Wabunge CCM wamlipua Kikwete, WADAI WANAKERWA JINSI RAIS ALIVYOMGEUKA PINDA, MAKINDA

Hali ya wabunge wengi wa CCM sasa ni tete baada ya kugundua kuwa vitendo vyao vya kuunga mkono kila hoja inayotolewa na serikali hata kama haina tija kwa Taifa ni usaliti kwa wananchi waliowachagua. Hii ni baada ya serikali kuirudisha bungeni sheria waliyoipitisha ya mabadiliko ya katiba ili ifanyiwe marekebisho hata kabla ya kufanya kazi! Wanaweweseka kwa nini hawakuweza kutumia akili na busara zao wakati muswada wa sheria hiyo ulipoletwa bungeni kwa mara ya kwanza na badala yake wakatumia muda huo kuwapiga vijembe wabunge wa CHADEMA na kuupitisha muswada huo kishabiki! Wanamlaani JK kwa kukubali maombi ya CHADEMA na wanaharakati wengine kuifanyia marekebisho sheria hiyo kabla ya kuanza kutumika.

Aidha wanahofu kubwa kuwa hivi sasa watumishi wengi wa serikali wanaunga mkono CHADEMA ni hivyo wanatarajia kuwashawishi wakuu wa wilaya wahakikishe wanawadhibiti kikamilifu watumishi wa serikali ili kupunguza nguvu za CHADEMA. Hivyo wanataka Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya wasipewe majukumu yo yote katika mchakato wa kuandaa katiba mpya na badala yake majukumu hayo wapewe wakuu wa wilaya!
 
Ni upotoshaji na hisia binafsi za mwandishi , siyo kilichosemwa na wabunge hao.
Inawezekana ukawa upotoshaji kweli, sasa si wewe utwambie kilichosemwa cha kweli ni kipi? Au ndio ubishi wa kurithi huo kwasababu tu unachokiona sio unachopenda kukiona?
 
Wabunge wa CCM wanamgomea Rais kwa sababu naye aliwagomea kusaini nyongeza ya Posh!!. Acha wakomoane, wakoboane, wavuane magamba na ngozi lakini mwisho wa vita vya panzi kunguru ( wananchi) ndio tutafaidika. Mfumo uliowekwa na Masisiem wa kutawala kwa posho na kudai rushwa, utawatokea puani safari hii!
 
Nilisoma habari hii kwenye Tanzania Daima ya jana lakini niliona kama watu walikuwa hawana uhakika nayo just because ilikuwa imeandikwa na gazeti lile. Sasa nilipoisoma kwenye hili pia nimeanza kujiuliza mara mbili................ I kinda believe it!

Nilikuwa mmoja wapo! Naona wazeewa CCM wameanza kubalehe sasa
 
Wabunge wa CCM wanamgomea Rais kwa sababu naye aliwagomea kusaini nyongeza ya Posh!!. Acha wakomoane, wakoboane, wavuane magamba na ngozi lakini mwisho wa vita vya panzi kunguru ( wananchi) ndio tutafaidika. Mfumo uliowekwa na Masisiem wa kutawala kwa posho na kudai rushwa, utawatokea puani safari hii!
Hahahahaaa kwahiyo unataka kusema msingi mkubwa wa maelewano kupungua ni ulaji?
 
Nilikuwa mmoja wapo! Naona wazeewa CCM wameanza kubalehe sasa
Mzee mwenzangu umeona eeh? Unajua kawaida ukisikia kuna kikao cha wabunge wote wa CCM pale bungeni ujue kuna kitu hakiendi sawa ama wanataka kuwa na maazimio ya pamoja na huko ndiko mambo yanapotokea
 
Duuuh acha ushabiki sidhani Kama hii habari Ina ukweli! Kuna siagi mingi hapo. Ni MCC yupi wa kumgomea mwenyekiti wake? Usimeze kila kitu
Mchungaji vipi tena? Malaria Sugu kakusilimisha nini? Aliyekuwa anaogopwa ni Nyerere tu!
 
Ilishatabilika kuwa TZ aitatawalika. Mambo haya yasiposhughulikiwa kwa busara hakuna wa kumsikiliza mwenzie kwani kila m2 ni mtawala.
 
Huu ni mwanzo wa mwisho wa CCM. Hao wabunge wanaogopa kuondolewa madarakani au wanajali mustakabali wa taifa. Die softly CCM
 
Hivi katiba inasemaje? Akivunja bunge, si atakuwa na yeye amepoteza nafasi yake ya urais? Ikiwa hivyo, yeye atarudi kwenye kiti chake baada ya huo uchaguzi mwingine? Halafu na huu ukata wa serikali yake, anao ubavu wa kuitisha uchaguzi sasa? Lakini ningekuwa JK ningevunja bunge kabla wao hawajanipigia kura ya kutokuwa na imani nami.
 
Hizo ndio dalili za saa ile ya anguko kuu la magamba. Kama sasa wanazungumzia kumpigia kura ya kutokuwa na imani Rais wao eti kwa sababu ya chuki na visasi vya posho badala ya maslahi ya Taifa,magamba mmekwisha puu! Tulisema toka mwanzo,Cdm inatawala na huu ndio ushahidi
 
Unajua tumekuwa na taifa lenye kujali maslahi binafsi kwa kipindi kirefu na mara zote watu wamekuwa wakipiga kelele kuhusu hili na kuonekana kuwa wapayukaji. Lakini ukiangalia sakata hili utaona ni namna gani maslahi binafsi yanachukua nafasi kubwa kwenye maamuzi makubwa ya nchi hii........

I think we need to change, haimaanishi kwasababu tu kuna mabadiliko ya chadema ndio tukatae muswada, au kwasababu tu rais amekataa posho ndio tumvote out mi sidhani kama hii ni sawa
 
Nampongeza JK for the 1st time kwa maamuzi aliyochukua.Afadhali ameona umuhimu wakutenda haki na yaliyo mema kwa Tanzania
 
Back
Top Bottom