Wanawake: Nahitaji ufafanuzi wenu katika jambo hili……..!

Aisee mnaniudhi na hili neno lenu la WAJIBU daah hamjui tu....kwani kabla hamjaoa nani huwa anawawekea maji bafuni? Na kama mnatumia shower inakuaje???
We The Boss na Mtambuzi hamuwezi kuwawekea wake zenu maji ya kuoga?!na kama mnaweza kufanya hivyo ina maana ni wajibu wenu???

wewe unaniwekea maneno mdomoni
nimesema wajibu kwa maana ya general..
sijataja maji ya kuoga
yes kwangu kuna shower....na heater pia lol
 
Tliza hasira mama, mijanaume ya
kiafrica ndivyo ilivyo..... Wanaoa ili wapate wakuwafulia na kuwapigia pasi, kuwazalia, n.k.....
Ndo maana ndoa za siku hizi hazidumu....maana bibi zetu ndo waliweza
vumilia hayo.....

Wanasahau hayo
yute mke atayafanya in the name of love, na si kwa
kuwa ni 'wajibu'.......

Hivi nyie wanaume kwanini mnafanana lakini??!??!!!!????!!!!mna maudhiiii, kwanza muache kuchanganya kitu kinaitwa WAJIBU na HIARI ndio tutaelewana.............hapo kwenye red huo sio WAJIBU wa mwanamke bali ni mapenzi/hiari ya huyo mwanamke kufanya hayo uliyoyataja na pengine kufanya zaidi ya hayo.
Niliwahi kuambiwa hivi we mwanamke kwanini leo hujanifulia boxers zangu unafikiri nilikutolea mahari ya nini???!!!!hivi kweli unafikiri mimi nitakua na moyo wa kuendelea kufanya hivyo tena wakati nilikua nafanya kwa mapenzi na sio lazima!!!!!
 
kwa hiyo mke hana 'wajibu wowote' kwa mume?
ni hiyari?
na mme nae ana wajibu au hiyari kwa mke?
 
Aisee.....!
Mtambuzi frankly speaking hakuna mwanamke mwenye akili timamu na mtashi na mwenye hekima pia ambaye mumewe akimuudhi ataacha kutimiza wajibu wake juu ya mumewe.

ila kuna kosa moja tu ambalo huwa lina waputoff akina mama incluiding me, yaani wewe mume wangu umekuja utokako nikakukuta unashombo la mwanamke mwingine wallah! nguo yako utafua mwenyewe. na kuipiga pasi mwenyewe manake huniheshimu mimi.

sikiliza wanaume mna mambo ya ajabu sana, wake zenu tun
 
Last edited by a moderator:
Khaaaa!
hee mtambuz asikwambie mtu harufu ya perfume inazungumzika. labda ungenijibu swali nililokuuliza mwishoni. huu ni ukweli labda wengine watapona kuna wanaume wasio jiheshimu hata chembe. mwanaume anarudi kwake chupi imeliwana shahawa, hapo mwanamke apate jibu gani?

kwamba alitoka kwa Anet so zile za mwishon ndo zinamalizikia, kasababu ya haraka. akiivua hadi aibu anaona. walah hata miye sifui. wanaume mjiheshimu kosa la kutembea nje ya ndoa lina uma
 
Last edited by a moderator:
kwa hiyo mke hana 'wajibu wowote' kwa mume?
ni hiyari?
na mme nae ana wajibu au hiyari kwa mke?
The Boss hapa kinachobishaniwa ni neno linalowakilisha kile mke anachomfanyia mume kama sehemu ya kukamilisha madhumuni ya kuolewa kwake............... Ili kukata mzizi wa fitna tukubali kuwa ni hiyari yao kutekeleza majukumu hayo, lakini ikumbukwe kwamba hiyari si utumwa hivyo hiyari hiyo haiwezi kulazimishwa. lakini ikumbukwe kwamba mwanaume yeyote rijali amefundishwa kwamba ndiye mwenye wajibu wa kutunza familia na ndivyo ilivyo........

Swali: Kwa nini kwa mume iwe ni wajibu na kwa mke ni hiyari?
 
tena mie nikiudhiwa ndo nakoleza kabisa mapenzi lol
ila namnunia mdomoni.
 
The Boss hapa kinachobishaniwa ni neno linalowakilisha kile mke anachomfanyia mume kama sehemu ya kukamilisha madhmuni ya kuolewa............... Ili kukata mzizi wa fitna tukubali kuwa ni hiyari yao kutekeleza majukumu hayo, lakini ikumbukwe kwamba hiyari si utumwa hivyo hiyari hiyo haiwezi kulazimishwa. lakini ikumbukwe kwamba mwanaume yeyote rijali amefundishwa kwamba ndiye mwenye wajibu wa kutunza familia na ndivyo ilivyo........

Swali: Kwa nini kwa mume iwe ni wajibu na kwa mke ni hiyari?

hapo ndo unataka kuanzisha mada mpya kabisa
nani aliesema wao ni hiyari
na sisi ni wajibu?
ndoa si mkataba?
mkataba huu unasemaje kwa wanawake?
mkataba ni hiyari?
 
The Boss niliwahi kuweka uzi hapa wakati fulani kuhusu sheria ya ndoa ya mwaka 1971 ambayo inampa mamlaka mke kukopa mahitaji ya msingi dukani kwa ajili ya familia pale inapotokea mume kasafiri kwa muda mrefu bila kuacha hela ya matumizi ya kutosha au kaitelekeza familia na mume huyo anaporudi analazimika kulipa deni hilo na asipolipa anabanwa kisheria, lakini pia sheria hiyo hiyo ya ndoa inamtaka mke kumtunza mume anapokuwa na mapungufu ya kimwili au kiakili na labda pia anapokuwa na afya mgogoro, lakini kichekesho ni kwamba sheria hiyo haim-bani mke pale anapokataa kumtunza mume huyo au kumtelekeza...............

Kwa mkabala huo ndio maana wanawake humu wanaona kwamba ni hiyari yao kutekeleza majukumu yao katika ndoa lakini kwa mume ni wajibu wake kutekeleza majukumu yake ya kuitunza familia..............
 
kwa wanawake wa TZ pekee i guess ..
 
kwa wanawake wa TZ pekee i guess ..

Yeah..! The Boss na ndio maana wanatokwa na povu hapa kwa kutetea ujinga, wanajua kabisa ni wajibu wao kutekeleza sehemu ya majukumu yao kama dhana ya ndoa inavyosema, lakini wao wamekazana kwamba ni hiyari yao na hawalazimiki, si umeona hata sheria inavyowalinda.............?
 
Last edited by a moderator:
ngoja niwape kisa cha kweli cha mtu wangu wa karibu sana.

Mary kamkuta mmewe na Joseph na mwanamke mwingine guest iliyo karibu kabisa na kwao, huyo mwanamke mwenyewe bonge la shangingi.

Akarudi home hapo saa moja jioni. Mume akarudi mida ya saa tatu na nusu kajiandaa kwa shari atakayopokelewa nayo.

Mary kamwekea chakula kama kawaida na maji ya kuoga, wakaenda kulala wala Mary hajauliza. Kesho yake jioni Jose akaenda kusema kwa wazazi wake jamani naombeni nisuluhishwe na mke wangu, asije akaniua bure.

Kanikuta na mtu afu wala hajanifokea wala kugomba.

Argument ya Mary ilikuwa, niseme au nigombe nini?
Hata nisipoweka chakula na maji, itabadili awe hajafanya alichofanya?
 
Kongosho ni wanawake wachache sana wenye busara kama Mary....................
 
Last edited by a moderator:
The Boss hapa kinachobishaniwa ni neno linalowakilisha kile mke anachomfanyia mume kama sehemu ya kukamilisha madhumuni ya kuolewa kwake............... Ili kukata mzizi wa fitna tukubali kuwa ni hiyari yao kutekeleza majukumu hayo, lakini ikumbukwe kwamba hiyari si utumwa hivyo hiyari hiyo haiwezi kulazimishwa. lakini ikumbukwe kwamba mwanaume yeyote rijali amefundishwa kwamba ndiye mwenye wajibu wa kutunza familia na ndivyo ilivyo........

Swali: Kwa nini kwa mume iwe ni wajibu na kwa mke ni hiyari?

Kwa bahati mbaya natumia simu nashindwa ku highlight na kuwa quote kwa wakati mmoja,kufupisha mambo.
Mtambuzi hebu rahisisha mambo kwa kuorodhesha majukumu ya mwanamke kwenye ndoa labda itasaidia maana hayo uliyoyataja hapo juu ni mambo yanayofanyika kwa hiari.
Yaweje wanaume hawa hawa wakitanzania wakiwa nje ya nchi na wake zao waweze kujifanyia kila kituuu....lakini wakisharudi nyumbani tu(Tz)wanakua vilema hawawezi tena kufanya yale waliyokua wakifanya hata kwenda kuchukua glass ya maji au kupeleka sahani aliyomaliza kulia chakula jikoni hawezi ataiacha hapo mezani mkewe aitoe. Hebu tuelimishane kidogo kwenye hili jamani na tuwe wakweli. Mambo mengine ni kujiendekeza na kuona kwamba hii sio kazi yangu ni kazi ya mke.
Ila ukiniambia vyakula vikiisha na mume hana taarifa hapo kweli lawama niza mke maana ndio jukumu lake kujua nini kipo na nini kinachohitajika!
 
Last edited by a moderator:
Mary is another . . . .
One in a million aisee

ana character ya ajabu sana kwa wanawake wa dunia hii ya leo, mie huwa namshangaa anawezaje?

Kongosho ni wanawake wachache sana wenye busara kama Mary....................
 
Last edited by a moderator:
aisee, position ya baadhi ya akina dada humu ndani inaweza kuwa summarized hivi: mwanamke hana wajibu wowote zaidi ya kuwa 'pambo' la nyumba' ... how pathetic
 
Kwa bahati mbaya natumia simu nashindwa ku highlight na kuwa quote kwa wakati mmoja,kufupisha mambo.
Mtambuzi hebu rahisisha mambo kwa kuorodhesha majukumu ya mwanamke kwenye ndoa labda itasaidia maana hayo uliyoyataja hapo juu ni mambo yanayofanyika kwa hiari.
Yaweje wanaume hawa hawa wakitanzania wakiwa nje ya nchi na wake zao waweze kujifanyia kila kituuu....lakini wakisharudi nyumbani tu(Tz)wanakua vilema hawawezi tena kufanya yale waliyokua wakifanya hata kwenda kuchukua glass ya maji au kupeleka sahani aliyomaliza kulia chakula jikoni hawezi ataiacha hapo mezani mkewe aitoe. Hebu tuelimishane kidogo kwenye hili jamani na tuwe wakweli. Mambo mengine ni kujiendekeza na kuona kwamba hii sio kazi yangu ni kazi ya mke.
Ila ukiniambia vyakula vikiisha na mume hana taarifa hapo kweli lawama niza mke maana ndio jukumu lake kujua nini kipo na nini kinachohitajika!
Yummy labda wewe usema hapa wajibu ya mume katika ndoa ni yapi?
labda tukijua wajibu wa mume katika familia itakuwa rahisi kujua wajibu wa hiyari wa mke.
 
Last edited by a moderator:
Yeah..! The Boss na ndio maana wanatokwa na povu hapa kwa kutetea ujinga, wanajua kabisa ni wajibu wao kutekeleza sehemu ya majukumu yao kama dhana ya ndoa inavyosema, lakini wao wamekazana kwamba ni hiyari yao na hawalazimiki, si umeona hata sheria inavyowalinda.............?

Hakuna anaetokwa na povu na wala hamna ujinga unaotetewa! Swala liko wazi kabisa hayo unayoyaongelea wewe Mtambuzi ni hiari yangu kuyafanya au laah! Majukumu yangu kama mke nayatambua vizuri sana. Ina maana mume akienda sokoni ni jukumu lake kwenda sokoni??mimi naamini haya yote yanafanyika kwa moyo mmoja mkiwa na mapenzi ya dhati sio swala la jukumu la nani kwenda sokoni.
Ndio haya mambo unasema jukumu la mume kununua luku kwhy ikiisha mke hatoi hela eti kisa sio jukumu lake si upuuzi huo!!
Inshort tunatakiwa kushare responsibilities haiwezekani mume aelemewe wakati mke nae anao uwezo mkubwa tu wa kumsaidia, hayo ni mambo ya kizamani!
 
Yummy wewe ndio unaelewa hivyo, lakini kuna wenzio wanafanya kazi na wanalipwa mshahara lakini wanataka hela ya matumizi atoe mume kila siku, yeye anasema sio jukumu lake...... na pia mume hapaswi kujua kipato chake haihu...........!

Na ndiom maana nikakuuliza kuwa ni yapi majukumu ya mume katika ndoa na kwa bahati nzuri umerudi pale pale kwamba wanandoa wanpaswa kushea majukumu ya kifamilia ................ Good and well

:focus:
Swali langu lilikuwa dogo sana:

Hivi inakuwaje?

Baadhi ya wanawake wanapowafanyia waume au wapenzi wao jambo zuri, hufanya hivyo huku wakihesabu na kutarajia wapenzi hao waone, watambue na pengine baadae kuwalipa kwa njia nyingine.

Kwa mfano.

Mke ana kawaida ya kumuwekea mume au mpenzi wake maji ya kuoga bafuni, anamwandalia chakula vizuri, anamnyooshea nguo zake au anazikagua nguo zake kwa umakini na kuzirekebisha pale zinapokuwa na kasoro na mengine yanayofanana na hayo. Badala ya kuchukulia au kujua kwamba huo ni wajibu wake, hufanya hivyo kama deni.

Mume anapomkosea, mke huacha kufanya au kumfanyia mumewe mambo hayo kwa maelezo kwamba, haoni sababu ya kufanya hivyo kwa sababu mumewe hana shukurani…………..
Kumbuka huu ni mfano tu na sikusema hayo ndiyo majukumu ya mke..................

Sasa naamini utakuwa umeelewa uzi huu ulikuwa unataka ufafanuzi gani kutoka kwenu maana nimeona unajadili maoni ya wachangiaji badala ya mada..........
 
Last edited by a moderator:
Hivi nyie wanaume kwanini mnafanana lakini??!??!!!!????!!!!mna maudhiiii, kwanza muache kuchanganya kitu kinaitwa WAJIBU na HIARI ndio tutaelewana.............hapo kwenye red huo sio WAJIBU wa mwanamke bali ni mapenzi/hiari ya huyo mwanamke kufanya hayo uliyoyataja na pengine kufanya zaidi ya hayo.
Niliwahi kuambiwa hivi we mwanamke kwanini leo hujanifulia boxers zangu unafikiri nilikutolea mahari ya nini???!!!!hivi kweli unafikiri mimi nitakua na moyo wa kuendelea kufanya hivyo tena wakati nilikua nafanya kwa mapenzi na sio lazima!!!!!

nimeunga mkono hoja....sio WAJIBU wa mwanamke huo ni maamuzi yake afanye au asifanye
 
Back
Top Bottom