Elections 2010 Wakili wa mdai wa Dr. Slaa ni mgombea udiwani wa CCM!

dah!
huyu jamaa ni mwenda wazimu sana yaani ameamua kutuaibisha wanaume maana mwanaume kamili huwezi kulia lia hadharani kuwa umeporwa mke
unaporwa!!!!!!!!

HUYU NI WA KIUME SIO MWANAUME, mwanaume huwa halalamiki hi hivyo
 
Si ndio nyinyi Wakristo munaosema ndoa hazivunjwi? Leo tena mambo yamekuwa vipi? Au mkuki kwa nguruwe lakini kwa binaadamu huwa mchungu?

Mimi nauliza tu jamani!!!!!!!!!!!!!

Kwe kampeni za mwaka huu kipaumbele ni kipi, mkeo na hawara zako ama Masklahi ya taifa, Uwajibikaji wa Serikali, Ujenzi wa Uchumi thabiti?
 
dah!
huyu jamaa ni mwenda wazimu sana yaani ameamua kutuaibisha wanaume maana mwanaume kamili huwezi kulia lia hadharani kuwa umeporwa mke
unaporwa!!!!!!!!

HUYU NI WA KIUME SIO MWANAUME, mwanaume huwa halalamiki hi hivyo

Waswahili bwana....! Usishangae bwana Edson, hawa kwao pwani mambo yao ni idadi ya wake na miti ya minazi huku muda wao mwingi wanautumia kujenga uswahiba wakinywa kahawa.
Watakumbuka saaa ngapi kuwa watanzania wanataka kusikia kuhusu uwajibikaji, ujenzi wa uchumi imara, maendeleo ya watu, uadilifu mahala pa kazi hasa hasa katika ofisi za umma, uboreshwaji wa huduma za afya, bara bara, mazingira n.k? Ndo maana hawa jamaa linapoibuka suala la wanawake wanaacha kuzungumzia suala lililoko mezani wanapoteza muda mwingi kuzungumzia udaku. Halafu wanataka eti watanzania wawape kura ili waendelee na uharo huu, haiwezekani hata kidogo!
 
Mwanaume kutoka hadharani na kudai ameporwa mkewe ni aibu ya mwaka!!! watu watajiulize kulikoni ? itabidi apimwe afya yake labda mtoto si.......Amekosa ushauri mimi ningemshauri akae kimya avumilie maumivu mwenyewe. Maana kwa ss hawezi pata tena mwingine
 
Siyo tu kwamba Josephine hamtaki, bali pia huyo jamaa ana matatizo mengine ya ziada. Ukisoma maelezo yake yaliyoandikwa kwenye gazeti la HabariLeo kuna kasoro kibao ambazo zinaacha maswali mengi:

1. Mwanamke aliondoka nyumbani, na kaondoka muda mrefu na alimuaga kabisa kwamba nakuachia kibanda chako nakwenda kwenye nyumba.

2. Josephine aliondoka na wanae, ajabu ni kwamba jamaa alikuwa hajui hata hao wanae wanaishi wapi, wanakula nini na maisha yao kwa ujumla yakoje.

3. Alikaa muda mrefu bila kuonana wanae, mwanaume ambaye yuko responsible sidhani kama anaweza kukubali "mke" aondoke na watoto na asijue hiyo familia inaenda kuishi wapi na itaishi vipi.

4. Kuna sehemu anasema mtoto alimpigia simu akiwa analia anataka kuondoka huko alikokuwa akiishi na mama yake, kama kweli jamaa yuko responsible, ilikuwaje asiende kumchukua mwanae kesho yake? Mpaka leo watoto bado wanaishi na mama yao.

Kwa ujumla jamaa anajidhalilisha mwenyewe na kujionyesha jinsi alivyo irresponsible.
.

hata mwanamke ambae yuko responsible hawezi kutoroka kitanda cha mume wake wa ndoa kihuni kihuni na kisha akaibukia kwa mume mwingine yaani Dk Slaa. Alitakiwa kukimbilia kanisani alikofunga ndoa kuomba msaada, kwa ndugu wa pande zote mbili au mahakamani kudai haki zake. Ukiona mwanamke anatoroka bila utaratibu kisha huko aliko anatangaza ndoa basi ameshindikana
 
Acha mahakama itoe hukumu yake wewe una base kwenye habari ya upande mmoja hujui huyo mwanamke aliondoka kwa sababu gani, unatoa judgement kisiasa na si kitaaluma.

Hata wewe Luteni umehadaika kiurahisii hivi? unashindwa kujua kuwa hii kesi inajaribu kurudisha kura za wakristu na pia kuwahadaa Maaskofu na waumini wao kuwa waraka wakikristu walioutoa unambana Dr Slaa kuwa hafai kimaadili yao ya kanisani na mwisho wa siku wapete? CCM huko kwenye kesi wao hawapo kabisa wapo kwenye waraka wa maaskofu tu
 
Huyu jamaa naye anatumiwa tu kisiasa. Ndiyo maana nasema hii ni frivolous lawsuit. Muda wote huo alikuwa wapi kufungua hayo mashitaka? Ina maana kajua wiki chache tu zilizopita baada ya Slaa kuteuliwa na CHADEMA kugombea uraisi? Timing yake mbaya na inanuka siasa za personal destruction. Hata kama ana hoja na sababu nzuri lakini huwezi ukaondoa shaka la kutumiwa na wapinzani wa Slaa.

Halafu wakili wake ni mwana CCM mgombea udiwani. Hahahahaa....naona kuna kosa la miiko flani flani hapo.


Dk Slaa alianza kumendea mke huyo wa mtu wakati wanaishi jirani Kijitonyama. Hapo ndipo Dk. Slaa alianza kwa kuiba na kutesa kwa kificho na Josephine bila kujali ni mke wa mtu hasa kwa kumpa vijisenti kama vya mzee chenge. Binti akazibuka hakutaka kumsikiliza jamaa. Kilichosababisha Dk Slaa kumlaghai Josephine ni ujirani pale kijitonyama.
 
Mkuu Mwiba,

Nani anatakiwa ku-report? Aliyekimbia au aliyekimbiwa? Kiutaratibu mume huwa anakabidhiwa mke au mke anakabidhiwa mume? Swali, je baada ya mkewe kuondoka nyumbani, huyo jamaa alifanya nini? Ali-report polisi? Alitoa taarifa kwa wazazi wa mkewe? Baada ya hapo alifanya nini? Ni nani anatakiwa ku-initiate process, mke au mume?

Mwanamke angetakiwa kutoa taarifa polisi iwapo angekuwa alipigwa na mumewe, lakini kama aliondoka tu bila ugomvi wowote, mwenye full responsibility ya ku-report kupotea kwa mkewe na wanae ni mwanaume maana ndiye aliyekabidhiwa mke.

Ninakubaliana na wewe kwamba sheria zitachukua mkondo wake, lakini naomba nikuhakikishie kwamba huyo jamaa yako atadhalilika zaidi na hayo madai ya bilioni moja yataishia hewani, ngoja tusubiri hiyo kesi itakapoanza kusikilizwa ili tujionee vimbwanga.

Ajabu ni kwamba siku anaongea na HabariLeo, mwandishi alimuuliza je ana mpango wa kwenda mahakamani? Akasema hana mpango huo. Ndio maana kuna watu wanasema jamaa anatumiwa na wana siasa. Ukishaingia kwenye siasa, akili huwa inasahau taaluma kwa muda, ndo maana hata wakili mwenyewe wanasema anagombea udiwani.

Kwangu mimi naona kesi imefunguliwa strategically kwa ajili ya uchaguzi tu na haitafika kokote. Uchaguzi ukipita na kesi hutakuja kuisikia tena.

Weka mbali kama mume wa Josephine ametumwa na CCM au hapana, Dk. Slaa anawajibika kutupa mashabiki wake ukweli. Je amezini na mke wa mtu au hapana. Acheni mjadala wa maji taka hapa twende kwenye hoja ya msingi ya wizi wa mke wa mtu.
 
Mkuu Mwiba,

Nani anatakiwa ku-report? Aliyekimbia au aliyekimbiwa? Kiutaratibu mume huwa anakabidhiwa mke au mke anakabidhiwa mume? Swali, je baada ya mkewe kuondoka nyumbani, huyo jamaa alifanya nini? Ali-report polisi? Alitoa taarifa kwa wazazi wa mkewe? Baada ya hapo alifanya nini? Ni nani anatakiwa ku-initiate process, mke au mume?

Mwanamke angetakiwa kutoa taarifa polisi iwapo angekuwa alipigwa na mumewe, lakini kama aliondoka tu bila ugomvi wowote, mwenye full responsibility ya ku-report kupotea kwa mkewe na wanae ni mwanaume maana ndiye aliyekabidhiwa mke.

Ninakubaliana na wewe kwamba sheria zitachukua mkondo wake, lakini naomba nikuhakikishie kwamba huyo jamaa yako atadhalilika zaidi na hayo madai ya bilioni moja yataishia hewani, ngoja tusubiri hiyo kesi itakapoanza kusikilizwa ili tujionee vimbwanga.

Ajabu ni kwamba siku anaongea na HabariLeo, mwandishi alimuuliza je ana mpango wa kwenda mahakamani? Akasema hana mpango huo. Ndio maana kuna watu wanasema jamaa anatumiwa na wana siasa. Ukishaingia kwenye siasa, akili huwa inasahau taaluma kwa muda, ndo maana hata wakili mwenyewe wanasema anagombea udiwani.

Kwangu mimi naona kesi imefunguliwa strategically kwa ajili ya uchaguzi tu na haitafika kokote. Uchaguzi ukipita na kesi hutakuja kuisikia tena.

Kuiba mke wa mtu ni utawala bora? Rais mtarajiwa anakuwa ni mwizi wa wake za watu hata kabla hajapata urais mmmmmh Dk Slaa akiwa Rais wake zetu watasalimik!!!!! maanake akimpenda tu atatuma watu wa kumtorosha. Dk. Jiuzulu kwa heshima yako.

Utawala bora ni pamoja na kufuata sheria za nchi. Hii ya Slaa inakiuka misingi ya utawala bora pale anaposhiriki kuisambatisha familia halali kisheria. Familia ndio hujenga taifa lakini Slaa anabomoa familia ili kuelekea Ikulu. Dk Slaa anashiriki kutengeneza watoto wa mitaani wasio na baba.nasita kukubali kwamba hili ni jambo binafsi.
 
BitiMkongwe,

Maandiko matakatifu ndo yanasema hivyo kwamba kilichounganishwa na Mungu, binadam hawezi kukitenganisha. Lakini katika uhalisia wa mambo kuna ndoa nyingi sana za kikristo ambazo zimevunjwa au zimevunjika. Maandiko matakatifu pia yana vipengele ambavyo vinaelezea sababu ambazo zinaweza kufanya ndoa ivunjwe/ivunjike.

Bottom line ni kwamba hata kwenye ukristo bado ndoa inaweza kuvunjwa na sababu ziko kwenye maandiko yao.

Na mimi nimesema tu jamani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
.

kwa hiyo katika ukristo ndoa inavunjika bila kufuta kanuni za kanisa?
 
Ata kesi ikingurum si mpaka iwe proven kuwa ni kweli.
Kama kesi akina Mramba,Chenge mbona wanapeta au ya Slaa ni ya mauaji?
Na kumbuka kama akishinda wakati kesi inaunguruma then analindwa na SHERIA so kesi itakufa kifo cha Mende
 
Mkuu Mwiba,

Dr Slaa hawezi kujiuzulu kwa kuwa sijaona kosa lake mpaka sasa. Hivi Mkuu Mwiba ukikutana na mwanamke akakuvutia, si unamuuliza kama ana mtu au la? Akisema alishawahi kuolewa na kwamba alishaachika utataka nini zaidi? Au mwanamke akishakuwa na watoto na akaachika anatakiwa asiolewe tena? Kisa? Maalim hapo sikubaliani na wewe, wacha tuiachie Mahakama ifanye kazi yake. Uzuri wa kesi yenyewe siyo criminal, kwa hiyo haiondoi sifa ya Dr. Slaa kuwa mgombea.
.

Kajaribu kujijitetea mahakamani hivyo kama hujafungwa au kulipa fidia kubwa. Nani kakuambia maneno ya mdomoni yanatosha kumshawishi hakimu kwamba ukikutana na mke wa mtu akisema tu kaachika unaanza kutembea naye. Dk. Slaa alikuwa na nafasi ya kuomba vielelezo zaidi kama kweli ni mtu wa kufauata misingi ya sheria
 
Na waliomsindikiza kwenye pres conference yake wote wapambe wa Makamba....hivi tingatinga lilipopora yule Mama mbona CCM hawakumsaidia mumewe?
.

wote ni wamoja hakuna atakayemtetea tingatinga kama alifanya hivyo ni sawa na Slaa. kama ni hivyo tingatinga ana bahati mbona hakuna aliyejitokeza kutoa madai
 
jamaa alikuwa anamsindikiza mkewe huyo majira ya jioni siku ya tukio ndipo slaa alimvizi jamaa akiwa anakojoa kichakani na kumpora mke wake wa siku zote........kwa kifupi..ukitaka sinema nzima livyochezwa ntakupa.ha...ha...haaaaaaaaaaaa
Hivi huyu bwana ameporwaje mke wake? Mimi bado hii kitu haijaingia akilini!
 
Inaelekea Mahimbo siyo riziki kutokana na ulevi wa kupindukia ndiyo maana ndoa ikamshinda
Ulevi wa Mahimbo unaweza kuwa ulisababishwa na mawazo baada ya Josephine kutoroka kila wakati kwenda kwa Dk. Slaa. IPo habari kuwa alikuwa hashikiki alipokutana na Slaa, nyodo na dharau kibao kwa mumewe.
 
Sheria itawatambuaje kuwa mume na mke bila uthibitisho wa marriage certificate? hiyo sheria inahitaji kwenda mbele zaidi..
.

kasome sheria ya ndoa, usiwe mbishi. Ushahidi wa majirani na ndugu wakithibitisha kuwa mwanamume na mwanamke wameishi pamoja zaidi ya miezi 6 ushahidi huo unatosha kuhalalisha hiyo ni ndoa kisheria chini ya kiapo cha mahakama. Dk Slaa ana ndoa mbili ya Rose Kamili na Josephine Mushimbusi kwa kuwa aliishi na mke wa kwanza hata kama hakumuoa zaidi ya miezi 6
 
.

kwa hiyo katika ukristo ndoa inavunjika bila kufuta kanuni za kanisa?

https://www.jamiiforums.com/members/fofofo.html
fofofo
  • profile.png
    View Profile
  • forum.png
    View Forum Posts
  • message.png
    Private Message
  • article.png
    View Articles
  • add.png
    Add as Contact
  • email.png
    Send Email
user-online.png
Junior Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
Join DateWed Sep 2010Posts6 Thanks : 0
Thanked 0 Times in 0 Posts

Umekaa kimaralia sugu vile vile any way nakusabahi tu komredi.
 
Back
Top Bottom