku akiyakodoa macho yake
“Nasema huku!” Sofia akamwambia huku akiachia pigo moja la nguvu, tena la kushtukiza!
“Oh!” Mlinzi yule akaguna na kuruka mbali!
Kwa haraka Sajini Sofia akambeba na kumlaza ndani mya kichaka kile kilichokuwa pale kando. Na ile ni baada ya kuhakikisha amepoteza fahamu, na bunduki yake akaiweka mbali na alipokuwa. Kwa vyovyote Sofia alijua kwamba lilie pigo alilompiga mlinzi yule, lilitosha kumfanya apoteze fahamu zaidi ya saa nne, labda awaishwe hospitali haraka!
Baada ya kumvutia yule mlinzi ndani ya kichaka, Sofia akaangaza macho pande zote, lakini hakuona mtu yeyote, basi, naye akajiingiza ndani ya kichaka hicho na kujichimbia kwa ustadi mkubwa. Ni sehemu ambayo haikuwa mbali na ule uzio wa michongoma na ukuta wa chumba alichofungiwa Luteni James, punde tu baada ya kumfikisha.
*******
Alipokuwa ndani ya chumba maalum, Luteni James alifungwa kamba za mikono na miguu, akiwa amekaa kwenye kiti kimoja kilichokuwa mle. Muda wote alikuwa amejifanya kuwa amepoteza fahamu, kiasi kwamba vijana, Pierre na Toni waliomfunga, wakaondoka na kumwacha kwa kumfungia kwa nje. Hata hivyo hakuwa na wasiwasi wowote, kwani alijua kwamba Sajini Sofia alikuwa karibu akifuatilia nyendo zao mpaka pale walipofikia.
Muda siyo mrefu, mlango ukafunguliwa na Paul Rugoye akaingia akiwa ameongozana na wale vijana wawili, Pierre na Toni. Wakamkuta James bado ameegemea kiti, akijifanya kama bado amepoteza fahamu tokea apate kile kipigo!
“Mmefika salama na huyu mshenzi?” Paul Rugoye akauliza kwa uchungu huku akimwangalia.
“Ndiyo bosi…” Pierre na Toni wakasema kwa pamoja.
“Na bado amepoteza fahamu?”
“Ndiyo, ni baada ya kumpa kipigo katika kumdhibiti…kama unavyojua huyu mni mtu hatari sana !” Pierre akasema.
“Hakuna shaka, ilibidi mfanye hivyo,” Paul akasema na kuendelea. “Lakini atazinduka tu, kwani dawa yake iko jikoni. Hebu nipe kiberiti cha gesi nimwonyeshe!”
“Kiberiti ninacho!” Toni akasema na kumkabidhi Paul Rugoye kile kiberiti cha gesi.
“Safi sana , mimi ni mtesaji namba moja. Ni lazima atazinduka!” Paul akasema huku akikisogeza kile kiberiti katika shavu la James, kiasi kwamba aliyasikia maumivu makali na ngozi kuchubuka!
“Ooohps!” James akaguna kwa maumivu!
“Ahahahaaaa!” Wote wakacheka!
“Mh, oh!” James akazidi kulalamika!
“Unaona mambo hayo? Mimi nawajulia watu hawa. Hawawezi kunisumbua!” Paul akaendelea kusema huku akiendelea kumwangalia kwa uchungu. CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Upande wa pili, Toni na Pierre, walikuwa wakimwangalia, nao bastola zao fupi zikimwelekea, ingawa walikuwa wamemfunga kamba za mikono na miguu! Ukweli ni kwamba hawakumwamini!
“Ndiyo Bw. Mika…hujambo?” Paul akamwambia.
“Mimi mzima!” James akajibu.
“Karibu sana ndani ya himaya yangu, ingawa hukuja kistaarabu, zaidi ya kuletwa kwa nguvu. Pia, napenda kukueleza wazi, kwamba hatukuwa na jinsi nyingine zaidi ya kukuleta hivi!” Paul akaendelea kusema huku akizunguka ndani ya kile chumba.
“Ahahahaaa, hivi kweli wewe unaitwa Mika?”
“Kwani unafikiri naitwa nani?”
“Ulipokuja kukodi gari muda ule wa mchana, ulijitambulisha kwa jina la Mika…lakini siamini kamwe!”
“Basi, elewa, ndiyo jina langu…”
“Wewe bwana mdogo usijifanye mjanja sana . Ingawa utakufa muda wowote, ni budi utueleze kuwa wewe ni nani, na kwa sababu gani unatufuatilia?”
“Ah!” James akaguna. Hakusema kitu, bali akabaki akiyazungusha macho yake kwa wale watu watatu, Paul, Pierre na Toni, halafu akayarudisha tena kwa Paul.
Ukweli ni kwamba Luteni James hakuwa na wasiwasi, kwani alishapata mawasiliano kutoka kwa Sofia , ambaye hakuwa mbali kutoka katika chumba kile, kwa upande wa nyuma. Ni sehemu iliyokuwa na uzio, pamoja na kichaka alichokuwa amejichimbia ndani yake. Tuseme alikuwa anavuta muda ili kumpa nafasi Sofia aweze kumwokoa. Na Sofia aliyekuwa amejichimbia ndani ya kichaka, alikuwa akiyasikiliza mazungumzo yote yaliyokuwa yakiongelewa ndani ya chumba kile. Baina ya James, Paul, Toni na Pierre.
Ni kutokana na chombo cha mawasiliano alichokuwa nacho, ambacho kilikuwa na uwezo wa kunasa mawasiliano kutoka kwa Luteni James, ambaye naye alikuwa na kifaa hicho kilichokuwa mfano wa pete kidoleni. Chombo hicho ndicho kilichompa ishara James, kwamba Sofia hakuwa mbali naye kwa wakati ule. Basi, muda wote ule damu ilikuwa ikimchemka Sofia . Sofia alipoiangalia saa yake, ilikuwa imetimu saa kumi na mbili na nusu za jioni. Giza lilishaanza kuingia kutokana na hali ya hewa ya Arusha ilivyokuwa siku ile, hakuwa na wasiwasi wa kuonekana na ndiyo muda muafaka wa kuandaa zana zake za kazi.
Sofia akalifungua begi lake dogo na kuhakikisha kila kilichokuwa ndani kilikuwa salama, kisha akalibeba na kumuangalia yule mlinzi aliyekuwa amepoteza fahamu amelala kwa kusambaratika! Sofia hakumsemesha, bali akachomoka mbio, halafu akauruka ule uzio na kutua ndani kwa tahadhari na bastola ikiwa wazi katika mkono wa kulia. Baada ya kutua ndani, Sofia akaangalia pande zote na kuona mambo ni shwari. Ndipo akalifungua tena lile begi na kutoa kopo dogo lililokuwa na gesi maalum kwa kukatia vyuma, ambalo ni kwa ajili ya kazi za upelelezi.
Sajini Sofia akaliendea dirisha lililokuwa na nondo madhubuti, na mbao, ambalo lilikuwa katika chumba alichofungiwa James. Akaiwasha gesi na kuanza kukata zile nondo kwa moto mwembamba uliokuwa unawake, ambapo alikata kwa ustadi mkubwa na kuweza kupata sehemu yakupita mtu mzima. Alipomaliza kukata, Sofia akaendelea kubanisha huku akisikiliza katika chombo chake jinsi mazungumzo yalivyokuwa yanaendelea mle ndani.
“Wewe! Hutaki kusema sivyo?” Paul Rugoye akasikika akimwuliza.
Luteni James akanyamaza kimya!
“Tapika yote!” Pierre akamwambia!
James hakujibu!
“Mimi naona tummalize huyu mshenzi!”
“Hebu niachieni mimi nimmalize!” Pierre akasikika akisema na pia mlio wa kukoki bastola ukasikika!
“Ruksa, mmalize!” Amri ikatolewa!
Kitendo bila kuchelewa, Sajini Sofia aliyekuwa kule nje, akalipiga kumbo lile dirisha la mbao na kuingia nalo kwa kishindo! Halafu akatua na kuwashangaza wote waliokuwa mle ndani na kuwafanya washikwe na bumbuwazi kwa muda! Kabla hajatulia akafyetua risasi mbili zilizompata Paul kifuani!
“Uuups!” Paul Rugoye akaguna na kuruka juu! Alipotua chini alikuwa maiti!
“Hatari!” Pierre akasema huku akili yake ikifanya kazi ya ziada ya kujiokoa! Hakika aliona ulikuwa ni mtafutano wa hali ya juu, na ni lazima akabiliane na hali ile!
“Mungu wangu!” Toni naye akasema huku akiangalia uelekeo pa kutokea!
Sajini Sofia akapiga risasi nyingine kuwaelekea Toni na Pierre waliokuwa wamesimama ukutani. Lakini cha ajabu ni kwamba watu wale wawili wakaruka kisarakasi na kuzikwepa zile risasi kiufundi, zikagota ukutani, na baada ya kutua chini, wakajizungusha tena na kuuvamia mlango wa mbao na kutoka nao nje huku wakitimua mbio!
Baada ya kutoka nje tu, Toni na Pierre wakalikimbilia gari lile, Land Rover Discover lililokuwa pale nje. Wakaingia ndani yake, kwani milango ilikuwa haijafungwa, Toni akiwa dereva, akalitia moto na kuliondoa kwa mwendo wa kasi kwa kupitia getini, kwa kuifuata barabara ya kokoto hadi katika barabara kuu ya lami inayoelekea Njiro. Toni akalisimamisha gari na kuangalia kushoto na kulia, palikuwa shwari, hakukuwa na gari.
“Toni,” Pierre akamwita.
“Sema...” akasema Toni.
“Unaona kile?”
“Kitu gani?”
“Kuna gari limepaki pale, bila shaka ndilo alilokuja nalo yule mwanamke aliyetuvamia mle ndani!”
“Ni kweli, ndiyo lenyewe!”
“Sasa?”
“Dawa ndogo, ili wasitufuatilie, ngoja nikategeshe Bomu !” Pierre akasema.
Pierre akachukua bomu moja lililokuwa ndani ya gari, halafu akashuka haraka na kulikimbilia gari lile, Nissan Patrol. Kwa vile milango ilikuwa imefungwa, hakupoteza muda, akavunja kioo kimoja cha upande wa kulia, halafu akategesha lile bomu kwenye kiti cha dereva. Baada ya kutegesha, Pierre akarudi tena kwa mwendo wa kasi na kupanda garini. Toni akaliondoa kwa mwendo wa kasi kuelekea upande wa Njiro!
Kazi moja tu!
Hatimaye wakafika Njiro. Gari likasimamishwa sehemu iliyokuwa na giza , halafu wakashuka na kuziendea nyumba zile za Umoja wa Mataifa kwa tahadhari ya hali ya juu. Bastola zao zilikuwa wazi mkononi, wakiwa wamepanga kulipua nyumba nzima kwa mabomu, na kusambaratisha wote waliokuwa wanaishi mle ndani, kisha watokomee zao! Hakika walidhamiria!
********

Sajini Sofia alimfungua kamba Luteni James, ambazo alikuwa amefungwa, na bila kupoteza muda wakatoka nje kwa kasi ili kuwawahi watu wake, Toni na Pierre, lakini wakakuta wameshapotea gizani! Nao wakapanga kuwafuatilia!
ITAENDELEA
0.jpeg
 
Simulizi : Msaliti Asakwe

Sehemu Ya Tano (5)

“ Sofia !” James akamwita.
“Mkuu!”
“Bado tuna kazi…”
“Tena si kidogo…”
“Inabidi tuwafuatilie…nahisi watakuwa wamekimbilia Njiro!” James akasema.
“Hata mimi nahisi hivyo!”
“Gari umeliacha wapi?”
“Ok, twende zetu!”
Basi, L:uteni James na Sajini Sofia wakatoka pale huku wakikimbilia na nusu wakitembea, kuliendea lile gari, Nissan Patrol, wakati huo wakiwa wameshagawana silaha tayari kwa mapambano. Damu ilikuwa inawachemka, na hata baada ya kulifikia gari hilo wakakuta dirisha moja limevunjwa!
“Mh, Sofia usipande!” Sofia akauliza.
“Kwa nini mkuu?” Sofia akauliza.
“Hebu subiri…” Luteni James akasema huku akiinamisha kiti cha dereva.
Akakuta bomu limetegeshwa!
“Vipi mkuu?” Sofia akazidi kuuliza!
“Kuna bomu!” Akasema James.
“ Bomu ?”
“Ndiyo, tusipoteze muda, kwani kazi ya kulitegua itazidi kutuchelewesha. Twende tuwafuatilie kule Njro!” James akasisitiza!
“Tukodi teksi.”
“Ni jambo la muhimu!” Luteni James na Sajini Sofia walijua kuwa waliotegesha bomu lile hawakuwa wengine zaidi ya Toni na Pierre. Hatimaye wakasimamisha teksi moja iliyopita pale, na kumwambia dereva awapeleke Njiro. Baada ya kupanda tu, dereva akaiondoa teksi kwa mwendo wa kasi kidogo. Lakini baada ya muda kiktu cha ajabu kilitokea nyuma, kwani kishindo kikubwa kilitokea nyuma yao ! Kilikuwa ni kishindo kikubwa kilichoambatana na moshi mkubwa na moto!
Ni lile bomu liliokuwa limetegwa kwenye gari lile na kulipuka na kulisambaratisha gari vipande vipande kiasi cha kutia hofu! Hata hivyo hawakukatisha safari yao baada ya lile tukio, wakaamua kuelekea Njiro kuwafuatilia Toni na Pierre. Baada ya kufika eneo la Njiro, wakashuka eneo la Njiro, wakashuka mbali kidogo na kumlipa dereva ambaye walimruhusu aondoke. James na Sofia wakaanza kuziendea zile nyumba za Umoja wa Mataifa kuwafuatilia Toni na Pierre.
Ili wasionekane, Luteni James na Sajini Sofia wakatembea kwa mwendo wa kuinama, na hatua za haraka haraka. Kwa bahati nzuri waliweza kuwaona Toni na Pierre wakielekea katika uzio wa nyumba zile ili wauruke na kuweza kutegesha bomu. Nao wakawafuatilia hadi walipofika kwenye uchochoro mmoja uliotenganisha nyumba na nyumba. Wakabanisha pale huku wakiwaangalia adui zao, ambao ndiyo kwanza walikuwa wakimaliza kuuruka uzio sehemu iliyokuwa na giza kutokana na kivuli.
“ Sofia , umewaona?” Luteni James akamwuliza.
“Nimewaona mkuu!”
“Basi, ni lazima tuwahi kabla hawajafanya madhara yoyote!”
“Na kweli,” Sofia akasema. “Ni lazima tuwatie mbaroni…”
Luteni James alipopata nafasi nzuri, akanyanyua bastola yake kwa mikono miwili. Akalenga shabaha kuelekea kwa Toni aliyekuwa ameongozana na Pierre, akafyetua risasi mbili ambazo zilimkosakosa na kuchimba ardhi! Toni akaanza kukimbia huku akijizungusha hewani kuelekea upande wa pili wa nyumba zile za Umoja wa Mataifa. James akaanza kumwandama kwa mwendo wa kasi hadi walipofika mwisho wa nyumba, palipokuwa na ukuta. Toni akashindwa kuendelea, na kusimama tayari kukabiliana na James kwa mtindo wa kareti, akimwita kwa hasira
“Njoo nikuonyeshe!” Toni akasema huku akijiweka tayari kutoa pigo!
“Huniwezi!” James akamwambia huku akirusha pigo la kushtukiza.
Lakini Toni alikuwa makini, kwani aliliona pigo lile na kuliepa kwa ustadi. Toni akarudisha pigo moja punde tu baada ya kukwepa. Ni pigo zuri ambalo lilimpata James na kumfanya apepesuke na kujigonga ukutani. Akayauma meno. Pamoja na kupata pigo lile, James hakukata tama, akajikusanya kwa nguvu zake na kuruka huku akijizungusha angani. Akatoa vipigo mfululizo vilivyompata Toni na kumfanya aanguke chini. Palepale James akamuwahi na kumdhibiti kwa kuikusanya mikono yake yote! Toni akaguna kwa maumivu makali sana !
“Ooohps!”
“Tulia, hapa umefika!” James akaendelea kumwambia Toni. Na wakati huo Toni alikuwa anajitahidi kujichomoa, lakini kamwe hakufanikiwa!
“Oohps! Mungu wangu!” Toni akaendelea kusema huku akigeuza kichwa chake kumwangalia James. Hakuwa na ujanja. Kiama chake alikiona wazi kikimnyemelea. Kwa mbali akawa anajuta kwa kujiingiza katika mpango ule wa uhalifu!
********
Upande wa pili, Sajini Sofia alimwandama Pierre kule alipokimbilia, kwani alishajua kuwa wamevamiwa. Wakakimbizana huku wakirushiana risasi na kuzikwepa kiufundi wa hali ya juu. Pierre akafyetua risasi mpaka zilipomwishia na kuamua kuitupa ile bastola aliyokuwa nayo, na wakati huo akiwa amejibanza na ukuta akipanga mbinu za kumkabili Sofia .
Baada ya kuona mambo magumu, Pierre akaamua kuchomoka na kuambaa na ukuta, kisha kuuruka uzio hadi nje! Sofia naye alikuwa akiendelea kumwandama tu, hadi alipotua kule nje ya uzio. Naye Sofia akauruka uzio, kuendelea kumfukuza, ambapo Pierre alilikimbilia lile gari, Land Rover Discover walilofika nalo pale. Akaufungua mlango na kupanda ndani yake haraka, kisha akalitia moto na kuliondoa kwa mwendo wa kasi huku magurudumu yake yakitimua vumbi jingi! Aliamua kutimua mbio kulikwepa sakata lile!
Baada ya Pierre kuondoka na lile gari, Sajini Sofia hakumkawiza hata kidogo, kwani alijipinda na kufyetua risasi tatu, ambazo zilimpata Pierre mkononi. Akauma meno kutokana na maumivu makali, na damu kumtoka kwa wingi mithili ya bomba. Na kwa vile gari lile lilikuwa linakwenda kwa mwendo wa kasi, lilikwenda kugonga mti mkubwa na kupinduka kama mita thelethini mbele ya Sofia. Sofia akabaki amesimama vilevile huku ameyauma meno yake kwa uchungu, akiliangalia jinsi gari lile lilivyokuwa linapinduka na kugota kwenye mtaro!
Kwa haraka Sajini Sofia akakimbilia na kumchomoa Pierre ndani ya gari ambalo lilikuwa limepondeka. Akamweka chini ya ulinzi na baadaye kuwaunganisha pamoja na Pierre, aliyekuwa amejeruhiwa mkono wake kwa risasi. Ikawa ni bahati kuwapata Toni na Pierre wakiwa hai, hivyo wakawalaza chini kifudifudi huku wakigugumia kwa maumivu! Ving’ora vya magari ya polisi viliweza kusikika kutoka mjini, kudhihirisha kwamba walikuwa wanakwenda kutoa msaada.
Pia, magari matatu aina ya Land Rover 110 Defender, yaliyosimama pale punde tu yalipofika. Askari polisi waliokuwa na silaha wakishuka haraka na kulizingira eneo lote. Muda wote ule, na pia wakiwa na watuhumiwa wale hatari! Baada ya dakika kumi na tano, Meja Bombe akafika na kuwakuta vijana wake, Luteni James na Sajini Sofia wakiwa na wale watuhumiwa wao, Toni n Pierre, ambapo aliwapongeza kwa kazi ile nzito. Hatimaye Meja Bombe na vijana wake, wakapanda gari la Idara ya Usalama wa Taifa, wakiwa na watuhumiwa wao. Wakaondoka kuwapeleka katika sehemu inayohusika tayari kwa kuwahoji ipasavyo, kieleweke kiini cha tatizo lile. Na hata walipoondoka katika eneo lile la Njiro, kazi nyingine waliwachia askari wa Jeshi la Polisi, ambao walianza kufanya uchunguzi na kulinda. Pia, Meja Bombe, Luteni James na Sajini Sofia walipitia eneo la Kijenge, nyumbani kwa Paul Rugoye, ambapo walikuta kuna askari polisi wengine wakifanya uchunguzi katika nyumba ile, pamoja na kuichukuwa maiti ya Paul Rugoye, na yule mlinzi aliyekuwa amepoteza fahamu baada ya kupata kipigo kutoka kwa Sajini Sofia . Maiti ya Paul ilikuwa inakwenda kuunganishwa na zile za Jean na France zilizokuwa zimehifadhiwa katika Hospitali ya Mount Meru , mjini Arusha.
Baada ya kutoka katika nyumba ya Paul Rugoye, wakaelekea sehemu ile walipokuwa wamelipaki gari aina ya Nissan Patrol la Idara ya Usalama wa Taifa, ambalo alikuwa amefika nalo Sofia wakati akiwafuatilia Toni na Pierre, walipokuwa wamemteka Luteni James. Walichokuta pale kilikuwa ni vipande vya mabati yaliyotapakaa baada ya kusambaratishwa na bomu lililotegwa na Pierre ili kuwamaliza kabla hawajawafikia!
Eneo la tukio walikuta kuna askari polisi waliokuwa wamezungushia utepe maalum wa rangi ya njano, ili kuzuia eneo hilo lisiingiliwe na kusubiri wataalam wa mabomu kutoka Jeshi la Wananchi kwenda kuchunguza mlipuko ule. Baada ya hapo wakaondoka kuelekea katikati ya jiji na watuhumiwa wao!
********
Saa kumi na mbili na nusu za asubuhi, Luteni James alishtuka kutoka katika usingizi uliokuwa umemwelemea kutokana na uchovu wa pilikapilika za usiku uliopita. Hata hivyo hakupenda kuendelea kulala, bali aliamka na kuelekea bafuni kuoga maji ya baridi ili kuuondoa uchovu ule. Alipomaliza kuoga akarudi chumbani na kuvalia nadhifu, tayari kwenda kupata kifungua kinywa kule hotelini. Lakini wakati akijiandaa kutoka, simu yake ya mkononi ikaita. Mpigaji alikuwa ni Meja Bombe.
“Mkuu…naomba maelekeza…”
“Habari za kuamka…”
“Ni nzuri mkuu!”
“ Kama umeamka salama ninashukuru,” Meja Bombe akasema na kuendelea. “Basi, ninawahitaji wewe na Sofia hapa ofisini kwa majukumu wengine. Sofia naye nimeshamjulisha, hivyo jiandaeni, nitamtuma dereva ampitie kila mmoja hotelini kwake. Ni matumaini yangu umenielewa!”
“Nimekuelewa mkuu!” Luteni James akasema.
“Ok, fanya hivyo,” Meja Bombe akamaliza.
Baada ya kumaliza maongezi, Luteni James akaufunga mlango wa chumba chake. Akatoka kuelekea hotelini ambapo alitafuta sehemu nzuri ya kukaa na kuagiza kifungua kinywa alichokula haraka haraka na kumaliza, kwani alikuwa anahitajiwa ofisini. James akatoka nje ya Hoteli ya Serena, na nje akalikuta gari la idara likimsubiri, likiwa limepaki upande wa pili wa barabara.
Dereva alikuwa ni kijana Robert, aliyekuwa anamsubiri ndani ya gari, na yeye akaliendea na kupanda. Wakasalimiana na kuendelea na safari huku wakimpitia Sofia kwenye hoteli ya Victoria Villa, mtaa wa Bondeni. Baadaya kufika wakakuta Sofia ameshajiandaa, akapanda garini na kuondoka. Gari likaondolewa kuelekea katikati ya mji ilipo ofisi. Baada ya robo saa tu wakafika na dereva akalipaki katikati ya magari mengine sehemu ya maegesho na wote wakashuka na kuingia ndani.
Mle ndani walimkuta Meja Bombe ameshafika muda mrefu, akawakaribisha ndani ya ofisi ile nadhifu na wote wakajichukulia nafasi kwenye viti na kukaa. Meja Bombe akavuta pumzi ndefu huku akiwaangalia, halafu akasema:
“Ni matumaini yangu nyote mmeamka salama, na poleni sana kwa misukosuko iliyowakuta usiku wa jana. Lakini yote ni majukumu yetu ya kazi zetu hizi ambazo tumeapa kuzifanya…”
“Ndiyo mkuu, kwa ujumla mimi nimeamka salama,” Luteni James akasema.
“Hata mimi nimeamka salama mkuu...” Sajini Sofia naye akasema huku akionekana mchangamfu, na uzuri wake kuongezeka.
“Nafurahi sana kama nyote muwazima. Hata hivyo nilichowaitia ni kwamba kuna kazi nyingine ya kuwahoji watuhumiwa wale, na pia kuandika maelezo yao kabla ya kuwakabidhi sehemu husika.”
“Tumekuelewa mkuu, tuko timamua...” James akasema kwa niaba yao wawili.
“Ok, twendeni chumba namba 10 ambacho ni maalum kwa mahojiano.”
“Sawa mkuu!” Wote wakasema kwa pamoja!
Halafu wakanyanyuka na kuelekea katika chumba namba 10. Ni chumba cha kuwahoji watuhumiwa wenye makosa makubwa ya kuhatarisha Usalama wa Taifa kwa ujumla, ambacho kilikuwa kikubwa chenye vifaa mbalimbali vya kumwezesha mtu auseme ukweli wa jambo analohojiwa. Baada ya kuingia wakakaa kwenye viti vilivyokuwa pembeni, na upande wa mbele paliwekwa viti viwili kwa ajili ya kukalia watuhumiwa wale, Toni na Pierre, waliotegemewa kuhojiwa.
Hatimaye majira ya saa nne za asubuhi, Toni na Pierre wakaingizwa ndani ya chumba kile wakisindikizwa na askari maalum, Polisi- Jeshi (Military Police. MP) waliokuwa na silaha. Wakawakalisha katika vile viti viwili, ambapo Pierre alikuwa amefungwa bendeji katika mkono wake uliokuwa umejeruhiwa kwa risasi usiku wa jana yake. Meja Bombe alikuwa amekaa mbele. Akakohoa kidogo ili kusafisha koo lake, huku pia akiwaangalia Toni na Pierre, halafu akasema kwa sauti ndogo lakini iliyosikika kwa kila mmoja aliyekuwa pale:
“Jamani, tumekutana hapa kwa ajili ya mahojiano maalum na nyie watu wawili. Hivyo tunaomba mtueleze ukweli mtupu juu ya maswali tutakayowauliza.”
Toni na Pierre wakabaki wakimkodolea macho!
“Haya, wewe jina lako nani?” Meja Bombe akamwuliza Pierre akiwa tayari kuandika.
“Naitwa Pierre Bisamo…” Pierre akasema huku akitaja umri wake, miaka na kabila.
“Kwa hivyo umetokea nchini Rwanda ?” “Ndiyo, nimetokea nchini Rwanda ,” Pierre akasema na kuendelea. “Na tulikuwa tumeongozana na wenzangu, Jean na France. Na safari ya kuja hapa Arusha tumetumwa na bosi wetu, Kanali Fabio Rushengo aliyeko Kibungo nchini Rwanda …”
“Kanali?” Akauliza Meja Bombe. “Aliwatuma kuja kufanya nini?”
“Alitutuma kuwafuatilia wale vijana watatu, Roman, Teobale na Laurent, ambao walikuwa wamemtoroka katika himaya yake ya siri, wakiwa na Diski zilizokuwa na mpango mzima wa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994…” Pierre akaeleza yote huku Meja Bombe akiwa anaandika katika faili maalum.
Baada ya kumaliza kumhoji Pierre , Meja Bombe akamgeukia Kijana Toni, ambaye naye alijieleza kuwa hakuongozana na watu wale, bali ni mwajiriwa wa kampuni ya Rugo Safaris, akiwa kama mlinzi, ambaye anafuata amri zote za bosi wake hata kama ni kuua mtu! Bombe alipomaliza kumhoji, akaona kuwa yule hakuwa mtu wao, bali iliwabidi wamkabidhi kwa Jeshi la Polisi kwa hatua nyingine za makosa ya Jinai.
Lakini kwa Pierre, Bombe akaona kuna umuhimu wa kumkabidhi kwa wahusika wa Mahakama ya Kimataifa ya Watuhumiwa wa Mauaji ya Rwanda , iliyoko jijini Arusha. Hatimaye Toni na Pierre wakaondolewa na kurudishwa katika sehemu waliyokuwa wamehifadhiwa mwanzo. Halafu akaamuru wale vijana mashahidi muhimu, Roman, Teobale na Laurent wapelekwe pale kwa ajili ya kuhojiwa. Baada ya dakika tano wakapelekwa ndani ndani ya chumba kile, na kwa vile kiongozi wao alikuwa ni Roman, basi Meja Bombe akamtaka yeye ndiye aeleze yote kwa niaba yao .
“Naomba unieleze hali halisi ilivyokuwa kutokea mwanzo…” Meja Bombe akamwambia Roman, ambaye alikuwa amekaa bila kuwa na wasiwasi wowote! Alikuwa anajiamini kwani hakuwa mtuhumiwa zaidi ya shahidi muhimu sana , huo ndiyo ukweli!
“Ni kwamba sisi watu watatu mnaotuona, ni kati ya watu zaidi ya mia nne, ambao tulikuwa chini ya himaya ya Kanali Fabio Rushengo, ambaye ni msaliti wa Serikali ya Rwanda , na mhusika mkuu wa mauaji ya Rwanda aliyokuwa akiyaongoza kwa njia moja ama nyingine kwa kuyahamasisha. Baada ya mauaji yale, Fabio alijificha porini bila kujulikana, kisha akakusanya baadhi ya askari waliokuwa wanamtii, tukiwemo sisi. Akatuweka katika kambi moja ya siri iliyok katika msitu wa Kibungo, nchini Rwanda …”
“…Kwa muda wote Kanali Fabio alikuwa anavalia sura ya bandia baada ya kufanyiwa upasuaji, kiasi ambacho ilikuwa siyo rahisi watu wengi kumfahamu hata siyo rahisi watu wengi kumfahamu hata maafisa wenzake. Basi, kipindi chote tulichokuwa ndani ya kambi, Fabio alikuwa akitutumikisha kazi pasipo malipo yoyote kwa muda wa miaka kumi. Ndipo tulipoamua kumsaliti nqa kukimbilia hapa nchini Tanzania ili kujisalimisha, na pia ikiwezekana kuyaeleza yote katika Mahakama ya Umoja wa Mataifa, inayohusika na mauaji ya Rwanda , kwani ushahidi tunao!” Roman akamaliza kusema.
“Nimekuelewa vizuri sana . Unasema kwamba ushahidi mnao?” Bombe akauliza.
“Ndiyo, ushahidi tunao. Baada ya kumkimbia Kanali Fabio, pia tuliondoka na Diski zilizokuwa na mpango wa maovu aliyoyafanya baada ya kupekuwa ndani ya ofisi yake. Ndiyo maana akawatuma watu wale watumalize kabla haijafika mikononi mwa wahusika!”
“Vizuri, tunashukuru kwa maelezo hayo,” Meja Bombe akasema akiwa ameridhika na maelezo yale ya Roman. Bila kupoteza muda akaruhusu vijana, Roman, Teobale na Laurent, waondolewe ndani ya chumba kile na kurudishwa katika makazi yao Njiro. Baada ya wote kuondoka ndani ya chumba namba 10, wakabaki, Meja Bombe, James na Sofia, wakimalizia kukusanya maelezo yale muhimu!
********
Baada ya kumaliza kazi ya kuandika maelezo yale, Meja Bombe akawageukia Luteni James na Sajini Sofian ambao walionyesha dhahiri kwamba wana uchovu uliokuwa umewajaa. Halafu akawaambia kwa sauti ndogo lakini yenye msisitizo:
“Bado tuna safari nyingine…”
“Ndiyo mkuu!” Luteni James akasema.
“Tunakwenda kwenye Hospitali ya Mount Meru kuzitambua maiti za watu wale!”
“Sawa mkuu…ni jambo la muhimu sana .”
Hawakupoteza muda, wote watatu wakatoka nje na kupanda gari kuelekea Hospitali ya Mount Meru , ambapo hapakuwa mbali sana na ilipo ofisi yao . Meja Bombe alikuwa na fikra nyingi sana baada ya kuupata ukweli wa kisa kizima kilichokuwa kinasababisha mauaji yale. Na hata baada ya kufika hospitali, wakajitambulisha na kuruhusiwa kuingia ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti.
Baada ya kuingia wakawakuta Maafisa wa Jeshi la Polisi na Daktari Maalum aliyekuwa akizifanyia uchunguzi maiti wale watatu, Paul Rugoye, Jean na France.
Wakasalimiana na kuongea mawili matatu hadi uchunguzi ule ulipokamilika. Kibali kikatolewa kwa familia ya Paul Rugoye kuuchukuwa mwili kwa ajili ya maziko, na zile maiti mbili za Jean na France zikaendelea kuhifadhiwa kusubiri utaratibu mwingine utakaofuata. Hivyo, Meja Bombe, James na Sofia wakaondoka pale hospitali na kwenda kupumzika kutokana na uchovu!

Pia, Meja Bombe aliwaambia James na Sofia wasubiri kwanza, wakiwa pale Arusha, mpaka watakapopata taarifa nyingine kutoka kwa Brigedia Matias Lubisi, Makao Makuu, Dar es Salaam , kwani kazi ilikuwa bado nzito. Ilibidi Msaliti Kanali Fabio asakwe na kukamatwa! Baada ya kuachana, Meja Bombe alifanya utaratibu wa kulishughulikia suala lile, kwa kuutaarifu Ubalozi wa nchi ya Rwanda , hapa nchini, ili umfuatilie msaliti yule aliyesemekana amejichimbia katika msitu mzito wa Kibungo.
Taarifa hizo zikafanyiwa kazi mara moja!
********
KIZAAZAA NGOMENI!
Nchini Rwanda katika ya ngome ya Kanali Fabio Rushengo, ndani ya msitu wa Kibungo, mambo yalikuwa magumu. Fabio alikuwa amechanganyikiwa baada ya kupata taarifa kwamba vijana wake, Jean na France, pamoja na mwenyeji wao, Paul Rugoye, walikuwa wamekufa katika pilika za kuwasaka wasaliti, Roman, Teobale na Laurent, waliotorokea nchini Tanzania. Isitoshe kijana wake mwingine, Pierre , alikuwa amekamatwa akiwa chini ya ulinzi akihojiwa juu ya aliyewatuma kazi ya kufuatilia wale mashahidi muhimu. Kwa vyovyote alijua kuwa ni lazima angeusema ukweli wote!
Basi, akaona cha muhimu ni ni kutoroka nchini Rwanda kabla hajakamatwa. Ingawa Fabio alizipata habari zile, hakuwaambia wafuasi wake kwanza, kwa kile alichodai yeye ni kuwavunja nguvu. Kwa hiyo akapanga atoroke peke yake na kuelekea sehemu yoyote ambayo angeiona inafaa hasa ukizingatia alikuwa na sura ya bandia iliyokuwa siyo rahisi kwa mtu yeyote kumtilia mashaka. Na kwa vile Kanali Fabio ndiyo alikuwa ndiye mwenye njia zote za mawasiliano, aliweza kuzidhibiti ili wafuasi wake wasizipate habari zile, halafu wakazivujisha.
Muda siyo mrefu akawa amejichimbia ndani ya handaki lake huku akikusanya nyaraka muhimu, pamoja na idadi kubwa ya fedha za Rwanda na zile za nje, hasa, faranga za Ufaransa na dola za Marekani. Zote akazijaza katika mkoba wake mkubwa wa ngozi Baada ya kuhakikisha kila kitu tayari, Kanali Fabio akawaambia vijana wake wawili, mafundi magari, walifanyie matengenezio gari moja aina ya Toyota Land Cruiser, lililokuwa gereji, na baada ya kumaliza matengenezo, walijaze mafuta ya kutosha na mengine ya akiba. Kusema kweli kila mmoja alishangaa baada ya kumwona kiongozi wao akifanya pilikapilika zile!
Lakini hakuna mtu aliyethubutu kumuuliza!
*******
Wakati Kanali Fabio Rushengo alipokuwa anapanga mikakati yake ya kutoroka, huku nyuma, Idara ya Usalama wa Taifa nchini Tanzania , ilikuwa imeshatuma ujumbe maalum nchini Rwanda , juu ya kuelezea kuwepo kwa mtu yule hatari, Kanali Fabio Rushengo, mhusika mkuu wa mauaji ya Rwanda , yaliyofanyika mwaka 1994, na yaliyosababisha vifo vya watu laki nane! Na mtu huyo kajichimbia katika msitu wa Kibungo akiwa na wafuasi wake wengi!
Habari zile zilipofika nchini Rwanda , hawakulaza damu. Wakuu wa Kijeshi wakaamua kupanga Operesheni Maalum kwa kutumia vikosi vya kijeshi, vya nchi kavu na angani. Baada ya kukamilika wakaelekea ndani yam situ wa Kibungo, uliokuwa umefungamana na miti na vichaka, bila kuacha milima na mabonde. Kwanza kabisa zilipita ndege aina ya helikopta za kijeshi, ambazo zilikuwa zinafanya uchunguzi katika eneo lile lililoweza kuonekana kama kijiji tu.
Kanali Fabio akiwa na wafuasi wake, aliweza kuziona zile helikopta mbili zikirandaranda angani, katika eneo la kambi yao . Ni helikopta zilizokuwa na uwezo wa kushambulia kutoka angani kwa mitutu iliyokuwa inazunguka na kutoa risasi mfululizo. Hakika lilikuwa si jambo la kawaida, hali ya hatari ikaanza kunukia! Kanali Fabio akajua kuwa mambo ndiyo yaleyale aliyokuwa anayawaza!
Limelipuka!
“Vipi mkuu…mbona naona helikopta za Jeshi la Serikali zinazunguka katika anga zetu muda mrefu?” Msaidizi wake mkuu, Emmanuel Miburo akamuuliza bosi wake.
“Hata mimi nashangaa…sijui wanafuata nini?” Kanali Fabio naye akasema.
“Sasa tufanyeje mkuu?” Emmanuel akamuuliza ili kupata ushauri.
“Inatubidi tuwe macho, Siyo bure!” Kanali Fabio akamwambia Emmanuel huku wasiwasi ukizidi kumwandama na kupanga la kufanya!
Wakati wakiendelea na maongezi yao , mara helikopta zile zikaendelea kupita tena chinichini, kiasi kwamba Mmrubani wawili pamoja na askari waliovalia sare za kijeshi waliweza kuonekana waziwazi. Walielekeza silaha zao mitutu yake chini, tayari kwa mashambulizi!

“Hizo zinapita tena!” Emmanuel akasema huku akiangalia juu angani.
“Mh, hii ni hatari! Kusanya askari tuwe tayari!” Kanali Fabio akatoa amri mara moja!
“Sawa mkuu!” Emmanuel akasema huku akiondoka pale. Halafu akaenda kukusanya askari kambini pale!
Baada ya Emmanuel kuondoka, naye Kanali Fabio akachomoka mbio na kuingia ndani ya handaki lake. Akavalia nguo zake za kiraia, suti nyeusi, viatu vyeusi na ndani shati jeupe lililofuatiwa na tai nyekundu. Baada ya dakika tano akawa ameshabadilika pamoja na ile sura ya bandia aliyokuwa nayo, halafu akatoka nje na kuziona zile helikopta bado zinaendelea kuzunguka angani. Fabio akachukuwa kionea mbali (Darubini) na kuangalia walioko ndani yake, akaona ni askari waliokuwa wamejizatiti huku wakionyesha ishara kuelekea katika kambi ile!
Kanali Fabio akachukuwa bunduki moja aina ya Sub Machine Gun AK 47 iliyoondolewa kitako chake, pamoja na bastola aina ya Magnum maalum kwa jeshi. Vyote akavitia ndani ya ule mkoba wake na kuvipeleka ndani ya gari Toyota Land Cruiser analotegemea kuondoka nalo. Mawazo yake yote yalkuwa ni kutoroka tu, na wakati huo, msaidizi wake, Emmanuel, alikuwa ameshakusanya askari wake waasi, na kuwapanga. Wote wakajibanza na kujificha katika maficho maalum ndani na nje ya kambi ile. Walikuwa na silaha kali, kama bunduki za rasha rasha zilizoweza kutema risasi mfululizo.
Hakika kambi nzima ilikuwa imeingiwa na wasiwasi, ingawa pia, walijiandaa kukabiliana na yeyote anayejaribu kuwashambulia kutoka pande zote za kambi ile pamoja na angani. Askari wa miguu wa Jeshi la Serikali, waliwasili eneo lile la Kibungo, wakiwa katrika magari maalum ya kijeshi. Baada ya kuhakikisha wamefika karibu na kambi, kwa mujibu wa maelekezo waliyoyapata kwa kiongozi aliyekuwa ndani ya helikopta kwa njia ya Radio Call, askari hao wakashuka wakiwa na silaha kali na kuanza kutembea kwa miguu kuiendea ile kambi ya waasi kwa tahadhari ya hali ya juu. Walipohakikisha wamefika, askari wale wakaizunguka kambi huku wakijificha kila mmoja sehemu yake!
Tayari kwa mapambano!
Kiongozi wa Kikosi cha Jeshi la Serikali akachukua kipaza sauti na kuanza kutoa amri kwa askari wale waasi kwamba wajisalimishe kwa kuwa walikuwa wameshajulikana maficho yao . Sauti ile ikasafirishwa na mwangwi kutokana na ukimya uliotawala sehemu ile. Baada ya kukaa zaidi ya dakika kumi, hakukuna mtu aliyejisalimisha! Sauti ya kipaza sauti ikarudia tena kwa mara ya pili, lakini mambo yakawa vilevile, hakuna aliyejisalimisha zaidi ya kuanza mashambulizi ya risasi!
Waasi walirusha risasi kwa vikosi vya majeshi ya Serikali, ambapo mapigano makali yakaanza kwa kurushiana risasi mithili ya mvua.
Vikosi vya Serikali vilikuwa vinasaidiwa na helikopta zile mbili, ambapo wafuasi wa Kanali Fabio wakaanza kukimbia na wengine kupoteza maisha! Kambi ikateketezwa kwa moto ukizingatia eneo kubwa lilikuwa limejengwa kwa vibanda vya nyasi. Wakati huo, Kanali Fabio alikuwa ameshakimbia kwa gari, akitorokea kuelekea upande wa Rusumo, mpakani mwa nchi za Rwanda na Tanzania .
Na kweli alifanikiwa kutoka eneo lile la mapigano yaliyokuwa yanaendelea na kumwacha msaidizi wake, Emmanuel akiendeleza mapambano na waasi wenzake. Hakuwa na habari nao tena! Kila mmoja afe kilwake! Waasi wakazidi kufa na wengine kutekwa au hata kukimbilia msituni zaidi! Askari wengi wa Serikali hawakumtilia mashaka Kanali Fabio, kwa jinsi alivyokuwa amevalia nadhifu suti na sura yake kubadilika tofauti na zamani.
Baada ya kukatiza katikati ya misitu na mabonde na kona kali, Fabio alifika Rusumo, karibu na mto, ikiwa ni ile sehemu iliyokuwa na boti maalum iliyotumika kuvusha watu ng’ambo ya pili. Hivyo, hakupenda kufika na gari lile hadi pale mtoni, isipokuwa aliliingiza ndani ya kichaka kimoja kilichofungamana. Baada ya kulipaki gari, Fabio akashuka akiwa amebeba lile begi kubwa, na ule mkoba wake uliokuwa na silaha ndani yake. Halafu akaanza kutembea kwa miguu kuelekea kule mtoni, ambapo alimkuta kijana mmoja aitwaye Bosco Kayenzi, anayehudumia boti ile kuvusha watu upande wa pili wa mto.
“Bosco!” Fabio akaita kwa sauti!
“Mkuu!” Bosco akaitikia kwa utii!
“Njoo!”
“Sawa mkuu…” Bosco akasema huku akimwendea. “Vipi Mkuu? Mbona saa hizi huku?” Akamuuliza.
“Hakuna haja ya kuhoji maswali! Nivushe ng’ambo ya pili ya mto!”
“Sawa mkuu!” Bosco akasema. Halafu akaiendea boti na kuisukuma kuielekeza majini.
Kanali Fabio akapanda na mizigo yake huku bado akiwa na wasiwasi mwingi umemtanda. Bosco akawasha injini na kuoiondoa boti kwa mwendo wa kasi kuelekea upande wan chi ya Tanzania .
“Mambo mabaya huko!” Fabio akamwambia Bosco!
“Kuna nini mkuu?”
“Kambi yetu imevamiwa na majeshi ya Serikali, na wafuasi wetu wengi wamekufa!”
“Mungu wangu! Sasa unakimbilia wapi?”
“Nakimbia tu!”
“Kweli mkuu?”
“Ni kweli…hata sijui nakimbilia wapi!”
“Sasa na mimi nitakimbilia wapi Mkuu?” “Huu siyo muda wa kuulizana maswali! Wewe twende!” Kanali Fabio akafoka!
Bosco akagwaya. Akaendelea kuiongoza boti iliyokuwa ikikata mawimbi kuelekea ng’ambo ya pili yam to, huku wote wawili wakiwa kimya kabisa. Hata hivyo kwa Kanali Fabio hakuwa na imani na kijana Fabio aliyekuwa anamvusha. Alipenda iwe siri yake, isije ikajulikana kama alikuwa amekimbilia upande ule. Hakumwamini mtu muda ule! Yeye alijua fika kwamba kama Bosco angeminywa kidogo tu, angetoa siri!
Boti ilipofika upande wa pili, Kanali Fabio akashuka akiwa na mizigo yake, na Bosco akabaki akimwangalia ataamua kitu gani, kama wataondoka wote ama la. Ni kitu ambacho Fabio alikuwa ameshakihisi, na hakupenda iwe hivyo! Aende naye wapi?
“Bosco!” Fabio akamwita.
“Mkuu!” Bosco akaitikia.
“Naona uishie hapa!” Fabio akamwambia huku akichomoa bastola!
“Niishie hapa?” Bosco akauliza huku macho yake akiyatoa!
“Ndiyo manaake…”
“Kivipi? Sijakuelewa mkuu…si tunasafiri wote?”
“Kwenda wapi?” Fabio akasema na kuongeza. “Nimesema siamini mtu yeyote!”
“Huniamini bosi?”
“Ndiyo. Nitasafiri mwenyewe kama nilivyo! Nina wasiwasi unaweza kunisaliti!”
“Siwezi kukusaliti mkuu!”
“Hapana…lazima nikuue tu, kwani nikikuacha hai utasema kwa majeshi ya Serikali! Hupaswi kuishi!” Kanali Fabio akasema huku akimlenga kwa bastola yake ya kijeshi!
Akafyetua risasi mbili zilizompata Bosco kichwani!
“Mama yangu! Oohps!” Bosco akapiga yowe kubwa! Akaruka juu na akatua ndani ya maji ya mto Rusumo!
Akazama majini, huku maji yakibadilika rangi na kuchukuwa wekundu wa damu!
Ni hatari sana !
“Mambo safi !” Kanali Fabio akasema huku akiibusu bastola yake. Kisha akauchukuwa mzigo wake na kuendelea na safari yake huku akiudhihirisha unyama wake!
********
Ni baada ya kumalizika kwa Operesheni ya kupambana na vijana wasaliti kutoka nchini Rwanda , ndipo Meja Bombe akabaki akisubiri taarifa kutoka kwa Brigedia Matias Lubisi, Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Pia, wapelelezi, Luteni James na Sajini Sofia, walikuwa wanataka kujua kilichokuwa kinaendelea baada ya kuhitimisha kazi yao !
Usiku wa siku hiyo, simu ya Meja Bombe iliita. Na alipoangalia namba za mpigaji, akaona ni za Brigedia Matias Lubisi, mkuu wake wa kazi, hivyo akaipokea:
“Haloo mkuu…naomba maelekezo…”
“Haloo…Bombe…habari za hapo Arusha..” Brigedia Matias Lubisi akasema.
“Habari ni nzuri mkuu…tunasubiri maelekezo yako…”
“Vizuri Meja…sikiliza kwa makini!”
“Sawa mkuu…”
“Kesho asubuhi, wote watatu mtaondoka hapo Arusha, kuelekea Ngara, Mkoani Kagera. Mtaondoka kwa ndege maalum ya jeshi kwani usafiri umeshaandaliwa. Hivyo basi, kesho hiyo asubuhi mtaripoti kwenye uwanja wa ndege wa Arusha, tayari kwa safari, sijui umenipata?”
“Nimekupata mkuu!” Meja Bombe akasema.
“Baada ya kufika hapo maelekezo yote mtayapata juu ya safari ya kwenda huko kwa kazi ya kumsaka msaliti, Kanali Fabio Rushengo, ambaye tuna wasiwasi anaweza kukimbilia hapa nchini. Majeshi ya Serikali ya Rwanda yameshaanza mashambulizi dhidi ya waasi!”
“Nimekuelewa mkuu!”
BAADA ya kupeana maelekezo, Meja Bombe hakukawia, akawataarifu Luteni James na Sajini Sofia , ambapo aliwaambia wajiandae kwa safari ile ya kwenda Wilayani Ngara. Asubuhi wote waliamka na kujiandaa, na dereva akawapitia kuondoka nao kuelekea uwanja wa ndege wa Arusha. Walipofika uwanjani, waliikuta ndege moja aina ya Twin Otter, ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania , ikiwa imepaki katika uwanja mdogo wa kuondokea.
Muda ulipowadia, Meja Bombe, Luteni James na Sajini Sofia walipanda ndani ya ndege, na ndege ikatiwa moto na hatimaye kuondolewa kuifuata barabara ya kurukia. Rubani akaongeza kasi na kuirusha kuelekea upande wa Mashariki. Hakika ilikuwa ni safari ndefu hadi walipotua katika uwanja wa ndege wa Ngara, uliokuwa unatumiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi. Wote wakashuka ndani ya ndege na kukuta gari moja aina ya Nissan Patrol likiwasubiri wao kuwapeleka sehemu husika walipokuwa wametayarishiwa malazi.
Wakati huo mapigano ndiyo yalikuwa yanaendelea baina ya majeshi ya Serikali ya Rwanda na wale waasi. Tuseme ni kwamba habari zile ndizo zilikuwa zimeenea na kutawala eneo zima la Ngara, sehemu iliyoko mpakani mwa nchi za Rwanda na Burundi . Hivyo Meja Bombe, James na Sofia, walipumzika kwa siku ile moja tu, ili kujiweka sawa kimazoezi.
Asubuhi yake iliwakuta wakiwa kwenye safari ya kuelekea Rusumo, mpakani mwa nchi mbili, Tanzania na Rwanda . Wakati huo, vikosi vya Jeshi la Wananchi wa Tanzania , vilikuwa vinafuatilia mapigano hayo ili kuhakikisha waasi wale hawavuki mpaka na kuingia nchini, kwa kuuvuka ule mto Rusumo, ambao ndiyo mpaka wenyewe. Baada ya kufika Rusumo, waliikuta ile helikopta ya jeshi ikiwa imepaki umbali wa kilometa kumi hivi kutoka ulipo mpaka, siyo mbali sana na mto Rusumo unaokatiza katikati ya milima mikubwa yenye mabonde na kona nyingi. Wote wakapanda ndani ya helikopta, ambako palikuwa na marubani wawili wanajeshi wenye vyeo vya Meja. Helikopta ikarushwa angani na kuanza kuzunguka eneo la mpakani, huku wakiwa na vyombo vya mawasiliano, ambapo walikuwa wakipata taarifa kwamba lile kundi la waasi lilikuwa limezidiwa. Lakini kilichowachanganya zaidi ni kwamba kiongozi wa waasi, Kanali Fabio Rushengo alikuwa ametoroka kwa kutumia gari na haijulikani amekimbilia wapi!
“Kanali Fabio hawezi kukimbilia sehemu nyingine zaidi ya huku Rusumo, kwani wamezingirwa…” Meja Bombe akasema huku akiendelea kuangalia kwa kionea mbali (Darubini) kilichoweza kuangaza kila sehemu na kuvuta kwa ukaribu.
“Vizuri, ngoja niilekeze helikopta upande wa Rusumo, halafu niishushe chini kiasi…” Rubani alisema, halafu akaielekeza kwa mwendo wa chinichini, kiasi ambacho ule mto Rusumo uliweza kuonekana vizuri wakiwa juu. Ulikuwa umefunikwa na miti mingi iliyofungamana sana .
“Naona kama kuna mtu pale ng’ambo yam to!” Meja Bombe akasema.
“Hata mimi namwona…tena amevaa suti nyeusi na kando yake kuna boti inayoonyesha kuwa amevuka nayo!” Akadakia Luteni James.
Rubani akairusha tena na kuwafanya wamwone vizuri, tena akiwa ameubeba ule mkoba wake wa ngozi. Alikuwa ni Kanali Fabio Rushengo, aliyekuwa anatafuta uelekeo wa kwenda, punde tu baada ya kumuua kijana Bosco, msaidizi wao na kumtupa ndani ya mto. Kanali Fabio akaanza kutimua mbio kuelekea kwenye kichaka cha miti iliyofungamana. Akajibanza pale huku akitweta ovyo, pengine akiangalia juu ilipo ile helikopta ya jeshi. Wakati huo, helikopta iliendelea kuzunguka katika eneo lile, huku Meja Bombe na wale marubani wakiomba msaada kwa kutumia redio ya mawasiliano.
Meja Bombe akiwa na kile kionea mbali, aliweza kumwona Kanali Fabio akiwa amejichimbia ndani ya kichaka huku akiufungua mkoba wake, ambapo aliitoa ile bunduki aina ya ‘Sub Machine Gun AK 47’ iliyokunjwa kitako na kuwa fupi. Pia, akachukuwa na ile bastola aina ya Magnum, vyote vikiwa vimesheheni risasi tayari kukabiliana nao wakiwa ndani ya helikopta. Rubani akaendelea kuishusha huku ikitimua vumbi, umbali wa mita mia moja tokea alipojichimbia Kanali Fabio.
“Naona ana bunduki…nafikiri ni kwamba anajiandaa kupambana!” Meja Bombe aliyekuwa anamwona vizuri, akasema kwa msisitizo!
“Huyu hafiki mbali! Sisi tuko wengi sana !” Luteni James akasema baada ya kugundua ni Fabio.
Ilibaki kazi moja tu!
Kumlipua!
*******
Akiwa bado ndani ya kichaka, Kanali Fabio Rushengo aliiangalia ile helikopta ilivyokuwa inazunguka angami. Kwa kiasi fulani ilimtia kichefuchefu kwa kuona kwamba ilikuwa inamsogeza karibu na kinywa cha mauti! Akaiweka vizuri bunduki yake na kujisemea moyoni:
“Hawaniwezi hawa washenzi! Hawanijui nini? Nitawamaliza wote! Mimi Komandoo!”
Na kweli wakati helikopta ile ilipogusa chini tu, mvua za risasi ziliwanyeshea kutoka kwa Kanali Fabio Rushengo aliyekuwa pale ndani ya kichaka amejichimbia! Lakini hakuna risasi hata moja iliyoleta madhara kwao, zaidi ya kupita kando. Kwa haraka wote watatu wakashuka na kuondoka kwa mwendo wa kuinama na silaha zao kuzielekeza juu!
Baada ya wote kushushwa, ile helikopta iliondoka na kwenda kutua sehemu nyingine kwa ajili ya usalama zaidi. Kila mmoja akaelekea upande wake kumzunguka mbabe yule wa kivita. Meja Bombe akatambaa kwa kujikinga na vichaka kuelekea alikojichimbia Kanali Fabio, na mkononi mwake alikuwa amekamata bastola nzito iliyosheheni risasi!
Luteni James yeye alitambaa kumzungukia upande wa nyuma wa kichaka kile. Sofia akamzungukia upande wa kulia kwa tahadhari ya hali ya juu. Muda wote Fabio alikuwa akifyetua risasi ovyo bila kujua kwamba nyuma yake alikuwa amezungukwa na James! Risasi alizokuwa anafyetua Fabio, zilikuwa zikichana matawi ya miti, vichaka na hata kung’oa magome ya miti!
Kilikuwa kizaazaa!
Lakini hakuna hata risasi moja iliyoweza kuleta madhara kwa wapiganaji wale mahiri. Ni mpaka risasi zilipomwishia na kumfanya abaki amechanganyikiwa asijue la kufanya! Hakutegemea kama angeweza kukamatwa hata siku moja, tena kibwege namna ile! Mtu aliyekuwa na himaya yake, akiwa na wafuasi wengi waliofuata amri yake! Tuseme ndiye aliyekuwa mwamuzi wa mwisho!
Luteni James alijivuta taratibu kutoka ndani ya kile kichaka hadi alipomfikia Kanali Fabio kwa nyuma yake, na muda huo alikuwa ameangalia mbele kuwaangalia. James hakupoteza muda, akamwambia kwa sauti kavu yenye kuamrisha:
“Simama hivyo hivyo ulivyo!”
“Mungu wangu!” Kanali Fabio Rushengo akasema
“Nyoosha mikono yako juu!”
“Ooohps!”
“Usijiguse!” Amri ikaendelea kutolewa. “Tembea hatua kumi mbele!”
Kanali Fabio akatii amri ile!
Akatembea kama alivyoamriwa huku akitupa bunduki na bastola chini! Halafu kwa mbele akakutana na mitutu miwili ya bastola ikimlenga! Walikuwa ni Meja Bombe na Sajini Sofia, ambao walimtokea mbele yake
Patamu hapo! “Mungu wangu!” Kanali Fabio akasema huku amechanganyikiwa!
“Umepatikana!” Meja Bombe akamwambia kwa sauti kavu!
“Na kweli nimepatikana!” Kanali Fabio akasema huku kweli akiliona giza !
Wakati huo Rubani wa helikopta alikuwa akiwasogelea kichinichini huku ikitimua vumbi jingi hadi pale walipokuwa. Wakamwingiza Kanali Fabio ndani na kuondoka naye kumpeleka kwenye Kituo maalum, ndani ya kambi ya kijeshi, eneo la Ngara.
Akahifadhiwa kusubiri hatua nyingine zitakazofuata!

MWISHO
 
Safi sana... Story nzuri...

Chapter Closed...

Cc: mahondaw
 
Habari mambo naitwa Mr Equator Nimeandika ujumbe huu kuku omba swala moja tu!
Mimi nimetengeza website ya ku share story ambayo ni EquatorStory
Je umekuwa ukipata tabu kupost story zako hapa?
Hili ndo suluhisho lako.
Mimi nataka nkupe nafasi ya kuwa mmoja wapo wa kwanza kutumia hii website
unda account yako na uweze kupost story yako mpya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom