Gurudumu
JF-Expert Member
- Feb 5, 2008
- 2,349
- 261
Uchafu, yaani namaanisha UCHAFU kweli kweli
Yaani binadamu kufurahia maisha, kula na kulala katikati ya takataka, uozo, harufu mbaya, maji yenye kinyesi na mikojo na wadudu kama inzi bila wasiwasi!
Tumeshindwa, tena tumeshindwa halafu tukashindwa kusema kwamba tumeshindwa. Tumeshindwa kufikiri, tukashindwa kupanga na kutekeleza. Yaani tumeshindwa kabisa, anayebisha anyooshe mkono.
Kwanza wahisani wanatupatia pesa kupitia mfuko mkuu wa bajeti ya serikali na miradi mbali mbali. Tunazitafuna kama mchwa!
Kisha wanatusaidia ushauri wa kisera na hata utaalamu wa hapa na pale. Hata kama ushauri wao ni mbovu basi mipango yetu wenyewe mizuri yenye tija ni ipi?
Yote yakashindikana bado hata mazingira tunamoishi ni hatari kutokana na uchafu unaotishia afya zetu na kuongeza gharama ya huduma za afya. Uchafu ambao pia unatishia maisha ya wahisani wanaoishi humu.
wakaamua basi bora wasafishe wenyewe, kama ilivyo kwenye hii picha hapa chini, na wataendelea kufanya hivyo