Namuacha ila roho inaniuma [emoji24]

Nafikiri Zaidi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
429
471
Habari wana JF humu ndani natumanini kila mmoja ni mzima wa afya kabisa

Bila kupoteza muda niiende moja kwa moja kwenye kisa changu cha kweli kilichonitokea na nitajitahidi sana kugusia mambo muhimu yaliopelekea kuandika uzi huu apa.

Well...Mm ni kijana mwenye umri wa miaka 26. Kiukweli safari yangu ya mahusiano ni wazi kabisa ilionekana kupotea baada ya kukutana na huyu mrembo.


Basi nakumbuka ilikua ni mwezi wa kumi mwaka 2021 nilikutana rasmi na huyu mrembo nikiwa katika majukumu yangu ya kila siku kupitia dada yake ambae tunafanya nae kazi,ambapo yeye alikua ana ofisi ya mgahawa iliyopo karibu kabisa na mazingira ya tunapofanya kazi.

Lengo la kumleta mdogo wake ilikua ni kumsaidia pamoja na kusimamia kwenye majukumu yake ya kazi kwani yeye alikua anabanwa sana na majukumu hivyo alivyomaliza chuo alikuja moja kwa moja kwa dada ake.(Dada ake tumpe Jina {Modesta} Hivyo basi ilikua ni utaratibu wangu na watumishi wengine wote kujipatia Breakfast pamoja lunch maeneo hayo.Kiukweli tangu nije kuonana na huyu binti ni kama moyo wangu ulitokea kumpenda sana mwanadada huyu na yeye bila kuficha kabisa alionekana kunielewa kwa iyo haikua ngumu kabisa kumpata ingawa ilichukua karibu miezi kadhaa mpaka tulivyoingia kwenye mahusiano yetu.

Mwezi mmoja baadae tulianza mahusiano yetu tukiwa tunapendana sana kama tujuavyo penzi jipya likianza ..alikua ni binti mrembo aliekamilika katika sekta zote nikisema Umbo,Rangi(Napenda Weupe).Basi tuliendelea hivyo ikafika hatua ya kuomba tunda.Ingawa mwanzoni alikua mgumu na kunipiga kalenda sana lakini badae nlikuja kugundua kua alikua bikra ni baada ya siku moja kufika mgahawani na ilikua ni weekend basi na mazungumzo yakawa ivi : huyu binti tumpe jina Debby (CODE)

MIMI: "Babe leo nataka nitoke mapema kazini mapema ujiandae nikutoe out vipi uko tayari?"

DEBBY : "Ooh Babe Kweli !?...natamani sana kweli kutoka ila dada atakataa maana hataki nitoke mwenyewe na tukitoka lazima niwe nae"

MIMI: Mbona shem hana shida na si anajua tayari mahusiano yetu mm na wewe mm sidhani kama kuna shida tena nakumbuka yeye ndio nlianza kumgusia hili ila akasema yeye anaingia shift kwa hiyo hataweza kujuika nasi

DEBBY : Mmh haya baby ngoja nitaongea na nae ili nimuage basi badae tutoke baby.

MIMI: Sawa kipenzi nlietee basi chakula mama au huoni nilivyo na njaa hapa.

DEBBY: Subiri kidogo nakuletea baby nikuletee nini baba.

MIMI : Chochote tuu kizuri we nichagulia nitakula.
DEBBY : Sawa.


Nlitumia dakika 30 kula then nikarudi ofisini na majukumu yangu lakini kichwani nikiwa na mawazo tu ya kumla maana dada ake leo hayupo ili Debby asinipe kisingizio

Ilifika mida ya kutoka Ni Sing-Out kuelekea tena kwa Debby kwa ajili ya kumuaga ili niende home mimi nikapumzike then nirudi badae kumpitia mgahawani. Nilifika pale nikam-kiss kwenye forehead na tukabadilishana mate pale nikaondoka ingawa alionekana kama ni mtu alikuekua anahitaji huduma ingawa kwa mazingira ya pale nikajisemea kimoyomoyo Yes ! Leo kunako 6x6 ni cheche.So ikabidi nimuage tu kibishi hivyo hivyo.

Sa 8:30PM Niliamka nikaoga tayari kujiandaa na kwa ajili ya out nilimcheki Debby akaniambia tayari alishafunga na yeye yuko nyumbani anajiandaa.Basi nlitumia muda mchache kujianda nikawasha gari tayari kumfata Debby.Nilipofika alikwa kawaka sana nikaishia kumsifia pale na makiss ya kutosha.

Debby : Baby twende huoni watu watuangalia?

Mimi : Ni shida zao kwani tumewakosea nini ? Aya twende mama

Nilimfungulia pale mlango akapanda na mm nikapanda moja kwa moja safari ya kuelekea moja ya kiwanja maarufu sana hapa Moshi Mjini "Mimi's Tarven".Tulifika pale mida ya sa tatu na tayari watu walikua wameanza kufika na sisi tukatafuta nafasi pale tukakaa muhudumu akaja kuuliza nikamwambia amsikilize kwanza mrembo

Muhudumu:Karibu boss karibu nikuhusumie nini?

Debby : Naomba niletee Desperados Please

Muhudumu: Na wewe boss ?

Mimi: Mm nilietee kama kawaida boss.

Muda huu Debby alininipiga jicho kali sana

Debby : Bby Inamaana wewe ni mwenyeji sana hapa basi wewe ni mtu wa starehe sana na sina imani na wewe wahudumu wanakujua na wanajua nini unakunywa !!?

Mimi: hahaha hapana baby mm nina mwaka wa 4 hapa kwa iyo muda mwingi weekend nakuja hiki ndio kiwanja changu pendwa kikifuatiwa na "AmuZz Bar and Grill" (wenyeji wa Moshi mjini nafikiri mnaelewa Vibe la hapa )

Debby: Mmmh aya nyie wanaume kwa kujietea mko vizuri ila bby hatukaa sana si unajua kesho wateja ni wengi na pia tusije tukamkwaza dada.

Mimi: Haina shida baby we ukiona tu umeanza kuchoka nambie nikurudishe home(kimoyomoyo nikijsemea huyu lazima nipige leo)

Basi muhudumu alileta vinywaji vetu pale tuaendelea kunywa mdogo mdogo na muda huu vibe ni kama lilikua linaanza kuwa kubwa kwani watu walionekana kujaa sana maeneo haya.

Wakati napepesa macho nlimuona staffmate mmoja alikua amekaa mwenyewe counter ilibidi nimfate aje tukae wote asiwe bored na alifurahi sana uwepo wetu na nikafanya utambulisho pale.

Staffmate: Kumbe mwanagu una mtoto mkali sana ndio mana sikuizi hukai ofisin we fala.

Mimi: hahaha we si unajionea bro nataka niweke chombo ndani niwachie nyie nyie ma bachelor.

Tuliendelea pale mpaka saa 11:30PM "Staffmate" aliomba tuhame kiwanja twende Kiwanja jirani "AmuZz Bar and Grill" kua kuna dem wake yupo pale.Kwa sababu sio mbali tuliacha gari pale ni mwendo wa dakika 2 tu kufika pale muda huu ni kama pombe ilikua ishaanza kumuingia kila mtu maana kila mtu anaongea sana isipokua Debby alionekana na aibu kwa Staffmate.


ITAENDELEA .... Based On True Story
 
I appreciate mnaoleta story, ila kuleta story punguzeni unnecessary dramas, sasa unaanza kutupa maneno mengiii wakati ungeweza summarize kwa dakika 2 tu
@Beberu unachosema ni sawa kuna vipengele haifai kuruka si unaona nimeanza tu kidogo tayari naambiwa ni story ya kutunga as if huo mda tulikua wote aisee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom