ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 43,109
- 49,811
Wananchi wa maeneo ya Sae na Ituha Jijini Mbeya wamekuwa na mgogoro mkubwa na Wizara ya Kilimo Kupitia Chuo Cha Utafiti TARI Uyole kwamba wamevamia eneo la Chuo na kujenga makazi.
Wizara ya Kilimo inadai Wananchi wamevamie eneo la Ukubwa ekari 60 ambazo wao walitenga Kwa Ajili ya kuweka miundombinu na mashamba ya Utafiti Kupitia TARI Uyole.
Kwamba Sasa Serikali inataka iwahamishe kwenye eneo Hilo lakini Wananchi wamekataa Kwa sababu mbalimbali ikiwemo kwamba Hilo eneo waliopewa vibali vya ujenzi na fidia ndogo ambayo Serikali inataka kuwapa japo ni mabilioni ya pesa.
Nini hoja yangu.
-Serikali walikuwa wapi Hadi watu zaidi ya 1000 wanafanya uendelezaji wa eneo Hilo na wao wako kimya?
-Kwa nini Serikali ing'ang'anie eneo la mjini tena Kwa kuwalipa fidia watu ambao wameendeleza maeneo hayo Kwa sehemu kubwa kiasi hiki? Hapo Sae Kuna majengo mengi ya Gharama kubwa.
-Kwa nini Serikali ilipe fidia ya mabilioni pesa za Walipakodi wakati wanaweza kwenda kununua eneo jingine Nje ya Jiji au Wilayani Kwa bei nafuu na wakaendeleza utafiti wao?
Binafsi naona hii sio jambo zuri na halikubaliki.Kwanza sikubalini na kujenga vyuo vya masuala ya Kilimo na mifugo mjini.
Mjini hakutakiwi kuwe na mashamba Bali biashara,bustani, taasisi,makazi nk.Kwa Mbeya eneo Katibu lote la Uyole ni mashamba ya Chuo Cha Kilimo Uyole.On top of that Kuna mashamba mengine makubwa ya JKT hapo hapo Uyole.
Pia kule Itende Kuna mashamba ya JKT wanalima Hadi Kahawa.Sasa Kwa Jiji kama Mbeya lenye uhaba wa Ardhi Jijini inakuaje Serikali inalazimisha kuwa na mashamba ya taasisi mjini? Tena Yako kwenye sura ya Jiji kabisa sehemu ambazo zingefaa kufanya uendelezaji wa Jiji.
Niiombe Serikali ihamishe taasisi zake kama Chuo Cha Uyole na Kambi za JKT Ili maeneo hayo yachukuliwe na Jiji Ili kufanya uendelezaji wa Jiji.
Tanzania haina upungufu wa maeneo,toeni taasisi zenu hizo ziende maeneo ya mashambani huko Wilayani Ili wakalime na kufanya shughuli zao Kwa uhuru huko badala ya Kugeuza Jiji kuwa mashamba ya maharage,Ngano,mahindi na kahawa Kwa visingizio visivyo na Tija.
Wananchi msikubali kuondoka hapo, Serikali ndio iondoe Vyuo vyao katikati ya Jiji Ili kutoa fursa ya Jiji kukua na kupangwa vizuri liwe la Kisasa kama Majiji mengine badala ya kuwa Mashamba.
Tunaomba Watu wa Tume ya Mipango na Wizara ya Ardhi mumshauri Rais afute Mashamba mjini Ili hizo taasisi zipewe maeneo mengine mawilayani huko ambako Kuna maeneo ya kutosha ya mashamba.
Wananchi wa Mbeya wanataka Jiji lao Lijengwe na kupangwa Upya na eneo la Uyole ndio eneo liko Kwenye uso wa Jiji hivyo likipimwa kama Viwanja na kuendelezwa litabadili sura ya Jiji la Mbeya.
View: https://youtu.be/alHTGZXe3bU?si=2xQbqhglFLO_Ryi4