Wabunge CCM wamlipua Kikwete, WADAI WANAKERWA JINSI RAIS ALIVYOMGEUKA PINDA, MAKINDA

leo katika maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa ccm,mwnyekiti wa ccm mh jakaya kikwete amesema amepokea maoni mbalimbali juu ya sheria ya kurekebisha katiba.ametaja makundi kadhaa yaliyopeleka mapendekezo ya kubadilisha sheria hiyo,mojawapo ya makundi hayo ni ya chama cha mapinduzi.amesema ccm imepeleka mapendekezo manane.sasa hapa utajiuliza ilikuaje wabunge wa ccm kupitisha muswada huu kwa kishindo huku wakiwa na mapendekezo nane?hapa ndipo ninapowashangaa wabunge wa ccm kwa kuendekeza ushabiki bungeni.

Hata nyumba yako Bro unapoijenga ikipita siku utakuwa na hamu ya kubadili sehemu fulani kulingana na uwezo au kuona kwengineko. Hata hivyo unaanzia kwa kuukubali mchoro wa awali! Si unahitaji pa kuanzia???
 
WAJIPANGA KUKWAMISHA MUSWADA MABADILIKO YA KATIBA
Midraji Ibrahim, Dodoma
SASA ni dhahiri kuwa wigo wa mpasuko kati ya wabunge wa CCM na Serikali unazidi kupanuka, baada ya wabunge hao kugoma kukutana na Rais Jakaya Kikwete mjini Dodoma.Katika kikao chao kilichofanyika Ijumaa usiku ukumbi wa Pius Msekwa mjini hapa, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliwaomba wabunge hao kukutana na Rais Kikwete ili kuwasilisha malalamiko yao dhidi ya Serikali badala ya kuendelea kuikwamisha bungeni.

Wabunge hao wanadaiwa kukataa rai hiyo huku wakimweleza waziwazi Pinda kwamba, itakuwa ni kumkosea heshima na adabu Rais, iwapo watakutana naye halafu wakwamishe marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inayotarajiwa kufikishwa bungeni wiki ijayo.

“Itakuwa siyo heshima kukutana na Rais halafu tukwamishe muswada wa marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, kwa sababu tumejipanga kuhakikisha kwamba haupiti,” vilieleza vyanzo vyetu vya uhakika kutoka ndani ya kikao hicho.

Badala yake, wabunge hao walikubali kuteua miongoni mwao watu watano ambao wataonana na Rais Kikwete leo atakapowasili mjini hapa akitokea Mwanza kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 34 ya CCM.

Wazungumzaji wakuu kwenye kikao hicho wanadaiwa walikuwa pamoja na, Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na Mbunge wa Shinyanga, Steven Masele.

Marekebisho hayo yalitarajiwa kuwasilishwa kesho, lakini walikataa hadi Ijumaa kwa kile walichodai kuwa, wengi wao watakuwa hawajarejea kutoka Mwanza kwenye sherehe za maadhimisho ya CCM.

Inadaiwa na wabunge hao wa CCM kuwa, marekebisho hayo yanalenga kukimaliza chama hicho na kukiweka madarakani Chadema baada ya kuondolewa kwa wakuu wa wilaya, kushiriki mchakato wa katiba na kazi hiyo kukabidhiwa wakurugenzi wa halmashauri.

“Hii ni dhahiri kuwa marekebisho haya yanaiumiza CCM na kuisimika Chadema madarakani. Kuwaondoa Ma-DC kwenye mchakato wa katiba na kuweka wakurugenzi wa wilaya ambao wote ni Chadema, hatuwezi kukubali kamwe,” kilieleza chanzo chetu.
Pia, inadaiwa na wabunge hao kuwa marekebisho waliyopewa Dar es Salaam kwenye kamati, ni tofauti na yale yaliyowasilishwa bungeni, huku kukiwa na ongezeko la kurasa nne.

Hata hivyo, inadaiwa baada ya wabunge hao kugoma kukutana na Rais Kikwete, alisimama Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uratibu na Uhusiano), Stephen Wasira, akiwataka kupitisha marekebisho hayo kwa sababu ni agizo la Rais, hali iliyosababisha azomewe huku akitupiwa maneno ya kashfa.

Hata hivyo, baadhi ya wabunge hao ambao hawakupenda kutajwa majina yao, walisema athari wanayoiona mbele kwa kutopitishwa kwa marekebisho hayo, Chadema watapeleka mashtaka kwa umma kwamba sheria ile ilipitishwa kulinda CCM, hivyo haina manufaa kwa umma.

“Lakini CCM hatujajipanga, kila siku anayesimama jukwaani anazungumzia kujivua gamba, kwa hali hii tusubiri mashambulizi mazito siyo tu kutoka kwa Chadema hata nchi za nje,” kilieleza chanzo chetu.

Pia, wabunge hao wa CCM wanadai kuwa miongoni mwa sababu za kukwamisha marekebisho hayo, ni kile walichodai Rais Kikwete kuwadharau kutokana na wao kupitisha muswada wa sheria hiyo, halafu yeye (Kikwete) anakutana na Chadema dakika chache na kukubaliana na hoja zao.

“Sisi tumekaa hapa (bungeni) kwa zaidi siku mbili na akili zetu timamu, tukapitisha muswada ule, anakutana (Kikwete) na Chadema dakika chache anatuletea marekebisho! Hiyo ni dharau na hatuwezi kukubali,” alilalamika mbunge mmoja.
 
"Hii ni dhahiri kuwa marekebisho haya yanaiumiza CCM na kuisimika Chadema madarakani. Kuwaondoa Ma-DC kwenye mchakato wa katiba na kuweka wakurugenzi wa wilaya ambao wote ni Chadema, hatuwezi kukubali kamwe," kilieleza chanzo chetu.
Sina uhakika kwa hili kwani hawa ndiyo walio itesa CHADEMA kwenye uchaguzi mkuu wa Wabunge, Uchadema wao unajionyesha katika lipi ???

"Sisi tumekaa hapa (bungeni) kwa zaidi siku mbili na akili zetu timamu, tukapitisha muswada ule, anakutana (Kikwete) na Chadema dakika chache anatuletea marekebisho! Hiyo ni dharau na hatuwezi kukubali," alilalamika mbunge mmoja.
Hakuna lolote walilo lijadili kwenye huo mswada zaidi zaid walispend muda mwingi kuwasimanga CHADEMA na LISSU wake Wangelikuwa wanajadili sheria hiyo mapungufu hayo wangeliyaona mapema Hadi leo Rais ameyaona wanajifanya kumgomea Hivi kwa hali hii tutafika 2015 salama kweli



 
Aaah kumbe habari za makanjanja. Nilifikiria umetoa kutoka chanzo cha kuaminika.

Wehu unapomuingia mtu mzima huwa ni huzuni kwa familia na jamii husika, tofauti na hali hiyo inapomtokea mtu mwanzoni mwa uwepo wake duniani
 
Binafsi nilisikia kuwa leo wabunge wa ccm watagomea kujadili marekebisho ya hiyo sheria. Kwa hiyo inawezekana habari hii ikawa na upukupuku wa ukweli. Lisemwalo lipo, kumbukeni hata issue ya EPA ilipotajwa mwanzoni wengi walidai ni uzushi lakini ukweli si ulikuja kujulikana?

Kunawezekana kukawa na ukweli ktk hii habari.................ni suala la muda tutajua
 
Aaah kumbe habari za makanjanja. Nilifikiria umetoa kutoka chanzo cha kuaminika.

Nategemea Salamu utakuwa umeipata toka kwa yule unae muamini,hivyo nahakika kila kichajacho ndani ya jamvi sio ubabaishaji kwa asilimia kubwa ni fact.Kazi kwao wabunge wa CCM, salamu toka kwa mwenyekiti wao uko Mwanza.
 
Ukitaka kujua hasira za wabunge wa magamba ww gusa posho zao tu wataanza kuzomea humo bungeni kama watoto vile,kikwete piga chini wote wanaotaka kukupelekesha kisa posho,hii nayo kali FF kumbe ni id ya mama Lwakatare si angejiweka wazi tu kuliko kijificha kumbe mchangiaji mzuri tu humu JF afu akienda bungeni anajifanya kuichongelea JF yetu,ni bora awe busy na kurudisha kondoo wake zizini kuliko kuangaika na majabari
 
Ukitaka kujua hasira za wabunge wa magamba ww gusa posho zao tu wataanza kuzomea humo bungeni kama watoto vile,kikwete piga chini wote wanaotaka kukupelekesha kisa posho,hii nayo kali FF kumbe ni id ya mama Lwakatare si angejiweka wazi tu kuliko kijificha kumbe mchangiaji mzuri tu humu JF afu akienda bungeni anajifanya kuichongelea JF yetu,ni bora awe busy na kurudisha kondoo wake zizini kuliko kuangaika na majabari

hahaha!
 
KATI YA WENGI NLOSOMA MICHANGO YAO HUMU, WEWE NDO UMEONA ALICHOKIONA JK NA WATANZANIA WENGINE WACHACHE KAMA WEWE NA MIMI!! TATIZO LA WABUNGE WENGI CCM WANALEWA NA LILE NENO "MHESHIMIWA"!! Nlimsikiliza Zambi/Hamad asubuhi TBC ati wanadai wanawawakilisha wananchi!! ukiwauliza ni lini huo mswada na mingine waliipeleka kwa wananchi kwa kuitisha mikutano ya hadhara wataanza kuuma maneno na kutoa shababu mfu!!
Ni lazima wakubaliane na ukweli kwamba wameshindwa kufikia matarajio ya watz!!!

JK ni mwanasiasa mjanja, mwenye uwezo wa kuona mbali sana...
Wakati mwingi amekuwa akijitofautisha na wabunge wa chama
chake kwa kuwa wamekuwa wakitenda katika namna ya kukitia
hasara chama, posho ni jambo ambalo wananchi wengi wanalipinga
sana kwa vile tayari wabunge wanakipato kikubwa sana, hivyo kujiongezea
posho ni kuongeza gap kati ya wananchi na CCM.
CDM walipotoka bungeni hali ya amani nchini ilikuwa ni tete sana, ilikuwa
ni busara sana kwake kukutana nao ili kuepusha shari...alifanya jambo jema
kwa manufaa ya taifa wabunge wa CCM walishupalia ushabiki ambao ungeliingiza taifa
katika machafuko... BIG UP JK!!!
 
quote_icon.png
By FaizaFoxy
Aaah kumbe habari za makanjanja. Nilifikiria umetoa kutoka chanzo cha kuaminika.

FF kaingia mitini toka juzi. Ukweli unazidi kudhiirika.................. Mgogoro CCM hautakwepeka hata kwa dawa!!!
 
Back
Top Bottom