Wananchi wa Mwanza walalamikia kuondolewa kwenye maeneo bila kulipwa fidia na kuuzwa kwa Vigogo wa Serikali

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,026
1,621
Eneo hilo lenye viwanja 39, linalalamikiwa na wananchi kuwa lilichukuliwa bila wao kulipwa fidia na kuuzwa kwa vigogo hao wa serikali. Dk. Mabula pia amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Allan Kijazi, kuunda tume huru ambayo itafanya uchunguzi wa kina kuhusu viwanja hivyo.

Alitoa agizo hilo jana jijini Mwanza alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu wizara yake ikiwamo mipango ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2022/23.

Alikiri kwamba eneo hilo la Isamilo ambalo lipo katikati ya Jiji la Mwanza, viwanja vyake vimeuzwa kwa vigogo hao, akitaka tume hiyo ifanye uchunguzi wa kina na kumpatia majibu ya nini cha kufanya.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa hivi karibuni katika tovuti ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza na vigogo hao ni pamoja na Spika wa Bunge, Dk. Tulia Akson, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Alphayo Kidata, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja.

Wengine waliouziwa viwanja hivyo ni pamoja na Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Sekiete Yahaya, Meya wa Jiji hilo, Sima Costantine Sima, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Ngusa Samike, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Amon Mpanju, na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, ambaye alipata sehemu nyingine ya Luchelele.

Wengine ni pamoja na mtoto wa Magufuli, Michael Magufuli pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadick.

Dk. Mabula alisema licha ya kuwa kila mtu wakiwamo watumishi wa umma wana haki ya kununua viwanja vinavyouzwa na serikali, lazima wawe wamefuata utaratibu. Jiji hilo la Mwanza lilitangaza kuuza viwanja hivyo katika maeneo ya Isamilo na Luchelele kuanzia Juni 2, mwaka huu na kila mwombaji alitakiwa kulipia Sh. 20,000 kwa ajili ya kuchukua fomu.

Fedha hizo zilikusanywa na Jiji la Mwanza huku wananchi wa kawaida wakijitokeza kulipia ili waweze kupata viwanja vya makazi na biashara. Kwa mujibu wa tangazo hilo la kuwapatia viwanja, wanatakiwa kufika ofisi za jiji kuchukua ankra ya malipo ili wakavilipie.

Mmoja wa wananchi waliomba kununua viwanja hivyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe, alisema alilipia benki Sh. 20,000 kwa ajili ya kuomba kiwanja eneo la Luchelele, lakini hakuwahi kujulishwa kama alipata ama alikosa. Alisema tangazo lililotolewa kwa wananchi wakati wa kutangaza kuuza viwanja hivyo, lilisema eneo la Luchelele mita moja ya mraba ilikuwa ikiuzwa Sh. 5,000 kwa viwanja vya makazi.

Aliongeza kuwa eneo la Isamilo mita moja ya mraba ilikuwa ikiuzwa Sh. 25,000 ambavyo vilikuwa vichache katika mradi huo. Katika maeneo hayo mawili, tangazo hilo pia lilisema kulikuwa na viwanja kwa ajili ya makazi na biashara.

Tangazo la Jiji la Mwanza lilisema watu waliopatiwa viwanja hivyo, walitakiwa kwenda kuchukua ankara za malipo kuanzia Juni 23 hadi Juni 30 mwaka huu. Katika eneo la Luchelele, watu 427 wametangazwa kupatiwa viwanja hivyo huku viwanja vilivyotangazwa Isamilo vikiwa ni 39 ambavyo vimechukuliwa na vigogo.

Wiki iliyopita alipoulizwa kuhusu vigogo hao kupatiwa viwanja, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Sekiete Yahaya ambaye ameuziwa kiwanja eneo hilo la Isamilo, alimtaka mwandishi kwenda ofisini kwake na wananchi wanaolalamika.

Akizungumzia kuhusu migogoro ya ardhi inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini, Dk. Mabula alisema moja ya vipaumbele vya wizara yake ni kuhakikisha inamaliza migogoro yote kwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan hataki kusikia suala hilo.

Alisema moja ya mipango ya kukabiliana na suala hilo ni pamoja na kuimarisha tume za mipango za ardhi ngazi ya mikoa pamoja na kuimarisha mabaraza ya ardhi ngazi za wilaya zote nchini.

Chanzo: Nipashe

Pia soma
Wananchi Mwanza walalamika vigogo kupendelewa viwanja
 
Mwanza ni shida! Hiyo Kamati ishiishie hapo, ichunguze pia mgogoro wa eneo la Kigoto. Huko wananchi walidhurumiwa maeneo yao.
 
Nchi hii jambo lolote likitokea
Wa kwanza kula ni vigogo serikali

Ova
 
Eneo hilo lenye viwanja 39, linalalamikiwa na wananchi kuwa lilichukuliwa bila wao kulipwa fidia na kuuzwa kwa vigogo hao wa serikali. Dk. Mabula pia amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Allan Kijazi, kuunda tume huru ambayo itafanya uchunguzi wa kina kuhusu viwanja hivyo.
Uandishi wako umejikita zaidi kwa vigogo walionunua kuliko kwa waliokosa fidia.
 
Mwanza ni shida! Hiyo Kamati ishiishie hapo, ichunguze pia mgogoro wa eneo la Kigoto. Huko wananchi walidhurumiwa maeneo yao.
Waliuza wenyewe kwa bei cheèe kuendekeza njaa zao japo walidanganywa na aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa Ndg. PETER MBUGA
 
Waliuza wenyewe kwa bei cheèe kuendekeza njaa zao japo walidanganywa na aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa Ndg. PETER MBUGA
Aisee, kumbe! Mimi niliasikia mmoja akilalamika kumbe waliingizwa mjini. Dah nchi hii baraaa
 
Waliuza wenyewe kwa bei cheèe kuendekeza njaa zao japo walidanganywa na aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa Ndg. PETER MBUGA
Siyo njaa! Serikali haitakiwi kuwa ni kikundi cha wapuuzi au waonesha mazingaombwe. Yaani ukizubaa tu serikali inakuliza! Nchi hovyo! Utawala Hovyo! Unapoona viwanja vinagawiwa Mwanza na waliopewa ni kutoka Dodoma, Mbeya, Dar es Salaam, n.k. unaelewa nini? Ifike mahari uongozi isiwe ni mkusanyiko wa wahuni fulani.
 
Hiyo hoja yake inafikirisha, huyo mwenyekiti Peter Mbuga anawezaje kupanga deal la kuhamisha wakazi wa mtaa mzima ili wampishe mwekezaji bila kupata baraka ya mkono wa serikali?
Kuunganisha na hiyo, iweje sasa Kigoto iwe miongoni mwa maeneo yaliyotajwa na jiji kuwa yamepata wawekezaji kutoka Brazil?
 
Hii nchi tunapopata rais hovyo, ndo tunawaona wajinga walioko serikalini. Tibaijuka naye alielekea kuwaliza watu wa Kigamboni. Bila PM Pinda kuingilia kati walishalizwa. Sasa hii ya Mwanza ni dalili zile zile za aina hiyo Eti hata Tulia anapata kiwanja Mwanza. Siajabu hata hajui ni eneo la aina gani hilo.

Huyo waziri naye ni pumbafu tu maana naelewa anafahamu yote na sasa anajidai kuigiza. Wasingeweza kujikusanya kwa wingi hivyo bila yeye kufahamu.
 
Back
Top Bottom