Wabunge Dr. Slaa na Dr. Tarab wafanyiwa umafia!

unapenda sana kutoa maagizo! Sijui kwanini!?

Napenda kutoa maagizo sababu maagizo ndiyo yanayofaa siku zote.Enzi za Mwalimu watu walikuwa wakipewa maagizo na kuyatekeleza ila kwa saasa watu wengi wameuwa wakifanya wanavyotaka wao bila kutekeleza maagizo.

Inawezekana ni tabia yako au ya mwingine kutopenda Maagizo.

Invisible nimekusoma Mkuu,Nilitumia jina lako makusudi ili kuweka mambo sawa sababu wachangiaji waliokuwa wakifuatilia mtiriko kutoka kwako hadi kwa Mzee Mwanakijiji walikuw akienda nje kidogo ya jambo lenyewe!
 
Mkuu Gembe,

Ninapoandika hivi sasa ITV wanaonesha kilichotokea na Polisi naambiwa hawajapinga wala kutoa statement yao juu ya kilichotokea.

Iwe ni usanii wa Slaa ama vinginevyo, wajibu wangu ilikuwa ni kuifahamisha Jamii juu ya kinachoendelea katika jamii yetu ndani ya Tanzania.
 
dr slaa na dr taarab wabunge toka vyama vya upinzani wamekuta wamewekewa majidude ambayo yanasadikika ni vinasa sauti kwenye vyumba vya hoteli walipofikia mjini dodoma.
hoteli hiyo ipo jirani kabisa na ukumbi wa bunge
alipoulizwa meneja kasema yeye anashangaa labda ni MIUJIZA!
 
Kama ilivyojiri leo bungeni katika kuchangia muswada wa sheria ya vyama vingi yafuatayo nimeyaona ni muhimu sana kwa ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi hapa nchi pia kwa mustabali wa nchi yetu tuipendayo ya Tanzania.

1. Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa.
-ni vyema akawa mtu mwingine na si msajili wa vyama kama ilivyopendekezwa kwenye muswada na ni vyema hawa na taaluma ya sheria(majaji wastaafu) kwani kazi kubwa mojawapo ya baraza hilo ni kumshauri msajiri wa vyama vya siasa nchini.
-Vile vile ni haki kabisa kuipa meno ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kama ilivyopendekezwa ktk muswada huu.

2. Kiwango cha elimu kwa wagombea.
--Ni suala muhimu sana kwa sheria hii mpya kuspecify viwango vya elimu kwa wagombea wanaoshika dola au kuwawakilisha wananchi kupitia vyama vya siasa.hii ni kutokana hali halisi ya maendeleo ya sayansi ,uchumi na technolojia yanayotokea ulimwenguni,na kujua kusoma na kuandika tu haitoshi

3. CAG

-Sasa utakuwa ni wakati muafaka wa kuondoa wingu na wasiwasi ulikuwepo na unaondelea kuhusu ni wapi vyama vya siasa vinatoa fedha za kampeni na jinsi gani vyama vya siasa vinavyotumia ruzuku toka serikali.

4. Demokrasia ndani na nje ya vyama.
Sheria hii mpya sasa itawezesha kupanuka na kukua kwa demokrasia sio tu nchini bali ndani ya vyama vya siasa kwani kwa mtazamo wangu haiwezekani chama cha siasa kikawa na mwenyekti mmoja toka kianzishwe mpaka sasa.

Sasa naamini Nchi yetu inaelekea pazuri kisiasa na kidemokrasia,napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza waziri ya nchi ofisi ya waziri mkuu(mh.marmo) pamoja na msajili wa vyama vya siasa nchi mh.Tendwa kwa kuandaa na kuwasilisha bungeni muswada huu muhimu kwa manufaa ya taifa letu.

Pia naunga mkono hoja ya mh.Zito ya kuwa na national consensus licha ya tofauti zetu kiitikadi ya vyama vyetu.

Nawatakia hekima na busara nyingi wabunge wote katika kipindi cha bunge leo jioni ili wajadili na kuupitisha muswada huu pamoja na marekebisho yenye tija kwa taifa letu.
 
Mkuu Gembe,

Ninapoandika hivi sasa ITV wanaonesha kilichotokea na Polisi naambiwa hawajapinga wala kutoa statement yao juu ya kilichotokea.

Iwe ni usanii wa Slaa ama vinginevyo, wajibu wangu ilikuwa ni kuifahamisha Jamii juu ya kinachoendelea katika jamii yetu ndani ya Tanzania.

nini ITV??
 
Lazima itakuwa kazi ya state security, ingawa kwa mkono halali wa serikali au mafisadi ili kumdhibiti jamaa...wanataka kujua nani anawasiliana na nani, anaongea nini etc ili kumtengenezea mazingira ya kumpa kichapo. Wenzetu wachina na warusi wanawatumia majasusi kuiba technolgy, sisi bado tunawajaza kwenye mabaa na mahoteli waangalie nani anachukua mademu wakali zaidi mana kama wangekuwa wanaangalia maslahi ya taifa, hali isingekuwa mbaya ilivyo.Wako busy na kufanya 'matakataka' na sio ku safeguard national interest
 
mtaambiwa kuwa "vyombo hivyo si vya kunasa sauti bali ni kwa ajili ya kuhakikisha joto la magodoro linabakia kuwa constant"! Atakayesema hivyo atakuwa Waziri Mkuu tena kwa uchungu wote na machozi yakimlenga "Dr. Slaa ni mtu muhimu sana, tumechoshwa kuona anatishiwa tishiwa hivyo kwa kutumia mbinu za kisasa tumemuongezea ulinzi na usalama. Sasa kama Watanzania wanafikiri sisi kumlinda Dr. Slaa ni kosa kubwa kulinganisha na yeye kuja kurudhika fine! Mungu atanisamehe na ninaomba mtusamehe"... atasema Waziri Mkuu..

Wabunge watasimama na kumpigia makofi. Vyombo vya habari vitaandika "Waziri Mkuu azikoga nyoyo za wabunge"

Mkuu hapa umeniacha hoi bin taaban
 
tuviachia vyombo vya dola vifanye kazi yake kwa kuviamini

Andrew, Nani alikwambia vyombo vyetu vya dola vinafanya kazi kwa ajili ya wananchi na kwa manufaa ya nchi?

Vinaitwa vyombo vya Dola= Vinafanya kazi za Dola= Kazi kuu ya Dola ni kuhakikisha Watawala wanashika hatamu za Uongozi kwa gharama yoyote.
 
Ninaona kama Mr Ndahani YOU HAVE A POINT HAPO.lakin bado NACHANGANYIKIWA ninapoliangalia hili tukio katika MULTI-DEMENSIONAL VIEW.kwamba KWANINI SERIKALI INATAKA KUUFICHA HUU UKWELI UNAOTAKA KUZUNGUMZWA?
.............kuna wakati naweza kuamini ni mbinu binafsi ZA MTAJWA
 
Kuna vifaa kama hivi vya kujikinga:

Description
Spy Camera Detector
Product Description :
1. Use for detecting spy camera
2. Wild-range: include 900, 1200, 1300MHz and 2.4GHz
3. Receiving sensitivity: 500MHz ~ 3GHz
4. Coverage range: 3 meter a radius
5. Signal O/P: red light LED flash
6. Battery: 3V. LR-44 x 2pcs
7. Outlook: keychain type are available,

Function:
1. Detective Area: A radius of 3 meter can precisely detect wireless signal of 900/12001300/2400 MHz.
2. Red LED Flash: The flashing frequency will increase when approaching to the target.
3. Touch-tone Design: Professional RF Detective design press the key only when detection is needed. Such a function can both save power and prevent interferences of mobile phone's signal.
4. Attach a Key Ring: Men can wear the key ring and women can wear it on the bag or wear it as a decoration.

Application:
1. Public place,dressing rooms,bathrooms or lavatories.
2. Hotel,dormitories,rooms or offices.
3. Any place that one needs privacy......

Description
Bug Detector

Product Description :
1. Use for detecting spy camera or bug detecting
2. Wild-range: include 900, 1200, 1300MHz and 2.4GHz
3. Receiving sensitivity: 500MHz ~ 3GHz
4. Coverage range: 3 meter a radius
5. Signal O/P: red light LED flash
6. Battery: 3V. LR-44 x 2pcs
7. Outlook: key chain type are available,customerdesigns are welcome

Function:
1. Detective Area: A radius of 3 meter can precisely detect wireless signal of 900/12001300/2400 MHz.
2. Red LED Flash: The flashing frequency will increase when approaching to the target.
3. Touch-tone Design: Professional RF Detective design press the key only when detection is needed. Such a function can both save power and prevent interferences of mobile phone's signal.
4. Attach a Key Ring: Men can wear the key ring and women can wear it on the bag or wear it as a decoration.

Application:
1. Public place,dressing rooms,bathrooms or lavatories.
2. Hotel,dormitories,rooms or offices.
3. Any place that one needs privacy......

Wanaohitaji kwa sasa wanaweza kunitumia PM. Nitaviweka vifaa vyote vya Security na Surveillance kwenye website siku za karibuni.
 
Tayari mamluki wameanza kazi ya kupindisha hizi habari zilizo wazi. MMetumwa na nani?????

Ukweli tayari unajulikana nani aliyepanga, aliyetekeleza, njia zilizotumika kufanya madudu yao. Na Dr, alishaambiwa muda mrefu kuhusu njama hizo, akakaa kimya asijeambiwa anataka kugombea URAIS kama Mengi, na alipofika na kuona kilichofanyika akauambia uongozi wa bunge, polisi, usalama na kuwaita wahandishi wa habari ili nao washuhudie ili lisije kupindishwa.
Waliohusika sasa wamaminyana map***u nani aliyemshitua Dr. Slaa.

Siku haitaisha ama wkend hii haitaisha mtasikia mtikisiko

wait and see. Mimi sina source ya info ni ``habari ya kutunga kama mlivyozoea kila mtu anakuja na habari ya kutunga``.
 
Mkuu Gembe,

Ninapoandika hivi sasa ITV wanaonesha kilichotokea na Polisi naambiwa hawajapinga wala kutoa statement yao juu ya kilichotokea.

Iwe ni usanii wa Slaa ama vinginevyo, wajibu wangu ilikuwa ni kuifahamisha Jamii juu ya kinachoendelea katika jamii yetu ndani ya Tanzania.

Sifa kubwa ya Ufalme unaofitinika ni kufanya mambo yanasababisha kuanguka kwa ufalme huo bila kujua. Hii inanikumbusha kisa cha Mfalme Nero wa Rumi (Roma) wakati Ukristo uliposhika kasi huko Italia. Baada ya kuwatafutia kila sababu ya kuwaangamiza na kuona kuwa haimsaidii bali unaendlea kwa kasi, aliamua kuuchoma moto Mji wa Roma na kuwasikingizia Wakristo kuwa ndiyo waliofanya kitendo hicho cha aibu. Lakini hatimaye Wananchi wakaamua kumgeuka na kumkimbiza kama mwizi na hatimaye kummaliza na hiyo ndiyo people power.

Nachokiona hapa ni kuwa lazima kuan watu ndani ya Serikali wanampinga JK kwa nguvu zote na wanafanya vitendo vya aibu ili kumuaibisha na kumdhalilisha JK mbele ya Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa, JK akiwaonea aibu basi ajue ni kwa hasara ya ufalme (utawala) wake mwenyewe. Lazima awatafute na kuwawajibisha watu hao waliofanya vitendo vya kuudhalilisha utawala wake na kuipaka nchi matope.
 
kwendoa kweli inabidi uchunguzi wa kina ufanywe kumbaini mtu au watu waliofanya tendo hilo,lakini mimi naamini kuwa hakuna mtiu anaeweza kuzuia vyombo vya dola kusikiliza au kurekodi mawasiliano ya mtu mpaka wafikie hatua ya kuweka vinasa sauti chini ya godoro,kwa msingi huo basi watakuwa ni wahuni fulani wamefanya hivyo na tena bila kushirikisha watu wenye hekima kwa faida zao binafsi.
 
wanasihasa hao wanacheza pilitiki hakuna kitu hapo
dr.tarab i know the dude personally was former biochemistry lecturer at muchs sasa leo sijui mbunge wa wapi manake sijamsikia popote akiongea chochote eti nae aje kuwa target ya mafisadi?

pengine si mfatiliaji wa matokeo ya bungeni lakini ungekwishamsikia. Kwa taarifa yako huyu ndie mhe pinda alisema hamtakii mema kwa kumuuliza suala bungeni. Mbali na jf pia soma magazeti yetu kwenye mtandao.
 
Wakulu Heshima Mbele,

Mpaka sasa sijapata Taarifa ambazo zinridhisha kuamini Dr. Slaa aliwekewa vifaa vivyo vya kurekodi sauti.Mambo mawili ambayo nasikitika tumeingia kwa mkumbo kwa mawazo ya kulia tu ni haya.

1.Kwanini tunashikilia Dr. slaa ndiyo amewekewa vifaa hivyo na watu ambao hawatuwafahamu ili khali inawezekana kabisa Dr. Slaaa na CHADEMA wakawa wameweka vifaa hivi kama kujitafutia Umaarufu.Hilo Linawezekana na ni moja ya mbinu za kisiasa ili watu waendelee kuamini kuwa unaweza kuleta Mabadiliko. Tusubiri uchunguzi na iiwezekana Mzee Mwanakijiji na Bongo Radio any mahojiano na wale wahudumu wa ile Hotel.

2. Kuanza kuhisi kuwa ni Masha ndiyo kafanya jambo hili, ama waziri kijana. Huu ni upotoshaji tena kwa hoja kwamba Masha alilipuliwa na Dr. Slaa. Kama tumefika katika siasa za chuki kama alivyosema Mzee Mkapa basi 2010 uchaguzi utakuwa ni wa aina ya ajabu kutokea katika Nchi hii.

Mzee Mwanakijiji na wengine hasa Invisible tuwe waangalifu sana katika Masuala kama haya na tusipende kutoa maamuzi mapema sana. Mpaka sasa niko kwenye msimamo wangu kuwa vile vifaa havijawekwa na mtu yeyote na nitafanya jitihada za kuongea na Mkuu wa upelelezi wa Mkoa wa Dodoma kujua ukweli.!

Gembe mbona unatokota? Unasema watu wamefata mkumbo na kudhani ni ni habari sahihi; wakati huo huo unajihakikishia kwamba detectors hazijawekwa na mtu yoyote? Zilishuka mbinguni? why ni kwa wabunge wawali?

Huyo kamanda hata ukimpata atakwambia tunafanyia utafiti then majibu ni forever!!!!
 
Sina haja ya kuhangaika kumtafuta 'mchawi' wa jambo hili. Wote waliohusika ni wapinga mmaendeleo yetu tu.Tutawahukumu wakati ukifika.
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 160 (41 members and 119 guests) Aljuniortz, AndrewMwanga, Bint, bob, Burn, Chief, Dr.W.Slaa, Hamad Yussuf, Hofstede, Kaduguda, Kamuzu, Kitia, Kwayu, M-bongo, MamaParoko, manundu, Mchana, MegaPyne, Mfuatiliaji, Midas Touch, Mkaa Mweupe, MkamaP, MKUDE WA MGETA, Mndundu, Mpita Njia, Mr. Politician, Mwamboni, Mwanamalundi, mwanazuoni, Mwanjelwa, mzeewadriver, NCHIMBI,J, Nenga, Nesindiso Sir, Next Level, Nikifufukammekwisha, njilembera, seleka, Severine, Sikonge
Jamani hapa namwona Dr Slaa naye yupo katika hii thread, Mheshimiwa utuhabarishe
 
Kama ilivyojiri leo bungeni katika kuchangia muswada wa sheria ya vyama vingi yafuatayo nimeyaona ni muhimu sana kwa ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi hapa nchi pia kwa mustabali wa nchi yetu tuipendayo ya Tanzania.

1. Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa.
-ni vyema akawa mtu mwingine na si msajili wa vyama kama ilivyopendekezwa kwenye muswada na ni vyema hawa na taaluma ya sheria(majaji wastaafu) kwani kazi kubwa mojawapo ya baraza hilo ni kumshauri msajiri wa vyama vya siasa nchini.
-Vile vile ni haki kabisa kuipa meno ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kama ilivyopendekezwa ktk muswada huu.

2. Kiwango cha elimu kwa wagombea.
--Ni suala muhimu sana kwa sheria hii mpya kuspecify viwango vya elimu kwa wagombea wanaoshika dola au kuwawakilisha wananchi kupitia vyama vya siasa.hii ni kutokana hali halisi ya maendeleo ya sayansi ,uchumi na technolojia yanayotokea ulimwenguni,na kujua kusoma na kuandika tu haitoshi

3. CAG

-Sasa utakuwa ni wakati muafaka wa kuondoa wingu na wasiwasi ulikuwepo na unaondelea kuhusu ni wapi vyama vya siasa vinatoa fedha za kampeni na jinsi gani vyama vya siasa vinavyotumia ruzuku toka serikali.

4. Demokrasia ndani na nje ya vyama.
Sheria hii mpya sasa itawezesha kupanuka na kukua kwa demokrasia sio tu nchini bali ndani ya vyama vya siasa kwani kwa mtazamo wangu haiwezekani chama cha siasa kikawa na mwenyekti mmoja toka kianzishwe mpaka sasa.

Sasa naamini Nchi yetu inaelekea pazuri kisiasa na kidemokrasia,napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza waziri ya nchi ofisi ya waziri mkuu(mh.marmo) pamoja na msajili wa vyama vya siasa nchi mh.Tendwa kwa kuandaa na kuwasilisha bungeni muswada huu muhimu kwa manufaa ya taifa letu.

Pia naunga mkono hoja ya mh.Zito ya kuwa na national consensus licha ya tofauti zetu kiitikadi ya vyama vyetu.

Nawatakia hekima na busara nyingi wabunge wote katika kipindi cha bunge leo jioni ili wajadili na kuupitisha muswada huu pamoja na marekebisho yenye tija kwa taifa letu.

Hii ya ''MUSWADA WA SHERIA WA VYAMA VINGI'' inakujaje hapa? mbona tunachanganyana?
 
Back
Top Bottom