Wabunge CCM wamlipua Kikwete, WADAI WANAKERWA JINSI RAIS ALIVYOMGEUKA PINDA, MAKINDA

Ama kweli wabunge wa ccm uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana!wanafanya mambo kishabiki ma dc na ma rc wote ni UWT
 
JK ana kazi nzito mbeleni kwa style hii!!hivi Posho zingepitishwa hawa wabunge wangeandaa haka kamgomo baridi??
 
rais kawafanya wajinga,watu wakupitisha tu,wanapitisha anabadili,watapitisha atabadili hii haiwezekani si kwamba mabadiliko ni mabaya bali,jinsi alivyohandle jambo lenyewe
 
JK ana kazi nzito mbeleni kwa style hii!!hivi Posho zingepitishwa hawa wabunge wangeandaa haka kamgomo baridi??
Unajua wanachokilalamikia zaidi ni kwamba JK amekuwa akiachia mambo yanatokea na wakubwa wenzie wanatoa maamuzi fulani halafu ye anakuwa against na wao pamoja na kuonekana walikuwa pamoja mwanazoni, hivyo kuonekana kigeugeu. Unakumbuka habari ya Jairo na Luhanjo? Posho ambayo PM alisema JK ameshasaini? Halafu hii ya muswada
 
Magamba wanaangalia maslai yao ktk swala la katiba. Likija swala linalofaidisha umma kwa ujumla wako radhi waharibu kisa hawataki kutoka madarakani. Posho ndio imewapagaisha wamechukia wanakataa hata vitu vya msingi.siku inakuja stupid magamba mtatoka madarakani
 
Aaah kumbe habari za makanjanja. Nilifikiria umetoa kutoka chanzo cha kuaminika.

Hii nayo ni Mwananchi ya leo:
Kura ya kukosa imani na Rais
Katika kikao cha wabunge hao kilichofanyika Alhamisi wiki hii, baadhi yao walihoji sababu zinazokwamisha masuala mbalimbali serikalini kutopatiwa ufumbuzi, huku Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo, akipendekeza kwamba kama tatizo ni Rais Kikwete, watumie utaratibu wa kumpigia kura ya kutokuwa na imani.

Shelukindo anadaiwa alitaka kujua sababu za masuala mbalimbali kukwama na kutopatiwa ufumbuzi wa haraka na kwamba, iwapo tatizo ni Rais Kikwete, wapo tayari kufuata utaratibu wa kumpigia kura ya kutokuwa na imani.

Hata hivyo, Mbunge wa Simanjiro, Christopher Olle Sendeka, alisimama na kumtaka mbunge huyo kufuta kauli yake, suala ambalo Shelukindo alikubali.
 
Hivyo ndivyo tunavyotaka wananchi, mambo ya kutudanganya mnajadili hoja bungeni wakati mumeshafikia mwafaka kwenye vikao vya ndani hatutaki mnatuboa. Kwani tunajiuliza inakuwaje kwenye mambo nyeti ya kitaifa wabunge zaidi ya 300 kupitisha hoja ya hovyo na yenye kuleta athari mapema. Wangefanya hivyo tungeona wameanza kula unga wa rutuba.
 
ccm nafiki huu ndio mwisho wake umefika kwa maana rais ameanza kujua umuimu wa Cdm kwakuwa magamba yapo tuu kwa ajili ya posho sio kwa maslai ya taifa
 
Unajua kumekuwa na ile notion ya kuwazomea na kuwacheka wabunge wa CDM wanapotoka nje ya bunge kwasababu ya kutosikilizwa au kuonewa kwa namna tofauti, sasa nahisi kwa haya nao wameona namna inavyokuwa pale unapoonewa
 
Kwani hiyo habari ipo kwenye tanzania daima tu mkuu?mbona hautaki kusumbua ubongo wako hata kidogo??amka kumekucha

Nitashawishika kama habari hii itakuwa na kwenye magazeti mengine! Tanzania Daima linakuwa kama gazeti la Uhuru sasa
 
Nitashawishika kama habari hii itakuwa na kwenye magazeti mengine! Tanzania Daima linakuwa kama gazeti la Uhuru sasa


Pekua Gazeti la Mwananchi la leo...vp Fr?au J'pili imekuchanganya kwa makusanyo madogo ya sadaka?fuga ata nguruwe kama mradi...utajiongezea kipato!Christus Semple
 
Hawa si walikataa mgomo wa madaktari ujadiliwe bungeni? Kitu gani kinawafanya watake wenzao wajiuzuru? AU POSHO?
 
Hv na mama lwakatare pia atamgomea jk ama ndo kupaka rangi hewa.
 
Kikwete hajui tena nini cha kufanya, ameharibu kwa wananchi, amewatibua wabunge wake-hawamtaki, amemgeuka waziri mkuu wake, amebaki sio moto wala baridi..Asubiri sasa inaanza kum-cost, siasa za kuotea na ujanja ujanja kwishney...I SWEAR MWISHO WA KIKWETE HAUKO MBALI,
 
Back
Top Bottom