Mwizi wa Alama za Barabarani akamatwa

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
1708356847140.png

JESHI la Polisi mkoani Tabora limemkamata Moshi, kwa tuhuma za uharibifu na wizi wa alama za usalama barabarani kutoka katika barabara mbalimbali katika mkoa huo baada ya kukutwa na alama zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 10 nyumbani kwake.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi, ACP Richard Abwao, amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa saa 12 asubuhi katika Kata ya Usege wilayani Kaliua.

Amesema walimkamata mtuhumiwa huyo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ambao wanapiga vita vitendo vya uharibifu wa alama za barabarani.

Source - Nipashe
 
Back
Top Bottom