DOKEZO Tuhuma za mauaji kwa mmiliki wa kampuni ya KOPAGAS, Andron Mendez

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

TheCrocodile

JF-Expert Member
May 31, 2021
1,077
2,814
Kampuni ya Ulinzi (HOMASA SECURITY) inapata bahati ya kuingia mkataba na Bilionea ANDRON MENDES

Mkataba huu unahusisha kumlinda Bilionea huyu nyumbani kwake na Pia kulinda kwenye ofisi ilipo kampuni yake ya KOPA GAS huko maeneo ya Skanska Tegeta karibu na IPTL.

Bilionea huyu wa kitanzania alipiga “mshindo” wa kutakata baada ya kugundua teknolojia ya “Lipa kadiri unavyotumia” (Pay as you go) Katika matuzi ya gesi za kupikia hasa majumbani.

Yaani unaweza ukanunua hata gesi ya buku moja, Sio lazima uwe na pesa ya limtungi looote la gesi

Ugunduzi huu unawavutia kampuni ya Uingereza ya CIRCLE GAS kununua technology wakishirikiana na Safaricom ili tekinolojia hii itumike kenya pia.

Deal hili linageuza kabisa maisha ya ANDRON MENDEZ akiwa na umri wa miaka 35.

Tarehe 20 November 2022

Saa 4 Usiku, Katika ofisi za KOPA GAS, anafika pale mmiliki wa ofisi ile bwana ANDRON MENDES aliwa na mkewe kwa kutumia gari aina ya Toyota Harrier Nyeusi lenye namba za usajili T 698 DRN

Anaonekana akiwa “Matingas” kwa sana.

Na anafika hapa baada ya ujumbe ambao mkewe alikuwa ametumiwa kwenye simu yake kutoka kwa kichomi kumuhusu mfanyakazi wao aitwaye ADINAN almaarufu kama “Uchebe”

Huko ndani watu wanaendelea na kazi zao yaani wako busy kama vile mchana wakipakua mitungi mitupu ya gas na kupakia iliyojazwa kwa ajili ya wateja.

Ndani kuna walinzi wawili. Mwenye bunduki aliyepo Getini na mwenye kirungu aliye ndani kabisa inapofanyika kazi.

Mara Unasikika mlio wa risasi kwa nje. Wote waliokuwa wanafanya kazi ndani wakaganda kama vinyago. Mkao wa kimasta kusikilizia kuna nini huko nje?

ANDRON akaenda getini na kumtaka mlinzi amfungulie. Kwa kuwa yule ndio mwenye ofisi, mlinzi akamfungulia mlango bila ubishi. ANDRON akafika katikati ya eneo la biashara yake (Godown lenye ukubwa kama nusu ya playground). Pale katikati kuna mitungi ya gas lakini pale tena akafyatua risasi nyingine hewani. Wafanyakazi wakaona huu mzaha sio mzaha, Kila mmoja alishindana na mwenzake mbio kutoka nje.

Dakika chache wakiwa nje ukasikika tena mlio mwingine wa risasi huku ikisikika sauti ya mkewe akisema “Andron Usimuue usimuue”. Sasa Andron akawa ameshafika kwenye eneo la kibanda cha mlinzi alipokuwa amekaa yule mlinzi mwenye siraha. Akamwamuru aweke chini Bunduki. Mlinzi kwa kujua Mteja wao hayuko tena kwenye masihala. Akagoma kuachia bunduki lakini akakimbilia nje huku akiwa amesahau simu yake kwenye kibanda chake. Akaenda zilipo Ofisi za N Gas maeneo ya karibu na pale kuomba msaada wa simu awataarifu waajiri wake kilichojili.

Alifanikiwa kutoa taarifa na kurudi lindoni kwake ambapo hakumkuta Andron wala Mkewe. Alipoingia getini mbele kidogo akaona dimbwi la damu hali hiyo ikamshtua akaanza kumtafuta mlinzi mwenzake kimya kimya bila kutoa sauti. Alipomkosa akaanza kumuita kwa sauti bila mafanikio. Akaenda getini na kuchukua simu yake ili ampigie huyo mlinzi mwenzake. Alipopiga simu, ikapokelewa lakini ikaachwa hewani bila yeyote kuzungumza. Baadae simu hii ikazimwa kabisa.

Baada ya kama Dk 20 ANDRON akarudi na kumtaka mlinzi afukie ile damu na atambadilishia maisha. Mlinzi akakataa kufuta damu asizojua ni za nani. Baada ya muda Operation Manager wa ile kampuni ya ulinzi akafika pale na akawa anamhoji mlinzi aliyekuwepo nini kimejiri.

Muda ule ule Mkurugenzi bwana JOE wa kampuni ya ulinzi naye akafika na kumfuata ANDRON. Akamuuliza Andron kuna shida gani pale?

Andron akajibu hakuna shida kuna mambo tu anaweka sawa. Wakamhoji ile damu pale ndani ni ya nini na mlinzi mwenzao yuko wapi? Badala yake, Mkurugenzi akajibu kuwa Kuanzia siku hiyo hataki huduma za ulinzi kutoka kwao. Akaondoka.

Mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi akaamuru ulinzi uinarishwe pale kwani hawezi kuacha lindo kiholela. Kisha yeye na Yule mlinzi aliyekuwepo tukioni na OP manager wakaongozana kwenda kituo cha polisi Wazo Hill. Ajabu wakamkuta ADRON pale polisi.

Viongozi wa Kampuni ya Ulinzi walimkuta Andron akitoa maelezo lakink wao walipofika Mkurugenzi huyo akaacha kutoa maelezo mapaka watolewe nje wale watu wa kampuni ya Ulinzi.

Kweli bwana! Viongozi wale wa kampuni ya ulinzi wakatolewa nje hivyo Andron akaendelea kutoa maelezo ndani akiwa peke yake. Alipomaliza kutoa maelezo Polisi, Viongozi wa HOMASA SECURITY na Andron wakaongozana kwenda eneo la tukio. Kule wakakuta damu na kuokota maganda matatu ya risasi. Timu nzima ikarudi tena polisi kituoni.

Andron akaambiwa asalimishe silaha iliyotumika ambapo baada ya kuulizwa juu ya umiliki wake akasema siyo ya kwake bali ni ya mkewe. Alipoulizwa nani alifyatua risasi? Androni akakili ni yeye ndiye aliyefyatua japo sio mmiliki wa silaha ile. Kisheria hili tayari ni kosa la Kwanza.

Andron akasema kuwa silaha ile ina risasi 15 na yeye alifyatua tatu hewani.

Katika hali ya kushangaza polisi wakawataka wote, Yaani Andron, Mkewe na Viongozi wa Homasa Security kuondoka na warudi kesho yake asubuhi. Viongozi wa kampuni ya ulinzi wakahoji inawezekana vipi watu ambao ni wanatuhuma kubwa ya uhalifu kama ile waruhusiwe kuondoka? Yaani mtu afyatue risasi, kisha mlinzi mmoja apotee asijulikane alipo na zinakutwa damu zisizo na maelezo ya kutosha kama ni za binadamu au mnyama na zaidi ya yote gari iliyotumika kwenye eneo la tukio waachiwe washukiwa kuondoka nalo?

Ndugu msomaji, Pesa ina nguvu bwana!

Polisi wakawajibu kuwa swala lile bado liko kwenye uchunguzi na hakuna mshukiwa hivyo waondoke na warudi kesho yake kufungua kesi.

Usiku wa deni haukawii!

Kesho yake majira ya saa 3 asubuhi viongozi wa Homasa Security walifika pale kituoni lakini cha ajabu si bwana Andron au mkewe walikuwa wamefika kituoni. Viongozi wa kampuni ya ulinzi wakatoa maelezo yao na pia wakataka gari iliyokuwa eneo la tukio ifikishwe pale kituoni. Polisi wakawa wanampigia simu bwana Andron, Sio kwamba aende yeye kituoni na mkewe kama walivyoamuru jana, bali walimtaka apeleke pale kituoni gari kama inavyotakiwa na walalamikaji.

Ukwasi una nguvu ya ajabu sana!

Andron hakutokea tangu apigiwe simu saa 3 ile asubuhi mpaka alipopeleka gari saa 10 jioni. Lazima hapa katikati alikuwa katika harakati za kuficha ushaidi. Naam! utamweleza nini mtuhumiwa huru? Sasa ndugu Andron alikuwa ni kama mtu ajifichaye kwenye jani la tembele akiamini amepata maficho ya kutosha.

Kwa nini nasema hivi? Ni kwamba pale kituoni alienda na gari Toyota Harrier New Model nyeusi lenye namba za usajili T 605 DXG akidai ndio lililokuwa tukioni. Alikuwa amesahau kabisa kuwa Kampuni iliyokuwa ikimlindia ofisi ndiyo ilikuwa ikilinda nyumbani kwake hivyo ilikuwa inayajua magari yake yote.

Viongozi wa kampuni ya Ulinzi wakasema gari lile siyo ambalo lilikuwa tukioni. Cha ajabu bado bwana Andron aliachiwa kuondoka huru kabisa akiwa na gari ile aliyokwenda nayo.

Viongozi wa kampuni ya ulinzi wakajiaminisha kabisa haki haitatendeka pale katika kituo cha polisi Wazo. Wakaamua kwenda kushitaki katika kituo kikubwa cha Mabwepande. Polisi wa Mabwepande wakaenda kumkamata bwana Andron pia wakaipeleka gari zote mbili, Iliyokuwa kituoni na ile aliyoipeleka awali kituo cha Wazo.

Kesi yahamishiwa Oysterbay Police

Tarehe 24 November 2022 jalada la kesi ile likahamishiwa kituo cha polisi Oysterbay. Hivyo Andron naye akahamishiwa kituo kile. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kichomi wangu ambaye alikiwa amewekwa korokoroni pale kituoni cha Oysterbay anadai Kituo kilikiwa kinajaa wazungu wengi kwenda kumuona Andron.

Aliponiuliza ni kwanini nikampa inawezekana kutokana na sababu mbili:

Andron anamiliki kampuni ya KOPAGAS pamoja na mbia mwenzake ambaye ni raia wa Mexico hivyo inawezekana wazungu wale wakawa ni jamaa wa mbia mwenzake.

Pia kampuni ya CIRCLE GAS ambayo ilinunua teknolojia yao ni kampuni ya Uingeleza hivyo labda wazungu wale wakawa ni sehemu ya watu wanaofanya nao biashara.

Basi kichomi huyu akadai kuwa kuna mazingira ya ushawishi mkubwa wa pesa unaoendelea pale lakini ni kama haelewielewi. (Nitafafanua mbeleni)

Lakini kichomi huyu akanipa taarifa zilizofanya nishtuke. Alinieleza kuwa alikuwa anamuona mke wa Andron akienda kumuona mmewe pale polisi kwa nyakati tofauti na kuondoka. Nikashangaa inakuwaje mwanamke huyu anakuwa huru uraiani? Huyu naye alipaswa kuwa ndani kwa sababu:
  1. Alikuwepo kwenye tukio
  2. Gari lililotumika kwenye tukio ni mali yake
  3. Bastola iliyotumika ni mali yake
Wakati haya yanaendelea, Zikaibuka habari mpya in connection with the case in question.

Kuwa tarehe 21 November 2022, Huko maeneo ya Vikawe mkoani Pwani, Msamalia mwema aliuona mwili wa binadamu asiye na uhai ukiwa umetelekezwa katika msitu wa Vikawe.

Taarifa hizi alienda kuzitoa katika kituo cha polisi Kibaha.

Polisi walipofika walikuta mwili ule ukiwa na jeraha kichwani lililosadikika kutokana na risasi. Baadae mwili ule uligundulika ni wa yule mlinzi wa Kirungu aliuekuwa akilinda katika kampuni ya KOPAGAS ambaye alitoweka siku ya tukio. Mlinzi yule alifahamika kwa jina la SALIM ALY HAJI.

Mmiliki wa kampuni ya Homasa baada ya kuutambuka mwili ule aliwajulisha ndugu wa marehemu akiwemo mkewe. Marehemu alikuwa anatokea wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Naamini ndugu msomaji mnaijua tabia ya watani zangu wasambaa wanavyopenda kesi. Basi ndugu wa kisambaa wakawa wanajaa pale kituo cha Oysterbay kutaka haki juu ya ndugu yao kutendeka. Yaani jitihada za kuifunika kesi ile zikawa zinazidi kuwa ngumu kwani ndugu hawa walikuwa wanaenda kwa shift pale kituoni.

Kichomi mmmoja akanitonya kuwa mmoja wa ndugu wale aliitwa ofisini ndani ya kituo cha polisi na kuonyeshwa maburungutu ya manoti kuwa awashawishi wenzake wafunge mdomo.

Kwa hiyo kulikiwa na nguvu kubwa iliyokuwa ikitumika kutaka kuzika kesi hii kuanzia kule Mabwepande mpaka Oysterbay ndio maana wazungu walikuwa hawaishi kituoni.

Kwa mujibu wa mmiliki wa Kampuni ya Homasa Bwana Jose Mangesho ni kwamba bwana Andron alifungia sana Kibubu kwenye kila kituo alichopelekwa.

Sasa turudi tena kwenye siku ya tukio.

Ni ujumbe gani aliotumiwa mke wa Andron hadi kusababisha kadhia hii?

Hapa inabidi kumtambua mfanyakazi wa KOPAGAS aitwaye ADINAN aka Uchebe.

Huyu alikuwa ni dereva wa pikipiki zilizokuwa zinatumika kusambaza gesi za KOPAGAS kwenda kwa wateja wao mbalimbali.

Mle ndani ya eneo la KOPAGAS, Kulikuwa kunapakiwa pia magari aina ya Virikuu ambavyo vilikiwa vinabeba mitungi mitupu ya kampuni ya Oryx Gas

Sasa Adinan alikuwa ni ntu ya dili

Ukiachana na kuwa ntu ya dili alikuwa pia na tabia za ubabe, kwani alikiwa akiishia kuwapa wenzake afutatu akishamaliza kupiga matukio yake.

Adnani alikiwa akiishi nyumba moja na jaaa fulani ambaye huyu naye alimletea ubabe wa kumpa afutatu kwenye dili fulani la majiko ya Gas waliyokuwa wamepiga.

Mtu huyu aliyedhurumiwa ndiye aliyekuja baadae kuwa Kichomi wa Adnani kwani alikuwa anaijua michongo yake yoye.

Alikuwa anajua kuwa Adnani alikiwa akiingia Godown Usiku akiwa na pipes ambazo alikuwa akizitumia kunyonya gesi kutoka kwenye mitungi ya M-Gas na kuihamishia kwenye mitungi mitupu ya kilo sita ya kampuni ya Oryx.

Kampuni ya M-Gas ni kampuni tanzu ya kampuni ya Circle Gas yaani wale walionunua tekinolojia ya Kopagas.
Hii ina maaana Adinani alikuwa akimuibia boss wake.

Katika dili hili Adinani alikuwa akipozwa na anawowawekea gesi.

Sasa siku ya siku ndio kichomi akatuma Sms kwa mke wa Andron kumjua kuwa Adinani yupo site akiendeleza wizi ule.

Mkewe alitumiwa sms ile kwa kuwa ni yeye ndiye anahusika na issues zote za store.

Message ile ikasomwa na Andron mwenyewe.

Sasa unaambiwa Andron si yeye tub ali ukoo wao mzima huko Babati una hulka ya hasira kali.

Akachukua bastola akaondoka na mkewe kwenda tukioni.

Huko katika harakati za kupiga chuma Adinani ndio akakosea na kumlipua mlinzi.

Kosa lake kubwa likawa ni kwenda kuficha maiti uko porini kibaha.

Na mkewe ndiye aliyanyoosha maelezo haya polisi siku moja baada ya yeye pia kushikiliwa alipoenda kumtembelea mmewe mahabusu Oysterbay.

Hii ilikuwa ni baada ya mimi kuibuka na Uzi huu Twitter jambo ambalo liliwafanya manjagu baadae waje na taarifa iliyoyanyoosha maelezo kama rula.

Lakini kuna infoma anadai hii sio mara ya kwanza kwa Andron Msomi kutoka DIT kufanya hivi lakini taarifa hizi sijazithibitisha kwani zimehusisha mambo ya kijadi zaidi

Credit: Fortunatus Buyobe (Telegram channel)
 
Naomba jina la Twitter lenye hyo story mkuu .... na km Andron sie aliyefyatua risasi why afiche .... na Adinani alipata wapi hyo silaha ya kumuua mlinzi....Naona ndugu Adnani anataka kuangushiwa jumba bovu apo....pesa inataka kufunika mambo
@fbuyobe
Ila twitter iko nusu, ukitaka full hadi kwenye Telegram channel yake ya kulipia.
 
Back
Top Bottom