Martoism
Member
- May 31, 2012
- 36
- 21
Ni saa chache tu zimepita tangu Mkt wa Taifa Chadema na Kiongozi wa upinzani Bungeni ambaye pia ni mbunge wa hai Mh, Freeman Mbowe kuutangazia uma wa watanzania kuwa atatua mkoani Iringa na makamanda wa vuguvugu la mabadiliko almaarufu "Movement for Change M4C" kuwatia nuru ya mapambazuko na mwangaza wa utajiri walioukalia kwa mda mrefu chini ya viongozi wa CCM akiwamo spika wa bunge Anna Makinda, Prof Msola, Lukuvi, Deo Sanga - ''Jaa people'' na wengine ambao kwa taarifa zinazozagaa mitaani wamejiapisha na kuwaagiza makatibu wa chama chao kuhakisha nguvu ya M4C inadhoofishwa hata kwa nguvu ya dola na ndumba ili waendele kutawala . Najua unaweza kujiuliza Iringa ina nini? kwa kifupi tu niwaambie Iringa ni mkoa wenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani milioni moja kwa mwaka , ina mbuga kubwa na ya pili barani Africa yaani Ruaha National Park, vivutio vya utali kama kalenga na isimila , mikunjo (ox-bow lakes) ya "The great Ruaha River unaotiririsha maji throughout a year, mazao ya misitu kutoka Sao hill forest , migodi mikubwa ya makaa ya mawe, kilimo cha chai kisichokuwa na mfano barani Africa, viwanda vikubwa east and centra Africa kama Mufindi paper mills na Chai Bora lakini pamoja na utajiri wote huo bado Iringa ina harufu ya umaskini wa kutisha huku ikisifiwa kutoa mayaya wengi wanaofanya kazi miji na majiji mashuhuri kama Dar-es -Saalamu na kwingineko je mwanaJF mwenzangu M4C waende au Wasinde Iringa?