Wananchi wa Goba wakarabati barabara wenyewe, Serikali za Mtaa washawishi bango litolewe

Kuna don mmoja alitaka kujenga kiwango cha lami barabara ya mtaani kwake, ili ndinga zake zisiguse tope kuanzia anatoka kwake mpaka anafika ofisini kwake, ila mamlaka ya pale ikamletea mtima nyongo. Inataka fedha ipitie kwao kisha wao ndio wajenge. šŸ˜‚
 
Goba tunaishi watu wa kaskazini wengi na wengi humu wapo vizuri financially utapalinganisha vp na huko uswahilini?
 
Hii ni picha ya bango la mradi wa ujenzi na ukarabati wa kilomita mbili (2) Goba kwa Awadhi ambayo imesambaa kwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mradi huu ni wa ukarabati na ujenzi wa mitaro ambapo unatokana na nguvu za wakazi wa eneo hilo.

Inaelezwa wakazi hao wamekubaliana kujenga mitaro kwa kutumia zege na makadirio ya bajeti ni Shilingi milioni 40 kutoka kwa wakazi 95 ambao wameahidi kuchangia. Hadi sasa, zaidi ya Shilingi milioni 16 zimekusanywa, na ujenzi umeshaanza.

Sema tofauti na mabango mengine ambayo mara nyingi yamekuwa na ujumbe uliozoeleka kwamba UKIMWI unaua, bango hili limehitimishwa na ujumbe wa ā€œTuchange wote kujenga barabara yetuā€.

Pia inasemekana kuwa mjadala huo umewaibua viongozi wa mtaa ambao waliwashawishi wananchi kuliondoa bango hili bila mafaniko. Wananchi wanasema kuwa endapo watalitoa, basi viongozi waitishe mkutano kuelezea barabara hiyo itatengenezwa lini.

Uamuzi wa wananchi wa Goba wa kujikomboa kwa kujenga barabara yao wenyewe ni ishara ya ujasiri na kujitolea katika kuleta mabadiliko katika jamii yao. Hii ni hatua ya kipekee ambayo inaonyesha nguvu ya umoja na dhamira ya kuboresha maeneo yetu.

Je, mtaani kwenu mnachukua hatua gani kama barabara inazingua?
Spirit ya Moshi hiyo. Sasa hiv kuna mahali tunajenga daraja kubwa sana wenyewe.
 
Ni upumbavu kuchanga pesa wakati Serikali imekopa pesa kwa ajili hiyo hiyo.

Ujanja ni kusimama kidete na kuhoji pesa zilizotolewa na WB Kwa ajili ya kujenga miundombinu ya nini la Dar?
ccmu ishaferi ,ukisubir utaoga kwenye madimbwi
 
Kiongozi wa kukusanya michango tutafuatilia taarifa zake TRA šŸ˜”šŸ˜”, 2025 tutakuja na hoja gani sasa šŸ˜”šŸ˜”šŸ˜”šŸš®šŸš®
 
Ili Barabara ikae miaka na miaka ikisubiri uchambuzi yakanifu.
Hao wakimaliza hiyo Barabara ni mwanzo wa State yao.Hakuna kima atapita huko kuongea ujinga.
Na kama wameanza na hilo juu watafanya makubwa kwa huo mtaa.

Sio dalili njema hizo.
Wakimaliza barabara watazungushia ukuta mtaa wao mara wamejijengea hospitali etc
 
Hii ni picha ya bango la mradi wa ujenzi na ukarabati wa kilomita mbili (2) Goba kwa Awadhi ambayo imesambaa kwa kwenye mitandao ya kijamii.

Mradi huu ni wa ukarabati na ujenzi wa mitaro ambapo unatokana na nguvu za wakazi wa eneo hilo.

Inaelezwa wakazi hao wamekubaliana kujenga mitaro kwa kutumia zege na makadirio ya bajeti ni Shilingi milioni 40 kutoka kwa wakazi 95 ambao wameahidi kuchangia. Hadi sasa, zaidi ya Shilingi milioni 16 zimekusanywa, na ujenzi umeshaanza.

Sema tofauti na mabango mengine ambayo mara nyingi yamekuwa na ujumbe uliozoeleka kwamba UKIMWI unaua, bango hili limehitimishwa na ujumbe wa ā€œTuchange wote kujenga barabara yetuā€.

Pia inasemekana kuwa mjadala huo umewaibua viongozi wa mtaa ambao waliwashawishi wananchi kuliondoa bango hili bila mafaniko. Wananchi wanasema kuwa endapo watalitoa, basi viongozi waitishe mkutano kuelezea barabara hiyo itatengenezwa lini.

Uamuzi wa wananchi wa Goba wa kujikomboa kwa kujenga barabara yao wenyewe ni ishara ya ujasiri na kujitolea katika kuleta mabadiliko katika jamii yao. Hii ni hatua ya kipekee ambayo inaonyesha nguvu ya umoja na dhamira ya kuboresha maeneo yetu.

Je, mtaani kwenu mnachukua hatua gani kama barabara inazingua?
Sisi tumekuwa tukichangia na kujenga barabara za kijijini kwetu kwa mamilioni mengi japo huwa hatuweki bango. Hawa wenzetu wa Goba wametufungua sababu nahisi tunapojenga wengine wanachukua credit
 
Hizi Barabara za mtaani ni changamoto mno. Hongereni watu wa goba kwa kujenga Barabara yenu.

Inatakiwa iwe mbinu ya nchi nzima. Wenye magrader na roller na wenye utaalam wa kujenga Barabara za mtaani hata za changarawe, mchangamkie fursa hiyo.

Wazo la bango ni zuri. Wangeweka na account ya kuchangia au hata lipa namba ya ujenzi kabisa, kwenye bango.
 
Back
Top Bottom