GITWA
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 1,495
- 1,690
MTUNZI : SELOPHEADY H. MAGEMBE
HAKI ZOTE ZIMEHIFADHIWA
Huruhusiwi kunakili au kutumia sehemu ya hadithi hii bila ruhusa ya mwandishi.
Nilikua nimehitimu masomo ya shule ya upili na kuchaguliwa kwenda kusomea ualimu katika chuo cha ualimu.Hii ilikuwa ni miaka ya 1990 hivi, ualimu ni kazi ambayo haikuniingia akilini kuifanya hivyo niliamua kutoenda chuo cha ualimu na kufuata mfumo wa maisha ambao ni UBATILI.
1
Ilikuwa yapata saa mbili asubuhi wakati nilipopokea telegram iliyonihitaji kwenda Tabora, nilikumbuka miaka mitano iliyopita,wakati nilipoacha masomo na kujiunga katika kikundi cha wizi kinachoitwa “COOL BLOOD”.Hiki ni kikundi chenye matawi mengi mikoani pamoja na matawi yake ya kitapeli,hii telegram ilitoka katika mojawapo ya ofisi hizo mkoani Tabora. Nilijaribu kubashiri ni kazi gani naitiwa lakini sikupata jibu la moja kwa moja kwani kulikuwa na aina nyingi za kazi nilizowahi kuzifanya chini ya kikundi hiki. Nilikumbuka jinsi nilivyotumwa kwa mara ya mwisho na ofisi iliyoko Musoma, kwenda Nairobi kutoa roho za watu watatu ambao hawakutakiwa kufika mahakamani kutoa ushaidi. Ilikuwa ni pata shika nguo chanika kwani watu wenyewe walikua maarufu na wana ulinzi wa nguvu.
Ghafl a nilirudisha mawazo yangu kwenye ujumbe niliopokea nilirudia kusoma ile telegram na kuona kuwa niliitajika kuripoti Tabora kabla ya kupita siku tatu kuanzia siku ya leo.Kutokana na usafiri ulivyo kutoka hapa Ukerewe kwenda Tabora ni safari isiyochukua zaidi ya siku mbili. Hivyo niliamua kuanza safari yangu hapo kesho jumapili.
Niliangalia saa yangu ya ukutani iliyokuwa ikipiga kelele majira haya ya alfajiri, ilionyesha kuwa ilitimia saa kumi na mbili kamili. Nilitoka kitandani na kuwasha jiko linalotumia mafuta ya taa tayari kwa kuchemsha maji ya kahawa.Baada ya hapo niliingia katika chumba changu cha mazoezi na kuanza kuupasha mwili kwa mazoezi ya viungo,kubeba chuma kidogo kwa ajili ya kuupa mwili nguvu pamoja na mazoezi mengine kama kuvuta na kutanua spring na kujinyoosha kwa kutumia kitairi kidogo. Ilipotimia saa mbili na nusu nilikuwa nimemaliza kufungua kinywa,kuoga pamoja na kupanga mizigo yangu katika begi maalumu la safari.
Nilianza safari yangu kwa kuelekea forodhani kukata tiketi huku begi langu nimeliacha nyumbani, kwani nilijua saa ya kuondoka meli hapa kwetu kisiwani Ukerewe ni saa saba mchana, hivyo niliamua kuacha mzigo nyumbani kwani kwangu na forodhani sio mbali ni mwendo wa dakika kumi kwa mguu. Nilipofika forodhani niliingia moja kwa moja katika chumba cha kukatia tiketi. Sikuwa na haja ya kujipanga katika foleni ya kukata tiketi kwani mkatisha tiketi tulielewana sana.
“Habari za asubuhi ndugu James” Nilimsalimu baada ya kukuta akigonga mihuli na tarehe katika tiketi.“nzuri” Alijibu na kuuliza “ Vipi mshirika wangu unasafiri leo nininini”“Ndio ndugu yangu unajua, unajua miangaiko ya tumbo ndio mingi” nilijibu na kuendelea “Naomba unupatie tiketi ya Tabora” Nilisema.
“Samahani Mr Pheady, tiketi za moja kwa moja kwenda Tabora zimekwisha zipo za Dodoma na kuendelea” Alisema.
“Haidhuru nipe ya Dodoma, ni shillingi ngapi?”
“Shilingi elfu moja na mia mbili” alijibu huku akiongezea na utani “Naona safari hii unaenda kutengeneza pesa sio za utani”
“Ha! Wapi ndugu yangu ni shida tu ndizo zinazotusumbua”“Shida wapi? Wakati mwenzangu unapendeza “ Alisema huku ananipatia tiketi.
“Nashukuru” Nilimwambia wakati nampatia pesa na kumtakia kazi njema naye alinitakia safari njema.
Nilishika barabara ya boma na kuanza kutembea, nilipofika Fora Hotel niliamua nipumzike kidogo na kupata soda baridi. Nilirudisha mawazo yangu katika kazi niliyoitiwa nilihisi sio kazi ya kawaida kutokana na hisia zilizopita kichwani mangu. Lakini la ajabu kama ninavyoelewa ofisi ya Tabora hushughurika hasa na mipango ya “kibeshi” yaani utendaji wake wa kazi ni mzuri hauna sekeseke yoyote, hutumii nguvu ni uongo mwingi unapata pesa bila haja ya kukunjiana ngumi.
Hivyo hizi hisia zilizokuwa zinakuja zilikuwa kama kitendawili mawazoni mwangu.
Nilpoangalia saa yangu ilinionyesha saa tano na dakika ishirini na nane,nililipia soda niliyokunywa na kuanza kuondoka kuelekea nyumbani ambako ni barabara ya Msoma.Nilichukua mzigo wangu na kuanza kuondoka, nilipofika mlangoni nilikumbuka saa moja pamoja na ringi ya mkononi ambayo nilipewa na jasusi mmoja aliyenifindisha kutumia silaha pamoja na michezo ya kareti na judo. Nilirudi na kufungua kabati ninayotunza vitu maalumu na kuchukua vitu hivyo na vingine nilivyoona ni muhimu.
Zilikuwa zimesalia dakika kumi meli iondoke wakati nilipochukua nafasi inayonifaa na kukaa,ilikuwwa ni baada ya kutoka nyumbani na kupita nyumba mbili tatu na kuaga ndugu zangu huku nikikabidhi uangalizi wa nyumba yangu kwa mmoja wao. Niliposhuka forodha ya Mwanza niliongoza moja kwa moja hadi stesheni kwani kulikuwa na treni jioni hiyo.
Niliwekewa namba ya behewa na ya kiti katika tiketi yangu na kuondoka maana mda wa kuondoka ulionyesha nina saa mbili za kusubiri.Nilipita madukani na kufanya window shopping kama wasemavyo waingereza,sikuwa na lolote muhumu hapa Mwana.Ilipotimu saa moja kasorobo nilikuwa tayari ndani ya treni nikisubiri kuondoka tayari kwa kazi ninayoitiwa.
…………………………………………………………………………………………….
Ilikuwa majira ya alfajiri wakati treni ilipofika Tabora, niliondoka stesheni na kuelekea Tabora Hotel kwani ipo karibu tu na ni hotel inayonifaa kwa kua ina hadhi ya kitalii. Nilimkuta mtu wa mapokezi akiawa anaelekea kulemewa na usingizi.
“Habari za saa hizi dada?” Nilimsalimia.
“nzuri kaka, karibu, nikusaidie nini?” Aliongea huku akipanusa uso wake kwa leso.
Nilikuwa sijamwangalia vizuri sasa ndio nilibaini kuwa ni mzuri wa sura,sikujua umbile lake kwani alikua amekaa.
“Nahitaji chumba” hatimaye nilijibu.
“vyumba vimebaki viwili vyote double”
Kutokana na jinsi ambavyo sikupenda Hotel za uswahilini niliamua kuchukua kimojawapo nitabadiri endapo kuna mtu atatoka katika chumba single.
“Nipatie kimoja ambacho utaona kinanifaa”
“Kipo kinachoangalia shule ya upili nadhani kitakufaa” Alisema.
“Ok, kanionyeshe”
Nililipa malopo ya chumba na kuondoka kuelekea chumbani, tuliongozana na huyu msichana mimi mbele yeye nyuma yangu huku akiwa amebeba mzigo wangu.Tulipofika njia panda ya korido nilifuata njia isiyo sahihi, nikamsikia akisema,”kaka umekosea,sio huko”
“Du! Unajua kitu ambacho hukijui ni sawa na usiku wa giza” Niliongea huku nikimfuata nyuma yake.
Nilipokuwa nyuma yake ndio niliweza kuona uzuri wa umbile lake,ukilinganisha na uzuri wa sura yake niliyoiona wakati naingia ni dhahiri kuwa nilikua naongozana na kiumbe mzuri kiasi kuwa ndugu msomaji kama wewe ni we kiume na rijali ungependa kuwa na uhusiano naye zaidi ya ule wa kawaida, ila kwa kuwa nilikuja kikazi sikutilia maanani mawazo hayo zaidi ya kumsifu Mwenyezi Mungu kwa uumbaji iliotukuka.
Hatimaye tulifika kwenye chumba na kukifungua huku akisema”Chumba ndio hiki natumaini utakifurahia”
“sitaweza kukifurahia iwapo nitaendelea kukaa peke yangu bila mtu wa kuniliwaza” nilimtania.
“Kwa jinsi unavyoonekana sidhani kama mabinti wa Tabora watakuruhusu ulale peke yako” Alisema
“Labda! Nilisema na kuendelea, vilevile sitajisikia raha iwapo hatakuwa mtu aliyeushitua moyo wangu” Nilisema huku nikikaa kwenye sofa iliyokuwa pembeni ya kitanda. “Samahani dada pamoja na kunihudumia ningependa kujua jina lako yamkini nikapata shida itakayohitaji msaada wako”
“Naitwa Saumu” Alijibu huku akiwa amesimama mlangoni.
“Jina zuri sana,unatoka kazini saa ngapi?” Niliendeleza maongezi.
“natoka saa nne asubuhi hii” Alisema.
“Ok, kazi njema” Nilimwambia
“kwa heri” Alisema akiwa nje ya mlango.
Sikumjibu kwa kuwa sikupendelea kuongea na mtu nisiyemuona.
Nlilipoangalia saa yangu ilinionyesha saa kumi na mbili kasoro dakika tano.Niliamua nipumzike mpaka saa mbili kwani nilikua na uchovu wa safari. Nilishituka usingizini saa mbili na robo,mawazo na akili yangu viliamia kwenye kazi niliyoitiwa. Niliondoka kitandani na kuliendea dirisha, niliona wanafunzi kwa wanafunzi mbali,nilitoka dirishani na kuelekea bafuni kuoga na ilipotimu saa tatu kamili nilikua tayari kuelekea ofisini. Nilichukua sigara na kuasha wakati huo lilinijia wazo hivyo nilichukua simu iliyokuwa mezani na kuzungusha namba za ofisi yetu ya hapa Tabora. Simu ilinyanuliwa upande wa pili.
“Halo nani mwenzangu?” Nilisikia sauti nzito
“Pheady” Nilijibu.
“Unaongea toka wapi” Sauti iliendelea.
“Mwanza” Nilidanganya.
“Hujapata ujumbe wowote wa kukuitaji toka kwa Chata”
Kwa jinsi ninavyoelewa Chata ndiye mkuu wa ofisi hii ya Tabora.
“Sikiliza ndugu, kabla hatujaongea zaidi ningependa kujua ninae ongea naye” Nilisema.
“Unaongea na Mr Kikakika” Alijibu.
“Ok. Vp mwenzangu una fununu zozote kuhusiana na huo ujumbe” Niliuliza.
“Sijui lolote hata mimi nimeitwa kama wewe na nilifika hapa jana sikuambiwa lolote zaidi ya kuambiwa wewe”
“Sawa, mimi nitafika hapo ofisini mida ya saa tano”
“ Sawa” Alijibu bila kufikiri.
“Kwa heri” Niliaga na kukata simu.
Mara nilianza kumfikilia Kikakika,nilikumbuka ujasiri wake kwani niliwahi kufanya naye kazi Kampala Uganda.
Niliondoka chumbani baada ya kuhakikisha kuwa vitu vyangu vyote nilivipanga katika mpangilio wa tahadhali.Nilipofika kaunta nilimkuta Saumu akijiandaa kutoka.
“Vipi Saumu? Uliniambia unaondoka saa nne, inakuwaje haraka yote hii saa tatu tu?” Nilimshitua baada ya kuona anaweka mfuko begani.
“Ohoo!!” Alishituka kwani alikuwa hajaniona, “Naona imekuwa bahati kwani mwenzangu amekuja kunipokea” Alisema.
“ Je? Tunaweza kuongozana.” Niliuliza.
“Kama hutaona usumbufu, kuna sehemu napitia kwanza kabla ya kufika mjini” Alisema.
“Unafikiri utatumia mda gani kabla ya kufika mjini?”
“Kama saa moja na nusu hivi.”
“Hakuna tabu tunaweza kuongozana” Nilieleza.
“Rose!!” Alimuita mwenzie aliyekuwa kwenye chumba cha wahudumu.
“Unasemaje? Rose aliitikia kwa njia ya swali”
“Mimi naondoka tutaonana kesho”
“Sawa shoga yangu” Alijibu huku akiwa chumbani.
Tuliondoka kaunta tukiongozana mpaka tulipofika maegesho ya gari nikachukua taxi.
Ilikuwa ni saa tano kasoro dakika kumi na mbili nilipofika ofisini, nilimkuta Chata akiwa amekaa na Kikakika pamoja na kijana mwingine wa kishombeshombe.
“Habari zenu, niliwasalimu kwa pamoja”
“Shikamoo” Nilimsalimu mzee Chata huku nikivuta kiti tayari kwa kukaa.
“Marahaba kijana, habari za safari? Alijibu na kuuliza.
“Sio mbaya maadamu Mungu anasaidia” nilijibu.
“Nimesikia taarifa ako kutoka kwa Kikakika kuwa utafika sasa hivi, hivyo inabidi mnisikilize kwa nyote makini” Alisema mzee Chata na kuendelea.
Kutokana na taarifa zilizopo hapa kutoka Head office mnatakiwa wote mkafanye kazi mjini Mwanza, alinyamaza na kutoa sigara akawasha.Wakati huo mawazo yaliniruka kwani sikupenda kufanya Mwanza hasa ukizingatia kuwa ni mkoa wa nyumbani hivyo nilifahamika kwa watu wengi. Nilitoka kwanye mawazo yangu baada ya kusikia mzee Chata akiendelea kuongea.
Kuna tajiri mmoja aitwae Sule Catto mwenye kiwanda cha kuunganisha radio ambaye hufanya biashara ya madini ya dhahabu kwa siri na kupeleka Japani na ndio kiini cha utajiri wake hata serikali haijashituka. Kutokana na habari tuluzozipokea, anategemea kuondoka juma mosi ya wiki hii kupeleka dhahabu yenye yenye thamani ya bilioni mia tano. Mnachotakiwa ni kuchukua hizo dhahabu, alinyamaza na kutuangalia usoni mmoja baada ya mwingine kama mtu ayesoma mawazo yetu.
Namna ya kuzipata mtajua wenyewe ila jinsi zinavyosafilrishwa ni kama ifuatavyo; Wananuliwa samaki na kuondolewa minofu badala yake hujazwa dhahabu kulingana na uzito alafu zinashonwa na kukaangwa tayari kwa kusafirishwa.Sasa ni juu yenu kuangalia ni wakati gani unaofaa kuzichukua. Mr Catto mwenyewe anaishi Isamilo nyumba namba 72 imezungushiwa uzio wa michongoma na seng’enge ambazo hutegeshwa nyaya za umeme. Vilevile ndani kuna ulinzi wa mbwa wanne. Je mpaka hapo kuna mtu mwenye swali? Alimaliza kwa kuuliza.
“Umesema anaishi Isamilo, Je hana familia hapo nyumbani? Aliuliza Kikakika.
“Tofauti na walinzi watatu kuna vijana wawili ambao ndio huandaa samaki na kupakia dhahabu tayari kwa safari. Mke na watoto wake wanaishi Nyakato. Nafikiri nyumba ya Isamilo ni maalumu kwa shughuli zake nyeti.” Alisema Kikakika.
“Ina maana hao vijana wanaoshughurika na samaki wanaelewa siri yake au?” Nilisahili.
“Haswaa, wanaelewa lakini sio rahisi kumsaliti maana wanalipwa donge nono, vilevile inasemekana ni ndugu zake.
“Sawa mpaka hapo tumekuelewa” Tulisema kwa pamoja.
Mzee Chata alivuta saraka ya meza na kutoa bunda la pesa ambazo alizigawanya laki tano tano kwa kila mtu. Kwa miaka hii ya Tisini zilikuwa ni pesa nyingi sana.Baada ya hapo alitoa bastola tatu zenye viwambo vya kuzuia sauti pamoja na magazine tatu tatu kwa kwa kila mtu. Baada ya kupokea kila kitu na kuweka sehemu salama, alitueleza turudi saa nane kuchukua tiketi zetu za safari ya Mwanza.
Palepale lilinijia wazo nikaamua nifanye kama akili yangu inavyojua. “Lakini mzee mimi ningependelea nichukue pikipiki ndio niondoke nayo ili iweze kuturahishia kazi hapo baadae.” Nilieleza.
“Sawa kabisa” Aliongea yule Chotara.
“Sawa nitashughurikia utaikuta tayari” Alisema mzee Chata na kuendelea kueleza kuwa “ Ndugu Pheady utakuwa mkuu wa msafara vilevile itabidi niwape gari badala ya kutumia usafiri wa public. Nadhani itakuwa njia nzuri kutekeleza majukumu yenu kwa urahisi. Sonno na Kikakika njooni baada ya masaa mawili mtakuta gari tayari.”
Tuliagana na mzee Chata, sisi tuliongozana kutoka nje na tulipofika nje tuliagana na wezangu kila mtu akaendela na shuguli zake huku tukiwa tumeahidiana tukutane juma tano Vijana Social Hall Kirumba Mwanza tayari kwa maandalzi ya kazi.
2
Ilkuwa saa tatu kasoro robo wakati nilipopaki pikipiki nje ya ukumbia wa Vijana Social Hall, nilisikia kelele za mziki wa disko pamoja na watu wakishangilia. Nilikata tiketi ya kuingia ukumbi wa disko na kuingia ndani, nilitafuta kona nzuri itakayoniwezesha eneo lote kwa urahisi. Niliagiza chupa ya konyagi baada ya muhudumu kuniletea nilianza kunywa huku nikiangalia wanaocheza disko.
Nilikuwa nimekaa zaidi ya nusu saa huku nikiangalia uwezekano wa kuwaona akina Kikakika, mara ghafla nilisikia naguswa begani kwa nyuma. Niligeuka na kukutanisha uso na Sonno.
“Ohoo!! Mr Sonno habari za siku?” Nilisaili
“Salama tu, sijui mwenzangu vipi?
“Kwangu poa, nimefika salama” Nilijibu.
“Sasa inabidi tutafute sehemu inayotufaa tujadili mambo yetu “ Nilieleza na kuendelea kuuliza “Kikakika yuko wapi?
“Yupo katika chumba cha faragha huko pembeni” Alijibu.
“Basi twende tukaongelee huko.” Nilieleza huku nikinyanyua chupa yangu ya konyagi tayari kwa kuondoka.
“Hapana, inabidi nimwaendee Kikakika tukaongelee sehemu nyingine, kwani kule kuna wasichana hivyo hapatufai.”
“Sawa kamuite, alafu wambie hao wasichana wenu wawasubiri kwani hatutachukua mda mrefu.” Sonno aliondoka akiniacha nikimimina konyagi kwenye bilauri, nilimimina pombe yote iliyokuwa imebaki kwenye chupa na kuinywa kwa mkupuo. Baada ya hapo niliwasha sigara na kuanza kuvuta taratibu.
Sonno na Kikakika walinipitia tukaongozana mpaka kwenye gari lao,niliamua kuacha pale pikipiki kwani nilijua tutawahi kurudi. Sonno alishika usukani nikamwambia aongoze moja kwa moja mpaka Msufini Restaurant iliyoko Nyamanolo kwani ndio nilitegemea kuchukua chumba.
“Vipi mmechukua vyumba wapi? Niliuliza.
“mimi nipo Mwanza Guest namba kumi na mbili na Sonno yupo Nsimbo namba thelathini na tatu.” Alisema Kikakika.
“mmefanya vizuri kuchukua guest tofauti,mimi nataka nikachukue chumba hapo msufini. Tulikuwa tumekata kona kushika barabara iendayo AIR PORT hivyo nilionelea huu ni wakati wa kutoa mikakati ya kazi. Sasa inabidi tufanye kazi iliyotuleta, nafikiri mnaelewa ninachoongelea” Nilieleza.
“Ndiyo” Walijibu kwa pamoja huku Sonno akipunguza mwendo.
“Kesho kuanzia saambili na nusu mnatakiwa muwe kiwandani kwake ili kuweza kufanya uchunguzi kabla ya vitendo, kwani ukitaka vitendo vipendeze jua nyendo za mtu umtakaye.Mukifika mtahitaji kuongea naye kwa ajili ya kununua radio kwa bei ya jumla ili nanyi mkauze kwa bei ya jumla. Katika maongezi yenu hakikisheni mnatumia ujanja wowote kujua kama juma mosi atakuwa na safari.Kesho ni Alhamisi na kufikia ijumaa tunatakiwa tuwe na mpango kamili wa kazi. Mimi nitaanza kufatilia nyendo zake kuanzia asubuhi akingali nymbani kwake hivyo tutaonana saa saba River Side kwa ajili ya chakula cha mchana. Nafikiri mmeelewa kipi mnachotakiwa kufanya pamoja na kuwa nimeeleza kwa kifupi.”
“Bila shaka” Alijibu Sonno huku akitabasamu.
“Ikibidi kuionana kabla ya hizo saa basi tuonane Mwaza Hotel, nadhani patakuwa mahali pazuri pa kupotezea muda.” Niliongezea.
“Nilitaka kuuliza swali lakini naona jibu lake umeishanipa. “Aliongea Kikakika huku gali likikata kona kuingia mwisho wa safari yetu.Sonno alielekeza gari mpaka maegesho ya Msufini Restaurant ndipo tukashuka.
“Ngoja sisi tuingie kwanza bar tupate bia moja moja wakati wewe unaendelea na shughuli zako.”Alieleza Sonno.
“Sawa nami nitapata moja kabla ya kuchukua chumba” Nilisema huku tukiwa tunaingia mlangoni pa bar.
Tulikaa baada ya kupata viti katika meza moja iliyokuwa pembeni ya bar ikitazamana na dirisha. “Tuletee safari tatu baridi” Aliagiza Sonno baada ya muhudumu kufika. Wakati muhudumu anaondoka kufuata vinywaji nami niliondoka kwenda kupata chumba sehemu ya guest.
“Habari za saa hizi?” Nilimsalimu muhudumu baada ya kumkuta akiandika stakabadhi za nyumba ya kulala wageni”
“Salama kaka, Karibu tupo.” Alijibu.
“Naitaji chumba, je nimepata?” Nliuliza.
“Bila wasiwasi, vipo vyumba vitatu bado” Alijibu.
“Naomba kimoja kizuri” Nilieleza naye alinyanyuka na kuniongoza kwenda kuangalia. Tuliongozana mpaka chumba namba ishirini na na saba, alinifungulia nikaangalia kilikuwa chumba chenye kuridhisha. Nilimlipa pesa yake huku nikiwambia kuwa nitapititia stakabadhi hapo mapokezi.
Nilikikagua vizuri chumba baada ya muhudumu kuondoka,baada ya ukaguzi wangu niliondoka na kupitia stakabadhi yangu mapokezi na kuongoza moja kwa moja bar ambapo niliwakuta Kikakika na Sonno wakiwa wanamalizia bia zao.Nilikunywa bia yangu haraka ili nisiwachelewashe jamaa zangu kwa wasichana wao.
Ilikuwa imetimu saa nne na nusu wakati tulipokuwa tumefika Vijana Social Hall na kuwakuta wasichana wa akina Sonno wakicheza mziki.Tulichagua meza tukakaa na kuagiza vinywaji, baada ya wimbo wa Nakei Nairobi kwisha wale wasichana waliangaza angaza baada ya kutuona walikuja na kuvuta viti vilivyokuwa wazi katika meza yetu na kukaa. Walikuwa wawili.
“Habari za saa hizi kaka” Walinisalimu kwa pamoja.
“Nzuri, je wenzangu mna khali gani?” Nilijibu na kuuliza.
“Salama tu” walijibu.
“Samahani” Alikatisha Sonno. Inabidi niwatambulishe, huyu ni rafiki yetu anaitwa Pheady na ni mfanya biashara vilevile na ndie kiini cha safari yetu kwani yeye ni mwenyeji wa Ukerewe. Aisee Pheady hawa ni Zinduna na rafike Mtuli. Ni wenyeji wa hapahapa Mwanza. Sonno alimaliza kutambuilisha.
“Nafurahi kufahamiana nanyi” Nilisema huku tukipeana mikono. Baada ya hapo Kikakika aliagiza vinywaji tukaendelea na kunywa. Ilipotimia saa sita kasoro robo niliwaaga huku nikiwakumbushia umuhimu wa kazi, nilipita maegesho nikamuaga mlinzi na kuchukua pikipiki yangu na ilipotimu saa sita na nusu nilishamaliza kupanga vitu vyangu chumbani na kuelekea kuoga tayari kwa kulala.