KWELI Waishio milimani Jijini Mwanza watakiwa kuondoka kupisha mwekezaji

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Ulivyo Soma ni sahihi kabisa wala hujakosea. Ndo habari ya mjini, zile nyumba zote zilizopo kwenye mountain inabidi zitoke jamaa wa Brazil aje ajenge na Familia yake.
X.jpg
 
Tunachokijua
Wakazi waishio maeneo ya mlimani jijini Mwanza wanatarajiwa kuhamishwa katika maeneo hayo ili kupisha wawekezaji kutoka nchini Brazili ambao wanatarajia kuwekeza kwenye sekta ya miundombinu, viwanda na utalii katika maeneo ya Igogo, Isamilo na Kegeto.

Akizungumza na Nipashe, Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Constantine amesema wawekezaji hao kutoka jiji la Rio de Janeiro walifika jijini humo kuangalia fursa za uwekezaji, na mpango wa kuwahamisha katika eneo hilo unalenga kuboresha miundombinu pamoja na kukuza sekta ya utalii utakaogharimu TZS bilioni 150.

Aidha, amebanisha maeneo mengine ambayo wawekezaji wanayalenga ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha pembejeo za kilimo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa kanda ya ziwa, ujenzi wa barabara pamoja na nyumba za ghorofa katika milima mbalimbali inayoangalia Ziwa Victoria.

Costantine ameeleza kuwa jiji limepewa jukumu la kulipa fidia katika maeneo ya Igogo, Isamilo na Kegoto ili kupisha uwekezaji huo.

Pia, wawekezaji hao wamekubaliana na jiji kutafuta ardhi na kukamilisha mipango ya ardhi ndani ya miezi mitatu kuanzia mwanzoni mwa mwezi huu kabla kazi hiyo kuanza.

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom