Wanaume wa kiMassai. . .

BT kama ulikuwepo vile. . .
Alafu bado utakuta nao wanajiita kichwa cha familia, wakati utendaji wao sawa na wa mkia!!!
kila jamii ina mila na desturi zake huwezi leta za kiyahudi au kihindi kwa wagogo,,,unataka mmasai aishi kama mzaramo,,,,,je mngependa makonde aishi kama mholanzi,,,,,,mimi masai bwana,,,rip mr ebbo,
 
kila jamii ina mila na desturi zake huwezi leta za kiyahudi au kihindi kwa wagogo,,,unataka mmasai aishi kama mzaramo,,,,,je mngependa makonde aishi kama mholanzi,,,,,,mimi masai bwana,,,rip mr ebbo,

Hiyo haiwahusu waMassai tu. . .hata uChaggani nimeona familia zinazoishi kwa ukandamizaji wa style hiyo.
 
Lizzy, siwezi kukuambia ubaya wa generalisation and judgement, b'cause nimesha kuona mara nyingi ukiwauliza watu kwa nini wanafanya hivo (hasa pale wanapojiuliza kuhusu mila ya kichaga).

Kila kabila na mila yake. Na wamaasai walijenga mila yao kufatana na maisha na mazingira walo kua nayo huko nyuma. Maisha yenyewe yalikua ni ya ufugaji na mazingira yalikua ni mazingira ya savanah.
Katika mazingira hayo hatari zilikua nyingi mno, toka kwa vinyama vya porini au toka kwa clans zingine za kimaasai. kwa hivo walihitaji kugawa kazi za ndani kwa mtindo huu: mwanamke afanye shughuli zote atakazo weza ili mwanaume aweze ku-concentrate katika kuilinda familia yake tokana na dangers hizo. Pia wanaume walikua wanawinda vinyama na kuongeza variety katika chakula cha nyumbani.

Sasa kutokana na 'promotion' ya sekta ya utalii, serikali imegeuza eneo lao asili kua eneo la utalii na wenyewe wamelazimika kubadili mfumo wa maisha from what I have just described hapo juu kugeuka walinzi (that is what they were raised to do). Expropriation hii ilifanyik bila compensation, bila reinsertion na bila msaada wowote wa training, finance au aina yoyote ile kuhakikisha wana-adapt in their new environment. Unaweza kusema kua muda umefika kwa wamaasai ku-revise taratibu zao, na nakubaliana na wewe but it takes time and lots of eeffort toka kwao na toka kwa serikali pia to change it.

I know of one maasai man, na anafanya kazi nzuri tu. But haikutokea by coincidence. Alisaidiwa kwa namna moja au nyingine. Babu yake alisomeshwa na serikali, akawa mwalimu na baba yake alisomeshwa na serikali pia akaingia jeshini na kuendelea hadi ngazi za juu. hiyo 'exposure' ilichangia katika uamuzi wa baba yao kuwapeleka watoto wake wote shule na leo wote wana masomo, wana kazi na wanaendesha maisha kama westerns walivo taka tuendeshe maisha.

Hata hivo turudi kwa hao maasai ambao unazungumzia, yani wale walio porwa eneo zao na kutelekezwa mahala ambapo walishindwa kabisa kuendelea kuhishi kama mila yao ilivo wafunza: are you sure they are useles to their household? labda nikuulize suali moja tu, then tutaendelea from there: Nini kazi ya simba dume?
 
Hii hapa Malkia wangu Lizzy

Unajua kila jamii ina utaratibu wake wa kufanya kazi, wenzetu wapemba mama kazi yake ni kupika tu kazi nyingine anafanya mwanaume kama kwenda sokoni anaenda mwanaume kutafuta pesa anatafuta mwanaume kupeleka watoto shule ni mwanaume hawataki wake zao watoke toke nje wao ndani kupika na kumwandalia chakula cha usiku mwanaume baaaaaaaaaasi top je jamii hii husika utasema mwanamke ni ovyo hajitumi?
 
Ukichwa wa mwanaume kwenye familia aliutoa Mungu.Sasa sijajua kama ukichwa huu unatokana na kuongoza kwa kutoa maelekezo au kwa kutenda.Maana anaweza kuwa mbunifu akawa mwingine na mtendaji akawa mwingine sijui hapo nani ni nani!
 
Dah. . . kumbe waMassai nao wanajua kuFLIRT ehhhh?Hehehe. . nilidhani hayo ni mambo ya watu wa mujini tu.

Nwy siku zote tunasikia na kuambizana kwamba mwanaume ni yule anaeweza kujali,lisha na kulinda familia yake (provide for them). Miongoni mwa watu wanaoonekana wanaume kwenye jamii yetu ni waMassai kwa uhodari wa kuwinda na hata kuua simba kwa mikono, tena wakiwa na mikuki/sime zao ndo kabisa wanaonekana wa ukweliii.

Pamoja na kwamba nimewahi kuishi nao miaka ya nyuma, sikuwahi kujua baadhi ya mila zao juu ya maisha ya kila siku na namna yanavyoendeshwa ila sasa nimejua na ndio nikapata maswali kadhaa juu ya wanaume hao.

Kwanza kabisa hawajengi. Anaejenga ni mwanamke (mke/wake zake), na ole wao mvua inyeshe alafu bwana anyeshewe. . . lazima mama aambulie kibano na aeleze kwanini 'bwana inyeshewe'( in a Massai accent).
Pili chakula anatafuta mama.
Kutwa nikiangalia naona wanawake ndio wanaopita na punda + madumu kwenda kutafuta maji na kuni wanakokujua wao.

Wanaume utawaona wanapita fimbo zao + mbuzi na ng'ombe kupeleka machungani tu BASI. Wakija dukani wanaume wengi ni wanaulizia kiroba na beer. . . wachache sana watataka chumvi, sukari, mafuta, mchele au hata pipi za watoto kuashiria anakumbuka na kujali familia.
Mashine (kusaga na kukoboa) wanaokuja ni wanawake. . .
Kukamua wao. . .
Kupika wao. . .
Malezi wao. . .
Yani wanaume wao ni machungani kwenda kupiga soga huko wakati wamama wanapanda na kushuka na barabara. Kwa ufupi. . .wanalelewa na kutunzwa na wake zao.

Je nao ni wanaume? Au ndo sawa na wale wanaoitwa 'MARIO' mjini? Au yeye sio muAfrika hivyo ule utamaduni wa 'mwanaume wa kiAfrika ni provider' hauwahusu?
Naomba utuwekee hapa jamvini tabia za wanaume wa kabila lako ili tuone ni jinsi gani zinatofautiana, isije ikawa hawafanyi kazi kabisa isipokuwa ile moja tunayoijua sote.
 
mmasai+na+kitu.jpg

!!!!!!!!!!!!!!@@@@@@@@@@@@@@@@@@XXXXXXXXXXXXXX andastandi nasingi
 
RR kwasababu sijawa karibu na waMassai wa sehemu nyingine nyingi (hii ni mara ya pili) mimi nimewaongelea hawa tu ambao nawaona kila siku kwahiyo hii haiwahusu waMassai WOTE bali waMassai wa hapa nilipo.

Nikirudi kwenye swali lako. . .
Jibu ni ndio na hapana. Pengine kwenda machungani is all some women need from their husbands ila sio wote. Na nnasena hivyo kwasababu wapo hata wanaume wanaoamini kwamba huo mfumo ni wa kinyanyasaji (kumwachia mwanamke majukumu mia kidogo).

Na uzuri ni kwamba hilo nimejidhihirishia mwenyewe baada ya mmoja kusema kwamba amechukua ng'ombe wawili tu wa mahari kwaajili ya bintiye kwasababu wanaume wengine wakishalipa mahari wanaenda kuwafashisha wake zao kazi kama punda na kuwanyanyasa (maneno yake), hivyo kachukua wawili tu ili hilo likitokea iwe rahisi kumrudishia jamaa ng'ombe wake na kumchukua bintiye.

Wa pili yeye alikua anasita kununua kitu kwa sababu ya bei ila baada ya kumuuliza kama nikirudishe kwenye shelf akanijibu kuwa 'nimpe tu maana yeye ndo aliyemchukua mtoto wa mtu (mkewe) hivyo anatakiwa kutimiza majukumu.

Kwahiyo wapo wanaojali na kuona kwamba mwanamke kuzunguka na jua kutwa huku kabeba mtoto mgongoni kichwa/shingo ikiwa imeangukia pembeni kuashiria kwamba mana hata hana habari nae kwa uchovu kama wanavyoonekana sio sahihi.

Nwy. . .maadam bado niko hapa, ntakua naanzisha maongezi na wale wanaoonekana hawana haraka sana (wanawake na wanaume) ili nijue msimamo wao juu ya huo mfumo wa maisha waliochagua ama kuchaguliw.
 
Ukichwa wa mwanaume kwenye familia aliutoa Mungu.Sasa sijajua kama ukichwa huu unatokana na kuongoza kwa kutoa maelekezo au kwa kutenda.Maana anaweza kuwa mbunifu akawa mwingine na mtendaji akawa mwingine sijui hapo nani ni nani!
Nadhani wanatumia huo huo ukichwa waliopewa hata kama hawatimizi majukumu yaliyotolewa pamoja na title.

Naomba utuwekee hapa jamvini tabia za wanaume wa kabila lako ili tuone ni jinsi gani zinatofautiana, isije ikawa hawafanyi kazi kabisa isipokuwa ile moja tunayoijua sote.

Will do. . .
Ila kidokezo tu, kwetu ni rahisi sana kunotice nyumba/familia isiyo na mwanaume kabisa (mume, mjomba, baba, kaka, binamu) au yenye mwanaume asiyejishughulisha kwaajili ya familia yake.Uzuri. . .sio wengi kama wanaojishughulisha.
 
Lizzy, naona umekaa ki-research zaidi. beware of your own bias. Ni kama una-compare wamaasai (a quite traditional and concervative tribe) na standards zile unazo amini kua sahihi. Jaribu kujali historia yao, mazingira yao, na aspirations zao. what is their idea of role distribution etc.
Enjoy your journey in their land, they are wonderful men and women. I married one of them :mwaaah:
 
Unajua kila jamii ina utaratibu wake wa kufanya kazi, wenzetu wapemba mama kazi yake ni kupika tu kazi nyingine anafanya mwanaume kama kwenda sokoni anaenda mwanaume kutafuta pesa anatafuta mwanaume kupeleka watoto shule ni mwanaume hawataki wake zao watoke toke nje wao ndani kupika na kumwandalia chakula cha usiku mwanaume baaaaaaaaaasi top je jamii hii husika utasema mwanamke ni ovyo hajitumi?

Ume-balance story mzazi....
Ahsante!
 
jf mambo iko hivi kila kabila lina taratibu zake na kila familia niliwahi kaa na wachaga mean wa kibosho mama anaamka anaingia shamba anapiga kazi anaandaa msosi hadi chai at same time anakata ndizi ya kupeleka town kuuza mean hiyo ni before saa mbili asubuh then anashuka mwendo wa masaa2 kufika moshi mjin kwaajili ya kutembeza ndizi mzeesa hiyo akiamka anakata matawi mawili matatu ya migomba anarushia mbuzi anaenda kilabun right time hana hela anaendelea kunywa anasubiri wife arud kuuza apitie kumlipia deni this mpaka sasa yani mambo ndo hivyo
tena some tyme baba anakua amejenga nyumba 2 moja kubwa ya kwake na kijumba hata cha udongo kwaajili ya mama na watoto na mifugo so mama anakua kama mlinzi wa mifugo tu xaxa si bora wamasai akirudi anatoa hitaji muhimu wazee wa kichaga dah yeye na kitochi tu ndo maana hata tunasema wachaga hawajui mapz ni kwamba hawafanyiwi mazoezi!!!!!:lock1:
 
Hii hapa Malkia wangu Lizzy

Sasa nimekupata jG.
Unajua kila jamii ina utaratibu wake wa kufanya kazi, wenzetu wapemba mama kazi yake ni kupika tu kazi nyingine anafanya mwanaume kama kwenda sokoni anaenda mwanaume kutafuta pesa anatafuta mwanaume kupeleka watoto shule ni mwanaume hawataki wake zao watoke toke nje wao ndani kupika na kumwandalia chakula cha usiku mwanaume baaaaaaaaaasi top je jamii hii husika utasema mwanamke ni ovyo hajitumi?

Mende kuna tofauti kati ya kukwambia "we osha vyombo tu mie mengine ntafanya" na mtu kukwambia "mi ntaosha tu vyombo mengine yote juu yako". Na kama ulivyosema hapo juu wanaume wakipemba ndio wanapenda kuwasaidia wake zao hayo yote, je mwanamke wa kiMassai nae kajitolea mwenyewe mpaka kumjengea mume nyumba ya kulala? Binafsi sidhani, ila ntawauliza kwa uhakika zaidi.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom