Wanaopata shida upataji wa Passport au Visa kwa ajili ya kusafiri

McMoze

Member
Oct 23, 2011
49
8
Wadau hbr zenu, kumekua hakuna haki sawa kwanza hapa Tanzania, kwenye upataji wa travelling document i.e passport. swali la msingi, je passport siyo haki ya kila mtu kua nayo kama ID's zingine? Pili ni upande wa visa, wazungu huja hapa kwetu kwa masharti nafuu sana. Lakini ukijaribu wewe kuomba visa ulaya au nchi zingine utaona joto lake.

Sasa mimi nasema hivi! kila mtu anahaki ya kusafiri sehemu yeyote duniani regardless of watever. Pia nipo tayari kutoa msaada wowote iwapo umepata shida kupata passport au visa bila mafanikio. Nitatoa msaada huo free of charge, hii ni harakati ya kutokomeza hali ya unyanyapaa kwa waliyonayo maafisa uhamiaji na mabalozi wa nchi za ughaibuni kuwakwamisha wananchi wetu kusafiri.

Wazungu walikuja huku karne izo bure bila visa, wakachukua dhahabu na rasilimali watu wengi sana. Ni lazima wazirudishe kwa njia moja au nyingine.

Wenu katika harakati.
 
pasport ni haki ya kikatiba. Kila mtanzania aliefikia umri wa miaka 18 na kuendelea ana haki ya kuwa na passport. Kama wewe ni raia halali wa tz,Hao maafisa wasikubabaishe kwa lolote!
 
Wadau hbr zenu, kumekua hakuna haki sawa kwanza hapa tanzania, kwenye upataji wa travelling document i.e passport. swali la msingi, je passport siyo haki ya kila mtu kua nayo kama ID's zingine? Pili ni upande wa visa, wazungu huja hapa kwetu kwa mashart nafuu sana. Lakini ukijaribu ww kuomba visa ulaya au nchi zingine utaona joto lake.

Sasa mimi nasema hv! kila mtu anahaki ya kusafiri sehem yyte duniani regardless of watever. Pia nipo tayari kutoa msaada wowote iwapo umepata shida kupata passport au visa bila mafanikio. Nitatoa msaada huo free of charge, hii ni harakari ya kutokomeza hali ya unyanyapaa kwa waliyonayo maafisa uhamiaji na mabalozi wa nchi za ughaibuni kuwakwamisha wananchi wetu kusafiri.

Wazungu walikuja huku karne izo bure bila visa, wakachukua dhahabu na rasilimali watu wengi sana. Ni lazima wazirudishe kwa njia moja au nyingine.

Wenu katika harakati.

shukrani sana mkuu
 
Visa pagumu sana ila ina uma yaani wazungu wana jaza fomu za visa ndani ya ndege nakumbuka ilikuwa nimepanda ndege kutoka Sweden ile tunakaribia Tanzania wakaanza kupewa fomu za visa wajaze kweli hakuna usawa...
 
Hiyo ndo Tz bhana
 
Ok ndugu yangu usijali. Ninachoweza kukushauri ni kwamba ogopa matapeli, hakuna mtu anayeweza kukuguarrantee visa asilimia 100%. ila tu mimi nitatumia ushauri wangu kwa uzoefu nilionao ktk kufanya kazi embassy mbalimbali. ushauri utakaokuwezesha wewe mwenyewe kuufata na kua na uhakika wa zaidi ya asilimia 90 wa kuipata hiyo visa. Kumbuka kusafiri ni haki yako!! Unaweza kuni PM namba yako ili nikupe maelekezo ya kina
 
nitakupataje mkuu?

Ningefurahi ungepost kile unachohitaji hapa ili umma kwa ujumla waweze kufaidika pia. unaweza kuni PM namba yako kama tu una specific info unaihitaji. Maana lengo hapa ni watanzania kwa ujumla waweze kufaidika. Kumbuka kusafiri popote duniani ni haki yako ya msingi, ila binadamu wameweka misingi isiyo sawa.
 
Nilifukuzwa kazi ubalozini baada ya kile kilichoonekana kua nilikua naaprove visa kirahisi bila kufata taratibu za balozi. Nilichukizwa sana na swala la watanzania kuwekewa vikwazo vigumu sana ktk swala la visa. Wakati nafahamu wao wanafika nchi hii wa masharti rahisi sana, tena % kubwa hawahitaji hata visa kuingia nchini.

Lakini sitojali hata kama nipo nje ya embassy nitaendelea kupigana na udhalimu huo kwa kuwapa nduguzanguni mbinu jinsi ya kujiandaa nchi yoyote unayohitaji kupata visa
 
Visa pagumu sana ila ina uma yaani wazungu wana jaza fomu za visa ndani ya ndege nakumbuka ilikuwa nimepanda ndege kutoka Sweden ile tunakaribia Tanzania wakaanza kupewa fomu za visa wajaze kweli hakuna usawa...

Sijakubaliana nawe kwamba wazungu wanajaza form za visa wakiwa ndani ya ndege kabla ya kutua, nimesafiri mara kadhaa kwa nchi kadhaa nimekutana na zoezi hilo, ile siyo form ya visa bali ni form inayorahizisha shughuli za uhamiaji unapofika pale airport na form hizo hutunzwa kama vielelezo.

Kuna baadhi ya nchi hata ukiwa raia unaporudi nchini mwako lazima ujaze na unaeleza ulivyo navyo iwe nguo, chakula, pesa nk. Tanzania tulikuwa na utaratibu huo pia lakini kwa sasa umesitishwa ila ni kwa wageni tu. Wageni hao kabla ya kuja huwa wanapata visa kwenye balozi zete isipo kuwa nchi zile ambazo zina makubaliano kupata visa ukishatua katika nchi husika.
 
Nadhani mhusika ameshaelewa kuhusu hilo. Ni kweli ulichosema ndugu. Japo kikubwa ni kwamba, wazungu hata kama wanakuja kwa visa huku kwetu. Hupata visa kwa mashart nafuu sana, tena kwa kubembelezwa. Sisi watz tunanyanyaswa sana na tunakua discouraged kufanya zoezi hilo
 
Kwenye passport nilipata shida zaidi ya miezi 2 kila nikienda narudishwa. Baadae nikampata mdau mmoja ambae anaofisi yake maeneo ya mjini, nikampa laki na 50 akanijazia upya, akamaliza kila kitu. Then akanipa elfu 50 ya kulipia uhamiaji na namba ya simu ya afisa wa pale, pamoja na bahasha ya kaki ambayo niliifungua mbele nikakuta kaweka elfu 40 kwa ajili ya huyo afisa. Kufika nikamcheki huyo afisa akaandika kitu juu ya fomu yangu, nikaenda nayo kwenye foleni nikapitisha ikapita nikafata process zote baada ya siku 10 nikapata passport yangu.
 
Naomba ni PM number ya jamaa aliekusaidia
 
  • Thanks
Reactions: GKM
Ndugu huhitaji kutoa pesa yote hiyo kupata passport. Unahitaji tu kufata taratibu zote husika. Kama kua na docs zote, kama vile cheti cha kuzaliwa, Id yako, affidavit ya mzazi, barua utambulisho kutoka (serikali mtaa/kazini/shuleni-chuoni), barua ya sababu ya safari. Au kama mfanyabiashara attach tin na leseni yako hapo. Passport ni shs elf 50 tu. Ukiwa unamiss docs au mashart kutotimiza ndio hapo unakaribisha rushwa kuchkua nafasi.
 
Tatizo letu Watanzania, tunapohitaji kitu flani ndio tunaanza kukitafuta. Mfano mimi nilianza kuangaikia cheti cha kuzaliwa niliposikia kinahitajika HESLB mwaka ule ninapotuma applications za chuo. Kutokana na haraka haraka, nikapigwa Tsh 25,000 pale vizazi na vifo wilayani.

Same applies mtu siku ukihitaji passport na unatakiwa maybe usafiri, kuna mchongo mnono, unashangaa kuna document ndogo unaimiss au ili uipate haraka haraka, unaombwa pesa ya ziada. Ndio chanzo cha kutoa 100,000Tshs instead of 50,000Tshs ambayo (nasikia) ndio halali.

Tujijengee katabia ka kujiandaa na vitu kama hivi mapemaa.

Haijawahi kukutokea unataka tuma application ya kazi hafu ata picha za passport huna?
 
ngoja nikupe my expirience, nilikua nina vyeti cha kuzaliwa, cha chuo, vya sekondari na high school, nikajaza fomu kwamba naenda safari ya kazi (nilikua na lengo la kwenda nchi flani kusaka kazi). Kupeleka wakaniambia unatakiwa uwe na barua ya kuitwa kwenye kazi na mavitu kibao, nikachange next day nkaenda nkajaza naenda kufanya biashara wakaniambia niattach leseni ya biashara, TIN number n.k, sikuchoka nikaandika safari binafsi nikaambiwa ni attach barua ya mwaliko next day nkaenda nayo kufika wakaniambia tena niweke copy ya passport ya alienialika na visa yake. Hapo nikachoka
 
Ndugu huhitaji kutoa pesa yote hiyo kupata passport. Unahitaji tu kufata taratibu zote husika. Kama kua na docs zote, kama vile cheti cha kuzaliwa, Id yako, affidavit ya mzazi, barua utambulisho kutoka (serikali mtaa/kazini/shuleni-chuoni), barua ya sababu ya safari. Au kama mfanyabiashara attach tin na leseni yako hapo. Passport ni shs elf 50 tu. Ukiwa unamiss docs au mashart kutotimiza ndio hapo unakaribisha rushwa kuchkua nafasi.

Kwa mfano mtu anataka passport akae nayo in case kuna safari yoyote mbeleni asiangaike ataatach nini? Ukijaza biashara unatakiwa TIN namba kitu ambacho huna na kila kipengele unachojaza kuna kitu cha ku attach ambacho obvius ni ngumu sana kupata
 
Kwa kusaidia wengine kama unataka passport na hauna attachment wanazotaka, kwanza andaa barua ya afisa mtendaji, 2, vyeti vya shule 3 cheti cha kuzaliwa cha mmoja kati ya wazazi 4. Barua ya kuomba passport 5. Cheti cha kuzaliwa. Kwenye kujaza andika dhumuni la safari ni biashara ndogo ndogo/ ujasiriamali na nchi unayotaka kwenda andika nchi za jirani kama zambia, malawi n.k
 
Back
Top Bottom