Hilo la mwanamke kujenga na kutafuta chakula na mmewe akinyeshewa mvua inakuwa kesi sitachangia chochote, mimi nitachangia hili la mwanamme kwenda kuchunga na mkewe kufanya shughuli zingine kama kutafuta kuni, kupika, kukamua na kulea mtoto.
Mimi natoka jamii ya kifugaji na ukulima, kazi ya kuchunga ni kazi ambayo inachukua zaidi ya masaa manane hadi kumi na mbili kwa siku kutegemea na wingi wa majani pamoja na umbali wa maji ya kunyweshea mifugo, ni kawaida kabisa kwa mchunga ng'ombe kutoka saa moja asubuhi na kurudi saa moja jioni, kumbuka hiyo ni shughuli ya kila siku, niambie hapo atapata muda wapi wa kufanya shughuli zingine, lakini suala la kutafuta kuni unaweza kwenda mara moja ukatafuta kuni za wiki nzima, unaweza kuchota maji hata ya siku tatu hadi nne kulingana na wingi wa vyombo vya kuhifadhia maji.
Nikichukulia kabila letu iwe kama case study, kuna kazi ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya wanawake na zingine kwa ajili ya wanaume, mfano kama familia inao wanaume wengi(watoto au ndugu wanaoishi kwenye familia) kazi zao ni kuchunga, kulima na ng'ombe, kujenga ingawa sio kazi ya mara kwa mara, kutengeneza zizi la ng'ombe, kuchinja na kuchuna wanyama, kwenda kuhemea chakula wakati wa njaa, kuchota maji na kwenda mashineni kama ni mbali, kuchimba visima wakati wa kiangazi na kuhakikisha mbwa wamekula, na kama mbwa atabweka usiku au ng'ombe wamevunja zizi na kutoka, kazi ya kutoka nje na kuangalia ni ya mwanamme, kama kuna mayowe yanapigwa kijijini kitu si cha kawaida kimejitokeza bado ni kazi ya mwanamme kujua upine, mishale au mkuli ulipo ili awahi kwenye tukio.
Kazi za wanawake kama wako wengi, kukamua, kupika, kulea watoto, kuchota maji na kwenda kusaga kama ni karibu, kulima mazao ambayo sio mazao makuu ya chakula wala biashara mfano: viazi, kunde, choroko, kukata kuni na wanaume ndo watakaozifuata kwa kutumia wanyama kazi.
Kazi ya kulima kwa mkono kwa maana ya kupalilia pamoja na kuvuna kwa mazao makuu ya chakula na biashara kama Mahindi, Mtama, Pamba na Mpunga hiyo ni kazi ya jamii zote.
Lakini kama familia haina watu wa kutosha ama wanawake ama wanaume si ajabu kukuta mwanamke anachunga na analima na ng'ombe na ukakuta mwanamme anakamua, anapika na amebeba mtoto wakati mkewe kafuata maji au yeye mwenyewe kufuata.
Kwa hiyo huko kwetu usukumani specifically kwa wanyantuzu huo ndo ulikuwa mgawanyo wa kazi, inawezekana hata kwa wamasai nao huo ndo mgawanyo wao wa kazi.