Waishio milimani Jijini Mwanza watakiwa kuondoka kupisha mwekezaji

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
14,303
29,865
Ulivyo Soma ni sahihi kabisa wala hujakosea. Ndo habari ya mjini, zile nyumba zote zilizopo kwenye mountain inabidi zitoke jamaa wa Brazil aje ajenge na Familia yake.

--------

Wawekezaji hao wanatarajia kuwekeza kwenye sekta ya miundombinu, viwanda na utalii katika maeneo ya Igogo, Isamilo na Kegeto.

Akizungumza na Nipashe ofisini kwake hivi karibuni, Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Constantine, alisema mpango huo unalenga kuboresha miundombinu pamoja na kukuza sekta ya utalii utakaogharimu Sh. bilioni 150.

Alisema makubaliano hayo yanahusisha wawekezaji kutoka nchini Brazil katika Jiji la Rio de Janeiro, ambao walifika jijini humo, kuangalia fursa za uwekezaji katika miundombinu, viwanda na utalii.

Costantine alisema maeneo mengine ambayo wawekezaji hao wanayalenga ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha pembejeo za kilimo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa Kanda ya Ziwa.

“Sehemu zingine ni ujenzi wa barabara pamoja na nyumba za ghorofa katika milima mbalimbali ambayo inaangalia ufukwe wa Ziwa Victoria,” alisema.

Alitaja sehemu zingine watakazozigusa kuwa ni pamoja na kutengeneza eneo la ufukwe wa Ziwa Victoria sehemu ya kliniki, Nera jirani na kituo cha polisi wa majini ambalo litatengenezwa na kuwa sehemu za uwekezaji na utalii.

Constantine alisema mpango huo utasaidia ukuaji wa uchumi wa Jiji la Mwanza na mtu mmoja mmoja.

Alisema wawekezaji hao wana umoja wao nchini Brazil unaojulikana kama ‘Africa Unity’ na mpaka sasa wamewekeza nchini Dubai na Ethiopia.

Aliongeza kuwa katika makubaliano ya mpango huo, Jiji la Mwanza litatoa ardhi na wawekezaji watatoa mtaji, teknolojia na mradi huo utakapokamilika utanufaisha pande zote mbili.

ULIPAJI FIDIA
Akizungumzia uwekezaji wa maeneo ya milimani, Constantine alisema, jiji limepewa jukumu la kulipa fidia katika maeneo ya Igogo, Isamilo na Kegoto ambayo yapo mlimani ili kupisha uwekezaji huo.

Constantine alisema wawekezaji hao wamekubaliana na jiji litafute ardhi na kukamilisha mipango yote ndani ya miezi mitatu kuanzia mwanzoni mwa mwezi huu kabla ya kazi hiyo kuanza.

Aliongeza kuwa wawekezaji hao wanaendelea kutafuta maeneo mengine ya kuwekeza ikiwamo mikoa ya Dodoma na Arusha.

Chanzo: Nipashe
 
Ulivyo Soma ni sahihi kabisa wala hujakosea. Ndohabari ya mjini, zile nyumba zote zilizopo kwenye mountain inabidi zitoke jamaa wa Brazil aje ajenge na Familia yake.

Source :nipashe media. View attachment 2260162
Sasa hizo ni nyumba au takataka? Walitakiwa waondolewe kitambo tuu maana wanachafua Mji..

Hao watu wa milimani Nina uhakika watakuwa wa kwanza kuitikia mwito maana watapewa maeneo mazuri yaliyopimwa na Fidia juu..

Nyanzaga Kule Sengerema wamehama kupisha Mwekezaji wa mgodi mkubwa dhahabu sembuse hao maskini wa huko milimani?
 
Hii mambo ya kuuza nchi vipande vipande tunapata hasara, kama vipi tuuze jumla kila mtu apewe chake asepe.

Lakini hiyo familia ya Brazil itajenga kwenye milima yote ya Mwanza Mabatini, Kirumba, Igogo, Mahina mpaka Ibanda huko?
 
Hasara gani? Anauziwa nani? China wangeendelea kuwachekea wajinga kama nyie isingekuwepo pale ilipo..

Maendeleo yana gharama ikiwemo kufyeka wajinga kama nyie,MKapa aliwafukia kule kwenye migodi walipoleta ubishi wa kitoto.
 
Sasa hizo ni nyumba au takataka? Walitakiwa waondolewe kitambo tuu maana wanachafua Mji..

Hao watu wa milimani Nina uhakika watakuwa wa kwanza kuitikia mwito maana watapewa maeneo mazuri yaliyopimwa na Fidia juu..

Nyanzaga Kule Sengerema wamehama kupisha Mwekezaji wa mgodi mkubwa dhahabu sembuse hao maskini wa huko milimani?
You are stupid!
 
Kuwa na utu acha dharau na kibri .
Utu gani? Hizo ni nyumba auntakataka? Kuwaacha kwenye Hali hiyo ya umaskini ndio utu? Acha upumbavu..

Kule magomeni wanapisha viwanja Serikali inajenga wanapewa floor za Juu harafu floor za Chini na vyumba vya Kati inakuwa mali ya Serikali inaingiza pesa..

Hata hao watoke kwenye huo umaskini wakapewa viwanja vizuri nje ya Mji na Fidia harafu hayo maeneo yako potential yaendelezwe serikali ipige pesa.
 
Sasa hizo ni nyumba au takataka? Walitakiwa waondolewe kitambo tuu maana wanachafua Mji..

Hao watu wa milimani Nina uhakika watakuwa wa kwanza kuitikia mwito maana watapewa maeneo mazuri yaliyopimwa na Fidia juu..

Nyanzaga Kule Sengerema wamehama kupisha Mwekezaji wa mgodi mkubwa dhahabu sembuse hao maskini wa huko milimani?
Babako bora angepiga nje tu aisee
 
Sasa hizo ni nyumba au takataka? Walitakiwa waondolewe kitambo tuu maana wanachafua Mji..

Hao watu wa milimani Nina uhakika watakuwa wa kwanza kuitikia mwito maana watapewa maeneo mazuri yaliyopimwa na Fidia juu..

Nyanzaga Kule Sengerema wamehama kupisha Mwekezaji wa mgodi mkubwa dhahabu sembuse hao maskini wa huko milimani?
Mwana umeandika kidharau sana..
 
Back
Top Bottom