DOKEZO Ubovu wa barabara za mtaa Luis kata ya Mbezi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

billben

New Member
Nov 29, 2023
1
2
Wadau kulingana na taswira ya jiji la Dar es Salaam kwa sasa, eneo la Mbezi Luis, ni eneo ambalo limekaa kimkakati katika kukuza uchumi wa Dar es Salaam na nchi kwa ujumla, cha kushangaza miundombinu yake ni mibovu sijapata kuona.

Kuna mtaa unaitwa Luis, leo ni karibu mwezi mzima, wananchi wanaacha magari barabarani, barabara haziingiliki, kuna barabara ambayo inaunganisha mtaa wa Luis kata ya Mbezi na Tegeta A kata ya Goba.

Ni barabara ya kimkakati lakini Serikali imeifumbia macho kabisa, kuna madaraja ya kujengwa hasa eneo linaloitwa kwa mama Ndeshi ndio kichomi kabisa.

Tunaomba mtusaidie kupaza sauti, ili barabara hii waifanyie kazi, hasa kuweka daraja la kwa mama ndeshi.
 
Ukiwa na Akili timamu ukaangalia mambo yanayoendelea kwenye hii nchi UTAUMIA MNO!.

Watu wote wanaoifurahia hii nchi ni watu WASIYOKUWA NA AKILI TIMAMU!
 
Tunaomba mtusaidie kupaza sauti, ili barabara hii waifanyie kazi, hasa kuweka daraja la kwa mama ndeshi.

Kwa sasa tunajenga chama...

Kuhusu madaraja subiri ahadi ya diwani wakati wa uchaguzi mwakani...

Asante...
 
Back
Top Bottom