Naibu Waziri atangaza Siku 14 kuondoa namba za 3D, madereva wa serikali kukiona

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imetangaza siku 14 kwa watumiaji wa Vyombo vya Moto barabarani kuondoa namba za magari zilizoongezwa ukubwa maarufu kama (3D) na Vimulimuli kwa magari yote yasiyoruhusiwa kuwekwa, namba zote zenye vibao vyeusi na zizonatumia namba za chasis, taa zozote na stika ambazo zimeongezwa kwa matakwa ya wamiliki au madereva.
Naibu Waziri.png

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini
Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya Kikao cha Baraza la Taifa la Usalama Barabarani leo Machi 04, 2024 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Mhe. Jumanne Sagini (Mb) alisema kuwa namba hizo hazitengenezwi na wakala aliyepata kibali kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), bali zinatengenezwa kiholela mtaani na herufi hizo kubandikwa juu ya namba halali na kutosomeka katika umbali unaotakiwa ambapo katika viwango vya TBS namba ya chombo cha moto isomeke kwa umbali usiopunga mita 100 ambapo 3D haifiki kiwango hicho.

"Mambo yote yanayohusiana na Usalama Barabarani hufanywa kwa mujibu wa sheria sio utashi wa mtu mmoja mmoja au binafsi kwa mujibu wa usalama barabarani kuhusu matumizi ya namba yamebainishwa vizuri sana na sheria kwamba Namba zinazowekwa zinatakiwa ziweje? ziwe zimeandikwa na nani? anayetambulika na nani? ziwe na ubora gani? namba hizi zote hazijawekwa kwa bahati mbaya," Alisema Sagini
bb1.png

bb.png

bb.png
Mhe. Sagini alisema kuwa, Ving'ora vinatoa ishara fulani ili magari mengine yaweza kupisha na hapa nisisitize kuwa, magari yanayotakiwa kuwekwa Ving'ora yanajulikana kama ya Polisi, Zimamoto ya Wagonjwa na yale yaliyopo katika misafara ya Viongozi kufanya hivyo bila kibali maalum ni ukiukwaji wa sheria.

Aidha, Naibu Waziri Sagini alisema kuwa, zoezi la ubanduaji wa namba zilizoongezwa ukubwa litaendeshwa hata kwenye magari ya Serikali ambapo yakibainika na makosa ya namna hiyo wanaotumia watachukuliwa hatua.

Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ramadhani Ng'anzi alisema kuwa, wanapiga marufuku namba zilizoongezeka ukubwa kwa sababu kiusalama Namba za 3D sio salama na namba za magari lazima ziwe 2D kutokana na mifumo na kamera kutotambua 3D.

"Baada ya Tarehe 15 Machi, 2024 tutaendelea kuzibandua na tukiona ile plate namba haisomeki vizuri tutakukamata na hili zoezi mnatakiwa muondoe wenyewe kwa hiyari lasivyo Jeshi la Polisi litakukamata kwa kuvunja sheria hata tukikuta namba haisomeki vizuri yaani imechubuka," Alisema.

Aidha, Kamanda Ng'anzi aliongezea kuwa, Operesheni itajumuisha na Taa/Sport light kinyume na taratibu za mtengenezaji au kibali kutoka kwa Mkaguzi wa magari na uwekaji wa stika za rangi mbalimbali kwenye taa kubwa mbele na nyuma ya gari, ambazo zinabadilisha mwanga wa taa halisi mfano stika nyeusi, blue nyekundu na tinted.
 
Hapo tatizo sio namba za 3D bali ni yule jamaa anaetengeza hizo namba akishilikiana na TBS ili asiendee kulala njaa. Watu ni wanjanja sana nchi hii ....Masasi, Kiboko & Co wameona isiwe kesi wameamua kukimbilia polisi na wao wale hata 10%, kwa tamko hili madereva mjipange na hela za chenchi za buku buku zakuwapoza la sivyo huko barabarani patawaka moto si kichaa kapewa rungu
 
Masasi, Kiboko & Co wao siku wakianza uzalishaji wa 3D wala hutoona wala kusikia matamko hayo ila kwa vile ni vijana wamejiongeza limekuwa kosa.

Duniani mambo mengi yanabadilika haraka sana hasa upande wa teknolojia kwa nini hayo makampuni yanayo tambulika yasiende na wakati, kuepusha hizi kero mshenzi kwa wananchi?

Tafadhali wabadhilifu wa mali za uma nao muwe mnawawajibisha haraka sana kama ambavyo mwananchi mnawahi kumchukulia hatua akienda kinyume!

USIPOBADILIKA KWA HIYARI WAKATI UTAKUBADILI PASIPO KUTAKA!
 
Kila nikisikia hii marufuku sioni wakifanya rejea ya kifungu gani hasa kimevunjwa? Wanatoa tuu kauli za jumla kwamba wamekiuka sheria. Hivi akitokea mtu akafungua kesi kuitaka mahakama iwatake walete ushahidi wa kifungu mahususi kilichovunjwa watamuona mbaya??
 
Hapo tatizo sio namba za 3D bali ni yule jamaa anaetengeza hizo namba akishilikiana na TBS ili asiendee kulala njaa. Watu ni wanjanja sana nchi hii ....Masasi, Kiboko & Co wameona isiwe kesi wameamua kukimbilia polisi na wao wale hata 10%, kwa tamko hili madereva mjipange na hela za chenchi za buku buku zakuwapoza la sivyo huko barabarani patawaka moto si kichaa kapewa rungu
Kwa mujibu wa huyo mshua alichokilenga ni hiki na sasa ulaji unarudi kwa Masasi,Kiboko & Co. sababu ukibandua 3D lazma ukafyatue kibao upya maana namba zinakuwa zimechubuka. Na baada ya hapo wataanza kuweka 3D zao wakidai zimethibitishwa na TBS huo ni mchongo.
 
Masasi, Kiboko & Co wao siku wakianza uzalishaji wa 3D wala hutoona wala kusikia matamko hayo ila kwa vile ni vijana wamejiongeza limekuwa kosa.

Duniani mambo mengi yanabadilika haraka sana hasa upande wa teknolojia kwa nini hayo makampuni yanayo tambulika yasiende na wakati, kuepusha hizi kero mshenzi kwa wananchi?

Tafadhali wabadhilifu wa mali za uma nao muwe mnawawajibisha haraka sana kama ambavyo mwananchi mnawahi kumchukulia hatua akienda kinyume!

USIPOBADILIKA KWA HIYARI WAKATI UTAKUBADILI PASIPO KUTAKA!
Hivi vituko vipo Tanzania tu, huwezi vikuta sehemu yeyote ya ulimwenguni. Raia tubadilike mindset zetu aisee. Mtu anaridhika kufanyiwa upumbavu na serikali maisha yote ila ukimgusa mkewe tu yupo radhi aende jela yani lazma afanye reaction mbaya tu.

Hatuna uchungu na maisha yetu kabisa, wao wafanye wanavyotaka tu kila kitu chema tunafanyiwa kama hisani. We seem to be the most Stupid Citizens on earth.

Wao wakikosea hawaguswi, raia akienda kinyume ni mlolongo wa vitisho na kelele za mujibu wa sheria. Double standards kwanini?
 
"Mambo yote yanayohusiana na Usalama Barabarani hufanywa kwa mujibu wa sheria sio utashi wa mtu mmoja mmoja au binafsi kwa mujibu wa usalama barabarani kuhusu matumizi ya namba yamebainishwa vizuri sana na sheria kwamba Namba zinazowekwa zinatakiwa ziweje? ziwe zimeandikwa na nani? anayetambulika na nani? ziwe na ubora gani? namba hizi zote hazijawekwa kwa bahati mbaya," Alisema Sagini
Huyu naye hafai kuwa kiongozi, alikuwa wapi mpaka tatizo limekuwa sugu kiasi hicho, traffic police hivi sasa ni kamaa wameongezewa mzigo wa kazi kukimbizana na hayo magari, isitoshe wanaoongoza kutembelea namba za chesis ni hao wasiojulikana and the like, na hizo kauli za kukiona zilishazorleka, hivi dereva wa serikali anapata wapi pesa na jeuri ya kuongeza urembo kwenye gari la umma kama siyo ushirika na maboss wao?
 
Nafikiri tatizo sio namba tatizo ni maslahi.
Sioni ubaya kuwa na namba za 3D ila ungewekwa utaratibu wa kuziboresha zionekane hata zaidi ya mita 100.Pili tamko la waziri halina vifungu vya sheria vya kuzuia namba hizo.
Tatu, serikali iangalie biashara huria ili mradi utaratibu ufuatwe.Mtu achague bidhaa tofauti sokoni ili kumridhisha mteja kuliko kuzuia uhuru wa mlaji.
 
Kama kuna sheria inayokataza aweke wazi.
Kitendo cha kusema wataendelea kubandua na si kuchukua hatua za kisheria ni ishara tosha kwamba hili suala halina nguvu kisheria.
Narudia tena huyu sagini hamna kitu...hadi wajinga wameshajua hii dili.
 
Hilo baraza la usalama halina kazi yaani wamekaa kujadili no plate za 3D, na vimulimuli kweli halafu ukute wamelipana posho kbs kwa kujadili hizo ajenda inasikitisha sana
Hapo utakuta MASASI SIGN katoa mpunga mrefu zoezi lifanyike ili yeye apige pesa.

Namshangaa Waziri anaongelea stika anaacha NGAO zilizopo kwenye Bajaj na Daladala
 
Kwamba serikali inapigana na technology?
Hapana hawapingani ila ni wazi wataruhusu lakini watakuja na hizi blaa blaa za TBS ili mtu mmoja tu anufaike na hili deal kuwa sole supplier na hii anayeumia ni sisi, nchi hii haitaki ushindani wa biashara watu waoga kushindana. Wametuumiza kwenye sukari kwa sababu hizihizi watu hawataki ushindani. Ushindani unatija na mtumiaji bidhaa anapata nafuu kwa kuwa anakuwa mfalme sio unampa ufalme mfanya biashara. Iko wapi wasimamizi wa biashara za ushindani kuhakikisha mteja analindwa.
 
Back
Top Bottom