Waliompora Malima Morogoro wanaswa, vitu vyapatikana.....

Hahah halafu wanaanza na .........hakuibiwa na mwanamke!! Mh. unatumia nguvu nyingi sana kujisafisha kitu kinachozidi kutufanya tuamini yale tunayoyaamini. Kaa kimya tu ushasomeka.

Kwani anataka kusema hakuna wezi wanawake? Akaende magerezani afanye utafiti - rapid asessment kisha aje aseme mwizi siyo mwanamke!Kama wamemkamata mwizi wa kiume kwanini hawajamweka kwenye vyombo vya habari ili kuzima minong'ono kama ndio lengo la kutoa taarifa mara kwa mara kwenye kesi hii?
Huenda ingesaidia zaidi kama kila mhusika angekaa kimya maana kila wanapokuja na taarifa mpya wanachochea minong'ono zaidi.
 
Kaimu kamanda huyo
ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi
wa Mkoa wa Morogoro, alisema
kuwa hata hivyo, mwizi aliyeiba vitu
hivyo hakuiba bastola na bunduki aina ya SMG alizokuwa nazo Naibu
Waziri huyo ambazo zilikuwa
sehemu iliyowazi.
 
Jeshi la Polisi ni kichaka cha kila aina ya uchafu na rushwa. Hapa wanatudanganya hakuwa na SMG wakati yeye alisema ni SMG baada ya kugundua kuwa wadau tunajua kuwa sheria haziruhusu kumiliki silaha ya kivita na kumbe walio JUU YA SHERIA wanamiliki silaha za kivita. Hii ndio tanzania bana, badala ya kulinda hadhi ya jeshi wao wanaigalagaza. No wonder hili jeshi ni la hovyo hovyo full kupokea rushwa kwani hata makamanda hawana maadili
 
Tangu sakata hili lianze mimi nilisema ingekuwa ni nchi za wenzetu walio makini POLISI angepandishwa cheo kwa ku-UNCOVER huu uongo wa Malima. Lakini nchi hii ya Wadanganyika huyo RPC Adolphina Chialo atapandishwa cheo kwa ku-COVER UP uongo wa Malima.

Lakini pia anapojaribu ku-cook up hii story ya Malima, awaapatie basi hata POLISI wenzake wajaribu kufukia fukia mashimo, kwani ina matundu mengi ambayo hata mtoto wa STD I atayachana chana vibaya
1. Vitu vilikutwa kwa mama Mdogo? Huyo mama Mdogo hatajwi jina wala sehemu anayoishi?!
2. Watuhumiwa tayari wamekamatwa, Majina yao na sehemu wanaoishi hayatajwi?
3. Aliyemuibia sio MWANAMKE! Ina maana mwizi wanamfahamu na atakuwa mawanaume, kwanini hawamsemi?
4. Nyao za mwizi zilikutwa nje ya dirisha la Malima,mwizi hakuwa na viatu, Asubuhi ya tukio nyao hizo hatukuziona!
5. Malima alikiri alikuwa na SMG, Kaimu kamanada amesema SMG haikuibiwa, RPC anasema hakuwa na SMG? Lakini pia hasemi ilikuwa ni bunduki ya aina gani?

Nchi hii kweli imejaa usanii, lakini kinachonisikitishwa kuna W.A.J.I.N.G.A tena wengi wanao buy hii cooked story!

I hope mama mdogo keshatiwa kolokoloni kwa kukutwa na mali ya wizi! Polisi msisahau kutujuza hili maana hii ni straight forward case! Huwaga haina madoido mengi ya upelelezi!Apply doctrine of RECENT POSSESSION fasta!
 
Kamanda umekula ngapi? Kwa hiyo huyo mama mdogo anashikiliwa pia? Hivi ni mdogo kiasi gani, na anaweza kupenya kwenye dirisha? Hao wengine wanne sio wafanyakazi/walinzi wa hoteli ambao ndo wanyonge wa kafara?

Na wewe malimao, lengo ni kumdanganya mkeo au na sisi manunda? Malimao, ilikuwa na ni kazi nyepesi kumtrace na kumpata huyo mama mdogo wewe mwenyewe kimya kimya kwani unajua ulimtoa wapi, na soo isingekuwa kubwa na hadharani kihivyo. Sisi ndo wanaume bana, tunajuana kwa vilemba!
 
Du, mwizi asiyekuwa mzoefu lakini ana uwezo wa kumwibia hata waziri ktk hotel kubwa kama hiyo, kazi kweli kweli.
 
Big gun ya Malima was it a shot gun, rifle, semi automatic rifle, smg, ak47, air gun, au rocket launcher?
 
Mi nina hofu kwa aliyemwibia kwa 85% ni jike halafu naye akapeleka anakojua na hawa makomredi nao wakampitia tena!

Na bila shaka wakapeleka kwa Mama Mdogo!
Hao ndio mawaziri wa jk!
Na arudie tena! Shenzi taip!!
 
najiuliza maswali mengi sana huyo kamanda wa polisi aliye itambua smg mara ya kwanza alikuwa hajuwi tofauti ya chombo hicho ambacho hata mtoto wa miaka saba wanaijuwa..

waseme tu wana tafuta mahali pakumkwamua huyo kigogo..

sawa kwenye hoteli nzima alikuwa peke yake ???Ndiyo kawaida ukinunua malay..a wa bei nafuu kwa kiwango alichonacho huyo NW.. lazima upigwe

amejidhalilisha kinomaaaaaa....
 
Inaonekana alikuwa na bunduki kubwa lakini sio SMG, sasa ajabu alikuwa anaipeleka wapi hiyo bunduki????? Hajakanusha kuwa na bunduki ila amekanusha sio SMG

Hawa polisi wetu kweli wanatuona majuha- wewe umeambiwa alikuwa na silaha kubwa unasema siyo SMG kaw hiyo ni LMG au MG? kama ungekuwa mkweili umeshindwa nini kusema siyo SMG ni GOBORI? au ulitak liwe swali la pili ?
 
alikuwa anajifunza kuiba! Vp kuhusu smg naona kama maelezo ya kaimu kamanda yananichanganya huko mwisho.

sio tu kukuchanganya bali hayaeleweki kabisa! Yamenifanya story mzima nisiikubali.
 
Back
Top Bottom