Wanaume wote wa JF someni hii,mmoja wenu ndo kafanya haya

Kaka,

Tuhuma za Makaburini ni kubwa mno na ndiyo maana katuacha solemba...Nafsi inamsuta!!

Hata hivyo, ukiitwa na shemeji yako anaomba msaada, unaanza kuomba ruhusa kwa jamaa au unam-attend na kudeal na hayo mambo mengine baadaye??

...wallahi ina depend na ukaribu wetu, hata hivyo nikishamsaidia shemeji...sitampigia tena kumuuliza "..enhe siku ile kwanini mumeo hakuja kukusaidia.?"....nitakabiliana na bro head on kumuuliza kilichojiri badala ya kuja 'kukaanga mbuyu na kuwachia wenye meno watafune..' Mama Maria -Marijani Rajab.
 
wanaume wa jf someni hii thread,na kwa sababu muhusika yupo humu basi ujumbe wake utakuwa umemfikia. Wiki ilopita kulikuwa na kauhaba ka mafuta ambako hakakuchukua siku nyingi, nikiwa njiani narudi kazini alinipigia simu dada mmoja ambaye tunafahamiana naye pamoja na mumewe akiniomba nimsaidie sababu gari lake halina mafuta, na yupo somewhere Morogoro road akiwa anatokea kazini na sheli za karibu hazikuwa na mafuta.

Nikapitia kumnunulia sheli moja nilipata taarifa kuwa inauza mafuta na ndipo nilipompelekea sehemu alipo na kumkuta mwenye majonzi lakini alijitahidi kutabasamu baada ya kuniona na baada ya kumuwekea mafuta nilimuuliza mumewe aliko akajibu kwa unyonge yupo kazini!

Nikamuuliza tena kwa nini usimwambie kwa kuwa hapa ni karibu na ofisini kwake dada machozi yakaaza kumtoka nikaamua nimuache aende!

Baada ya siku chache nilimpigia kumuuliza akaniambia shemeji, naishi bila matumaini bora ya mgonjwa wa ukimwi! Akasema kuwa siku ile alimueleza mumewe tatizo hilo akamjibu" kwa hiyo.......unataka nikusaidiaje.....kwani mimi nauza mafuta ya gari???

Kama uliweza kununua gari iweje ushindwe kulihudumia, kwanza mimi nina kazi zangu ofisini sina muda .........dada akaamua akate simu maana angeendelea kumsikiliza angemuumiza maana maneno yaliyokuwa yanatoka kwa mumewe wa ndoa ni makali.

Najiuliza hivi sisi wanaume hawa wadada wa watu huwa tunawaoa ili kuwakomoa? Au hatujui maana ya ndoa? Au ni ushamba? Utoto? Au ni ukatili tu tunaamua kuwafanyia?

alitaka amwambie nani amsaidie kama si mumewe? why jamani tunakuwa wakatili hivi?? aghhhhhhhhh

Hebu wanaume wenye hekima jf tusaidiane kumshauri mwenzetu naona hajielewi na haelewi majukumu yake.

Kijana angalia usijekuwa wewe ndio unayetaka kuivunza hiyo ndoa, uhusiano wako na huyo dada na mumewe hauniridhishi wewe kuombwa mafuta na kuyapeleka kwa haraka kiasi hicho. Na huyo dada kukueleza matatizo yake ya ndoa wewe mtu mnayefahamiana tuu, hiyo inatosha kutia shaka kubwa inakuwaje, na mnavyowasiliana wewe na mke wa mtu. Hapo kuna kitu kinaendelea kati yenu. Angalia utauwawa, achana na wake za watu na maisha yao. Na inawezekana huyo dada yote aliyokueleza ni uongo mtupu ili uone kwamba mumewe anamnyanyasa, uanze kumliwaza mpaka mfike kileleni.
 
kwani huyo mwanamke hawezi kununua mafuta hadi mumewe amnunulie agrrrrrrrrrrrrrrrrrr
ameshanunuliwa gari nae achakarike anunua mafuta inakera kufanyiwa kila kitu na umesema anafanya kazi so hela anazifanyia nn
mda wa kupokea kila kitu umeshapitwa na wakati bwana,
i think hata huyo mumewe kakereka na tabia hii,nadhani kwa wanaume walioowa wanajua kadhia hii
mke anafanya kazi afu hatoi senti ndani ya nyumba anataka kila kitu afanye mume hiyo inauma
mambo ya ndani ya nyumba ni ngumu sana kutolea ushauri bila kujua kilichomo baina ya wawili
 
wanaume wa jf someni hii thread,na kwa sababu muhusika yupo humu basi ujumbe wake utakuwa umemfikia. Wiki ilopita kulikuwa na kauhaba ka mafuta ambako hakakuchukua siku nyingi, nikiwa njiani narudi kazini alinipigia simu dada mmoja ambaye tunafahamiana naye pamoja na mumewe akiniomba nimsaidie sababu gari lake halina mafuta, na yupo somewhere Morogoro road akiwa anatokea kazini na sheli za karibu hazikuwa na mafuta.

Nikapitia kumnunulia sheli moja nilipata taarifa kuwa inauza mafuta na ndipo nilipompelekea sehemu alipo na kumkuta mwenye majonzi lakini alijitahidi kutabasamu baada ya kuniona na baada ya kumuwekea mafuta nilimuuliza mumewe aliko akajibu kwa unyonge yupo kazini!

Nikamuuliza tena kwa nini usimwambie kwa kuwa hapa ni karibu na ofisini kwake dada machozi yakaaza kumtoka nikaamua nimuache aende!

Baada ya siku chache nilimpigia kumuuliza akaniambia shemeji, naishi bila matumaini bora ya mgonjwa wa ukimwi! Akasema kuwa siku ile alimueleza mumewe tatizo hilo akamjibu" kwa hiyo.......unataka nikusaidiaje.....kwani mimi nauza mafuta ya gari???

Kama uliweza kununua gari iweje ushindwe kulihudumia, kwanza mimi nina kazi zangu ofisini sina muda .........dada akaamua akate simu maana angeendelea kumsikiliza angemuumiza maana maneno yaliyokuwa yanatoka kwa mumewe wa ndoa ni makali.

Najiuliza hivi sisi wanaume hawa wadada wa watu huwa tunawaoa ili kuwakomoa? Au hatujui maana ya ndoa? Au ni ushamba? Utoto? Au ni ukatili tu tunaamua kuwafanyia?

alitaka amwambie nani amsaidie kama si mumewe? why jamani tunakuwa wakatili hivi?? aghhhhhhhhh

Hebu wanaume wenye hekima jf tusaidiane kumshauri mwenzetu naona hajielewi na haelewi majukumu yake.

Kwanza kabisa inabidi uwe makini na huduma unazotoa kwa wake za watu, kama ulivyosema mumewe ni rafiki yako sasa akisikia wewe umetoka mbali kote ofisini kwako kuja kumletea mkewe mafuta itakuletea uwalakini kidogo. Vilevile hauwezi jua kuwa labda mumewe alitaka kuona uvumilivu wa mkewe uko vipi? Yaani mafuta tu kuishiwa kaanza kuwapigia mashemeji simu...je ingekuwa issue nene si anakimbia nyumba huyo..
 
may be huyo mwanamke anakutaka thus y akakueleza matatizo ya mumeo ili umuone huruma na kumfariji.na kama kweli ni hvyo hlo gari la kuhongwa thus y hajui kuliangaikia nakupenda misaada kwa wanaume kama wewe ndio mana hata mumewe anachukia
 
jamani naomba kujibu hoja zenu kwa ujumla coz mmenilaumu sana sijaonekana jamani mafuriko haya yamezua mambo,napenda kuwajibu kama ifuatavyo.
wengi mlishindwa kuielewa thread hii vizuri mkaanza kuporomosha maneno makali kwa huyo dada,ni kuwa dada huyo kwanza anafanya kazi nzuri na nadhani hana shida likija suala la mafuta,hoja ilikuwa kulikuwa na uhaba wa mafuta,kwa hiyo mliokurupuka kujibu bila kutumia macho yenu kusoma na kumlaumu dada wa watu mshindwe !!!1ndio maana watu huwa mnafeli mitihani kwa kutokusoma instruction.
pili wengi mlipenda kujua kama alinirudishia hela yangu baada ya kumletea mafuta ni kuwa hela yangu nilipewa yote
kuhusu gari kuwa labda lilinunul;iwa pasipo maelewano kati ya dada na mume wake ni kuwa ninavyoona mimi gari lilinunuliwa kwa makubaliano kwa sababu hata huyo mume wake huwa analiendesha sasa kama lingekuwa limenunuliwa bila makubaliano sidhani kama angekuwa analiendesha .
kwa wale mliohisi kuwa dada alikuwa ananimaindi eti akatumia kigezo hicho kunialika ni kuwa shemeji yangu huyo ni kati wa wale wanawake wenye hekima na busara na jinsi anavyo behave sina hofu kuwa alikuwa na mpango huo kwa sababu ya busara na heshima zake na sikuona dalili zozote kama hizo mlizoorodhesha jamani kwa hilo mmekosea.
hoja ya kuwa walikuwa wamegombana s\asubuhi siwezi kuisemea kwa sababu angekuwa amegombana nae asingempigia first mume wake angatafuta msaada moja kwa moja kwa mtu mwingine.
nionavyo mimi ni ukatili tu wa huyu bwana kwa sababu mara nyingi amekuwa akimfokea kwenye simu na sisi tukiwepo kitendo ambacho wafanyakazi wenzie wengi huwa hawakipendi na kinawaudhi hivyo tunamuomba aacheeeee
 
...ubarikiwe sana na uwe na mwaka mpya wenye kila lililo na heri na wewe.
Kwa kizazi hiki cha dot.com, ndoa za aina hii zinashika kasi sana, inakuwa kana
kwamba watu wanatofutiana sababu ya kuachana...

...umejibu hoja kwa hekima, bila jazba na kwa mtazamo huu naomba radhi kwa
niaba ya wenzangu tuliokuwa tunakutupia madongo ulipotimka baada ya ile post ya kwanza.
Kila la kheri, karibu tena jamiiforums kila upatapo nafasi tubadilishane mawazo juu ya maisha.

Mbu.
 
Baadae aambiwe..hakuna mchele nyumbani...hakuna sukari..hakuna mafuta...luku imeisha..naomba hela. Halafu tena huyo mwanamke aje kwako akuombe umpe hela eeeh.....Akili mukichwa!!!!!
 
Hayo si majibu mazuri kwa mwenzi wako wa ukweli hata kama hakukushirikisha walati wa kununua ilo gari. Ndoa ni sehemu tu ya maisha na si maisha. Hivyo huyu mwanaume atakuwa na shida tayari, na asipo angalia wazee wa mjini wata anza kumfunulia mke muda si mrefu.
 
Baadae aambiwe..hakuna mchele nyumbani...hakuna sukari..hakuna mafuta...luku imeisha..naomba hela. Halafu tena huyo mwanamke aje kwako akuombe umpe hela eeeh.....Akili mukichwa!!!!!
 
Lol! Umenikumbusha my best gakfrnd, kuna siku alikamatwa na polisi wakam-harrass kweli. Wa kwanza kumpigia ni bf. Jamaa baada ya missed call kadhaa anapokea ' baby niko calabash na washkaji. Wewe wasikilize tu wanataka hela hao. Wape afu unistue!'. Dada kaparangana nao, tukwa tunapiga kuulizia updates hadi issue ikaisha. Jamaa hakupiga wala kuulizia for 2 days, na wanaishi kama 1km apart. Jamaa anaongelea kuoa tu, dada akajionea hapa tu mchumba hivi nikiwa mke? Tupa kulee!
majibu kama haya mbona mengi tu jamani!! unaweza mwambia mi naumwa sana uko wapi, anakujibu kwani mie doctor?
kawaida sana wala asione ndio jambo ziiiito limemwelemea, sasa yeye mafuta tu kuna mwengine anaibiwa kila kitu anamwita mumewe aje anamwambia nenda police chezea wanaume wa kibongo eeee
 
Hata mie sijaelewa kwa nini huu mjadala umekita zaidi katika hoja za kunyambua badala ya hoja za msingi ambazo ametuletea huyu Bwana Makaburini.....!!

Kwamba wote wana makosa, hilo liko wazi..Ila pamoja na makosa, ni fair kumtelekeza mkeo wakati kakwama kwenye emergency??

Na ukirudi home mnalala kitanda kimoja na kukumbatiana??? I still can't understand!!

Ila suala la huyo mama na Mzee Makaburini nalo......mhhhhhh, ni utata mtupu!!

Babu DC!!

Hii mada ni outdated! Mideko mingine ya wanawake inakera! ndiyo maana wanaume wanaachukua jukumu la kwenda kule wasikooombwa misaada ya kipuuzi! Beba dumu niletee mafuta! huo ujinga wafanye wengine mimi sifanyi na sitaomba huo msaada.

Unaomba vocha unatumiwa na mumeo, halafu unabeep upigiwe kutoa asante! wanawake hivi akili zetu huwa ziko ama zinahama sometimes? Ngoja nilale nina hasira na hawa watu wasiojua kujitegemea.What if ni yatima? Mjane? nani angemfanyia? Shukuruni Mungu kwa vile mlivyo!
 
Mmm! Wadau its like michango mingi inalenga kumponda huyu dada just because she drive! tatizo ni kwamba mume anamnyanyasa, na sidhani kwamba issue ni mafuta au hilo gari, inawezekana she is a victim na ananyanyaswa kwa mengi! If you a real man, huwezi muacha mkeo ame stuck hana mafuta and you are comfortably in your office working! Something is just not right!
 
Haya mambo yana mzizi wake wa tatizo, siyo mafuta kama wewe unavyofikiria! Usi-jump kwenye conclusion, utaumia!
 
"MMOJA WENU NDO KAFANYA HAYA" Huyo dem kakwambia mumewe yupo JF?
Uhusiano wenu uko zaidi ya hapo na wewe ndio chanzo cha mgogoro kam si mwendelezo wa mgogoro!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom