Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,559
- 41,075
Taifa au jamii yoyote ili kuyapata maendeleo ya kweli lazima kuwepo na viongozi. Nchi au jamii ikikosa viongozi, haiwezi kuwa na maendeleo ya kweli wala amani ya kweli.
Ili uwe na jamii yenye viongozi na wanaoongozwa ni lazima uwepo mfumo uliotengenezwa, unaoheshimika na uliokubalika na wale wanaoongozwa, ambao kimsingi ndio walio wengi. Hili Tanzania tumelikosa.
Uhalali wa mtu kuwa kiongozi, kwanza kabisa ni kuchaguliwa kiuhalali na kwa uwazi kwa mfumo uliotengenezwa na kukubalika na wale wanaoongozwa, na siyo vinginevyo.
Tanzania imekosa viongozi, ila ina watawala. Watawala wamewawekea utaratibu wananchi jinsi wao watawala watakavyokuwa wakipatikana na jinsi watakavyowatawala. Na kila wazo jema linalotaka nchi iwe na viongozi, watu wanaopatikana kwa utaratibu wa haki na wa wazi, watawala hawataki.
Watawala kukataa matakwa ya wanaotawaliwa jinsi wanavyotaka viongozi wapatikane kwa njia ya wazi na ya haki, ni uthibitisho tosha kuwa watawala wanataka wabakie kuwa watawala na siyo viongozi wa wananchi.
Ndiyo maana wameweka utaratibu wao ambao wananchi wapende wasipende, lazima waitii.
1) Watendaji wakuu wa Tume ya uchaguzi watateuliwa na watawala.
2) Kura zitahesabiwa na Tume ya Uchaguzi ya watawala.
3) Tume ya watawala ndiyo itamtangaza waliyeamua awe mshindi.
4) Tume ya watawala itahesabia kura gizani, na wananchi hawatakiwi kushuhudia wala kuthibitisha uhesabuji wa kura kama ni halisia au bandia.
Halafu wajinga wachache, naamini ni wale machawa, wanataka kuwadanganya watu kuwa Samia ni mpenda demokrasia na haki.
NB: Laana ya Tanzania imebebwa na CCM, chama ambacho hakijawahi kufikiria hata siku moja kuwapa Watanzania haki yao ya msingi ya kuwachagua viongozi wanaowataka. Wakati wote wamebakia kufikiria na kubuni mbinu za kuendelea kuwatawala Watanzania kwa mbinu zote, chafu na njema, alimradi wanaendelea kutawala, japo ni dhahiri hakuna mwanga wowote kupitia wao.
Naomba mod, rekebisha heading. Isomeke Tanzania badala ya Tamzania.