Wanafunzi kufukuzwa kusoma somo la chemistry ilhali wamepata grade "C na D"

Martin Hamza

New Member
Jan 13, 2024
2
3
Naomba wadau wa Jamiiforums waweze kufatilia uovu unaofanywa na mwalimu mmoja katika shule ya secondary Kanoge ambayo ipo wilaya ya Nsimbo mkoani Katavi kwani katika shule hiyo kuna mwalimu wa somo la Chemistry pia ni mwalimu wa nidhamu.

Ana tabia ya kukataza wanafunzi wasisome somo la Chemistry akidai anahitaji wanafunzi wachache anaweza kuwafundisha table teach maana ukianglia Kwa wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2024 hata 15 hawafiki wengi aliwatoa kwenye somo hilo kisa wamepata wastani wa "C na D".

Kwenye somo hilo pia hata wanafunzi waliomaliza kidato cha nne 2023 aliwafukuza kwenye somo lake, kuwarudisha aliwambia hao aliwafukuza kila mmoja alipe elfu5 ndo arudi.

Sasa naomba waziri wa elimu , afisa elimu mkoa na wilaya, mkuu wa mkoa , na wilaya waweze kulishughlikia swala hilo mana kuna wanafunzi wana ndoto ya kusoma masomo ya sayansi lakini mwalimu huyo anakatisha ndoto zako kwa interest zake binafsi.
 
Sasa Chemistry ya Form 2 mwanafunzi anapata D, mimi naona ni sawa tu kwa mwalimu kumkataza mwanafunzi wa hivyo kuendelea na hilo somo, maana utakua ni mzigo tu kwa mwanafunzi, bora akomae na masomo mengine anayoyaweza zaidi.

Chemistry ya Form 2 ukipata D, most likely hapo form 3 itamtesa sana sana, na form 4 ataishia tu kupata F au akikomaa sana hiyo hiyo D. Mwalimu anafanya hivyo kwa faida ya wanafunzi, wazazi acheni kulazimishia watoto wasome masomo ambayo yanawakimbiza, na muwe waelewa msipende kulazimisha mambo.
 
katika shule ya secondary Kanoge iliyopo wilayani Nsimbo mkoani KATAVI Kuna tatizo la mwalimu wa somo la chemistry kuwatoa wanafuzi kwenye somo analofundisha akidai yeye anahitaji wanafunz atakao wafu Disha table teach mfano wanafunz WALIOPO kidato Cha nne mwaka 2024 hawafiki hata15 wengi wao aliwaondoa kwenye somo Hilo Bada ya kuwapa mtihani walipo kua kidato Cha tatu wote waliopata grade C na D aliwafukuza pia Kwa waliomaliza kidato Cha nne mwaka 2023 wapi aliowatoa hali kama hii inakatisha ndoto za wanafunz wengi wenye malengo ya kusoma masomo ya sayansi
 
Ni Kawaida kwa shule nyingi kuweka wastani kwenye masomo complicated kupunguza miswaki hapo baadaye mtihani wa taifa.
Wanaojitoa kusoma basi wasome bila kubabaisha..wavivu wavivu wapambane na masomo Saba yaliyobakia.
 
Sasa Chemistry ya Form 2 mwanafunzi anapata D, mimi naona ni sawa tu kwa mwalimu kumkataza mwanafunzi wa hivyo kuendelea na hilo somo, maana utakua ni mzigo tu kwa mwanafunzi, bora akomae na masomo mengine anayoyaweza zaidi.

Chemistry ya Form 2 ukipata D, most likely hapo form 3 itamtesa sana sana, na form 4 ataishia tu kupata F au akikomaa sana hiyo hiyo D. Mwalimu anafanya hivyo kwa faida ya wanafunzi, wazazi acheni kulazimishia watoto wasome masomo ambayo yanawakimbiza, na muwe waelewa msipende kulazimisha mambo.
Mimi nikiwa olevo nilikua sitaki kusoma chem ila mwalimu alinilazimisha na form4 nikapata D. Kama sio kulazimishwa kama sio kupata D nisingekuwepo nilipo leo.

Acha watoto wasome usimnyime kusoma kisa ana D au C!
 
Sasa Chemistry ya Form 2 mwanafunzi anapata D, mimi naona ni sawa tu kwa mwalimu kumkataza mwanafunzi wa hivyo kuendelea na hilo somo, maana utakua ni mzigo tu kwa mwanafunzi, bora akomae na masomo mengine anayoyaweza zaidi.

Chemistry ya Form 2 ukipata D, most likely hapo form 3 itamtesa sana sana, na form 4 ataishia tu kupata F au akikomaa sana hiyo hiyo D. Mwalimu anafanya hivyo kwa faida ya wanafunzi, wazazi acheni kulazimishia watoto wasome masomo ambayo yanawakimbiza, na muwe waelewa msipende kulazimisha mambo.
Kwa elimu ya sasa wacha watu wasome tu jamani.

Hizo D za chemistry na Bios. Zitamsaidia kusoma course ya afya ambayo itampa Maisha baadae.

So kuwa na wanafunzi wachache sio kigezo cha kufundisha na wakaelewa
 
Mtoto asome alicho na uwezo nacho,

Sasa Kama apo form 2 anapata C na D,

Uyo akifika form 4 atapata mswaki kabisa,

Na hao wanafunz ving'an'ganizi ndo uziletea shule nyingi sifuri kila mwaka,

Apo mzazi ongea na mwalimu wake amsaidie mwanao ata kwa masomo ya ziada aweze kumudu masomo ya sayansi, Kisha akasomee michepuo ya sayansi

Sio kung'ang'aniza asome ukasifiwe mitaani mwanao anasoma sayansi wkt unajua uwezo wa mwanao Ni mdg au ujamwandaa vzur.

Wazazi Kama nyie,
Ndo Mkituona Tunawalipia watoto wetu twisheni mitaani mnatuonaga Kama tunachezea pesa vile, kisa TU tayar mshakaririshwa na CCM Ni elimu bure.

ALOKUDANGANYA ELIMU NI BURE NANI?

MZAZI GHARAMIA ELIMU YA MWANAO UPATE KILICHO BORA.

"Kama elimu Ni ghali, jaribu ujinga"
 
Mtoto asome alicho na uwezo nacho,

Sasa Kama apo form 2 anapata C na D,

Uyo akifika form 4 atapata mswaki kabisa,

Na hao wanafunz ving'an'ganizi ndo uziletea shule nyingi sifuri kila mwaka,

Apo mzazi ongea na mwalimu wake amsaidie mwanao ata kwa masomo ya ziada aweze kumudu masomo ya sayansi, Kisha akasomee michepuo ya sayansi

Sio kung'ang'aniza asome ukasifiwe mitaani mwanao anasoma sayansi wkt unajua uwezo wa mwanao Ni mdg au ujamwandaa vzur.
Ingekua ni mtoto hataki kusoma ila mzazi anamlazimisha ningekuunga mkono! Mtoto anataka kusoma, mwalimu hutaki asome? Hii sio sawa!
 
Kwanza Ni aibu mzazi kuhoji sh Elfu 5 kwa mwezi ajili ya masomo ya ziada kwa ajili ya mwanao, Tena anaesoma masomo ya sayansi, Tena shule hizi za elimu bure, ticha mmoja wanafunzi mamia darasani.

Enzi zetu tulikua tunalipia kwa topic, Tena mitaani na ukimwambia mzazi hata hakuulizi Mara mbili mbili ili usilete visingizio vyako Siku ukifeli, maana kifuatacho Ni stick Kwenda mbele.

Sasa mwanao unataka afaulu afu ata kutoa motisha ya elfu 5 kwa mwalimu wake akufundishie mwanao vzur unahisi Kama unatapeliwa.

Hivi wazazi Kama nyie Ni mnajielewa kweli?
 
  • Thanks
Reactions: K11
katika shule ya secondary Kanoge iliyopo wilayani Nsimbo mkoani KATAVI Kuna tatizo la mwalimu wa somo la chemistry kuwatoa wanafuzi kwenye somo analofundisha akidai yeye anahitaji wanafunz atakao wafu Disha table teach mfano wanafunz WALIOPO kidato Cha nne mwaka 2024 hawafiki hata15 wengi wao aliwaondoa kwenye somo Hilo Bada ya kuwapa mtihani walipo kua kidato Cha tatu wote waliopata grade C na D aliwafukuza pia Kwa waliomaliza kidato Cha nne mwaka 2023 wapi aliowatoa hali kama hii inakatisha ndoto za wanafunz wengi wenye malengo ya kusoma masomo ya sayansi

Yupo sahihi sasa C and D za nini? Nenda kasome history huko.
 
Yuko sahihi. Kama wazazi ni wapumbavu mwalimu afanyeje? Badala ya ninyi wazazi kukemea huo upuuzi unakimbilia kupost hapa.
 
Ingekua ni mtoto hataki kusoma ila mzazi anamlazimisha ningekuunga mkono! Mtoto anataka kusoma, mwalimu hutaki asome? Hii sio sawa!
Mtoto Kutaka kusoma asicho na uwezo nacho kisa tu anakipenda nao Ni ujinga mwngine, Mtoto asome anachokimudu.

Kama angekua anakipenda Basi angejibidiisha kukisoma na angefaulu Kama wengine ili kusiwe na longolongo.

Ningekua wewe,
Ningemuuliza mtt sababu za kufeli na anajua mwalimu keshaweka standard zake anazopaswa kuzipass ili kusoma sayansi. Na sio kumlaumu ticha.
 
Back
Top Bottom