CHADEMA hongereni sana wananchi wanaanza kuwaelewa msikate tamaa kuwazindua wananchi wanahitaji mtu wa kuwasemea

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,819
18,555
Juhudi za CHADEMA kuwasemea watanzania na kuwasaidia kujielewa na kuelewa hali zao zinaonekana kuzaa matunda. Ukweli ni kwamba watanzania wengi wanahitaji mtu anayeelewa mambo awafafanulie na kuwapa mwanga kwani kwa kawaida watawala hutumia mwanya wa watu kutoelewa mambo na kuwakandamiza wananchi.

Nimeona taratibu watu wanaanza kuwaelewa CHADEMA kuhusu umuhimu wa katiba mpya, demokrasia nzuri na uhuru wa kujieleza. Tangu CHADEMA waanze kuongoza maandamano ya wananchi nimeona wananchi wameanza kupata mwamko na kujiongeza katika uelewa wao wa mambo muhimu yanayowahusu. Mtaani kuna vuguvugu la kutaka mabadiliko na watu kwa kweli wameichoka CCM, inasubiriwa tu namna ya kuimalizia CCM ikate pumzi moja kwa moja.

Ushauri wangu kwa CHADEMA ni huu:

CHADEMA endeleeni kuwa sauti ya wanyonge. Msikatishwe tamaa na mtu, hata pale mnapoona upinzani wa serikali na wananchi kutowaelewa, msikate tamaa, endeleeni tu sio kwamba ni bure, hapana watu wanawaelewa zaidi kila siku.

Waelezeni wananchi ukweli kuwa hali ngumu ya maisha inatokana na uongozi mbovu chini ya CCM.

Zungumzieni sera mbadala. Zungumzieni matatizo ya umeme, sukari, gharama kubwa za matibabu na ugumu wa maisha unaotokana na uongozi mbovu wa CCM.

Watanzania tunawaelewa, kazeni buti tunawategemea kwa uhai wa taifa letu.

Hongera sana Mbowe, Mnyika na makamanda wengine wote!
 
Naunga MKONO hoja,na pia naongeza haya matatu;
1.Baada ya kumaliza Arusha ,warudi tena Dar,..kwa wana Dar EsSalaam ,JOTO limeanza kupanda zaidi,MILIO imeanza kusikika

2.Hizi changamoto nazo waziaddress,usafiri mbovu wa DART,Kivuko Ferry + train za Gongo la mboto

3.Waendelee kuwekeza zaidi kwenye MEDIA..amsha amsha iendelee..Uzuri now ,MEDIA nyingi zimeanza kuwapa coverage

N.B
MMM kule Tweeter apunguze MATUSI,ila spana ziendelee kama kawa
 
Kimsingi vuguvugu la kutaka mabadiliko chanya limeongezeka..
Hadi waombe poo,maana KENGE huwa haelewi hadi atoke DAMU..CHADEMA ongezeni NGUVU,soon kunakucha

Leo asubuhi, sikuamini masikio na macho yangu baada ya kuona watangazaji wa kipindi cha Baragumu Channel 10,inayomilikiwa na CCM wakiongozwa na Dorcas Mtenga wakipiga SPANA kuhusu JANGA la UMEME..
 
Juhudi za CHADEMA kuwasemea watanzania na kuwasaidia kujielewa na kuelewa hali zao zinaonekana kuzaa matunda. Ukweli ni kwamba watanzania wengi wanahitaji mtu anayeelewa mambo awafafanulie na kuwapa mwanga kwani kwa kawaida watawala hutumia mwanya wa watu kutoelewa mambo na kuwakandamiza wananchi.

Nimeona taratibu watu wanaanza kuwaelewa CHADEMA kuhusu umuhimu wa katiba mpya, demokrasia nzuri na uhuru wa kujieleza. Tangu CHADEMA waanze kuongoza maandamano ya wananchi nimeona wananchi wameanza kupata mwamko na kujiongeza katika uelewa wao wa mambo muhimu yanayowahusu. Mtaani kuna vuguvugu la kutaka mabadiliko na watu kwa kweli wameichoka CCM, inasubiriwa tu namna ya kuimalizia CCM ikate pumzi moja kwa moja.

Ushauri wangu kwa CHADEMA ni huu:

CHADEMA endeleeni kuwa sauti ya wanyonge. Msikatishwe tamaa na mtu, hata pale mnapoona upinzani wa serikali na wananchi kutowaelewa, msikate tamaa, endeleeni tu sio kwamba ni bure, hapana watu wanawaelewa zaidi kila siku.

Waelezeni wananchi ukweli kuwa hali ngumu ya maisha inatokana na uongozi mbovu chini ya CCM.

Zungumzieni sera mbadala. Zungumzieni matatizo ya umeme, sukari, gharama kubwa za matibabu na ugumu wa maisha unaotokana na uongozi mbovu wa CCM.

Watanzania tunawaelewa, kazeni buti tunawategemea kwa uhai wa taifa letu.

Hongera sana Mbowe, Mnyika na makamanda wengine wote!
Kuna Mtu alifanya branda 2020 bila kujua anajikaanga Kwa mafuta yake. Kitendo cha CCM kuwa Peke yao Kila mahali huku màmbo yakizidi kuwa ovyo na maisha ya Wananchi yakiwà magumu zaidi kumesaidia Wananchi kujua umuhimu wa kuwa na upinzani imara.
 
Screenshot_2024-02-20-14-02-29-1.png
 
Back
Top Bottom