Denis1729
Member
- Sep 9, 2021
- 34
- 109
Nimekuwa nikiuliza wanafunzi wengi kuhusu ndoto zao za baadae lakini wengi wao walionekana kukata tamaa kutokana na tabia za walimu wengi wanaofundisha masomo ya sayansi na walimu wa taaluma kuwatoa kwenye orodha ya wanafunzi watakaosoma masomo ya sayansi kuanzia kidato cha tatu na nne kutokana na kutakuwa na matokeo mazuri ya masomo hayo katika mtihani wa taifa wa kidato cha pili.
Wengi wao walitolewa kusoma masomo ya sayansi bila ya kuwauliza uhiyari wao wa kusoma masomo hayo bali kwa lazima kwa kigezo kwamba hawayawezi masomo hayo na kuwapelekea kuishia kusoma masomo ya sanaa yaani arts peke yake.
Naombeni wizara ya elimu na wadau wa elimu waweze kutoa elimu kwa walimu wote kuwa mwanafunzi ana haki ya kusoma masomo anayotaka bila kujali ufaulu anaotaka kwa sababu hakuna sehemu inayosema mwanafunzi asipofanya vizuri kwenye masomo ya sayansi akasome masomo ya Sanaa.
Walimu waache tabia hiyo kwani inaharibu na kupoteza kwa baadhi ya matumaini na ndoto kwa wanafunzi waliokuwa na ndoto za masuala ya sayansi.
Kwanini wanafunzi wasiofanya vizuri masomo ya sanaa hawapelekwi kusoma masomo ya sayansi kama ilivyo kwa wanafunzi wasiofanya vizuri masomo ya sanansi wanapelekwa kusoma masomo ya sanaa?