Wana JF Hawa Wako Wapi?...

Saidi Yakubu yupo Tanzania,aliacha kazi huko BBC - UK. Anafanyakazi ya Mkataba kwenye kitendo cha sheria kwenye Kamati ya Bunge la Commonwealth,wanaangalia Ufanyajikazi wa Mabunge ya Tanzania,kenya, Uganda na Bunge la Shirikisho la EA.Kwa Taaluma Yakubu ni mwanasheria/Mwandishi,nafahamu kuwa anaingia humu lakini kwa ajili ya conflict of interests anaweza kuwa ni mchunguliaji tu!!

Kumbe alishaondoka kwenye idara ya habari ya Bunge la Tanzania? Sikuwa na habari maana wakati wa kikao cha bajeti nilikutana naye pale Bungeni
 
Kada mpinzani alikuwa mpinzani sana wa mwafrika wa kike sijui sikuhizi yuko wapi lagatege shishi atarudi usijali wacha apate likizo fupi mwezi wa 12 labda
 
Kama wapo majuu huenda maboksi yamekuwa mengi na yamewazidi sana.
Nakumbuka tulishamuuliza Invisible kuhusu Kada (kwa kudhani kafungiwa jumla), akasema hajafungiwa. Huenda naye kilimo kimembana (kwa kuhisi ni mkulima)!
Mwenye taarifa zaidi tunahitaji tafadhali!

Hata Mama Lao siku nyingi sijamuona hapa.
 
Nina muda mrefu sana sijamuona Mwan JF mmoja aliyejulikana kwa Jina la Dua na Signature yake "Dua la Kuku halimpati mwewe". Huyu ndugu nadhani alikuwa/yuko UK na alikuwa mchangiaji mzuri sana kwenye midahalo ya hapa JF. Yuko wapi Dua?
 
Huwa wana kauli moja wakiwa likizo mitandao mibovu hawapatikani.Sijui sisi tuko wapi.Miezi hii wanaoana sana alianza bwana max akaja Mwafrika wa kike may be atakuwa honeymoon.
 
Kuna jamaa mwingine anaitwa RICHARD alikuwa anachangia kwenye forum ya IT yuko wapi naye
 
Unajua haya majina yetu ya JF yanatufanya tusijue nini kinawapata wadau. Mungu apishie mbali sisi kama ni binadamu wote ni wa kupita tu hapa duniani na hakuna anayejua ni lini, wapi na saa ngapi itakuwa mwisho wa hatima yake, wengi wanatutoka tunawajua kwa majina halisi na wengine wanafungwa jela n.k ambako hakuna internet. Nafikiri MODS Mngeanzisha system ya kutrace users kama mtu hata login in three concecutive months basi tunamdiclare ama yupo mahututi, na ikifika mwaka tunamdiclare ametuacha, si mwenzetu(hapa nina maana kuwa si mwana JF au kwa maana hana uwezo tena wa kuwasiliana na sisi ama kwa kupenda au kwa mapenzi ya mungu(yaani amefariki)), na kama mtu anaona atakuwa na matatizo ya mtandao mwaka mmoja ujao basi atueleze hapa jamvini au am PM MOD.
 
Huyo Brazameni yupo Brazil kalowea huko huko
53.jpg

Kwa vitu hivi simlaumu.
 
Namtafuta Sabribachchan nae simsikii kuandika wala kujibu sijui kanuna ?
 
"Naona kawekwa kizuizini tena na Mugabe kwa kumuandika vibaya pale alipojifanya embedded journalist na msafara wa Jendayi Frazer .... !!!"
 
Jama, napenda kuuliza, members hawa wametowekea wapi? Kuna anayejua...


--Mchongoma
--KadaMpinzani
--Pangupakavu
--AmazingFriend
--

STEVE,D
Umefanya vema kuwatafuta wa JAMII wenzako.
Mimi sijui waliko.
Nashauri uangalie kama kwenye kumbukumbu zao kuna njia ya mawasiliano.
 
'...burudani isiyobadilika si burudani tena...' - Freeman A. Mbowe, Mmiliki wa Club Billicanas ya Jijini Dar es Salaam

Binadamu tumeuumbwa kukinai na jambo pale hasa kama hakuna mabadiliko, ni vema ubunifu ukachukua nafasi yake ili kuleta ladha tofauti. Mbali na baadhi ya watu hawapo kabisa, pia kuwa baadhi wamepunguza kasi ya kufika hapa barazani na wengine huja hapa tu kama kuna issue maalum anataka kuchungulia.
 
Back
Top Bottom