Wananchi Mwanza walalamika vigogo kupendelewa viwanja

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Baadhi ya wananchi walioomba kuuziwa viwanja eneo la Luchelele na Isamilo, jijini Mwanza, wamelalamika kukosa viwanja hivyo na kudai viongozi wa serikali na wabunge kuviwahi.

Halmashauri ya Jiji la Mwanza ilitangaza kuuza viwanja hivyo na kuwataka wanaovitaka kuchukua fomu kuanzia Juni 2 hadi 6, 2021.

Wakizungumza na gazeti hili, walidai waliomba viwanja hivyo baada ya kujaza fomu na kukamilisha malipo ya maombi ya Sh. 20,000, lakini orodha iliyotoka ina majina ya vigogo.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kuwekwa kwenye tovuti yao ina orodha ya watu 427 waliopata eneo la Luchelele na 39 Isamilo.

Majina ya vigogo yalijitokeza kwenye viwanja vya Isamilo ni ya Spika wa Bunge Tulia Akson, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Alphayo Kidata, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mery Masanja.

Wengine ni Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Seleman Yahaya na Meya wa Jiji hilo, Sima Costantine Sima na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Ngusa Samike.

Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, Michael Magufuli na Mkuu wa Mkoa mstaafu, Said Meck Sadik, ambao wengi wamepewa viwanja eneo la Isamilo ambalo lipo katikati ya Jiji la Mwanza.

Fedha za kuchukua fomu zilikusanywa na Jiji la Mwanza huku wananchi wa kawaida wakijitokeza kulipia ili waweze kupata viwanja vya makazi na biashara.

Kwa mujibu wa tangazo hilo la kuwapatia viwanja vigogo hao, walitakiwa kufika ofisi za jiji kuchukua ankara ya malipo ili wakavilipie.

Mmoja wa wananchi walioomba kununua viwanja hivyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alidai alilipia benki Sh. 20,000 kwa ajili ya kuomba kiwanja eneo la Luchelele.

Vilevile, tangazo lililotolewa kwa wananchi wakati wa kutangaza kuuza viwanga hivyo, Luchelele mita moja ya mraba ilikuwa ikiuzwa Sh. 5,000 kwa viwanja vya makazi. Eneo la Isamilo mita moja ya mraba ilikuwa ikiuzwa Sh. 25,000.

Katika maeneo hayo mawili pia alisema kulikuwa na viwanja kwa ajili ya makazi na biashara.

Tangazo la Jiji la Mwanza lilisema watu waliopatiwa viwanja hivyo walitakiwa kwenda kuchukua ankara za malipo kuanzia Juni 23 hadi Juni 30, 2021.

Aidha, tangazo hilo ambalo lipo kwenye tovuti hiyo, lilisisitiza kuwa mtu yeyote atakayeshindwa kuzingatia muda huo atanyang'anywa kiwanja na kumpatia mtu mwingine.

Alipoulizwa kuhusu vigogo hao kupatiwa viwanja, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Seleman Yahaya alisema amtumie ujumbe mfupi wa simu na kisha kukata simu.

Hata hivyo, ujumbe huo haukujibiwa.

Chanzo: NIPASHE
 
Walizingatia uwezo wa mtu kujenga nyumba ya maana hapo Isamilo ambapo ni kati kati ya jiji, ualimu manesi wanajeshi na watumishi wengine uwezo wao wakujenga nyumba za hadhi yao ni Luchelele
 
Ngokongosha laizerg Kitombile Mikdde Vege MoseKing Cha asubuhi
 
Mkuu hao wananchi wanaolilia viwanja maeneo ya isamilo wanataka kuweka nyumba za tembe? Wananchi wa kawaida wanamaeneo yao huko luchelele ndani, maeneo hot cake kama Isamilo waachie walamba asali waweke mahotel na mansion ya maana, wewe mtumishi mwalimu mwenzangu umepata pesa za mkopo unakimbilia kiwanja isamilo ili ukifanyie nini? Naipongeza halmashauri kwa kuangalia mbele🤣🤣🤣
 
Mkuu hao wananchi wanaolilia viwtanja maeneo ya isamilo wanataka kuweka nyumba za tembe? Wananchi wa kawaida wanamaeneo yao huko luchelele ndani, maeneo hot cake kama Isamilo waachie walamba asali waweke mahotel na mansion ya maana, wewe mtumishi mwalimu mwenzangu umepata pesa za mkopo unakimbilia kiwanja isamilo ili ukifanyie nini? Naipongeza halmashauri kwa kuangalia mbele🤣🤣🤣
Tetetete CCM ya kibaguzi imerudi haswa
 
Walizingatia uwezo wa mtu kujenga nyumba ya maana hapo Isamilo ambapo ni kati kati ya jiji, ualimu manesi wanajeshi na watumishi wengine uwezo wao wakujenga nyumba za hadhi yao ni Luchelele

Kama kulikuwa na masharti kuwa lazima ujenge nyumba ya aina hii sawa au thamani ya nyumba inayojengwa iwe kiasi hiki sawa kama 200m ok
 
Baadhi ya wananchi walioomba kuuziwa viwanja eneo la Luchelele na Isamilo, jijini Mwanza, wamelalamika kukosa viwanja hivyo na kudai viongozi wa serikali na wabunge kuviwahi.

Halmashauri ya Jiji la Mwanza ilitangaza kuuza viwanja hivyo na kuwataka wanaovitaka kuchukua fomu kuanzia Juni 2 hadi 6, 2021.

Wakizungumza na gazeti hili, walidai waliomba viwanja hivyo baada ya kujaza fomu na kukamilisha malipo ya maombi ya Sh. 20,000, lakini orodha iliyotoka ina majina ya vigogo.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kuwekwa kwenye tovuti yao ina orodha ya watu 427 waliopata eneo la Luchelele na 39 Isamilo.

Majina ya vigogo yalijitokeza kwenye viwanja vya Isamilo ni ya Spika wa Bunge Tulia Akson, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Alphayo Kidata, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mery Masanja.

Wengine ni Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Seleman Yahaya na Meya wa Jiji hilo, Sima Costantine Sima na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Ngusa Samike.

Wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Amon Mpanju na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, Michael Magufuli na Mkuu wa Mkoa mstaafu, Said Meck Sadik, ambao wengi wamepewa viwanja eneo la Isamilo ambalo lipo katikati ya Jiji la Mwanza.

Fedha za kuchukua fomu zilikusanywa na Jiji la Mwanza huku wananchi wa kawaida wakijitokeza kulipia ili waweze kupata viwanja vya makazi na biashara.

Kwa mujibu wa tangazo hilo la kuwapatia viwanja vigogo hao, walitakiwa kufika ofisi za jiji kuchukua ankara ya malipo ili wakavilipie.

Mmoja wa wananchi walioomba kununua viwanja hivyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alidai alilipia benki Sh. 20,000 kwa ajili ya kuomba kiwanja eneo la Luchelele.

Vilevile, tangazo lililotolewa kwa wananchi wakati wa kutangaza kuuza viwanga hivyo, Luchelele mita moja ya mraba ilikuwa ikiuzwa Sh. 5,000 kwa viwanja vya makazi. Eneo la Isamilo mita moja ya mraba ilikuwa ikiuzwa Sh. 25,000.

Katika maeneo hayo mawili pia alisema kulikuwa na viwanja kwa ajili ya makazi na biashara.

Tangazo la Jiji la Mwanza lilisema watu waliopatiwa viwanja hivyo walitakiwa kwenda kuchukua ankara za malipo kuanzia Juni 23 hadi Juni 30, 2021.

Aidha, tangazo hilo ambalo lipo kwenye tovuti hiyo, lilisisitiza kuwa mtu yeyote atakayeshindwa kuzingatia muda huo atanyang'anywa kiwanja na kumpatia mtu mwingine.

Alipoulizwa kuhusu vigogo hao kupatiwa viwanja, Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Seleman Yahaya alisema amtumie ujumbe mfupi wa simu na kisha kukata simu.

Hata hivyo, ujumbe huo haukujibiwa.

Chanzo: NIPASHE
Waziri angelina mabula from SKG original wakule mama hao mburula
 
Duh nimekumbuka bia za pale The Joint-Isamilo.Mwezi wa 9 nitakua na tour hapo ya kula byereeee.
Karibu sana mkuu, japo kuna wananchi wanataka viwanja hapo isamilo kuweka vibanda umiza, nasi tuna mshukuru mkurugenzi wa jiji kuwapuuzia wananchi wanaotaka kuharibu mandhari ya jiji la Mwanza kwa kuuza viwanja kwa walamba asali tu🙏🙏🙏🙏
 
Kama na wewe ulitaka kununua imekula kwako, mwanachi wakawaida tuna maeneo yetu kama bulale, luchelele, igombe n.k kwanini ugombane na walamba asali wakati kuna ardhi kubwa nenda ata huko magu
😄😄 Luchelele Kule karibu na jembe ni jembe mtu ukipata kiwanja karibu na ziwani pako poa kishenzi,tatizo Ni barabara tu sijui Kama zineshatengenezwa.
 
Back
Top Bottom