Wanawake wengi tumebadilika kitabia kutokana na tabia za waume zetu

Jiulize kwanini yeye ndie aliyekubadilisha wewe badala ya wewe kumbadilosha yeye au kumweka kwenye mstari mmoja.Ni kwasababu umemruhusu kufanya hivyo....meaning he is got more power over you than you do.Swali la pili kama yeye kafanikiwa kukutoa kwenye mstari kidogo (anaweza) kwanini na wewe hukumrudisha kwenye mstari kabla hujabadilika kabisa??!Unaona kwamba huwezi au umejaribu ukashindwa?!Kama jibu la swali la kwanza ni ndio hujuamini...kama jibu la swali la pili ni ndio tofauti ya mumeo ni kwamba yeye ndo mwenye nguvu yake ila wewe huna juu yake.Hajarihusu wewe uweze kuinfluence matendo yake wakati wewe umemruhusu yeye.


Badala ya kulaumu BADILIKA. Hata siku moja usi-sacrifise mambo ambayo binafsi yanakuweka chini na kumwinua mwenzako kama ambavyo umefanya tayari.Amua kwamba kwanzia sasa nataka KUTOA na KUPOKEA na sio kutoa tu mpaka unaishiwa nguvu huku mwenzako anajilimbikizia tu bila kukupa wewe chochote.

Kama umekua vuvuzela kwa tabia yake ya kuchelewa nyumbani au mabadiliko ya tabia ACHA maana mpaka sasa hivi hujaona matokeo yoyote kwahiyo jua kwamba haisaidii.Anza kutomwonyesha kwamba ana nguvu sana ya kukukera maana ye hajali na sio ajabu anafurahia maana anaendelea tu na anajua huwezi kufanya lolote zaidi ya kuongea.Muonyeshe kwamba unaweza kwa kupunguza mdomo....we majukumu yako kama kawaida....badala ya kumpokea kwa maneno mengi ya lawama na malalamiko mpe tu pole yake ulizia siku yake ilikuaje basi.

Kama unakunywa pombe kwasababu ya kero yake ACHA....kunywa tu iwapo wewe unataka kufanya hivyo!

Kama unaishi kwa gubu acha na ujifunze KUTABASAMU UPYA...kama mna watoto furaha yako ielekeze kwao.

Mruhusu akuone unafuraha hata pamoja na matendo yake ya ajabu....atabadilika wenyewe pale ulimbukeni wa pesa utakapomuisha....huwezi kumlazimisha maana ukiendelea hivi nae atakosa sababu ya kubadilika na kuanza kuwahi nyumbani (mf) kwaajili ya kelele.CONTROL YOURSELF WOMAN!
 
hakuna cha kupanga vitumu wala ulevu solutioni ni kila mtu kwenda kivyake mkajipange upya
Yeah hiyo ndio solution.., na hii issue sio kwa wanawake pekee hata wanaume wengine wanaweza kufanya vitu ndivyo sivyo...
 
Nakumbuka wakati nakutana na soul mate wangu,sikupenda hata kumsemesha kwa kua hadhi zetu hazikuendana, si kwamba mimi nilikua na hadhi kuliko yeye ila kuanzia muonekano,msimamo,tabia na faith aliniacha mbali...muda ukapita na hatimaye ukafikia wakati ambapo tulikaa chini na ku analise wishes za kila mmoja then tukapita mengi till leo tuko tulipo...Nilipata kumuliza several times,kwamba kwanini moyo wake uliangukia kwangu na si kwa mwingine,majibu aliyonipa ni ya kinadharia tu...nina mengi ya kusema ila nisichoshe watu nihitimishe tu kuwa niliyojifunza kwa huyu mwana mama ni mengi na yatosha kusema kua kanibadilisha mengi na kunishape kiasi kwamba leo km si uadilifu niliojifunza kwa wazazi ningetumia hiyo advantage kumpasua kichwa aliyenifikisha nilipo!
 
Nakubaliana na wewe 100% ,kuna wakati unafika unajitazama na kuona kabisa sio wewe na hii haimanishi kwamba ni wabaya kama Boss anavosema laiti kama tungepewa mioyo kama yao ndoa nyingi zisingekuwepo.

kudharauliwa,kukandamizwa na mateso mengi wanayopitia wamama(wanavumilia sana) huwageuza na kuwa tofauti kabisa
.

Poleni zenu mnaofanyiwa hivyo mimi na wangu tumeshibana mpaka tukavimbiwa na nam - treat kama The QUEEN
 
Karen hivi vitu vinakuja vyenyewe automatic unashangaa hutamani kumjibu vizuri cos kakujia asubuhi hutamani hata kuongea cos akifungua mdomo wake ni pombe tupu na maneno ya kuudhu. so vitu vyote hivyo unashangaa unavifanya japo hukulelewa hivyo

Mhhh!!! Pole sana Karina. Muombe Mungu akusaidie na ambadilishe! Hakuna lisilowezekana kwa Mungu!
 
Jamani wanawake wa JF nafikiri mtakubaliana na mimi kuwa wanawake wengi tulioko kwenye ndoa sivyo tulivyo. Tumebadilika kutokana na tabia mbaya za waume zetu. wametusababisha tumekuwa na Gubu, Hasira, Kiburi, Dharau, Mawazo, Magonjwa, Ulevi, na hata utumiaji wa pesa hovyo kwa madai kwamba mbona yeye anapeleka kwa wanawake zake huko nje let me enjoy. Wanawke hoyeeeeeeeeeeee:israel:
Wanaume wengine tuko tofaut na Mumeo,wake zetu wana Enjoy Mbaya na wana tu miss pindituwapo mbali nao.
Kalaghabhaoooo
 
Jamani wanawake wa JF nafikiri mtakubaliana na mimi kuwa wanawake wengi tulioko kwenye ndoa sivyo tulivyo. Tumebadilika kutokana na tabia mbaya za waume zetu. wametusababisha tumekuwa na Gubu, Hasira, Kiburi, Dharau, Mawazo, Magonjwa, Ulevi, na hata utumiaji wa pesa hovyo kwa madai kwamba mbona yeye anapeleka kwa wanawake zake huko nje let me enjoy. Wanawke hoyeeeeeeeeeeee:israel:

Je hiyo ni solution ya matatizo ya ndoa?au barabara to Mirembe??Dawa ya moto sio moto bwana,kama unatabia nzuri keep it up dont singizia wanaume.Why wewe ubadilike sababu ya mume na not mume sababu ya kwako?nafikiri vyote vinawezekana so dont advocate mcharuko bana.
 
Karina na mimi nakuunga mkono. Niliwahi kuhisi nimekwazika sana maishani sababu ya ndoa. Nikafikia kudiscuss na best friend wangu ambaye nae ni mke wa mtu kuwa we have to enjoy lives hawa wanaume wanatufanya mabwege wakati tuna kipato cha kutuwezesha kutanua. Nusu tuanze tabia ya kwenda kula bata kwenye hotel kubwa every week ends. SI kwa nia ya kuwinda vidumu la asha ila kupoteza mawazo maana ukikaa ndani sana hawa vidume wanadhni wewe ni piece ya furniture. Thanks God tuliwezsa ku control hasira zetu.


Kwa hiyo mimi sikushangai mleta mada hawa wanaume wanaweza kukubadili tabia kabisa ukawa mtu wa viwanja just kushindana au ukae nyumbani uugue BP. Ila ukiwatisha wanatii amri! Aaah
 
Pole sana, ila hiyo siyo njia sahihi ya kutatua tatizo lako, ni kukaa naye na kuongea naye na umiambie hiyo tabia huipendi, kama habadiliki muombe Mungu hata kwa kufunga na kuomba ili ambadilishe mumeo, pia tafuta mtu mwenye heshima zake ambaye unaona ndoa yake iko vizuri akushauri. Otherwise utakuwa unajikomoa mwenyewe na mwenzako anaendelea kutesa tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kuna principle moja nimeshaithibitisha inayofanya kazi vizuri sana kwenye migogoro ya ndoa, kuwa: The part of your life that intercept with your partners life, should not exceed 20 percent. Cwez kuifafanua hapa kwani itakuwa na maelezo marefu sana. Kwa anaetaka tuidiscuss anitafute kwenye chat yangu huko inbox, of coz co sasa maana hata umeme hamna nilipo. Kwa wale ambao wanadhani kuwa patna wako hawezi kukubadilisha wanakosea, na wale ambao wanadhani namna ya kumhandle patna mwenye mapungufu ya tabia ni kwa kumuacha, wanakosea zaidi.

Tuko nimeipenda hii
Na ninaomba uidondoshe tu hapa sebuleni ili wote tunufaike
pliz,please,puliiiiiz
 
Jamani wanawake wa JF nafikiri mtakubaliana na mimi kuwa wanawake wengi tulioko kwenye ndoa sivyo tulivyo. Tumebadilika kutokana na tabia mbaya za waume zetu. wametusababisha tumekuwa na Gubu, Hasira, Kiburi, Dharau, Mawazo, Magonjwa, Ulevi, na hata utumiaji wa pesa hovyo kwa madai kwamba mbona yeye anapeleka kwa wanawake zake huko nje let me enjoy. Wanawke hoyeeeeeeeeeeee:israel:

Hasira hasara. Badala ya kumalizia frustrations hizo kwenye maulevi na mambo ambayo yatakusababishia low or lack of self esteem, kwa nini msikae chini mjadili na kupata suluhisho na hao waume? Kumbuka society yetu leo hii iko very biased when it comes to gender. Mume akicheat ama kuwa fuska ama akiwa mlevi people don't care. Lakini mke akicheat ama akiwa fuska au mlevi basi ni kashfa na it's a big deal to everybody. Kaeni chini na waume zenu muyatatue badala ya kulipiza
 
Ongeeni yooote lakini asilimia kubwa ya ndoa za siku hizi ni siasa tuuu, unaishi ili watu wakuone una furaha na sio kuishi ili ufurahi, mimi ndio maana nimemwambia huyu mwanaume tulee tu watoto coz umalaya wake umezidi, nimesali makanisa yote kumuombea, nimefanya kila aina ya maufundi lakini wapiii!! miaka 10 mambo hayohayo, nimemwambia tuwe marafiki na tuishi nyumba moja kila mmoja akatafute furaha yake anapoweza, siku tukipendana tena na kuridhia kutulia tutapima na kufanya hivyo, yanini presha na vidonda vya tumbo maisha yenyewe mafupi, wote tuinjoy babu weee.
 
Nyie mnawaonea wanaume tu bure hapa! Tabia unajibadilisha mwenyewe, wapo kina mama waume zao walezi, wazinzi lakini wao wakemua wanaenda kusali makanisani na misikitini kuwaombea waume zao, na wala wao wahakubadilisha tabia na wao wakawa walezi na wazinifu! Kwa hiyo nyie mnaobadilisha tabia zenu kwa visingizio vya kulipisa kisasi kazi kwenu. Eti umemfumania mumeo na wewe unaenda kutafuta kabwana kako unasema mumeo kakubadilisha wapi wewe! Source hapa ni uwezo wa kufikri wala sio mumeo, kuna mambo mwengi unayoweza kufanya pindi ukimkuta mumeo na kosa sio lazima ufanye kama yeye alivyofanya. Kwa hiyo mnajibadilisha wenyeweee siyo wanaume wanawabadilisha
 
Ni kweli kwa asilimia 100% Tena yaani maskini tunabadilika maana kila unapojaribu kumbadilisha inashindika unaishia kuumia!!! Ili usife mapema inabidi ukubali matokeo na ubadilike ili maisha yanendelee tu na sio mapenzi yaendelee.
 
Naona kama unachanganya madesa mpendwa, kubadilika tabia sio lazima ziwe mbaya unaweza ukaanza kushinda kanisani na mwisho wake ukageuka mwehu sababu ya depression na hiyo nayo ni tabia mbaya.


Nyie mnawaonea wanaume tu bure hapa! Tabia unajibadilisha mwenyewe, wapo kina mama waume zao walezi, wazinzi lakini wao wakemua wanaenda kusali makanisani na misikitini kuwaombea waume zao, na wala wao wahakubadilisha tabia na wao wakawa walezi na wazinifu! Kwa hiyo nyie mnaobadilisha tabia zenu kwa visingizio vya kulipisa kisasi kazi kwenu. Eti umemfumania mumeo na wewe unaenda kutafuta kabwana kako unasema mumeo kakubadilisha wapi wewe! Source hapa ni uwezo wa kufikri wala sio mumeo, kuna mambo mwengi unayoweza kufanya pindi ukimkuta mumeo na kosa sio lazima ufanye kama yeye alivyofanya. Kwa hiyo mnajibadilisha wenyeweee siyo wanaume wanawabadilisha
 
Back
Top Bottom