Wanajamii hii imekaaje kimaadili?

PetCash

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
1,997
1,999
Nnaishi kwenye nyumba mojawapo kati ya nyumba mbili zilizoko ndani ya geti moja. Kwa hiyo tuko karibu sana na Jirani ya ngu kama vile marafiki wazuri.
Jirani yangu ana mtoto mmoja wa kiume na pia wanaishi na mtoto mmoja wa kike(umri sawa na huyo wa kiume kwenye miaka 19 hivi) ambaye ni mtoto wa dada yake mkewe.
Siku moja asubuhi nimelala(dirisha moja la chumba changu liko upande wa mbele ya nyumba yao) nikasikia hao watoto wakidiscuss jambo lililonishtua sana;
Dogo wa kiume alipita vibaya kwenye kamba adondosha ch*pi ya huyo dada yake aliyoianika mda mfupi baada ya kutoka bafuni.
Dada mtu akasema, umedondosha ch*pi yangu iokote na uifue. Basi wakaanza kubishana kiutaniutani oh ww unavaa boxer, ww unavaa nn..kwa mda mrefu kweli.
Sasa mi niko rum naboreka kwa maneno nnayoyasikia na hisia kwamba wanakoelekea c kwema. Sasa nataka niwaite na kuwashauri naomba mchango wenu tafadhali.
Je wanavyofanya hakuna matatizo ya kimaadili au mi ndo na 'complicate'?
 
wanakoelekea si pazuri kivipi?
Nlichomaanisha hapo ni hiki, kama waliweza kuzungumza hayo na bado maongezi yalikuwa yanaendelea- nlikuwa tu na wacwac masikio yangu yasijesikia visivyo vyema kusikiwa...thats all!
 
mhhh naona kama kawaida vile,sidhani kama walikuwa na nia mbaya,unaweza kuwashauri ndio wakaanza kupata mawazo mengine
 
wewe tatizo unaloliona hapo ni nini? Bila shaka wewe ni complicator tu, pilipili usizozila zinakuwashia nini? Hayo ni mambo ya majirani na maisha yao, wewe unayatakia nini? Kama kila linalotokea kwa majirani utakuwa concerned si watakuchoka hapo mtaani?
 
Hakikisha kuwa wanauhusia wa aina gani, saa nyingi they aren't serious about what they say. Halafu kama utaongea nao bila kuwahusisha wazee wao yawezakuwa nomerrr baadaye
 
Kwani we umewaza nini ulivowasikia neno chupi lilivyotajwa?
 
wewe tatizo unaloliona hapo ni nini? Bila shaka wewe ni complicator tu, pilipili usizozila zinakuwashia nini? Hayo ni mambo ya majirani na maisha yao, wewe unayatakia nini? Kama kila linalotokea kwa majirani utakuwa concerned si watakuchoka hapo mtaani?

Hili nalo neno, precisely when it is coming from a person who can think like this;
Hakuna nchi rahisi kuongoza kama Tanzania. Hata mtoto wa darasa la tatu anaweza kuiongoza, ilimradi awe na jeshi tu.
 
Kwani we umewaza nini ulivowasikia neno chupi lilivyotajwa?
Hakuna nilichowaza mi kwa nilivyolelewa naona it is improper kwa kaka na dada kudiscuss habari za ch*pi sasa sijui kwa wengine wanaonaje ndo maana nauliza kabla sijawashauri nsijeonekana nawacomplicatia maisha yao
 
Ni maneno tuu may be hayana mwelekeo wowote au yana mwelekeo baadae na unaweza kuwashtua wakaishia kufanya kile ambacho walikuwa hawategemei
 
Nnaishi kwenye nyumba mojawapo kati ya nyumba mbili zilizoko ndani ya geti moja. Kwa hiyo tuko karibu sana na Jirani ya ngu kama vile marafiki wazuri.
Jirani yangu ana mtoto mmoja wa kiume na pia wanaishi na mtoto mmoja wa kike(umri sawa na huyo wa kiume kwenye miaka 19 hivi) ambaye ni mtoto wa dada yake mkewe.
Siku moja asubuhi nimelala(dirisha moja la chumba changu liko upande wa mbele ya nyumba yao) nikasikia hao watoto wakidiscuss jambo lililonishtua sana;
Dogo wa kiume alipita vibaya kwenye kamba adondosha ch*pi ya huyo dada yake aliyoianika mda mfupi baada ya kutoka bafuni.
Dada mtu akasema, umedondosha ch*pi yangu iokote na uifue. Basi wakaanza kubishana kiutaniutani oh ww unavaa boxer, ww unavaa nn..kwa mda mrefu kweli.
Sasa mi niko rum naboreka kwa maneno nnayoyasikia na hisia kwamba wanakoelekea c kwema. Sasa nataka niwaite na kuwashauri naomba mchango wenu tafadhali.
Je wanavyofanya hakuna matatizo ya kimaadili au mi ndo na 'complicate'?

Una moyo mzuri, ila kumbuka age yao ni zaidi ya 19, maana yake ni watu wazima wanaoshindwa kuliandiana heshima baina yao, yumkini wao wanajambo usilolijiua! Watu husema samaki mkunje angali mbichi na siyo akishakuwa mkavu .... Jiulize utaanza vipi? Watakutusi, kaaa chonjo na endeleza moyo huo kwa watu chini ya 15.

Wenu,
HorsePower
 
Back
Top Bottom