Wananchi hatuitaki CHADEMA

Hiki Chama cha Mapinduzi kimeshindwa kufanya mapinduzi yoyote ya kimaendeleo kwa miaka zaidi ya 50 kikiwa kimeshika nchi,kilichofanya na kinachoendelea kufanya ni kuendelea kuziba viraka vya kiuchumi,kijamii na kiutawala bila kuwa na njia zozote za kuleta mapinduzi ya kweli.
Hayati Mwl. Nyerere na Karume na mashujaa wengine walipokuwa wanapigania uhuru wa Tanzania ya sasa hawakuweka vyama mbele halafu wakakaa nyuma yake wakitegemea uhuru uletwe na kikundi kidogo cha watu wanaofanya vikao na mikutano ya mara kwa mara.(Tukumbuke Nyerere hakupenda kubweteka kama wanasiasa wa leo bali aliendelea kupenda aitwe Mwalimu akifanya kazi kuleta uhuru na maendeleo kwa kadri ya hali za kipindi hiko na uwezo wake.Sio hawa maafande wanaopenda kuitwa Dr bila kuusomea wala kuwa na taaluma).
Mapinduzi ya kweli hayataletwa na vyama vya siasa pekee bali mtanzania wa kawaida anapaswa kuchukua hatua na kubadilisha mfumo huu mzee mambo ili kuyaleta mapinduzi ya kweli.

Hapa ndipo tuliposhindwa kuwaelewa CCM kwani wakati Nyerere anaongelea mapinduzi ya kiuchumi na maendeleo wenzake walimaanisha mapinduzi ya kimfumo kutoka kwenye ujamaa kwenda kwenye ubepari!. Kumbuka Nyerere alipotoka tu madaraka wakafanya 'mapinduzi' ya azimio la Arusha kuwa azimio la Zanzibar, baadaye wakafanya 'mapinduzi' ya viwanda kwa kubinafsisha na sasa hivi wapo busy na mapinduzi ya uongozi kutoka ule wa wananchi kumchagua wampendae kwenda kwenye uongozi wa kurithishana. Hayo ndiyo mapinduzi ya 'chama cha mapinduzi'
 
Kwanza ningetaka kujua ww ni nani ila kwa ufupi ningesema ww ni Mipasho ya MAGAMBA.Nikuulize kuwa ww nani alikwambia kuwa Watz hawaitaki CDM.Na ni nani kasema CDM ni ya Wachaga.Acha kuwa na fikra potofu.Watz tushajanjaruka na hatutaki Propaganda.Kati ya CDM na CCM ni nani chama cha Familia.Obvious ni CCM.Kwa ufupi angalia Arumeru, Eti mpeni SIOI ubunge ana majukumu ya kifamilia.Kwa ni mtanzania yupi asiekuwa na majukumu ya kifamilia.Ningekushauri uwe na fikra endelevu, kwanza noi bora ukafanya Research. WITHOUT RESEARCH,NO RIGHT TO SPEAK. CCM ndio chama cha familia,na kurithishana au ww Huoni.ACHA KUWA NA MAWAZO MGANDO YA KCCM.
Mkuu soma vizuri post ya Sangarara, bila shaka hujamuelewa vizuri mwandishi amelenga nini!!!!! Tuliza akili kwanza tafakali upate jibu!!!!

 
Hivi hakuna mtu wa kumuwekea mtoa mada picha za mikutano ya kampeni za CDM? Halafu mimi namchalenji mtoa mada atoe hata picha moja ya Fuso lililojaa wamaCDM wakielekea kwenye mikutano yao.
 
Kwanza ningetaka kujua ww ni nani ila kwa ufupi ningesema ww ni Mipasho ya MAGAMBA.Nikuulize kuwa ww nani alikwambia kuwa Watz hawaitaki CDM.Na ni nani kasema CDM ni ya Wachaga.Acha kuwa na fikra potofu.Watz tushajanjaruka na hatutaki Propaganda.Kati ya CDM na CCM ni nani chama cha Familia.Obvious ni CCM.Kwa ufupi angalia Arumeru, Eti mpeni SIOI ubunge ana majukumu ya kifamilia.Kwa ni mtanzania yupi asiekuwa na majukumu ya kifamilia.Ningekushauri uwe na fikra endelevu, kwanza noi bora ukafanya Research. WITHOUT RESEARCH,NO RIGHT TO SPEAK. CCM ndio chama cha familia,na kurithishana au ww Huoni.ACHA KUWA NA MAWAZO MGANDO YA KCCM.
Mkuu mbona naona kama unamuunga mkono Sangarara ki aina. Maoni yako ni ya kwake. Au hujamwelewa?
 
Kifo ni lazima kitokee kwa kiumbe chochote kilicho na uhai, vivyo CCM ni lazima ife kutokana na umri wake.

Haijalishi utapata matibabu bora kiasi gani umri ukikutupa mkono lazima ufe, haijalishi serikali iliyoko madarakani inatumia hila na mbinu chafu kiasi gani kuisaidia CCM ishinde uchguzia ni lazima kife.

Kila ukiangalia mambo yanavyokwenda katika chama hiki kizee unaona dalili zote za kifo zinakiandama, na si muda mrefu tutashuhudi mazishi ya CCM.
 
Hapa ndipo tuliposhindwa kuwaelewa CCM kwani wakati Nyerere anaongelea mapinduzi ya kiuchumi na maendeleo wenzake walimaanisha mapinduzi ya kimfumo kutoka kwenye ujamaa kwenda kwenye ubepari!. Kumbuka Nyerere alipotoka tu madaraka wakafanya 'mapinduzi' ya azimio la Arusha kuwa azimio la Zanzibar, baadaye wakafanya 'mapinduzi' ya viwanda kwa kubinafsisha na sasa hivi wapo busy na mapinduzi ya uongozi kutoka ule wa wananchi kumchagua wampendae kwenda kwenye uongozi wa kurithishana. Hayo ndiyo mapinduzi ya 'chama cha mapinduzi'

Wameuvamia ubepari bila kujiandaa na sasa unatupalia na hilo liko wazi kwa kesi nyingi za kifisadi na kumilikishana mali bila kufuata taratibu husika(lugha ya kisiasa ni 'Ubinafsishaji').
Sitaki kusema mengi lakini ni wazi misingi aliyoweka Mwalimu imesalitiwa na hiki Chama cha Magamba na kama kweli walimuua ili waharakishe na kuhalalisha uhayawani wao basi laana ya mwanaume yule aliyehangaika kwa jasho na vitendea kazi hafifu kufanikisha uhalali wa nchi hii kujitawala yenyewe itawarudia CCM vibaya sana.
Mwalimu hakupendelea mtoto wake wala ndugu yake yeyote aje kutawala taifa hili(alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo) bali alitaka mtanzania yeyote apewe haki ya kuongoza taifa hili kuelekea maendeleo ya kweli.Lakini angalia jinsi ikulu na taasisi nyingine zinavyotumiwa kama namna ya kuvuna utajiri.
 
CCM wataendelea kujifariji na hekaya za kuwahadaa wanachama wake ambao rais anapenda kuwahutubia pale Dar. Ila kwa wale ambao bado wanajua wana miaka kuanzia 15 mbele siyo rahisi kukaa na kukubali kusimuliwa hekaya. Vijana wamecharuka wanataka kuona the other side of the coin na siyo CCM, CCM,CCM mpaka ladha inaisha
 
Kuna upotoshaji mkubwa sana unafanyika hivi sasa ambao unafanyika katika namna ya hatari sana, naiweza kuifafanisha namna hiyo sawa sawa na mtu anaesema moto ni joto au upofu ni usingizi. Wanasiasa waliomadarakani wanajaribu kuyawekea mahitaji ya wananchi dhana ya kisiasa.

Wakati wananchi wanasema tunataka Mfumo bora wa elimu watawala wanasema CHADEMA haiwezi kuuleta, sababu DR SLAA Aliiba pesa kanisani.

Wananchi wanasema tunataka mfumuko wa bei udhibitiwe, watawala wanasema CHADEMA haiwezi kudhiti mfumuko wa bei sababu MBOWE ni DJ

Wananchi wanasema tunataka huduma bora za afya, watawala wanasema, DR Slaa anampenda sana Josephine.

Wananchi walia wanakufa njaa, watawala wanasema, CHADEMA ni chama cha Kichaga.

Wananchi wanapiga kelele wanalalamika mariasiri za Taifa letu zinanufaisha wachache na nyingi zinaibiwa na wageni, watawala wetu wanasema Ushindi ni Lazima.

Naomba tukumbushane historia mbichi kabisa, waliomfurumusha Hussein Mubarak kutoka Madarakani sio wanasiasa, Kijana aliyejichoma moto tunisia na kuacha laana nyuma yake hakuwa analalamikia wizi wa kura, waliomkamata Gadafi kwenye mtaro wa daraja walikuwa hawajebaba bendera ya chama chochote kile cha siasa, Hata sasa huko Siria wananchi hawapiganii kuundwa katika mpya wala kuwa na tume huru ya Uchaguzi.

Wito wangu kwa viongozi wa CCM ni huu ufuatao.
Kwanza, kuna ushahidi wa kutosha kwamba hivi sasa duniani, mabadiriko yanatokea kwa kasi ambayo haijawahi kutokea huko nyuma katika kila nyanja ya maisha.

Pili na mwisho, Muda si mrefu watanzania watagundua kwamba wanachokihitaji sio katiba mpya na wala sio tume huru ya uchaguzi wala sio maridhiano ya kitaifa ya namna yoyote ile wala sio ushindi wa wagombea wao.

Narudia tena, Punde kidogo, upepo wa mabadiriko utabidiri mkondo wake, watu watakapoamua kuweka magwanda na kuachana na ustaarabu wa kuonyeshana alama ya V sijui mtawaambia nini.

sema kuwa wewe na mme wako ndo hautaki.p.u.m.b.a.v sana
 
Kweli mkuu uliyoyasema, ila umma wowote ili uweze kufikia huko unakokusema ni lazima upitie msukumo mkubwa sana wa kisiasa (elimu ya uraia)....
Ukifuatilia vizuri mapinduzi ya hzo nchi ulizotaja hamna ambayo eti hakuna harufu ya vyama vya siasa.

Hivyo mi napenda niongezee nyama kwenye hoja yako kuwa Watanzania wanavitaka sana vyama vya siasa vyenye kuwafunza zaidi kuhusu nguvu wanazomiliki (nguvu ya umma) na utajiri wao!
Kwa njia hii pekee ndio umma utaamka mapema zaidi kabla ya madhara na uharibifu zaidi.
 
Back
Top Bottom