makaburini
Member
- Dec 14, 2011
- 19
- 22
wanaume wa jf someni hii thread,na kwa sababu muhusika yupo humu basi ujumbe wake utakuwa umemfikia. Wiki ilopita kulikuwa na kauhaba ka mafuta ambako hakakuchukua siku nyingi, nikiwa njiani narudi kazini alinipigia simu dada mmoja ambaye tunafahamiana naye pamoja na mumewe akiniomba nimsaidie sababu gari lake halina mafuta, na yupo somewhere Morogoro road akiwa anatokea kazini na sheli za karibu hazikuwa na mafuta.
Nikapitia kumnunulia sheli moja nilipata taarifa kuwa inauza mafuta na ndipo nilipompelekea sehemu alipo na kumkuta mwenye majonzi lakini alijitahidi kutabasamu baada ya kuniona na baada ya kumuwekea mafuta nilimuuliza mumewe aliko akajibu kwa unyonge yupo kazini!
Nikamuuliza tena kwa nini usimwambie kwa kuwa hapa ni karibu na ofisini kwake dada machozi yakaaza kumtoka nikaamua nimuache aende!
Baada ya siku chache nilimpigia kumuuliza akaniambia shemeji, naishi bila matumaini bora ya mgonjwa wa ukimwi! Akasema kuwa siku ile alimueleza mumewe tatizo hilo akamjibu" kwa hiyo.......unataka nikusaidiaje.....kwani mimi nauza mafuta ya gari???
Kama uliweza kununua gari iweje ushindwe kulihudumia, kwanza mimi nina kazi zangu ofisini sina muda .........dada akaamua akate simu maana angeendelea kumsikiliza angemuumiza maana maneno yaliyokuwa yanatoka kwa mumewe wa ndoa ni makali.
Najiuliza hivi sisi wanaume hawa wadada wa watu huwa tunawaoa ili kuwakomoa? Au hatujui maana ya ndoa? Au ni ushamba? Utoto? Au ni ukatili tu tunaamua kuwafanyia?
alitaka amwambie nani amsaidie kama si mumewe? why jamani tunakuwa wakatili hivi?? aghhhhhhhhh
Hebu wanaume wenye hekima jf tusaidiane kumshauri mwenzetu naona hajielewi na haelewi majukumu yake.