Utoroshaji wanyama hai, Ikulu ya Kikwete yahusika

Shebbydo

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
1,174
1,937
UTOROSHAJI WANYAMA HAI
Ikulu ya Kikwete yahusika
Waandishi Wetu
Toleo la 443
3 Feb 2016

Walipewa blank cheque kujaza ‘mapesa’ wanayotaka SAKATA la kutoroshwa na kusafirishwa kwa wanyama hai kwenda Doha nchini Qatar limezidi kupata sura mpya baada ya kubainika kuwa miongoni mwa maofisa waandamizi Ikulu ya Tanzania walihusika katika biashara ya kuuza wanyama hao, Raia Mwema linafichua.

Taarifa mpya kuhusu sakata hilo pamoja na nyaraka zilizopatikana zinathibitisha kuwa hatua ya kutua nchini kwa ndege hiyo kijeshi ilitokana na kupata baraka zote kutoka kwa viongozi wa ngazi za juu, wakiwamo baadhi ya maofisa waandamizi wa Ikulu ya Dar es Salaam.

Chanzo chetu kimeeleza kuwa ndege hiyo ya kijeshi kutoka Qatar ilikuja nchini baada ya wakala wa kununua wanyama hao, Kamran Ahmed, kukamilisha biashara ya kununua wanyama hao hai na kupata vibali vyote vilivyoiwezesha kutua nchini kisha kuondoka na wanyama hai.

“Baada Kamran kulipia vibali vyote halali kwa ajili ya kusafirisha wanyama hao na baadaye kupata soko la kuwauza kwa Familia ya Kifalme ya Qatar, walituma ndege ya jeshi la nchi hiyo kuwachukua wanyama hao.” kilieleza chanzo chetu na kuongeza; “Wakati ndege hiyo inakuja nchini mamlaka zote zinazohusika, ikiwamo Wizara ya Ulinzi, Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Mambo ya Ndani na watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii walifahamu na walitoa ushirikiano.”

Kauli hiyo ya mtoa taarifa huyo inathibitishwa na Hukumu ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Kobelo, iliyotolewa mwaka jana kuwa ndege ya kijeshi ya Qatar ilikuwa na vibali vyote halali na vya kidiplomasia kutua nchini.

Hakimu Kobelo alisema ndege hiyo ilikuwa na vibali vyote halali vya kuingia nchini kwa safari ya kidiplomasia kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati akitoa hukumu ya kesi ya Kamran na wenzake watatu.

“Ndege iliyobeba wanyama hao ilikuwa na hadhi ya kidiplomasia na ilifuata taratibu zote na kuruhusiwa na mamlaka za nchi ikiwamo Wizara ya Mambo ya Nje,” alikaririwa hakimu huyo.

Aidha baada ya mipango yote kukamilika, wanyama hao walisafirishwa Novemba 26 mwaka 2011, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na Ndege ya Jeshi la Qatar iliondoka kuelekea Doha ikiwa na shehena ya wanyamapori hai.

Inadaiwa kuwa kwa kufanikisha “dili” hilo, Kamran alipokea fedha ya udalali kutoka kwa familia ya kifalme kiasi cha dola za Marekani 300,000 na kutumia dola 100,000 kuwapa washirika wake walioko katika Idara ya Wanyapori nchini.

Taarifa zaidi zinadai kuwa baada ya wanyama hao kuwasili nchini humo, familia hiyo ya kifalme ilitoa hundi ya wazi (blank check) kwa baadhi ya maofisa waandamizi wa Ikulu ya Tanzania, walioshiriki kufanikisha mipango hiyo wajaze kiasi cha fedha wanazotaka kwa ajili ya malipo ya shukrani.

Raia Mwema imearifiwa kuwa miongoni mwa maofisa waliohusika katika kashfa hiyo ni kiongozi mmoja wa juu wa Ikulu aliyekuwa akihusika na masuala ya utumishi wa umma (jina linahifadhiwa kwa sasa) ambaye hata hivyo, amekwishastaafu. Kigogo huyo mstaafu ndiye aliyehusika kusimamia taratibu zote za ndege hiyo kutua nchini.

“Mipango hiyo ilifanyika kwa kumtumia mfanyabiashara mwenye asili ya Kiarabu anayefanya shughuli zake hapa nchini, ambaye alikuwa kiunganishi kati ya maofisa wa Ikulu na familia ya kifalme,” aliongeza mtoa taarifa mwingine.

Inadaiwa kuwa familia hiyo ya kifalme ilitoa kiasi kikubwa cha fedha kwa maofisa hao na fedha hizo ziligawanywa kwa wahusika kulingana na mchango wa kila mmoja kwenye ‘dili’ hilo na hakuna hata senti moja iliyoingia serikalini.

Juhudi za kumpata kiongozi huyo mwandamizi wa Ikulu ambaye amestaafu kwa sasa ili aeleze kuhusu ushiriki wake katika kadhia hiyo na kwa nini alisaidia kuruhusu ndege hiyo kuingia nchini kwa hadhi ya kidiplomasia wakati ilikuja kuhujumu rasilimali za taifa, hazijafanikiwa kwa wiki tatu sasa. Juhudi hizo za kumtafuta bado zinaendelea.

Hata hivyo gazeti hili lilimtafuta wa Waziri wa Maliaasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, kuelezea pamoja na mambo mengine, hatma ya wafanyakazi wa Idara ya Wanyamapori ambao walihusika katika kuuzwa kwa wanyama hao hai kama ilivyoripotiwa na gazeti hili, toleo la wiki iliyopita, sambamba na kujua jinsi wizara hiyo ilivyohusika na kuruhusu ndege hiyo kuingia nchini na kupakia wanyama kwa usimamizi wa maofisa wanyamapori, alisema bado ni mgeni ofisini hapo.

“Mimi nina wiki nne tu ofisini tangu nimeteuliwa, hayo majina (ya wafanyakazi waliohusika na utoroshaji wanyama kama wanaendelea na kazi) nileteeni,” alijibu kifupi.
Kuhusu ndege hiyo kuingia nchini na hadhi ya kidiplomasia, Waziri Maghembe alisema halijui suala hilo.

Akizungumzia sakata hilo, aliyekuwa Waziri (kivuli) wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa, alisema kashfa hiyo hiyo ilikuwa fedheha kwa utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Msigwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (Chadema) alidai kuwa hakuna jinsi Ikulu ya Dar es Salaam inaweza kuepuka lawama za kuhusika katika usafirishaji wa wanyama hao kwenda Doha nchini Qatar.

“Sisi wajumbe wa (iliyokuwa) Kamati ya Ardhi, Mazingira na Maliasili tuliomba sana kupitia kwa Mwenyekiti wetu James Lembeli (wakati huo) kupitia maazimio bungeni kwamba wanyama waliosafirishwa warudishwe nchini na maofisa waliohusika wafikishwe mahakamani, lakini maazimio yetu yalipuuzwa na serikali,” anadai Msigwa.

Kwa mujibu wa mbunge huyo, juhudi zote za wabunge wa Bunge la 10 kutaka sakata hilo na wahusika wake wachukuliwe hatua ziligonga mwamba kutokana na wahusika wakuu kuwa miongoni mwa maofisa wa juu waliokuwa karibu na watawala.

“Hilo liko wazi kwamba waliohusika ni watu wa karibu sana na watawala na ndiyo waliohusika kukwamisha juhudi zote za wabunge na wadau wengine kuhusu hatua ya kuwarudisha wanyama pamoja na wahusika kufikishwa katika vyombo vya sheria,” aliongeza Msigwa.

Waarabu washinikiza
Sakata hilo baada ya kufichuliwa na gazeti la Raia Mwema kwa wakati huo, liliibua mjadala mzito nchini hatua iliyosababisha mamlaka za kiserikali kumfungulia kesi Kamran pamoja na Watanzania wengine wanne.

Hata hivyo wakati kesi hiyo inaendelea taarifa zinaeleza kuwa Serikali ya Qatar ilishinikiza Serikali ya Tanzania kumwachia huru Kamran, kwa kuwa biashara iliyofanyika ilikuwa halali kabisa na maofisa wake walipokea fedha.

“Ndipo ilipochorwa mipango ya kumtorosha Kamran ambapo ofisi ya Kamanda wa Upelelezi Mkoa wa Kilimanjaro (RCO) ilimrudishia kinyemela hati yake ya kusafiria na aliondoka nchini huku nyuma akiacha kesi yake ikiendelea kusikilizwa,” anaeleza mtoa taarifa wetu.

Kamran alitoweka nchini tangu Februari mwaka 2014 ambapo kesi ilipotajwa kati ya Februari 26 na Machi 25, hakutokea mahakamani.

Katika hali iliyoashiria kuwa kulikuwa na maigizo katika suala hilo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, aliwaambia waandishi wa habari kuwa walikuwa wanamtafuta mtuhumiwa huyo na walikuwa wanashikilia hati yake ya kusafiria.

“Ni kweli tumepokea arrest warrant (hati ya kumkamata) kutoka mahakamani na tumeshaanza kazi ya kumtafuta ila hadi sasa bado hatujapata taarifa sahihi kuhusu mahali alipo mtuhumiwa na bado tunashikilia hati yake ya kusafiria,” alikaririwa akisema Kamanda Boaz, wakati huo.

Hata hivyo kwa muda mrefu jeshi hilo la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, halikuwahi kuweka hadharani hati hiyo ya kusafiria na hakukuwa na jitihada zozote za kumtafuta Kamran.

Kamanda huyo alieleza kuwa bado wanashikilia hati ya kusafiria ya mtuhumiwa huyo, hivyo uwezekano wa kuondoka nchini ni mdogo na jeshi hilo limeanza mchakato wa kumsaka ambapo hata hivyo, mpaka leo mtuhumiwa huyo hakuwahi kutiwa mbaroni.

Taarifa za kipolisi kutoka mkoani Kilimanjaro zinabainisha kuwa jeshi hilo ni kati ya taasisi zilizotumika kupotosha umma kuhusu sakata hilo na watendaji wake hawakuwa na dhamira yoyote ya kumtafuta mtuhumiwa aliyetoweka akiwa mikononi mwao.

Wanahabari watolewa kafara
Katika sakata hilo waandishi wa habari wawili wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro ambao walijitolea kumdhamini Kamran katika kesi yake, walijikuta matatani kutokana na Mahakama kuwahukumu kifungo cha miezi sita baada ya Kamran kutoroka.

Waandishi hao, Jackson Kimambo na Peter Temba, walipatwa na kadhia hiyo baada ya Kamran kushindwa kutokea mahakamani na hivyo kuhukumiwa kwenda jela.

Temba alitumikia kifungo chake kwa zaidi ya miezi mitatu kabla ya kutolewa kwa sababu za kiafya na kumalizia sehemu ya kifungo kilichobakia akiwa nje.

Kwa upande wake, Kimambo alitoweka na hadi leo haijulikani alipo lakini hatua hiyo ya kuhukumiwa imezua malalamiko makubwa miongoni mwa ndugu na marafiki wa waandishi hao, wakituhumu serikali kusuka mipango ya kumtorosha Kamran na ndugu zao hao kutolewa kafara.

Juhudi za gazeti hili kuzungumza na Temba hazikuweza kufanikiwa baada ya kuelezwa kuwa mwandishi hiyo anakabiliwa na matatizo ya kiafya na kwamba, akiugua ugonjwa kiharusi na kisukari.

Lakini msemaji wa familia Deo Temba alilimbia Raia Mwema kuwa afya ya baba yao huyo ilidorora baada ya kuhukumiwa na Mahakama kufungwa jela miezi sita kwa madai kuwa mtuhumiwa Kamran (waliyemdhamini) ametoroka.

“Ni kweli mzee alikuwa na matatizo ya kiafya akisumbuliwa na ugonjwa kisukari na shinikizo la damu, lakini hali yake ilibadilika baada ya Mahakama kumhukumu kifungo jela, ila kwa sasa hatuna la kufanya bali kumwachia Mungu,” alieleza na kuongeza; “Tumefuatilia habari mlizochapisha Raia Mwema wiki iliyopita tunashukuru Mungu mmeeleza ukweli kuhusu suala hilo na sisi pia tangu mwanzo tulihisi kuna mchezo mchafu na Baba yetu alitolewa kama kondoo wa kafara na wahusika walikuwa wanajua alipo mtuhumiwa.”

Biashara ya wanyama hai
Katika kadhia hii aina 14 tofauti walisafirishwa Novemba 26 mwaka 2011, kwa Ndege ya Jeshi ya Qatar (Emiri Air force) kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA).

Aidha, pia imebainika kama ilivyoripotiwa na Raia Mwema katika toleo la wiki iliyopita kuwa kabla ya kuibuka kwa kashfa hiyo, kati ya mwaka 2009-2011 idadi kubwa ya wanyama hai waliuzwa katika nchi za China, Pakistan na nchi nyingine za Asia na Uarabuni.

Nyaraka zinaonyeha kuwa Kamran alitumia leseni za kusafirisha nyara za serikali za kampuni tofauti zinazomilikiwa na Watanzania, kusafirisha wanyama hao kwa kuwauza katika nchi hizo.

Aidha, biashara hiyo ya kuuzwa wanyama kwa mujibu nyaraka hizo ilisimamiwa na maofisa wa Idara ya Wanyamapori iliyoko chini ya Wizara ya Maliaili na Utalii, wakimtumia Kamran kama wakala.

Sakata la Twiga
Katika sakata la kusafirisha twiga na wanyama wengine 130 wa aina 14 tofauti, Kamran kwa kutumia uzoefu wake katika biashara ya wanyama hai ndiye alitafuta soko la kuwauza wanyama hao kwa familia ya kifalme ya Qatar ambapo walilipa kiwango kikubwa cha fedha.

Taarifa zinadai kuwa baada ya kukamatwa kwa wanyama hao kutoka katika mapori yaliyoko katika Wilaya za Monduli na Simanjiro, mkoani Arusha na Manyara walihifadhiwa kwa muda katika zizi liloko kwa eneo la Kwa Mrefu, nje kidogo ya Mji wa Arusha.

Nyaraka zilizopatikana zinaonyesha kuwa Kamran aliwalipia wanyama hao tozo zote za kiserikali na kupewa hati ya madai (Invoice) namba 01311271 ya Agosti 16, mwaka 2010, ikimtaka alipe kiasi cha shilingi 11,709,040.

Baada ya kufanya malipo hayo kupitia kampuni ya HAM Marketing ya jijini Dar es Salaam, Kamran, alipewa stakabadhi ya serikali namba 38922956 na 41140006 iliyotolewa Agosti 24, mwaka 2010.

Uchambuzi wa ushahidi huo unaonyesha kuwa raia huyo wa Pakistan aliruhusiwa na mamlaka za Tanzania kukamata wanyama kwa kutumia leseni za kampuni mbalimbali zinazomilikiwa na Watanzania.

Chanzo: Raia Mwema
 
..hii habari ina mambo mengi sana ya kushtua na kusikitisha.

..lakini kwangu mimi kubwa kuliko yote ni tuhuma kwamba jeshi la Polisi lilimsaidia mmoja wa watuhumiwa kutoroka, na kupelekea waliomuwekea dhamana kufungwa jela.

..hizi ni tuhuma nzito sana sana dhidi ya jeshi letu la Polisi.
 
Ni aibu sana kwa jeshi la polisi kutumiwa na Mafisadi. Wote waliohusika wawajibishwe hata kama wamestaafu. Ni aibu kubwa kwa nchi!
Mkuu ni rahisi kuongea hivyo hapa jukwaani lkn tukija kwenye uhalisia wa hili sakata ni kuwa walioteseka na kuumizwa ni vidagaa,wenyewe hawawezi kuguswa hata ile kunyooshewa kidole wameachwa wana kula pensheni zao kijijini
 
UTOROSHAJI WANYAMA HAI
Ikulu ya Kikwete yahusika
Waandishi Wetu
Toleo la 443
3 Feb 2016

Walipewa blank cheque kujaza ‘mapesa’ wanayotaka
SAKATA la kutoroshwa na kusafirishwa kwa wanyama hai kwenda Doha nchini Qatar limezidi kupata sura mpya baada ya kubainika kuwa miongoni mwa maofisa waandamizi Ikulu ya Tanzania walihusika katika biashara ya kuuza wanyama hao, Raia Mwema linafichua.
Taarifa mpya kuhusu sakata hilo pamoja na nyaraka zilizopatikana zinathibitisha kuwa hatua ya kutua nchini kwa ndege hiyo kijeshi ilitokana na kupata baraka zote kutoka kwa viongozi wa ngazi za juu, wakiwamo baadhi ya maofisa waandamizi wa Ikulu ya Dar es Salaam.
Chanzo chetu kimeeleza kuwa ndege hiyo ya kijeshi kutoka Qatar ilikuja nchini baada ya wakala wa kununua wanyama hao, Kamran Ahmed, kukamilisha biashara ya kununua wanyama hao hai na kupata vibali vyote vilivyoiwezesha kutua nchini kisha kuondoka na wanyama hai.
“Baada Kamran kulipia vibali vyote halali kwa ajili ya kusafirisha wanyama hao na baadaye kupata soko la kuwauza kwa Familia ya Kifalme ya Qatar, walituma ndege ya jeshi la nchi hiyo kuwachukua wanyama hao.” kilieleza chanzo chetu na kuongeza; “Wakati ndege hiyo inakuja nchini mamlaka zote zinazohusika, ikiwamo Wizara ya Ulinzi, Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Mambo ya Ndani na watendaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii walifahamu na walitoa ushirikiano.”
Kauli hiyo ya mtoa taarifa huyo inathibitishwa na Hukumu ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Kobelo, iliyotolewa mwaka jana kuwa ndege ya kijeshi ya Qatar ilikuwa na vibali vyote halali na vya kidiplomasia kutua nchini.
Hakimu Kobelo alisema ndege hiyo ilikuwa na vibali vyote halali vya kuingia nchini kwa safari ya kidiplomasia kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati akitoa hukumu ya kesi ya Kamran na wenzake watatu.
“Ndege iliyobeba wanyama hao ilikuwa na hadhi ya kidiplomasia na ilifuata taratibu zote na kuruhusiwa na mamlaka za nchi ikiwamo Wizara ya Mambo ya Nje,” alikaririwa hakimu huyo.
Aidha baada ya mipango yote kukamilika, wanyama hao walisafirishwa Novemba 26 mwaka 2011, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na Ndege ya Jeshi la Qatar iliondoka kuelekea Doha ikiwa na shehena ya wanyamapori hai.
Inadaiwa kuwa kwa kufanikisha “dili” hilo, Kamran alipokea fedha ya udalali kutoka kwa familia ya kifalme kiasi cha dola za Marekani 300,000 na kutumia dola 100,000 kuwapa washirika wake walioko katika Idara ya Wanyapori nchini.
Taarifa zaidi zinadai kuwa baada ya wanyama hao kuwasili nchini humo, familia hiyo ya kifalme ilitoa hundi ya wazi (blank check) kwa baadhi ya maofisa waandamizi wa Ikulu ya Tanzania, walioshiriki kufanikisha mipango hiyo wajaze kiasi cha fedha wanazotaka kwa ajili ya malipo ya shukrani.
Raia Mwema imearifiwa kuwa miongoni mwa maofisa waliohusika katika kashfa hiyo ni kiongozi mmoja wa juu wa Ikulu aliyekuwa akihusika na masuala ya utumishi wa umma (jina linahifadhiwa kwa sasa) ambaye hata hivyo, amekwishastaafu. Kigogo huyo mstaafu ndiye aliyehusika kusimamia taratibu zote za ndege hiyo kutua nchini.
“Mipango hiyo ilifanyika kwa kumtumia mfanyabiashara mwenye asili ya Kiarabu anayefanya shughuli zake hapa nchini, ambaye alikuwa kiunganishi kati ya maofisa wa Ikulu na familia ya kifalme,” aliongeza mtoa taarifa mwingine.
Inadaiwa kuwa familia hiyo ya kifalme ilitoa kiasi kikubwa cha fedha kwa maofisa hao na fedha hizo ziligawanywa kwa wahusika kulingana na mchango wa kila mmoja kwenye ‘dili’ hilo na hakuna hata senti moja iliyoingia serikalini.
Juhudi za kumpata kiongozi huyo mwandamizi wa Ikulu ambaye amestaafu kwa sasa ili aeleze kuhusu ushiriki wake katika kadhia hiyo na kwa nini alisaidia kuruhusu ndege hiyo kuingia nchini kwa hadhi ya kidiplomasia wakati ilikuja kuhujumu rasilimali za taifa, hazijafanikiwa kwa wiki tatu sasa. Juhudi hizo za kumtafuta bado zinaendelea.
Hata hivyo gazeti hili lilimtafuta wa Waziri wa Maliaasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, kuelezea pamoja na mambo mengine, hatma ya wafanyakazi wa Idara ya Wanyamapori ambao walihusika katika kuuzwa kwa wanyama hao hai kama ilivyoripotiwa na gazeti hili, toleo la wiki iliyopita, sambamba na kujua jinsi wizara hiyo ilivyohusika na kuruhusu ndege hiyo kuingia nchini na kupakia wanyama kwa usimamizi wa maofisa wanyamapori, alisema bado ni mgeni ofisini hapo.
“Mimi nina wiki nne tu ofisini tangu nimeteuliwa, hayo majina (ya wafanyakazi waliohusika na utoroshaji wanyama kama wanaendelea na kazi) nileteeni,” alijibu kifupi.
Kuhusu ndege hiyo kuingia nchini na hadhi ya kidiplomasia, Waziri Maghembe alisema halijui suala hilo.
Akizungumzia sakata hilo, aliyekuwa Waziri (kivuli) wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa, alisema kashfa hiyo hiyo ilikuwa fedheha kwa utawala wa Serikali ya Awamu ya Nne.
Msigwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (Chadema) alidai kuwa hakuna jinsi Ikulu ya Dar es Salaam inaweza kuepuka lawama za kuhusika katika usafirishaji wa wanyama hao kwenda Doha nchini Qatar.
“Sisi wajumbe wa (iliyokuwa) Kamati ya Ardhi, Mazingira na Maliasili tuliomba sana kupitia kwa Mwenyekiti wetu James Lembeli (wakati huo) kupitia maazimio bungeni kwamba wanyama waliosafirishwa warudishwe nchini na maofisa waliohusika wafikishwe mahakamani, lakini maazimio yetu yalipuuzwa na serikali,” anadai Msigwa.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, juhudi zote za wabunge wa Bunge la 10 kutaka sakata hilo na wahusika wake wachukuliwe hatua ziligonga mwamba kutokana na wahusika wakuu kuwa miongoni mwa maofisa wa juu waliokuwa karibu na watawala.
“Hilo liko wazi kwamba waliohusika ni watu wa karibu sana na watawala na ndiyo waliohusika kukwamisha juhudi zote za wabunge na wadau wengine kuhusu hatua ya kuwarudisha wanyama pamoja na wahusika kufikishwa katika vyombo vya sheria,” aliongeza Msigwa.
Waarabu wa washinikiza
Sakata hilo baada ya kufichuliwa na gazeti la Raia Mwema kwa wakati huo, liliibua mjadala mzito nchini hatua iliyosababisha mamlaka za kiserikali kumfungulia kesi Kamran pamoja na Watanzania wengine wanne.
Hata hivyo wakati kesi hiyo inaendelea taarifa zinaeleza kuwa Serikali ya Qatar ilishinikiza Serikali ya Tanzania kumwachia huru Kamran, kwa kuwa biashara iliyofanyika ilikuwa halali kabisa na maofisa wake walipokea fedha.
“Ndipo ilipochorwa mipango ya kumtorosha Kamran ambapo ofisi ya Kamanda wa Upelelezi Mkoa wa Kilimanjaro (RCO) ilimrudishia kinyemela hati yake ya kusafiria na aliondoka nchini huku nyuma akiacha kesi yake ikiendelea kusikilizwa,” anaeleza mtoa taarifa wetu.
Kamran alitoweka nchini tangu Februari mwaka 2014 ambapo kesi ilipotajwa kati ya Februari 26 na Machi 25, hakutokea mahakamani.
Katika hali iliyoashiria kuwa kulikuwa na maigizo katika suala hilo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, aliwaambia waandishi wa habari kuwa walikuwa wanamtafuta mtuhumiwa huyo na walikuwa wanashikilia hati yake ya kusafiria.
“Ni kweli tumepokea arrest warrant (hati ya kumkamata) kutoka mahakamani na tumeshaanza kazi ya kumtafuta ila hadi sasa bado hatujapata taarifa sahihi kuhusu mahali alipo mtuhumiwa na bado tunashikilia hati yake ya kusafiria,” alikaririwa akisema Kamanda Boaz, wakati huo.
Hata hivyo kwa muda mrefu jeshi hilo la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, halikuwahi kuweka hadharani hati hiyo ya kusafiria na hakukuwa na jitihada zozote za kumtafuta Kamran.
Kamanda huyo alieleza kuwa bado wanashikilia hati ya kusafiria ya mtuhumiwa huyo, hivyo uwezekano wa kuondoka nchini ni mdogo na jeshi hilo limeanza mchakato wa kumsaka ambapo hata hivyo, mpaka leo mtuhumiwa huyo hakuwahi kutiwa mbaroni.
Taarifa za kipolisi kutoka mkoani Kilimanjaro zinabainisha kuwa jeshi hilo ni kati ya taasisi zilizotumika kupotosha umma kuhusu sakata hilo na watendaji wake hawakuwa na dhamira yoyote ya kumtafuta mtuhumiwa aliyetoweka akiwa mikononi mwao.
Wanahabari watolewa kafara
Katika sakata hilo waandishi wa habari wawili wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro ambao walijitolea kumdhamini Kamran katika kesi yake, walijikuta matatani kutokana na Mahakama kuwahukumu kifungo cha miezi sita baada ya Kamran kutoroka.
Waandishi hao, Jackson Kimambo na Peter Temba, walipatwa na kadhia hiyo baada ya Kamran kushindwa kutokea mahakamani na hivyo kuhukumiwa kwenda jela.
Temba alitumikia kifungo chake kwa zaidi ya miezi mitatu kabla ya kutolewa kwa sababu za kiafya na kumalizia sehemu ya kifungo kilichobakia akiwa nje.
Kwa upande wake, Kimambo alitoweka na hadi leo haijulikani alipo lakini hatua hiyo ya kuhukumiwa imezua malalamiko makubwa miongoni mwa ndugu na marafiki wa waandishi hao, wakituhumu serikali kusuka mipango ya kumtorosha Kamran na ndugu zao hao kutolewa kafara.
Juhudi za gazeti hili kuzungumza na Temba hazikuweza kufanikiwa baada ya kuelezwa kuwa mwandishi hiyo anakabiliwa na matatizo ya kiafya na kwamba, akiugua ugonjwa kiharusi na kisukari.
Lakini msemaji wa familia Deo Temba alilimbia Raia Mwema kuwa afya ya baba yao huyo ilidorora baada ya kuhukumiwa na Mahakama kufungwa jela miezi sita kwa madai kuwa mtuhumiwa Kamran (waliyemdhamini) ametoroka.
“Ni kweli mzee alikuwa na matatizo ya kiafya akisumbuliwa na ugonjwa kisukari na shinikizo la damu, lakini hali yake ilibadilika baada ya Mahakama kumhukumu kifungo jela, ila kwa sasa hatuna la kufanya bali kumwachia Mungu,” alieleza na kuongeza; “Tumefuatilia habari mlizochapisha Raia Mwema wiki iliyopita tunashukuru Mungu mmeeleza ukweli kuhusu suala hilo na sisi pia tangu mwanzo tulihisi kuna mchezo mchafu na Baba yetu alitolewa kama kondoo wa kafara na wahusika walikuwa wanajua alipo mtuhumiwa.”
Biashara ya wanyama hai
Katika kadhia hii aina 14 tofauti walisafirishwa Novemba 26 mwaka 2011, kwa Ndege ya Jeshi ya Qatar (Emiri Air force) kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA).
Aidha, pia imebainika kama ilivyoripotiwa na Raia Mwema katika toleo la wiki iliyopita kuwa kabla ya kuibuka kwa kashfa hiyo, kati ya mwaka 2009-2011 idadi kubwa ya wanyama hai waliuzwa katika nchi za China, Pakistan na nchi nyingine za Asia na Uarabuni.
Nyaraka zinaonyeha kuwa Kamran alitumia leseni za kusafirisha nyara za serikali za kampuni tofauti zinazomilikiwa na Watanzania, kusafirisha wanyama hao kwa kuwauza katika nchi hizo.
Aidha, biashara hiyo ya kuuzwa wanyama kwa mujibu nyaraka hizo ilisimamiwa na maofisa wa Idara ya Wanyamapori iliyoko chini ya Wizara ya Maliaili na Utalii, wakimtumia Kamran kama wakala.
Sakata la Twiga
Katika sakata la kusafirisha twiga na wanyama wengine 130 wa aina 14 tofauti, Kamran kwa kutumia uzoefu wake katika biashara ya wanyama hai ndiye alitafuta soko la kuwauza wanyama hao kwa familia ya kifalme ya Qatar ambapo walilipa kiwango kikubwa cha fedha.
Taarifa zinadai kuwa baada ya kukamatwa kwa wanyama hao kutoka katika mapori yaliyoko katika Wilaya za Monduli na Simanjiro, mkoani Arusha na Manyara walihifadhiwa kwa muda katika zizi liloko kwa eneo la Kwa Mrefu, nje kidogo ya Mji wa Arusha.
Nyaraka zilizopatikana zinaonyesha kuwa Kamran aliwalipia wanyama hao tozo zote za kiserikali na kupewa hati ya madai (Invoice) namba 01311271 ya Agosti 16, mwaka 2010, ikimtaka alipe kiasi cha shilingi 11,709,040.
Baada ya kufanya malipo hayo kupitia kampuni ya HAM Marketing ya jijini Dar es Salaam, Kamran, alipewa stakabadhi ya serikali namba 38922956 na 41140006 iliyotolewa Agosti 24, mwaka 2010.
Uchambuzi wa ushahidi huo unaonyesha kuwa raia huyo wa Pakistan aliruhusiwa na mamlaka za Tanzania kukamata wanyama kwa kutumia leseni za kampuni mbalimbali zinazomilikiwa na Watanzania.
Kuna muda natamani nisingezaliwa Tanzania. Kwa staili hii tutabakia masikini milele yote. Sijui nani aliyeturoga
 
Katika sakata la kusafirisha twiga na wanyama wengine 130 wa aina 14 tofauti, Kamran kwa kutumia uzoefu wake katika biashara ya wanyama hai ndiye alitafuta soko la kuwauza wanyama hao kwa familia ya kifalme ya Qatar ambapo walilipa kiwango kikubwa cha fedha.
Taarifa zinadai kuwa baada ya kukamatwa kwa wanyama hao kutoka katika mapori yaliyoko katika Wilaya za Monduli na Simanjiro, mkoani Arusha na Manyara walihifadhiwa kwa muda katika zizi liloko kwa eneo la Kwa Mrefu, nje kidogo ya Mji wa Arusha.
Nyaraka zilizopatikana zinaonyesha kuwa Kamran aliwalipia wanyama hao tozo zote za kiserikali na kupewa hati ya madai (Invoice) namba 01311271 ya Agosti 16, mwaka 2010, ikimtaka alipe kiasi cha shilingi 11,709,040.

Duh! yani hata kama taratibu zote zingefatwa, na biashara yote ikawa halali na bila rushwa, unawezaje kuuza wanyama 130 wa aina 14 tofauti kwa shilingi 11,709,040/=? Hii si bei ya ng'ombe kama 11 tu? Kuna sehemu nimeona mbwa aina ya American Pitbull akiuzwa dola 50,000 (yani zaidi ya shilingi milioni 100).

Hii ni kufuru!
 
Kwenye maisha ogopa kitu kinaitwa "njaa" na mtu kuwa "masikini". Yaani huwa hawa watu kwa muda huo wanawaza watakulanin
 
ERi ndio anaenda kupiga kampeni za kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa UN, kichekesho, si atauza hadi nchi za wenzie!!
 
..hii habari ina mambo mengi sana ya kushtua na kusikitisha.

..lakini kwangu mimi kubwa kuliko yote ni tuhuma kwamba jeshi la Polisi lilimsaidia mmoja wa watuhumiwa kutoroka, na kupelekea waliomuwekea dhamana kufungwa jela.

..hizi ni tuhuma nzito sana sana dhidi ya jeshi letu la Polisi.
Tatizo kubwa lilikuwa pale kwenye JENGO JEUPE hao Polis niwatu wakuamrishwa tu....hawa jeuri ya kukataa.....ndio maana wanufaika na Ufisadi hataki kusikia mambo ya Katiba ya wananchi...yakummulika mpangaji wa pale anapomaliza utawala wake
 
Tutabakia maskini Mimi nawewe mkuu, walio kwenye mfumo wanatajirika na wametajirika mno
Kuna muda huwa najiwazia ni bora nchi ijulikane inaenda kinyume na haki za binadamu kuliko tunacho fanyiwa. Yaani ni mala 100 mtu akijulikana kama hawa wany'ongwe kwenye haraiki ya watu au kupigwa risasi. Bora tuwe kama china tu.
 
Akiiona hii comments yako Atakuuliza kwani kachomeka nini? Ila jamaa ameifanyia mabaya sana hii Nchi
Pabaya sanaa. Aibu kila sehemu. Hakuna ata pa kukimbilia. Kama kuna moto mbinguni. Mie namuomba mungu akamgeuze kuni za kuchome wengine. Maana kuni ndo hupata maumivu makali
 
Back
Top Bottom