Polisi Jamii Malima aliyetajwa na JamiiForums kuwa anatumia madaraka vibaya, asimamishwa kazi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460

View: https://www.youtube.com/watch?v=_fJw7MIsJZk



Siku chache baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai Polisi Jamii Kata ya Nala, Yohana Nyagalu “Malima” kutumia Madaraka yake vibaya ikiwemo kunyanyasa na kudhalilisha Wananchi, Jeshi la Polisi limechukua hatua ya kumsimamisha Askari huyo kwa muda wa miezi mitatu na kumtaka kujirekebisha.

Mdau alidai Malima amekuwa akichukua nafasi kuwa kama Polisi, Mwanasheria, Hakimu na Magereza kutokana na maamuzi yake, pia akadai amekuwa na tabia ya kulazimisha Watu anaowakamata wampe Rushwa.

Akijibu tuhuma hizo katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na Polisi, Malima amesema baadhi ya tuhuma ni za kweli na nyingine anasingiziwa.

Afisa Ushirikishaji Jamii Mkoa wa Dodoma, Eva Stesheni amesema “Ngoma ikivuma sana inapasuka, Malima amefanya kazi hiyo miaka 11, eneo moja, hapo kuna shida kidogo, hakukuwa na Watu wa kuchukua nafasi yake, nawashauri vijana mjitokeze kushiriki mafunzo mjiunge na Polisi Jamii, Malima atasimama kwa miezi mitatu kwa makosa ya Kimaadili.”

Chanzo Video: Mkuti TV
Pia soma - RC na RPC Dodoma, Polisi Jamii Kata ya Nala anatunyanyasa sana, tafadhali muondoeni
 
Kazi nzuri JF, tuendelee kuwaripoti hawa Polisi jamii/Migambo maana huwa wanajiona miungu watu kwenye biashara ndogo ndogo za watu.
 
Back
Top Bottom